PreGE2025 Stephen Wasira akutana na Kadinali Protase Rugambwa Tabora

PreGE2025 Stephen Wasira akutana na Kadinali Protase Rugambwa Tabora

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na Muadhama Kadinali Protase Rugambwa katika Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.

Wasira amekutana na Kadinali Rugambwa leo Aprili 16, 2025 katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani Tabora.
WhatsApp Image 2025-04-16 at 15.56.00_eb06d1b3.jpg

WhatsApp Image 2025-04-16 at 15.56.01_89a76de4.jpg

WhatsApp Image 2025-04-16 at 15.56.03_6d4f2304.jpg
Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na ustawi wa Tanzania.

Aidha, baada ya mazungumzo yao Wasira ametembelea Shule ya Sekondari ya St Marrys (Mihayo) iliyopo mjini Tabora.

Shule ya Sekondari ya St. Mary's imebeba historia kubwa kwani ndiyo Shule ya kwanza ambayo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifundisha kwa miaka mitatu.
WhatsApp Image 2025-04-16 at 15.56.02_efd7af0a.jpg
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na Muadhama Kadinali Protase Rugambwa katika Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.

Wasira amekutana na Kadinali Rugambwa leo Aprili 16, 2025 katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani Tabora.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na ustawi wa Tanzania.

Aidha, baada ya mazungumzo yao Wasira ametembelea Shule ya Sekondari ya St Marrys (Mihayo) iliyopo mjini Tabora.

Shule ya Sekondari ya St. Mary's imebeba historia kubwa kwani ndiyo Shule ya kwanza ambayo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifundisha kwa miaka mitatu.

IMG-20250416-WA1427(1).jpg

IMG-20250416-WA1415(1).jpg

IMG-20250416-WA1425(1).jpg
 
Attachments

  • IMG-20250416-WA1417(1).jpg
    IMG-20250416-WA1417(1).jpg
    512 KB · Views: 21
"Muadhama Kadinali Protase Rugambwa" Lichunge Kanisa la Bwana,
alilolinunua
kwa Damu yake Mwenyewe.
 
1744819785823.jpeg
1744819871485.jpeg

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na Muadhama Kadinali Protase Rugambwa katika Jimbo Kuu Katoliki la Tabora. Wasira amekutana na Kadinali Rugambwa leo Aprili 16, 2025 katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 mkoani Tabora.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na ustawi wa Tanzania. Aidha, baada ya mazungumzo yao Wasira ametembelea Shule ya Sekondari ya St Marrys (Mihayo) iliyopo mjini Tabora. Shule ya Sekondari ya St. Mary's imebeba historia kubwa kwani ndiyo Shule ya kwanza ambayo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifundisha kwa miaka mitatu.

My take : Mwadhama Kardiali Rugambwa , jiepushe na kukutana na watu waovu tena wa uovu wa makusudi
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na Muadhama Kadinali Protase Rugambwa katika Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.

Wasira amekutana na Kadinali Rugambwa leo Aprili 16, 2025 katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani Tabora.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na ustawi wa Tanzania.

Aidha, baada ya mazungumzo yao Wasira ametembelea Shule ya Sekondari ya St Marrys (Mihayo) iliyopo mjini Tabora.

Shule ya Sekondari ya St. Mary's imebeba historia kubwa kwani ndiyo Shule ya kwanza ambayo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifundisha kwa miaka mitatu.
Viongoz wa dini ni njaa tu,
 
Mwadhama Kadinali anatakiwa kuwa makini zaidi. Tukio hili CCM watalitumia kwa dhamira ovu, kutaka kuthibitisha kuwa Kanisa Katoliki linaunga mkono uovu wa CCM na Serikali yake.

Kadili alistahili kutumia nafaisi hiyo kuionya CCM dhidi ya dhuluma, na uvunjifu wa haki unaofanywa na CCM dhidi ya wananchi na vyama vya upinzani, na wale wanaoikosoa Serikali, badala ya kukutana na kupiga picha za kusambaza mitandaoni.
 
Labda alimchana live huko ndani, huwezi jua.
 
Huyu Wasira sasa ni wakala wa shetani. Kakubali kutumika na kupoteza heshima hata katika uzee wake!
Sasa anacho pigania hasa ni kitu gani katika kushiriki katika uovu unaofanyiwa nchi hii!

Anajijengea historia ya kutambulika kuwa mmoja wa adui wakubwa wal waTanzania. Hivyo vipesa anavyo vipata vitamsaidia kitu gani tena huyu katika hatua aliyofikia katika uhai wake?
 
Cardinal Rugambwa, Cardinal Rugambwa, Cardinal Rugambwa, kuwa makini sana na wanasiasa sisi wananchi hatuliziki namna mambo yanovyoendeshwa. Mambo ya uchumi Kwa watanzania waliowengi ni magumu sana. Hivyo viongozi wa dini epukeni mitego ya wanasiasa na mkaingia mkenge wa kuwatetea na kutesa wananchi. Mateso yamekuwa mengi sana ndani ya nchi yetu sote yaani watawala waliopo wamefanya nchi ni yakwao na familia zao. Chondechonde kweni makini.

