Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona

Waziri wa habari atahatibu kabisa yule-..hajuagi chochote za ya kujiinua mabega na kujimwambafai na degree 4 zisizo na impact yoyote kwenye jamii.

...ila huyu Msemaji wa serikali nimemkubali ,.yuko calm na anaongea hoja/logic bila mbwembwe.
Mkuu Kaka Mkubwa Wakudadavuwa, kiukweli Dr. Abbas yuko vizuri, baada ya Dr, Waziri wa Habari, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe pia ataalikwa na kisha Naibu Waziri, Mhe. Juliana Shonza pia wataalikwa.
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo Mayalla unataka kusema Kuna makabila (wasukuma) kwao mafua sio ugongwa ndio maana Magufuli akaenda kulala kwenye majabali sio?
Ndio maana yake. Mwanza, Shinyanga, Simiyu,
mtu ukisema unaumwa mafua, watakushangaa!, ndio maana watu mna panic bure tuu, majitu yenye ma confidence wako calm, relaxed and just busking sun kwenye majabali on Monday. Hata kale kaugonjwa, Wasukuma hakatuhusu japo ni wagonjwa sana wa kule... lakini waliotuletea ni wale jirani zetu wale wanaopenda ule mchezo wa jina la kile kijiji cha "siku ya gulioni....
P
 
Paskali kwanini Tanzania hakuna mwakilishi wa CNN?Hii nafasi ilikuwa inakufaa sana wewe,fanya mpango uwasiliane nao uwe Mwakilishi wa CNN Tanzania
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante Mkuu Alex Fredrick, CNN ni shirika la kibeberu, hivyo Tanzania inaonekana kama nchi ya kijamaa, hivyo wako Kenya na Uganda.
Ni kweli hata mimi niliitamani hiyo kazi, ila kwa bahati mbaya sana, nilisoma primari enzi za UPE, hivyo ngeli yangu kwa levels za CNN ingegomba.

Japo kwa sasa kupitia jf, ngeli imeipruvu pruvu kidogo, lakini umri ndio hivyo tena, nimeishakata 50 naitafuta 60!.
P
 
Asante kwa Taarifa,

Naomba umuulize mpaka sasa serikali inauwezo wa kupima watu wangapi kwa siku na mpaka jana wapimwa watu wangapi nchi nzima.?


Hao wanaoumwa familia zao zimefuatiliwa kujua kama hawajaambukizwa.?

Inaonekana wanaotoka nje wengi wanatoroka kwenye karantini kwa ushiriki wa karibu na polisi, na wengine hawapiti kabisa.

Sababu haiwezekeni mtu ametoka nje na passport yake inashilikiwa jeshi la polisi aweze kutoka kirahisi.?
Asante kwa maswali haya, nimemfikishia, utajibiwa next week during the same program.
P
 
Muulize, serikali inaonekana kuchukulia poa ugonjwa huu, je inaamini ugonjwa hautuathiri kivile kwa kuwa Kuna tetesi ulikuwepo tangu disemba mwaka Jana na watu wanapona wenyewe?
Hili nimemuuliza, Dr. Abbas akajibu sii kweli kuwa serikali inachukulia poa, serikali iko very serious ndio maana imefunga shule zote na vyuo vyote.

Dr. Abbas amesisitiza hatuwezi kukurupuka kufunga mipaka kwa kuiga.
Kila nchi inadeal na Corona kwa namna yake inayofit mazingira yake.
P
 
Asante kwa maswali haya, nimemfikishia, utajibiwa next week during the same program.
P
Mwambie apunguze vitisho na lugha ya kidikteta, unapowaambia wananchi wakivunja sheria ama taratibu watakumbana na Mkono wa Chuma hiyo siyo lugha nzuri kwa Taifa linalojinasibu kuheshimu Katiba na taratibu za nchi.

Katika tafsiri ya kawaida Mkono wa Chuma ni bunduki...
 
Wanabodi
Wale wenye nafasi, fuatilieni Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho kiko Live on Star TV. Kipindi cha leo, Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, Anazungumzia Wajibu wa Vyombo Vya Habari Kwenye Kuripoti Janga la Ugonjwa wa Corona.

Kipindi kinaongozwa na Nguli Dotto Emmanuel Bulendo kutokea Mwanza, Dr. Hassan Abbas atazungumza kutokea Dodoma, na kwa upande wa Dar es Salaam, nitakuwepo mimi.

Kipindi hiki ni interactive, wana jf wenye hoja muhimu za kumuuliza Dr. Abbas, unaoweza kuuliza humu na mimi nikamuuliza.

Karibuni sana.
Paskali
Kule kustaafu vipi kaka..!?
 
Je...Serikali inaliona hili janga kama linachafua hali ya kisiasa Tanzania?
Je...Inawezekana kusitisha na kusogeza mbele kwa hata kwa miezi kadhaa Uchaguzi mkuu?
 
