Star TV na ITV kujitoa rasmi Startimes muda si mrefu!

Star TV na ITV kujitoa rasmi Startimes muda si mrefu!

Si walituambia kuwa ving'amuzi vyote vitakua vinaonyesha 5 local channels bure including itv, star tv, tbc 1,chanel 5 na channel 10?
UBABAISHAJI WA Hawa wa-china.... naunga mkono TV zote zijitoe wabaki na TBC pekee....!!!!! Wametuchosha na scratches zao....
 
Wadau kuhamia digital kwa haraka hivi ilikua shinikizo toka kwa baadhi ya wadau wa mawasiliano kwani wanazihitaji hizo frequency hususan kwa ajili ya LTE technology. Baada ya kurelease baadhi ya hizo frequency tumepewa baadhi kwaajili ya kutest hii teknolojia ya LTE . kwasasa inajaribiwa yenye kasi kati ya 40-50 mbps(kumbuka hii teknolojia ni mzao mpya baada ya ile 3G tuliozoea)
Nawakilisha.
 
Mkuu wewe ndio unaleta habari za vijiweni. Tayari tangazo la kujitoa kwa STAR TV linapita kwenye screen, wakisema

Ndugu mteja kutokana na matakwa ya STAR TV inatulazimu kuitoa katika orodha ya chaneli zetu. kwa maelezo zaidi piga STAR TV 0202503262. Samahani kwa usumbufu utakao jitokeza.

Jambo hili limekuja kipindi kizuri wakati watunga sheria wetu wakiwa kazini. Tuone basi kama hii ishu iaibuliwa bungeni.

Hili ndo tatizo la serikali ya Tanzania kuwa na ving'ang'anizi vya kijinga, tangu awali wadau walisema wapewe muda wa kutosha na matangazo yaendelee kwa analogy na digitali wakagoma, nadhani sasa umefika wakati sasa wananchi tufanyie kazi maamuzi yao yasokuwa na tija kwa wananchi....
 
Kama kuna suala lililofanywa kwa pupa bila maandaliz na kujal maslah mapana ya upatikanaj wa habar kwa jamii ya Tanzania, bas ni hil la kukimbilia kuzima mitambo ya analog.. ona hii text kutoka moja ya kingamuz cha walalahoi hapa tzania...'kutokana na matakwa ya Startv, tumeamua kuitoa kwenye channel zetu, kwa maelezo zaid wasiliana na star tv kwa namba 02825XXX.,,' naomba kuuliza, sasa inabid mtu uwe na vingamuz vingap ndan il uweze kuangalia habari walau kwa channel za nyumbani? vip ITV, Channel ten nao wajitoe? kila channel hapa tz na kingamuz chake, then? alaf mkiambiwa mtasema kuna mkono kutoka nje, n.k. mnashindwa kutunga sheria za kuwalazmisha watoa huduma kuweka channel za nyumbani hata kama nyingine zitalipiwa? mh. makamba tulikuaminia sana, au na wewe wamekuweka kwenye angleQ ?? fikiria sasa hiv nina vingamuz v2 cioni channel zote za hapa nchini.....vp huko mbele itakuwaje?? sa iv tunasubir mfunge line za cm!!!


Mkuu kifupi samaki wakubwa wanakula samaki wadogo,tutalalamika sana hakuna atakaetusikia kabisa ndio kwanza wenye nchi wanapandisha viatu juu ya meza.
 
Ikumbukwe kuwa Dr.Nkoma alitoka povu akisistiza mabadiliko ya kutoka analogia kwenda digitali ni lazima yawepo kwa nguvu zote hata kama kuna changamoto nyingi.Kiasi waendeshaji vyombo vya habari walilalamika kupata hasara ya matangazo ya biashara; sababu watazamaji wamepungua kiasi kikubwa baadaya kuhamia digitali.Dr.nkoma alizidi kuuthibitishia umma wa kitanzania kuwa Tvs tano zikiwemo start tv, ITV, EATV,channel ten na TBC1 zitaonekana kwenye ving'amuzi vyote bila kujali mmiliki wake.Kuanzia jana STAR TV wamejitoa kingamuzi cha startimes huku kiongozi mkuu akitoka puvu kuwa haitatoka .kwahiyo TCRA watujuze, je tuwe na ving'amuzi vingapi kupata Tv zote.Na ,je watanzania wote wanaweza kununua vingamuzi vyote kama sasa ilivyojitokeza kupata star tv mpaka uwe na kinga'muzi cha continental?
 
Bora sasa hata wao vinavyofanya kazi!
Hapa kwangu na majiran zangu kama wa 3 hivi
kuna tatzo ambalo limetupata
ukiwasha tu ki decoder cha *times kinaanza ku update mara
unable to download dnt shutdown
kitaanza kuonyesha picha ikitokea tu! Kuna bango linatokea
Flash update baada ya hapa linazima na kujiwasha toka jana hali ndo hii
kuna jamaa kanipgia simu na kwake hali hiyohyo!!!
 
