Stop Foreign Aid to Tanzania Campaign!!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Jana katika "press briefs" ambazo zinaingia KLHN kila siku nilipata ujumbe toka Ubalozi wa Marekani kuelezea mradi wa kliniki iliyofunguliwa Mpwapwa leo. Sehemu ya ujumbe huo (kama note kwa Wahariri) ilidokeza vipi (maneno ya mabano ya kwangu):

The United States of America is a global leader in combating HIV/AIDS worldwide through PEPFAR, the U.S. President's Emergency Plan for AIDS Relief. This 10-year, $30 billion program, is the largest initiative in history to combat a single disease. Since its inception in 2003 (ndani ya miaka mitano iliyopita MM), the American people have provided over $817 million to combat HIV/AIDS throughout Tanzania.

Leo nikiwa na "mind my own dann business" nikapata briefs nyingine toka Ubalozi wa Uingereza (check habari kwenye mwanakijiji.com) na sehemu yake inasema hivi:


6. Elimu ya shule ya msingi, pamoja na Shule ya Uhuru Mchanganyiko, inasaidiwa na Serikali ya Uingereza kupitia mchango wake wa Kuunga mkono Bajeti ya Tanzania ujulikanao kama General Budget Support (GBS). Katika miaka mitano iliopita, Tanzania imepokea $900 milioni za Marekani (takriban £500 milioni) kama msaada kutoka Uingereza. Na mwaka huu, Uingereza itatoa £120 milioni moja kwa moja kwa Tanzania, ambayo £105 milioni ni za Msaada wa Bajeti ya Kupunguza Umasikini (PRBS) kwa serikali ya Tanzania. Uingereza ndio mfadhili mkubwa kati ya wafadhili 14 wa PRBS Tanzania. Fedha za PRBS zikichanganywa huwezesha serikali kutekeleza mpango wake wa kupunguza umasikini unaojulikana kama MKUKUTA.


My Take:
Taifa lililodekwa halijalii matumizi ya vitu vyake kwani linajua wajomba wataendelea kulimwagia vitu vingine zaidi. Tuanzishe kampeni ya kusitisha misaada ili kuwalazimisha watawala wetu kuanza kupanga na kusimamia kidogo walichonacho? Haya ni mataifa mawili tu, sijaingia kwenye Ujerumani, Japani, Ufaransa, na Scandinavia!!!!

Katika mazingira haya, mnaweza kweli kuona athari ya upotevu wa karibu dola bilioni 1 toka Benki Kuu in the past 10 years? Of course not!
 
Last edited by a moderator:
Mmh,nafikiri kama ghafla wakasitisha hiyo misaada hali itakuwa mbaya zaidi!Suala ni misaada hiyo inapitia kwenye mikono ya akina nani!?Je tuna udhibiti wa kutosha katika hizo fedha kutoka kwa wafadhili??Naona wanazidi kuweka bidhaa katika kapu lililotoboka.Tukizuia mianya ya 'wajanja' wachache kuzifuja fedha hizo kitakuwa kitu cha msingi.Lakini hii misaada ni mpaka lini?Mtazamo wangu ni kuwa mpaka pale Tanzania itakapopata viongozi walio commited and they are clean!
 
Kwanini wakisitisha misaada hali iwe "mbaya"? Ina maana pasipo hii misaada Watanzania hawawezi kuishi?
 
Kwanini wakisitisha misaada hali iwe "mbaya"? Ina maana pasipo hii misaada Watanzania hawawezi kuishi?

Ndo hapo mimi nashindwa kuelewa....yaani kuna watu wanadhani misaada ikisitishwa ndio itakuwa mwisho wa Tanzania. Mimi sidhani hivyo. Nadhani ikisitishwa itatufanya kama taifa tuwe na nidhamu (disciplined) katika matumizi na kupangilia vipaumbele vyetu. I dunno...I could be wrong....
 
Ni busara kabla ya kusitisha hiyo misaada pakawa na sera zilizo wazi na zinazotekelezeka reasonably za ni kwa vipi tutasimama sisi kama sisi.Je,zipo?Au tukishasitisha ndo tutaanza ku_iformulate.Ila nakubaliana kuwa in the long-run we need to say no,enough is enough.
 