Kule kustaafu vipi kaka..!?
Ilikuwa nistaafu baada ya kumpata Polepole kabla ya saa 4:00 asubuhi. Muda huo ulipita, hivyo bado nipo nipo huku nikiendelea kumsaka Polepole, nikimpata ananiandikisha CCM, ananipa kadi yangu, kisha humu tunaagana.
P
 
Mwambie apunguze vitisho na lugha ya kidikteta, unapowaambia wananchi wakivunja sheria ama taratibu watakumbana na Mkono wa Chuma hiyo siyo lugha nzuri kwa Taifa linalojinasibu kuheshimu Katiba na taratibu za nchi.

Katika tafsiri ya kawaida Mkono wa Chuma ni bunduki...
Tunaendelea nae next week, nitamfikishia, ila duh...!, kumbe mkono wa chuma ndio zile pyu pyu!, kwa hivyo usikute hata yuke naniihii waliye mpyu pyu kule nanihii wanaweza kuwa ni hawa hawa?!.
P
 
Mwambie apunguze vitisho na lugha ya kidikteta, unapowaambia wananchi wakivunja sheria ama taratibu watakumbana na Mkono wa Chuma hiyo siyo lugha nzuri kwa Taifa linalojinasibu kuheshimu Katiba na taratibu za nchi.

Katika tafsiri ya kawaida Mkono wa Chuma ni bunduki...
Mkono wa chuma vs Corona!
 
Wanabodi
Wale wenye nafasi, fuatilieni Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho kiko Live on Star TV. Kipindi cha leo, Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, Anazungumzia Wajibu wa Vyombo Vya Habari Kwenye Kuripoti Janga la Ugonjwa wa Corona.

Kipindi kinaongozwa na Nguli Dotto Emmanuel Bulendo kutokea Mwanza, Dr. Hassan Abbas atazungumza kutokea Dodoma, na kwa upande wa Dar es Salaam, nitakuwepo mimi.

Kipindi hiki ni interactive, wana jf wenye hoja muhimu za kumuuliza Dr. Abbas, unaoweza kuuliza humu na mimi nikamuuliza.

Karibuni sana.
Paskali
Ni wananchi wangapi wanaomiliki tv Tanzania.Hii ni njia sahihi ya kuwafikishia ujumbe jamii ya watanzania?Kwanza huyo Dr mm sijawahi sikia aliongea huko awali au naye ni Kiki za Corona?maphd wa tz ni was ajabu ni Bora ukamsikiliza std seven utamwelewa.wafuatilieni kauli zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh...!. Wakudadavua ni mkaka, tena ni mkubwa kwangu, ndio maana namuita Kaka Mkubwa Wakudadavua. Tena kwenye jibu langu kwa kwenye post ya Kaka Mkubwa Wakudadavuwa, akimsifia Dr. Abbas, sio umeona nimemweza kuwa sitaishia kwa Dr. Abbas pekee, kuna siku tutamwalika Waziri wa Habari Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri, mwana jf mwenzetu, Mhe. Juliana Shonza.

P
Juliana anajua nini? Yeye anaongea kama nani??!

Kuongea kwenye TV leo mbona wamechelewa sana
Wachukue hatua sasa sio kujifanyia kampeni kimtindo
Waondoe uvyama au kuabudu na kusujudu mtu badala yake WAOKOE ROHO ZA WATANZANIA

Lockdown itaokoa roho za WaTz Tumieni JWTZ kuweka mambo sawa mijini zaidi Polisi hapana
COVID-19 is for real
 
  1. Ni wananchi wangapi wanaomiliki tv Tanzania.
  2. Hii ni njia sahihi ya kuwafikishia ujumbe jamii ya watanzania?
  3. Kwanza huyo Dr mm sijawahi sikia aliongea huko awali au naye ni Kiki za Corona?
  4. maphd wa tz ni was ajabu ni Bora ukamsikiliza std seven utamwelewa.wafuatilieni kauli zao

  1. Kwa hiyo Mkuu Katitu, kwa vile sio Watanzania wote wanaomiliki TV, hivyo tusitumie TV kufikisha ujumbe kwasababu wengine kama Katitu hawataona?!.
  2. Ujumbe unafikishwa kwa TV zote, Redio Zote, Magazeti yote, Mitandao yote ya kijamii. Kwenye mbao zote za matangazo kuanzia ofisi ya Serikali za mitaa, jee bado kuna ambaye hata sikia?.
  3. Kama wewe ni Mtanzania, na una TV, Redio, Gazeti au mitandao ya kijamii ikiwemo JF, kama hujawahi kumsikia Dr. Abbas, then wewe mwenzetu aendelea kusoma yale magazeti yetu ya makorokocho, endelea kutembelea jukwaa la MMU na ile mitandao ya ubuyu.
  4. Kumbe mwenzetu unawaelewa zaidi wale Std Seven kuliko hawa ma Ph.D wetu, then endelea kuwasikiliza, maana kusikiliza kitu usichoelewa ni kupoteza muda, karibu Watoto wetu, Ubongo Kids na katuni za kumwaga. Sisi wa kuwasikiliza wataalamu wetu, tutaendelea nao.
Asante kuchangia uzi huu Katitu, MMU hata mimi pia utanikuta.
P
 
Back
Top Bottom