Watanzania tumekuwa wapole sana, tunaendeshwa kama maroboti. Sijui kama watu wameumia kama nilivyoumia mimi. Ila ukweli ni kwamba Tanzania ni nchi ya ajabu sana, tukisema kuwa wanatukomoa watanzania kwa maslahi yao binafsi tutakuwa tumekosea? Tunahitaji mtu wa kututetea katika hili, wako wapi wamiliki wa vyombo vya habari? wako wapi wanaharakati wa haki za binadamu, wakati haki ya kupata habari inavunjwa? Kwanini tusidai haki hii kwa lazima mbele ya watawala?


mdau naona jinsi ulivyoguswa, je haki hiyo inalindwa na sheria gani thabiti inayotekelezeka au bora sheria?TCRA ipo kisiasa sababu jiulize startimes kuondolewa kodi huku waingiza vingamuzi wengine hawapewi , hujiulizi hilo?je kama kuna sheria kivipi mtazamaji abebeshwe kuwa na mzigo wa kununua ving'amuzi cha kiala kitua cha Tv?Dr.Nkoma yupo kwa masilahi ya ccm na mafisadi wengine na si kulinda watanzania.hata hao wanaharakati mbona wamesema sana, lakini akaibuka profesa makame Mbalawa kwa nadharia za kiccm kulaani wanaharakati wanapotosha?mdau nchi hii hakuna sheria nzuri itatungwa na kutekelezeka kwa bunge imeafikiwa , "NDIYOO" hata kinachoafikiwa ni pumba.jiulize mafao ya kujitoa, sheria iliyotungwa ya mtu kupata mafao mpaka afikishe miaka 55, je hilo linawezekana?je wabunge waliopitisha walikuwa vichaa ilipoulizwa imeafikiwa wakakubali NDIYOOO.INAKERA SANA ni nchi ya ajabu waziri kama KAWAMBWA KUTETEA WATOTO WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA AKISIFIA WAMEFANIKIWA KUANDISHA WATOTO WENGI huku akiungwa mkono wa wabunge wengi wa CCM.

 
Hata mimi nawapongeza sana Star Tv Kujitoa kwao kumesaidia sana habari zao za kichama zaidi zisiwafikie watz wenye visimbuzi vya startimes ambazo zinapotosha
 
Wapi TCRA? au ndio tenda zao jamani? mbona tunaumizana na viongozi wasio na akili
 
jamani mimi nimenunua satellite dish langu taratibu na enjoy maisha katika mwanga bora. channels za kutosha na redio juu.
Star times kwa heri hahahahaa
 
Wajitoe na ITV ili nipate sabubu ya ku2pa kisimbuzi changu cha startimes
 
Ze comed ya serikali dhaifu inaendekea, mmewanyima wananchi kuangalia news kwa hofu ya cdm! MPAKA 2015 MTAONA MENGI!
 
Dira YA DUNIA YA BBC MKUU NI TAMU SANA!
Statv nawapata kupitia dishi. Hawana vipindi vya mana, ukiangalia taarifa yao ya habari hawana mvuto kabisa, nadhani wadau hamtapungukiwa sana kama hawa jamaa watajitoa!
 
Ha ha ha ha.waweke supersport zote ndio ntajshulisha nao.wez tu!!!
 
NARUDIA TENA MPAKA 2015 MTAONA MENGI SANA CCM INAJIPANGA KUHAKIKISHA WANANCHI WENGI HAWAPATI HABARI ZA CHADEMA! Hiyo ni siri iliyovuja toka ktk njama zao.
Hawa TBC1 hawataki wenye madishi ft 6 ambao ndo wengi TZ wasiangalie bunge.Hiyo ni kwa mtazamo wangu.
 
lakini cha kushangaza kwenye hili swala kuna baadhi ya ving;amuzi hasa hivi vipy vya star times startv inaonekana na huku lile tangazo la kujitoa likipita. lakini kwa vile vya mwanzo kabisa walisitisha toka jana na wakaandika ni kutokana na matakwa ya star tv?
Lakini TCRA si walisema star tv ni moja ya free channel? kwa nini wajitoe star times wakati hata hawlipi?
hapa kuna haja ya TCRA kutoa ufafanuzi kwenye hili isije ikawa startv wana lazimisha watu kununua ving'amuzi vyao huku watu wana humia.
 
Mkuu ni professor Nkoma, mkuu ni shinikizo toka ccm, siku wakiamua wanazima utawafanyaje sasa! Hii nchi ni mbaya
Ikumbukwe kuwa Dr.Nkoma alitoka povu akisistiza mabadiliko ya kutoka analogia kwenda digitali ni lazima yawepo kwa nguvu zote hata kama kuna changamoto nyingi.Kiasi waendeshaji vyombo vya habari walilalamika kupata hasara ya matangazo ya biashara; sababu watazamaji wamepungua kiasi kikubwa baadaya kuhamia digitali.Dr.nkoma alizidi kuuthibitishia umma wa kitanzania kuwa Tvs tano zikiwemo start tv, ITV, EATV,channel ten na TBC1 zitaonekana kwenye ving'amuzi vyote bila kujali mmiliki wake.Kuanzia jana STAR TV wamejitoa kingamuzi cha startimes huku kiongozi mkuu akitoka puvu kuwa haitatoka .kwahiyo TCRA watujuze, je tuwe na ving'amuzi vingapi kupata Tv zote.Na ,je watanzania wote wanaweza kununua vingamuzi vyote kama sasa ilivyojitokeza kupata star tv mpaka uwe na kinga'muzi cha continental?
 
Majanga...
HII NCHI SIKU HIZI TUNAELEKEA KUNYIMWA HAKI YA KUPATA HABARI..HASA KTK KIPINDI HICHI CHA KUELEKEA KWENYE UCHAGUZI...
 
Jaman nchi yetu haina sheria, au sheria zetu ni mbovu? Kama ndivyo jaji mkuu wa nn kwa nn 2naish bila kuheshimu sheria, 2naishi kama Yatima ambaye ni chokoraa inauma sana.
 
Back
Top Bottom