Mzee Mwanakijiji mimi ninakubakiana nawe kabisa, hii misaada tunayopokea ndio ambayo inatufanya tusiendelee mbele, akili zetu hatuzishughulishi ipasavyo tukijua kuwa tutasaidiwa, na msaada tunaopewa ni kidogo ambayo haikizi haja ya mahataji yetu
 
Wanajf,
Nawapa pongezi kwa mijadala yenu inayozidi kuiamsha jamii ya kitz kila siku zinavyokwenda. Hii mijadala yenu imesaidia sana watz kuamka,hali hii nimejionea mwenyewe nilipokuwa kyela na mbeya mjini week 3 zilizopita.Naandaa andiko langu kuunga mkono ule waraka wa mchungaji.Kwenye hilo andiko nitaonyesha ni wapi pana hitilafu katika dhana nzima ya mchakato wa maendeleo vijijini na wadau wa maendeleo(donors). Naomba sana msikate tamaa kazi na michango yenu imeanza kuamsha jamii ya vijijini.
 
Sehemu kubwa ya misaada hiyo inarudi kwao! hii inatokana watekelezaji wa miradi hiyo ni raia wa nchi hizo zinazotoa misaada. Sidhani kama ni misaada kama tunavyotakiwa kuamini, ni namna nyingine ya wamerekani na waingereza kutengeneza masoko ya bidhaa zao na kuongeza ajira kwa watu wao.

Wamerekani wana sheria inaitwa BAA (Buy American Act), sheria inalazimisha manunuzi yafanyike kutoka kwao hata kama ni gharama. Tutaendelea kusoma figure kubwa billions or millions of dollar za misaada wakati mwananchi ataambulia sanasana condom au chandarua tena kwa bei nafuu wakati hela ya maan inarudi back home state.

Labda ningalikuwa mwandishi nisngeishia katika ukasuku wa kuchukua kilichosemwa na huyo mzungu bali ningalimuuliza adadavue kidogo huo msaada ni wanamna gani na tender wanapewa wa kinanani. Kuliko kuendelea kutoa walinzi na madereva wakati wataalamu wetu wako katika migomo na kuendelea kukosa sifa za kupiga hela za hawa jamaa.
 
Ukimsaidia sanaaaaaa baba wmenyenyumba ambaye hajali watoto wala mke msaada huo ni bure kwani hatapeleka watoto shule kupitia huo msaada, hataingiza maji safi na umeme nyumbani kumsaidia mama na watoto, hatapelekawatoto hospitali kama wanaumwa, hatajenga kanjia kazuri kakumfanya mama na watoto wapite vizuri kuelekea sehemu nyingine. Hii misaada inatumiwa vibaya Selikarini kwa wachache kujineemesha na kusahau madhumuni waliyoambiwa na mfadhili husika. Nchi zile zimejiwekea mafungu mbalimbali kutoka kwa walipa kodi wao na kusaidia nchi masikini kama bongo lakini wachache hata hawaogopi wanatumia asilimia kubwa ya pesa hizo kwa matumizi yao binafsi mwisho wa siku jamii iliyokusudiwa kupata unafuu kupitia mikopo hiyo haipati bali ugumu wa maisha unazidi siku hadi siku tubadilike.

Kuna wahusika wengine wamo humuhumu JF wanashiriki ipasavyo kutafuna pesa za misaada hiyo jamani tuanze kubadilika humuhumu jf na tukemee wale wanaotaka kutushirikisha ktk utafunaji huu haramu.

Nini kifanyika, kuanzishwe ufatiliaji wa kila shilingi inayokusanya huko bongo na zile za kutoka kwa wahisani, tupange matumizi vizuri na kufatilia mwenendo wa pesa na kuhakikisha kila pesa ina documents za halali na pesa imetumika kihalali linawezekana hili tubadilike hata nchi za wenzetu wanatushangaa.

Tuache milolongo isiyo ya lazima na kusaidia misaada kuwafikia walengwa bila kuchelewa kwa kusubiri sahihi ya fisadi mmoja ambaye hata hajui mtu wa kawaida anahangaika vipi mitaani inauma sana.

