Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi
Wale wenye nafasi, fuatilieni Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho kiko Live on Star TV. Kipindi cha leo, Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, Anazungumzia Wajibu wa Vyombo Vya Habari Kwenye Kuripoti Janga la Ugonjwa wa Corona.

Kipindi kinaongozwa na Nguli Dotto Emmanuel Bulendo kutokea Mwanza, Dr. Hassan Abbas atazungumza kutokea Dodoma, na kwa upande wa Dar es Salaam, nitakuwepo mimi.

Kipindi hiki ni interactive, wana jf wenye hoja muhimu za kumuuliza Dr. Abbas, unaoweza kuuliza humu na mimi nikamuuliza.

Karibuni sana.
Paskali
Up Date.
Awamu ya pili ya Kipindi hiki kitakuwa live kesho asubuhi, hivyo maswali ambayo hayakujibiwa last week, nimeya foward kwa Dr. Abbas yatajibiwa kesho.
Karibu.
Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV. - JamiiForums
P

Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
  1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
  2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
  3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
  4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
  5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
  6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
  7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
  8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
  9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
  10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
  11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
  12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
  13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
 
Asante kwa Taarifa,

Naomba umuulize mpaka sasa serikali inauwezo wa kupima watu wangapi kwa siku na mpaka jana wapimwa watu wangapi nchi nzima.?


Hao wanaoumwa familia zao zimefuatiliwa kujua kama hawajaambukizwa.?

Inaonekana wanaotoka nje wengi wanatoroka kwenye karantini kwa ushiriki wa karibu na polisi, na wengine hawapiti kabisa.

Sababu haiwezekeni mtu ametoka nje na passport yake inashilikiwa jeshi la polisi aweze kutoka kirahisi.?
 
Je ni kweli bado tuna visa 20 tuu au tunasubiri ifike Jumatatu ndio tutangaze?

Na serikali inawachukulia hatua gani watu waliokiuka maelekezo ya waziri mkuu juu ya utoaji wa habari za corona akiwemo RC makonda?

Serikali haioni umuhimu wakuwa ma account rasim ya serikali humu jf ili kuunga mkono product za nchi yetu?
 
Mkuu Kaka Mkubwa Wakudadavuwa, kiukweli Dr. Abbas yuko vizuri, baada ya Dr, Waziri wa Habari, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe pia ataalikwa na kisha Naibu Waziri, Mhe. Juliana Shonza pia wataalikwa.
P
1.Muulize ni bajeti kiasi gani serikali imetenga kukabiliana na hili janga la covid-19?
2.Ni hatua zipi mahususi serikali inapanga kuchukua endapo maambukizo ya hili janga la covid-19 yataendelea kwa kasi?
3.Iwapo serikali itaweka zuio la kutotoka ndani tuna chakula cha kutosha kulisha wa Tanzania wote kwa mwezi mmoja?
 
Asante kwa Taarifa,

Naomba umuulize mpaka sasa serikali inauwezo wa kupima watu wangapi kwa siku na mpaka jana wapimwa watu wangapi nchi nzima.?


Hao wanaoumwa familia zao zimefuatiliwa kujua kama hawajaambukizwa.?

Inaonekana wanaotoka nje wengi wanatoroka kwenye karantini kwa ushiriki wa karibu na polisi, na wengine hawapiti kabisa.

Sababu haiwezekeni mtu ametoka nje na passport yake inashilikiwa jeshi la polisi aweze kutoka kirahisi.?
Asante mkuu...nawafuatilia live ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, ni hatua gani zimechukuliwa na serikali juu ya baadhi ya maafisa elimu kuwalazimisha walimu waripoti shuleni kila siku wakati serikali imezifunga shule zote ili kuzuia kutokusambaa kwa Corona?
 
Mm napenda kumuuliza; kwa nn baadhi ya wanahabari wakiriport ukosefu wa elimu kwa wananchi kuhusu COVID19 maeneo kadhaa ya nchi wanakamatwa na viongozi wa serikali wa maeneo hayo?
 
Mkuu Kaka Mkubwa Wakudadavuwa, kiukweli Dr. Abbas yuko vizuri, baada ya Dr, Waziri wa Habari, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe pia ataalikwa na kisha Naibu Waziri, Mhe. Juliana Shonza pia wataalikwa.
P

Huyo wa mwisho kwenye hiyo list ndio ilikuwa lengo lako, ndio maana umemsifia hapo studio. Paskali una tatizo na rangi nyeupe hivyo unajiwekea mazingira vizuri. Anyway, ngoja tumuone hiyo msemaji mkuu wa serikali kama ana jipya, maana naye ana tabia ya kuongea kwa mikwara ile mbaya.
 
Huu ukaribu wa Wakudadavuwa na Pascal Mayalla siku hizi unatia mashaka hasa ukizingatia kabila LA Pascal na allergy yao na rangi ya chungwa.
Kuna msemo wa hawa vijana wa mjini eti 'ukiona manyoya ujue ameliwa' unanichanganya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh...!. Wakudadavua ni mkaka, tena ni mkubwa kwangu, ndio maana namuita Kaka Mkubwa Wakudadavua. Tena kwenye jibu langu kwa kwenye post ya Kaka Mkubwa Wakudadavuwa, akimsifia Dr. Abbas, sio umeona nimemweza kuwa sitaishia kwa Dr. Abbas pekee, kuna siku tutamwalika Waziri wa Habari Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri, mwana jf mwenzetu, Mhe. Juliana Shonza.

P
 
Back
Top Bottom