Startimes hiki kiburi chenu kitakuwa anguko lenu nashangaa TCRA wanawachekea tu

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Hivi TCRA mpo kweli? TCRA mpo kweli? Ninaona mkiyashughulikia makampuni ya simu kisawa sawa mnayaacha haya makampuni ya visimbuzi yakiwanyanyasa wateja tu

Mfano nzuri ni hii kampuni ya StarMedia wanaomiliki visimbusi vya Startimes hawa kwanza hawaeleweki na wanaibia wateja

Kwanza kabisa vifurushi vya siku inafahamika siku ina masaa 24 lakini wao wameamua kufanya nusu siku mfano ukilipa 3600 kifurushi cha siku ukilipa usiku saa 5 ikifika kesho yake saa 6 mchana washakata huo si wizi huo?

Vifurushi vya mwezi havieleweki wanaweka huduma kijanja janja na kihuni huni ili waibie wateja mfano kifurushi cha nyota hakipo kwenye menyu yao ya malipo kwahiyo ukilipa elfu 11 yako usishangaa kikakaa week tu wakakata ukipiga wanakujibu kwa jeur kwamba kifurush hicho lazima upige simu uwaombe kikae mwezi huo si wizi huo

Juzi mmewapiga makampuni ya simu faini kwa kushindwa kufafanua maudhui vizuri naombeni na hawa wapigwe faini kubwa ili iwe funzo maana haiwezekani wacheze na kuibia wateja

Kingine ni suala la kupandisha vifurushi hovyo hovyo tu japo hili halihusu sana kuzungumza ila inawezekana vipi miaka miwili tu kifurushi kipande toka 4000 hadi 9000?... toka 6000 hadi 11000?sasa hapo inamaana ifikapo 2022 vifurushi vyao vitakua vishafika 30000 kwa kifurushi cha chini?
Wenzao wanajitahidi kushuka wao wanapanda tu

Startimes hichi kiburi chenu nawaambia kitakuja kuwashusha daima na mutaanguka chini moja moja jifunzeni kwa airtel enzi zile wakijiita celtel sahv wako wapi?

Jifunzeni kwa continental decoder sahivi washakufa kifo cha mende

Startimes mmekuwa ni watu wa kutoa channels hasa zile ambazo ndo nyie mnacopy huko tamthilia ili kuwazuia watu wasifahamu chimbo mnaloenda kucopy tamthilia
 
Halafu zile channel za Tz wanalipisha wakati waliambiwa wasilipishe sijui wakoje wanabakisha TBC na SAFARI tu
 
wajeuri kweli mfano. channel ya st. swahili siku nzima wanaweka tamthilia za kihindi wanadhani kila mtu anapenda maigizo hayo badala ya kuweka za kitanzania duh.
 
Za kitanzania ni nani ataangalia bongo movie?
wajeuri kweli mfano. channel ya st. swahili siku nzima wanaweka tamthilia za kihindi wanadhani kila mtu anapenda maigizo hayo badala ya kuweka za kitanzania duh.
 
Wezi aisee hili kampuni. Mfano kisimbusi cha dish, ukilipia kifurushi cha chini elfu 11 hamna cha maana unachoangalia zaidi ya st swahili
 
Back
Top Bottom