Tuache ukabila tuangalie utendaji wa kazi na usawa tutafika tu otherwise pesa za wahisani(vijisenti) zitzendelea kujenga majumba ufukweni na zingine kuozea kwenye account za nje.

Eti kuna walimu nawafanyakazi waliokwenda mbele za haki lakini wajanja wanaendelea kuwithdraw mishahara yao. How this is happening?

Eti kuna cheti kimoja kinatumika ktk wizara mbalimbali na watu wawili tofauti how how why why when when naenda kutapika ntarudi

Mungu tusaidie
 
Maisha tegemezi ni jadi ya Watanzania,Kwani hata JK anaona misaada ni ujiko,Wanancjhi hata wasomi wanaona kusaidiwa ndiyo ajira.Unadhani katika hali ya kawaida wataelewa unaongea kitu gani?
Hakuna zawadi ya bure duniani,Kila akupae kitu ana lengo lake.Yamkini waingereza na Marekani siyo kwamba wana mapenzi mema sana nasi>LA HASHA,Wafadhili wote wana agenda ya sisi tuendelee kuchapa usingizi tuu,Kwa kuambiwa kufadhiliwa.Leo hii hata mtoto mdogo huko Meatu au Nkasi anakwambia bila ufadhili wa hili na lile serikali haina uweo!Jamani tutafika kweli?
 
Misaada ambayo Tanzania imewahi kupewa tangu uhuru kama ingetumika vizuri nchi ingekuwa mbali sana inavyoelekea nchi hii haina vipaumbele{priority}.Tatizo linaloikabili nchi yetu pia ni ukosefu wa uwazi katika matumizi ya fedha za misaada tunazopewa na nchi wahisani.Fedha nyingi tunazopewa kwaajili ya miradi ya maendeleo zinatumika kwenye semina,kongamano,warsha & nk,tuchukue mfano wa mradi umwagiliaji.Asilimia 50% ya fedha zitatumika kwenye semina,20% usafiri {L / Cruiser VX & GX,Prado,mafuta & vipuli},20% technical {wataalamu kutoka nchi iliyotoa msaada}& 10% zitawafikia wananchi.Mara nyingi ninaposikia Tanzania imepata msaada wa mabilioni kutoka nchi wahisani picha ya semina na makongamano kwa wigi inanijia kichwani.
Misaada pia imetulemaza kwa kiasi kikubwa.sina figures kamili lakini waziri wetu wa fedha anaposoma budget nadhani kuna mahali anatamka bila aibu kabisa kwamba budget hii ina nakisi ya 40 % ambayo nchi wahisani wanategemewa kuchangia nakisi halafu nchi ambazo zimetoa ahadi ya kuchangia pengo la budget zinatajwa moja baada ya nyingine waheshimiwa wabunge nao hawako nyuma kushangilia kwa kupiga meza!.Mahali ninapoishiwa nguvu kabisa ni pale serekali inapoagiza magari ya kifahari kwa mawaziri,wakuu wa mikoa,makatibu wakuu,wakurugenzi & makamishna.Land Cruiser moja thamani yake ni zaidi ya Tsh 100 milioni kwa mikoa 22 ni sawa Tsh 2.2 bilioni hii ni hesabu ya wakuu wa mikoa tu bado makatibu tawala wa mikoa nao wako 22 tena siku hizi wamezalisha cheo cha katibu tawala msaidizi wote hawa wanastahili kutumia magari ya kifahari.Sijui kuna tatizo gani kama mkuu wa mkoa au waziri atatumia Suzuki,Land Rover au Land Cruiser hardtop.Nimezungumzia kipengele kimoja cha matumizi ya magari tukienda katika kila kipengele utagundua Tanzania hatuna haja ya kuomba misaada.Fedha za manunuzi ya magari ya kifahari pekee yake kama zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa shule za sekondari hakuna mtanzania atakayelazimishwa kuchangia ujenzi wa hizi shule za kata.
 
Lazima tuweze kuishi bila kusaidiwa, tupende tusipende. Na hii recession...unadhani watatusaidia waache kusaidia watu wao kwanza.
 
Back
Top Bottom