Head to Head: Zuku vs Star Times

Endangered

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
922
228
Wakuu heshima mbele,
leo natamani tutathmini kwa pamoja huduma zinazotolewa na hizi kampuni mbili.

1. Vifurushi
Zuku wana vifurushi vya aina 4: Zuku classic, Zuku premium, Asia classic na Asia premium.
Zuku classic ina 35+ video channels, 40+ audio channels, na Local channels, hapa sijajua ni zipi hizo. (20,000 / mwezi)
Zuku Premium ina 60+ video channels, 40+ audio channels, na local channels. (40,000 / mwezi)
Asia classic ina 40+ video channels, 40+ audio channels, na local channels (30,000 / mwezi)
Asia Premium ina 70+ video channels, 40+ audio channels (60,000 / mwezi)

Star times wana vifurushi vya aina 3: Mambo/Basic, Uhuru na Kili
Mambo/Basic ina takriban stesheni 35 and growing (9,000 / mwezi)
Uhuru ikiwa na takriban stesheni 47 and growing (18,000 / mwezi)
na Kili (latest entry) ikiwa na stesheni 52 and growing (35,000 / mwezi)

2. Installation
A complete Zuku TV kit + Installation itakugharimu 92,000. (hawa wakufungia kidish chao - to your decoder)

With star times, you can do it yourself, mana ni antenna yako tu to the decoder (ya ndani au nje kulingana na sehemu uliyopo) na gharama iliyopo kwa ofa sasaivi ni 39,000. bei ya kawaida ni 70,000.

3. Malipo
Zuku inalipiwa through mobile money: M-pesa, airtel money. Sina hakika kama wameshaongeza miotandao mingine. But also wana option ya kulipa online na visa card.(nadhan hii ni mostly applicable Uganda)

Startimes wao pia wana mobile money kama njia ya malipo, kuna m-pesa, tigo pesa, na pia kupitia "wakala" maxcom, na selcom paypoint.

4. Goodies
Well, hapa actually namaanisha huduma za ziada zitakazokufanya ununue huduma mojawapo.

Zuku wana online schedule ya stecheni zao, na pia upcoming stuffs, ikiwemo youtube channel, ambapo wana-advertise program (including movies & etc) na kiujumla website yao imekaa njema. (hosting yao ni Kenya) kuna namba, facebook page, na twitter, hivyo ni rahisi kuwapata kwa medium unayoprefer.

Star times, aka wawekezaji - hawana website yenye mvuto kivile (imehostiwa bongo), ila wameweka taarifa za maduka yao kila mkoa (wanapo-operate) na namba zao (picha zikiwemo pia) This is nice kwa kuwa hutapotea ama kutapeliwa kirahisi.

Conclusion:
Kama hutaki watu, especially mwenye nyumba wajue kuwa una kin'gamuzi, basi nunua Star times na uendelee kutumia antena yako ya kawaida. Though kufikia tarehe 31 disemba atajua tu ya kwamba umenunua, otherwise wewe huangalii taarifa ya habari TBC. teh teh.

kama hujali sana, basi nenda kwa Zuku, huduma yao ya Nairobi wana kitu kinaitwa triple play, hapa wanakupa kin'gamuzi, simu na internet uhangaike nayo mwenyewe kwa malipo yaleyale, ambayo ni fast kuliko hizi nilizowahi kutumia bongo (ttcl, voda, tigo na wenzao) 1MB kwa 2999, kama 60,000 ya kibongo - au 8MB kwa 3999, kama 80,000 ya kibongo, na pia 20MB kwa 9999 - takriban kilo 2 za bongo, japo tunatumia nyumba nzima (aka watu watatu) kwa wireless, ukitaka cable pia ipo (spidio yao ni noma, I have to stress this). So ninahope siku wata-uipgrade huduma hii kwa hapa tz ili nasi tufaidi.

Mimi nitakuwa mtu wa Zuku, sijajua tu kama bei itapanda ama itapungua baada ya disemba, naskilizia kwanza kabloa ya kununua. Enough for now, ni muda wa kuskia toka kwa wadau.

Bibliography:
Zuku Kenya
Zuku Tanzania
Startimes Tanzania
Japo Tz
 
Shukran mkuu, chief-mkwawa. Hapa nadhan inaweza kuwa interms of reception, customer care, updates and upgrades, na mengineyo.
 