Wekeni msimamo kama wa kanisa la Anglican Kenya wamezuia viongozi wa siasa kutoa hutuba kanisani. Nanyi fanyeni vivyohivyo.

Kumbukeni "YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIKUWA MKALI KWA VIONGOZI DHARIMU NA UTAWALA WA UNYONYAJI, ALIFIKA SIKU MOJA HEKALUNI NAKUKUTA HEKALU LIMEKUWA SOKO AKAWAFURUSHA WOTE. PIA WAKATI WAKUTESWA ALIVUMILIA NA HAKUWATAYARI KUFUATA MATAKWA YA WATAWALA NA VIONGOZI DHARIMU. MAANA ANGEKUWA DHAIFU WA IMANI ANGEWEZA KUWABEMBELEZA WATAWALA NA KUWA UPANDE WAO NA AKAFAIDI MIHELA NA UFAHARI WA DUNIA. LAKINI ALIKUWA IMARA AKAWA MTII MPAKA MAUTI NAAM MAUTI YA MSALABA" Mwisho wa kunukuu.

Cardinal Rugambwa epuka mitego ya wanasiasa. Nakuamini sana Kwa weredi wako wa mambo na Imani katika KRISTO YESU.

Kumbuka hata kuzaliwa kwako ilikuwa ni miujiza mkubwa baada ya kukaa tumboni mwa mama yako miezi Kumi na Moja (11) akajaja marehemu Cardinal Rugambwa kusalimu nyumbani kwenu maana alikuwa rafiki mzuri sana na mjomba wako. Ndipo mjomba wako akamwambia rafiki yangu hapa nyumbani tunamatatizo maana dada yangu anamimba na sasa ni mwezi wa Kumi na Moja bado hakuna matumaini. Ndipo akatoa baraka na kumuombea mama yako na ukazaliwa siku hiyohiyo na ukaitwa jina Rugambwa.

Tafadhari sana narudia kuwa makini sana na wanasiasa maana wanajua viongozi wa dini mnanguvu ya ushawishi. Ni hayo tu.

NIMEANDIKA HUKU NIKITOA CHOZI LA ROHONI.
 
Strategically, the politicians want the unchallenged support from the church, especially church princes like Cardinal Rugambwa
That's precisely what they are after. It will be very disheartening if the church is gullible enough not to see what is being sought from them.
It is possible they are being issued with threats right now if they will not cooperate and acquiesce with what they have been vocal against in the past.
Seems the money that has been dished out to them to buy their silence hasn't been enough!
 
NIMEANDIKA HUKU NIKITOA CHOZI LA ROHONI.
Pole zako na kwetu sote mkuu. Sote tunatoa machozi ya rohoni, kila mmoja wetu kwa njia zake kwa kuona nchi yetu inavyo najisiwa na hawa viongozi wasiokuwa na chembe hata ndogo mioyoni mwao juu ya hali duni inayo wakabili waTanzania.

Itasikitisha sana kuona hata hawa viongozi wa kanisa watafumbia macho uozo unaoendelea sasa ndani ya nchi hii.
 
Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na ustawi wa Tanzania.
"...umuhimu wa kudumisha amani na ustawi wa Tanzania", ni kuhakikisha kuwa HAKI inapatikana kila mahali; nje ya hapo, hakuna amani ya kweli.
CCM sasa wanatumia hadaa ya amani, huku wakinyima HAKI raia zake. Ni lazima waTanzania tuanze kuukataa ulaghai wa aina hii.
 
Wamekwisha pewa ONYO kali hawa, katika ile hotuba ya kuadhimisha Ramadhani, hivi karibuni.
Aliyetoa onyo hawajui hawa vizuri. Viongozi wa kanisa catholic ni level nyingine yaani ni zaidi ya nchi, ndio maana viongozi wa serikali wanajipendekeza Kwa kuwatembelea maana wanajua.
 
Aliyetoa onyo hawajui hawa vizuri. Viongozi wa kanisa catholic ni level nyingine yaani ni zaidi ya nchi, ndio maana viongozi wa serikali wanajipendekeza Kwa kuwatembelea maana wanajua.
Nasikiliza tu kusikia kitakacho semwa au kitakacho achwa kusemwa.

Aliyetoa onyo anawajuwa, ndiyo maana nguvu kubwa zinatumika sasa hivi kuwanyamazisha hata kwa vitisho. Ule mkasa wa Bandari, baada ya kuwalaghai na kuwahadaa, na kuwatia aibu kubwa, sasa anajiandaa kwa njia mbalimbali kuwaweka mstarini. Hata kuwahonga pesa(RUSHWA) kwake haikuwa tatizo, na kama hilo halitatosha, vitisho na njia zingine mbadala zitatumika.
 
Back
Top Bottom