Star TV na ITV kujitoa rasmi Startimes muda si mrefu!

Star TV na ITV kujitoa rasmi Startimes muda si mrefu!

Star tv wana kila sababu ya kufanya hivyo, ikiwa ni wamiliki, pia kama hajaridhika huyo star times, inabidi wafanye hivyo bila kuzuru sheria ya nchi na vifungu vingine,ikiwa star times haeleweki, na vyema sasa local chanels zote zijitoe ilitubako na anologia yetu ili hawa digital wajiandae kwa upya.
 
Kwa wateja wa Easy TV, Star Tv hawapo hewani kwa wiki tatu sasa, huenda nako wamejitoa
 
Haya majanga kwel maana zle.local channel zote zikimiliki dekoda zao binafc kama walivyo star tv na continental yao je watanzania tutanunua dekoda ngapi
 
Hizo habari ni uongo na uzushi wa vijiweni!

Sheria ya mawasiliano kupitia TCRA inazitamka ITV, TBC, STAR TV, CHANNEL 10 na EATV kama ni FTA yaani Free To Air channels na sio Pay TV.

Sheria inawataka wamiliki wote wa visimbuzi vyenye local license kuziweka kwenye list hizo channels bure bila walaji kulipia!

Wakuu endeleeni kuumiza macho kupitia visimbuzi vyenu!

Rudi ukanushe habari yako hii maana tayari star tv wameshajitoa...
 
mtalakamika sn lkn kwa tz hii hakuna kitakachofanyika!
Mi naona na Itv wafanye faster wajitoe...mpaka wachina warudi kwao
 
ninafarijika kujitoa na ni msimamo makini, nawaamini ni tv pekee nilioanza kuiona ktk internet siku nyingi, kwao kurusha channel yao na nyingine nyingi hawashindwi, kikubwa ni kwamba startv kupitia kontinental waakuwa na mapinduzi makubwa i believe so.

Nimechoshwa na sana na startime amabao unakaa na king'amuzi amabacho hakina tija

kuhusu cavoirage yao hawa walianza na setilite kurusha mawimbi angani wkt huo startime wakiwa ardhini wakisuasua

naamini watakuwa poa sana. kama ilivyo rfa
 
Yaani watu wakiongelea Startimes ndiyo nakumbuka king'amuzi changu kama kweli kitafaa tena! Manake nilikiweka pembeni mwezi mmoja tu baada ya kashkash za kuhamishiwa digitali kwa kishindo. Ndani ya huo mwezi hakikuwahi kuniridhisha mteja wake...
 
lakini mjue startimes inalindwa na tcra, that why hata mpige kelele vipi, silikali haitawasikiliza
 
Kwani nyie huko kwenu hakuna Cable operators mkazipata hizo chanels zote pamoja?
 
Hakika bora wajitoe kwa sababu Startime walikuwa wakifanya biashara kupitia TV za hapa nchini kwa king'amuzi chao. Hapo si mwisho TV zote isipokuwa TBC watajiondoa na TCRA watatakiwa kutoa suluhisho kuwa Startime wakishauza king'amuzi chao wasiendelee kufanya biashara yao ya kila mwezi a.k.a. Tsh 10,000/=

Startimes = Wizi mtupu!!!
 
sasa star tv tutaipata wapi sasa au warekodi vipindi watuuzie cd kama magazeti
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itatoa Taarifa na Tamko la Kidhibiti (Regulatory Order) saa saba mchana Kwa saa za Africa Mashariki.

Aidha hakuna ukweli kwamba ITV na Watoa huduma wengine Wa Maudhui wanakusudia kujitoa katika Platform ya Star Media Tanzania Limited.

Hivi sasa kikao kinaendelea Kati ya Mamlaka na Watoa Huduma hao wawil na Maamuzi ya TCRA yatatangazwa saa saba mchana mbele ya vyombo vya Habari Mawasiliano Towers.

Msemaji Wa Mamlaka
 
  • Thanks
Reactions: Izz
Ni vizuri kuuelewa mfumo mpya Wa Utangazaji, Sheria na Kanuni zake badala ya kutoa kauli ambazo sio za ukweli na zenye nia ya kupotosha umma. Free to Air Channel zote ni Must Carry Kwa Multplex Operator Wote, yaani Agape Associates, Basic Transmission na Star Media Tanzania Limited Kwa mujibu Wa Sheria ya EPOCA, 2010 na Kanuni zake za 2011 kama ilivyoainishwa.

Kwa taarifa na Maelezo zaidi soma Sheia hiyo na Kanuni zake katika website ya TCRA www.tcra.go.tz.
 
  • Thanks
Reactions: Izz
digtali wapi pale palikuwa pana kamchongo ka viongozi ndo maana huyo mzee povu lilikuwa linamtoka
 
tutaishitaki serikali kwa kutudanganya kama watoto wadogo
 
Sabayi, nami nimeona hicho unachokisema....au ndio sheria imepewa ufizi nini?

Hatutendewi haki sisi watazamaji, kama kuna mtu ameweza kupata sababu za Star TV kufanya hivyo aziweke hapa tuzichambue!

Nilikuwa nafikiri Local TVs zote lazima ziwepo kwenye kila king'amuzi sasa hapo kila TV itakuja na king'amuzi chake na itakuwa kwenye hicho king'amuzi tu ukitaka kuona local channels zote uwe na ving'amuzi vyote this is very unfair
 
Hii nchi iz noman's land kwakweli,,kila mtu anaamua anavyojiskia hakuna cha kufuata sheria na hakuna wakuwahoji!! Maajabu hayaishi nchini Tanganyika..
hii nchi imekuwa kama nyumba ya urithi yaani warithi wenyewe wote akili zao mbovu......
 
Back
Top Bottom