Last edited by a moderator:
Nimeipenda topic na analysis yako.
Sometimes unapochagua king'amuzi ni zaidi ya bei na idadi ya channels. Kuna watu wanatafuta aina fulani ya Channel eg kuna watu ni wapenzi wa movies na wengine soccer or documentaries.
  • Mie naona Zuku kwa soccer wako chini wana station za zuku sports, setanta na euro sport news. Mwingine ani-update kwa Startimes lakini kuna wakati walikuwa wanaonyesha league ya Italy (Serie A) and Spain (La Liga)
  • Kwa Tz Zuku wana local channels chache sana (only 2), na local channels nyingi za kenya na uganda hapa tz hazifunguki. Walipokuja Zuku waliahidi kuwa na ITV pamoja na EATV (ch. 5) lakini naona mambo ya mikataba walishindina na IPP wakaishia kuweka Channel 10 na TBC peke yake. Nadhani wakenya wanafurahia zaidi Zuku kwa sababu local channel nyingi ni za Kenya
  • Kwa channel nyingine kama news (International), documentary na movies Zuku wanamuacha Startimes kwa mbali sana. Labda hicho kibando cha kili walichokiongezea kinasogea kwa mbali saana.
  • Kitu nisochokipenda zaidi kwa Zuku ni "Decoder" yao. Inatumia remote tu! Ikiharibika na kama huko mikoani una taabu. Kuna wakati remote yangu iliharibika nikajikuta naangalia channel moja tu. Kuwatafuta customer care is headache. I hope Zuku will change this.
Nawakilisha!
 
Sie wazee wa cable zinachuliwa channel bomba zote toka kila king'amuzi na chanel zingine za ziada na tunapewa mzigo ambao umekamilika
 
Sie wazee wa cable zinachuliwa channel bomba zote toka kila king'amuzi na chanel zingine za ziada na tunapewa mzigo ambao umekamilika
Kuna baadhi ya mikoa hapa TZ cable imegoma kabisaaa! Kila watu wakijaribu kuweka cable zinashindwa. Kuna mmoja aliweka cable akawa anarusha DSTV (S3) wakamkamata wakafunguliwa mashitaka na kufilisiwa. Wenzake wakaogopa wakaondoa SuperSport na hivyo zikawa hazivutii tena
 
kuhusu hayo mambo ya internet nadhani ndipo watakapo ni kamatia hawa zuku ngoja tuona kama wataileta hiyo huduma na bongo..
 
Zuku vs startimes nadhani bado wote hawajanivutia vya kutosha labda wakija na hicho triple internet service labda hao zuku kwa sasa natamba na EasyTv channel local Kama 6 bora kabisa total channel 26 zikiwemo za movie series kenya na uganda pia .

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
wakuu heshima mbele,
leo natamani tutathmini kwa pamoja huduma zinazotolewa na hizi kampuni mbili.

1. Vifurushi
zuku wana vifurushi vya aina 4: Zuku classic, zuku premium, asia classic na asia premium.
Zuku classic ina 35+ video channels, 40+ audio channels, na local channels, hapa sijajua ni zipi hizo. (20,000 / mwezi)
zuku premium ina 60+ video channels, 40+ audio channels, na local channels. (40,000 / mwezi)
asia classic ina 40+ video channels, 40+ audio channels, na local channels (30,000 / mwezi)
asia premium ina 70+ video channels, 40+ audio channels (60,000 / mwezi)

star times wana vifurushi vya aina 3: Mambo/basic, uhuru na kili
mambo/basic ina takriban stesheni 35 and growing (9,000 / mwezi)
uhuru ikiwa na takriban stesheni 47 and growing (18,000 / mwezi)
na kili (latest entry) ikiwa na stesheni 52 and growing (35,000 / mwezi)

2. Installation
a complete zuku tv kit + installation itakugharimu 92,000. (hawa wakufungia kidish chao - to your decoder)

with star times, you can do it yourself, mana ni antenna yako tu to the decoder (ya ndani au nje kulingana na sehemu uliyopo) na gharama iliyopo kwa ofa sasaivi ni 39,000. Bei ya kawaida ni 70,000.

