terabojo
JF-Expert Member
- Aug 3, 2010
- 215
- 45
Wana jf mtakuwa ama mumeona au hata kununua vingamuzi (decoder) na antena za kampuni ya star times ambayo ni mshiriki wa tbc katika mambo ya tv. Jirani yangu alinunua decoder hiyo kwa shs. 79,000.= na akaelekezwa namna ya kufunga na kuanza kutumia/kupata picha. Kifupi ilimchukua siku 9 (baada ya kutemebelea duka lao mara 4 pale msimbazi road karibu na polisi station) ndipo alipoanza kuona picha. Kifupi wale pale wanakuuzia na nadhani hawapeleki taarifa huko tbc mwenge ambako naambiwa ndo hasa wana "activate" decoder ile. Swali: Kwa nini wanakuwa wazembe kiasi hicho. Kwa nini wanamuibia mteja kwa kutomuwezesha kuona tv kwa siku 9? Kibaya zaidi ukipiga nmaba za customer care hakuna hata moja inayopokelewa na unapojaribu kuongeza airtime pia simu zao hazifanyi kazi. Jamani wachina na tbc ya mheshimiwa sana wa wizara ya habari...