Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,933
- 4,706
Baada ya familia kukosa "tamthilia" kwa karibia wiki mbili, jana nilienda kununua "decoder" ya StarTimes na "Antenna" na "Cable". Nilivunga kadri ya maelekezo lakini sikupata "signal"! Baadaye nikaamua kutumia "antenna na cable" ya zamani ya "analogia" ni kafanya "Search" nikapata "channels"!
Jioni nikapigiwa simu na "huduma kwa wateja" na kuniuliza kama nimefanikiwa kupata "channels". Niliwaambia nimefanikiwa lakini sijatumia "antenna" yao! Yule mpiga simu akaniambia nigeuze antenna "iangalie kisarawe"!!!! nilimshukuru kwa kunipigia simu na nikamwambia hapa nilipo Bunju B siwezi kuwa na uhakika nigeuze vipi "antenna" iangalie Kisarawe!!!
Karibu Katika Ulimwengu Wa Digitali...!
.
Chacha naona uonevu wa wazi wazi. Kila Kitu kicharawe, gesi Kicharawe, antena Kicharawe nini kimebaki chacha kama sio kutuamuru na wake zetu tuwaelekeze Kicharawe?
.