3. Malipo
zuku inalipiwa through mobile money: M-pesa, airtel money. Sina hakika kama wameshaongeza miotandao mingine. But also wana option ya kulipa online na visa card.(nadhan hii ni mostly applicable uganda)

startimes wao pia wana mobile money kama njia ya malipo, kuna m-pesa, tigo pesa, na pia kupitia "wakala" maxcom, na selcom paypoint.

4. Goodies
well, hapa actually namaanisha huduma za ziada zitakazokufanya ununue huduma mojawapo.

Zuku wana online schedule ya stecheni zao, na pia upcoming stuffs, ikiwemo youtube channel, ambapo wana-advertise program (including movies & etc) na kiujumla website yao imekaa njema. (hosting yao ni kenya) kuna namba, facebook page, na twitter, hivyo ni rahisi kuwapata kwa medium unayoprefer.

Star times, aka wawekezaji - hawana website yenye mvuto kivile (imehostiwa bongo), ila wameweka taarifa za maduka yao kila mkoa (wanapo-operate) na namba zao (picha zikiwemo pia) this is nice kwa kuwa hutapotea ama kutapeliwa kirahisi.

conclusion:
kama hutaki watu, especially mwenye nyumba wajue kuwa una kin'gamuzi, basi nunua star times na uendelee kutumia antena yako ya kawaida. Though kufikia tarehe 31 disemba atajua tu ya kwamba umenunua, otherwise wewe huangalii taarifa ya habari tbc. Teh teh.

Kama hujali sana, basi nenda kwa zuku, huduma yao ya nairobi wana kitu kinaitwa triple play, hapa wanakupa kin'gamuzi, simu na internet uhangaike nayo mwenyewe kwa malipo yaleyale, ambayo ni fast kuliko hizi nilizowahi kutumia bongo (ttcl, voda, tigo na wenzao) 1mb kwa 2999, kama 60,000 ya kibongo - au 8mb kwa 3999, kama 80,000 ya kibongo, na pia 20mb kwa 9999 - takriban kilo 2 za bongo, japo tunatumia nyumba nzima (aka watu watatu) kwa wireless, ukitaka cable pia ipo (spidio yao ni noma, i have to stress this). So ninahope siku wata-uipgrade huduma hii kwa hapa tz ili nasi tufaidi.

Mimi nitakuwa mtu wa zuku, sijajua tu kama bei itapanda ama itapungua baada ya disemba, naskilizia kwanza kabloa ya kununua. Enough for now, ni muda wa kuskia toka kwa wadau.

Bibliography:
zuku kenya
zuku tanzania
startimes tanzania
japo tz

we mkali, umenifurahisha mwisho wa mada yako umeweka refernces. Inaonekana uko good katika kujali mawazo ya wengine.
 
  • ...Nadhani wakenya wanafurahia zaidi Zuku kwa sababu local channel nyingi ni za Kenya
  • Kwa channel nyingine kama news (International), documentary na movies Zuku wanamuacha Startimes kwa mbali sana. Labda hicho kibando cha kili walichokiongezea kinasogea kwa mbali saana.
Nawakilisha!
Mkuu that's true, na kwa kenya kuna stesheni maalum kipindi cha bunge, nadhan inaitwa Zuku Bunge kama sijakosea. Uncut and uncensored watu wanawaona wawakilishi wao.Mkuu tindikalikali, kama alivyoainisha mkuu, ch10 na tbc1 ndo zipo zuku, ila star times wana tbc1, tbc2, ch10, na sibukaBy the way bundle waliyoongeza ni steshen 5 tu! Star plus ya India, Stargold (kwa lugha ya kihindi tu.) True movies, Fox ent. Na Viasat Explorer/Crime (documentaries)Kwa upande wa cable, nlijaribu ku-inquire Milan Cable hapa a-town wakaniambia nilipie 150,000 kwa ajili ya nguzo, hapo bado decoder ambayo wanaanzisha sasahivi, nikablow.Anyway both Zuku na Startimes hawana Russia Today, inasikitisha!
 
