Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #21
Nani aliwasaidia Wamarekani na Waingereza?
watumwa???
Nani aliwasaidia Wamarekani na Waingereza?
watumwa???
Nani aliwasaidia Waswidishi, Wanorwei, Wajerumani?
Wamarekani! Which means you can't ask me "nani aliwasaidia Wamarekani"
Nani aliwasaidia Waaustrelia....? Waswisi?
Majibu yangu yatarudi huko huko Wamarekani. Nchi yoyote utakayouliza jibu lake ni Wamarekani.
Hihihihihiiiiii...this is funny!! Kweli Wamarekani wana moyo mzuri kweli....
Kwa nini Wamarekani wanasaidia kila nchi?
Kwanini wakisitisha misaada hali iwe "mbaya"? Ina maana pasipo hii misaada Watanzania hawawezi kuishi?
Sisi tumeshindwa kujitawala basi tuwaache watutawale kiutekelezaji, kazi yezi yetu uwe kuwaambia kuwa barabara ile mbovu wao wanatujengea, vyoo vile vimeziba wao wanatumia pesa zao kutuzibulia. Nafikiri tukifanya hivyo Ndani ya miaka mitano nchi itakuwa na mandhali tofauti kabisa.
Katika mazingira hayo tunaweza kuomba watuchagulia Rais na wasaidizi wake; Sasa tukiwakaribisha kwa hiari yetu waje watutawale tunaweza kuuita huo ni "ukoloni" au ndiyo "urafiki wa karibu"?
kwa sababu "wana moyo mzuri kweli"... usiulize kwanini wana moyo mzuri..
Misaada ambayo Tanzania imewahi kupewa tangu uhuru kama ingetumika vizuri nchi ingekuwa mbali sana inavyoelekea nchi hii haina vipaumbele{priority}.Tatizo linaloikabili nchi yetu pia ni ukosefu wa uwazi katika matumizi ya fedha za misaada tunazopewa na nchi wahisani.Fedha nyingi tunazopewa kwaajili ya miradi ya maendeleo zinatumika kwenye semina,kongamano,warsha & nk,tuchukue mfano wa mradi umwagiliaji.Asilimia 50% ya fedha zitatumika kwenye semina,20% usafiri {L / Cruiser VX & GX,Prado,mafuta & vipuli},20% technical {wataalamu kutoka nchi iliyotoa msaada}& 10% zitawafikia wananchi.Mara nyingi ninaposikia Tanzania imepata msaada wa mabilioni kutoka nchi wahisani picha ya semina na makongamano kwa wigi inanijia kichwani.
Misaada pia imetulemaza kwa kiasi kikubwa.sina figures kamili lakini waziri wetu wa fedha anaposoma budget nadhani kuna mahali anatamka bila aibu kabisa kwamba budget hii ina nakisi ya 40 % ambayo nchi wahisani wanategemewa kuchangia nakisi halafu nchi ambazo zimetoa ahadi ya kuchangia pengo la budget zinatajwa moja baada ya nyingine waheshimiwa wabunge nao hawako nyuma kushangilia kwa kupiga meza!.Mahali ninapoishiwa nguvu kabisa ni pale serekali inapoagiza magari ya kifahari kwa mawaziri,wakuu wa mikoa,makatibu wakuu,wakurugenzi & makamishna.Land Cruiser moja thamani yake ni zaidi ya Tsh 100 milioni kwa mikoa 22 ni sawa Tsh 2.2 bilioni hii ni hesabu ya wakuu wa mikoa tu bado makatibu tawala wa mikoa nao wako 22 tena siku hizi wamezalisha cheo cha katibu tawala msaidizi wote hawa wanastahili kutumia magari ya kifahari.Sijui kuna tatizo gani kama mkuu wa mkoa au waziri atatumia Suzuki,Land Rover au Land Cruiser hardtop.Nimezungumzia kipengele kimoja cha matumizi ya magari tukienda katika kila kipengele utagundua Tanzania hatuna haja ya kuomba misaada.Fedha za manunuzi ya magari ya kifahari pekee yake kama zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa shule za sekondari hakuna mtanzania atakayelazimishwa kuchangia ujenzi wa hizi shule za kata.
Kuna mtu kaniambia leo ingekuwa inawezekana tubadilishane na wazungu-yaani wazungu waende kwetu Africa na sisi tuhamie kwao. Akasema baada ya miaka miwili tungeanza kujipanga kuomba visa kwenda Tanzania na nchi zingine za Africa tena! Inawezekana hii ni kweli hee??
Ndo hapo mimi nashindwa kuelewa....yaani kuna watu wanadhani misaada ikisitishwa ndio itakuwa mwisho wa Tanzania. Mimi sidhani hivyo. Nadhani ikisitishwa itatufanya kama taifa tuwe na nidhamu (disciplined) katika matumizi na kupangilia vipaumbele vyetu. I dunno...I could be wrong....
Ngabu, nimeipenda sana post yako. Great. ngoja nisake moja niliyowahi andika hapo kitambo inayofanana..