Last edited by a moderator:
Kuna baadhi ya mikoa hapa TZ cable imegoma kabisaaa! Kila watu wakijaribu kuweka cable zinashindwa. Kuna mmoja aliweka cable akawa anarusha DSTV (S3) wakamkamata wakafunguliwa mashitaka na kufilisiwa. Wenzake wakaogopa wakaondoa SuperSport na hivyo zikawa hazivutii tena

Ukiweka DSTV lazima wakukamate kama upo makao makuu ya mkoa si unajua wana ma-agent wao, kwa lake zone especially Mwanza technolojia ya cable wapo juu na wanajitahidi kuweka mzigo mzito zaidi ya channel 70 local channel zote, nchi jirani zote na international channel zote na za movie ya kizungu na kiafrica pamoja na za soka ambazo wanazichukulia uarabuni (kuna ambazo zinatangazwa kiarabu na kiingereza). Nje ya makao makuu ya wilaya DSTV kama kawa si unajua nao wamekalili hawataki kushusha bei
 
sasa hapa najiuliza, is cable going to die after migrating to digital broadcasting? Kwa mfano atown kuna Milan Cable company. Wao saivi wameanza kutoa vingamuzi, kwa hiyo baada ya mitambo ya analog kuzimwa, no access kwa ambao watakuwa hawajanunua decoders, eventhough you will still need their cable to your decoder (kwa mujibu wao)
 
Cable itaendelea mdai usihofu, kinachofanyika wenye cable watakuwa na facilities za kupokea matangazo kwa njia ya digital toka wadau mbalimbali alafu wao wanasambaza kwa wananchi kupitia huduma ya cable kama kawaida na hata kuna baadhi ya wadau kama bwana Diallo aliwaomba watu wa cable wafanye kazi kwa karibu sana pindi king'amuzi chao na ITV kitakapoanza kwa kuwa coverage ya king'amuzi si kubwa itakuwa everywhere kutokana na gharama hivyo wakawaomba watu wa cable waangalie namna ya kushirikiana ili kuweza kusaidia kusambaza huduma hii hasa katika maeneo ambayo huduma itakuwa bado haijafika
 
Wakuu, there is great news undisclosed to the public, (as far as I know) mida mida nimetoka kuongea na customer carewa ZUKU na kumuuliza kwa bahati nzuri kama huduma ya triple play itakuja bongo. Akaniambia ya kuwa ngoma inakuja this december. Nilistuka lakini ilikuwa kwa furaha!!

Mimi: Kwa hiyo ikianza tutakuwa na haja ya kubadili system tuliyonayo (ving'amuzi)?
Customer care: Hapana, ni hizo hizo.

kwa mantiki hii muda si mrefu competitor mpya wa internet atakuwa bongo, swali ni je kama ataingia na gharama ikawa ikawa nafuu wewe utazifanyia nini unlimited 1MB/s au 8MB/s, leave alone 20MB/s ambazo najua hutazihitaji, eti mzee kushusha vitu a.k.a shem leh :wink:, MziziMkavu, King Kong III, nachojua chief-mkwawa ataupdate firmware za nokia zake zote, teh teh teh. na hapo najua ndetichia ataachana na hivi vimodem, labda akiwa anaenda field.

So, hopefully hoping things become.
 
Last edited by a moderator:
Local channels za Tz na mechi za ulaya zinaongezwa hv karbun mwz 10... source: Zuku Dealer 0713268836

Si mchezo, sasa it looks like Star Times anaachwa kimoja, unless naye aeleze ni local channels ngapi ataprovide na kuanzia lini. By the way Star Times yuko ahead na huduma yake ya TV built in king'amuzi aka (King'amuzi ready TV) Na pia kwa matangazo yake analeta mobile TV, hapa atapiga bao, hasahasa kwa watu walio mobile and remote. sijajua tu ukaaji wa chaji ukoje.[h=1]
1_268814.jpg
1_263060.jpg
[/h]
Decoder built-in
Analog and digital signals
Wild range voltage adaptability
One Remote Control - Easy to Use
More digital channels than other LCD TV and CRT TV brands
Free replacement for One week
One Year Warranty
Life-long maintenance
USB Access (LCD)
PC Monitor (LCD)
CRT 21" TV: Tsh285,000
LCD 24" TV: Tsh544,000
LCD 32" TV: Tsh835,000

Anyways, nitawacheki kujua wanatuletea ofa gani soon.
 
Back
Top Bottom