DSTV na Utapeli wa Ofa

muonamambo

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
875
545
#DSTV_na_Utapeli_wa_ofa_Nashauri_Muache.

Tarehe 10 July 2023, Nipo ndani ya Kikao muhimu na wadau wa serikali tukijadili issues muhimu kwa mstakabali wa nchi yetu.

Mara Simu yangu inaita na ni namba ngeni, Nawaomba hudhuru wana kikao naomba nipokee simu maana ni namba ngeni, wananikubalia.

Napokea Simu , Sauti ya kike inajitambulisha kuwa anapiga simu toka @DSTV,namtambulisha kuwa naitwa fulani lakini nipo kwenye kikao naomba unipigie baadaye, anasisitiza kuna ofa na kuwa angependa nisikilize nisije kukosa ofa hiyo.

Natoka kwenye kikao kidogo kusogea pembeni kusikiliza ofa hiyo , Dada anatiririka.

Ananifahamisha kuwa kama nilipokea simu yeyote week hiyo inayohusu ofa namwambia yes lakini sikutulia maanani.

Anasema sasa siku hiyo saa sita usiku ni dead line. Ofa inataka mteja kulipia 50% ya kifurushi chako na DSTV wataongeza nusu.

Anasisitiza kuwa ni vyema nifanye malipo kabla ya saa 6 Usiku na kwamba nikifanya malipo nitazidishiwa ndani ya masaa 24.

Tunamaliza mazungumzo narudi kuendelea na mkutano.

Baada ya pilika pilika nyingi za siku najikuta nyumbani saa 2 :30 Usiku .. Nakumbuka ile ofa.

Kwa kawaida mimi si mpenzi wa vya bure au ofa hata ku bet. lakini nasema ngoja leo nijaribu hii ofa kama Kweli DSTV wameamua kujali wateja wao.

Nachukua simu nalipia kifurushi changu cha compact kwa kuweka 50% ( 30,000Tsh).

Siku mbili zikapita hakuna huduma kwenye TV yangu . napiga simu huduma kwa wateja wa DSTV anapokea mdada mmoja , namfahamisha kuhusu zoezi zima hilo ananipa pole na ku ahidi kurejesha huduma hiyo kwanza aongee na kitengo cha ofa kisha atanipigia ..Kimya hakuna aliyenipigia.

Siku mbili zinapita napiga tena DSTV anapokea mkaka. Baada ya utambulisho namueleza tena issue yangu ananipa pole na kuniambia ni kweli anaona muamala na umeandikwa ofa lakini anashangaa kwa nini sijapewa huduma mpaka sasa. anatoa ahadi ya kulishughulikia na kuniomba nisikae mbali na simu .

Nusu saa inapita hakuna mrejesho napiga tena huduma kwa wateja anapokea mdada naomba kuongea na yule mkaka. anaomba nimweleza tu shida yangu maana itakuwa vigumu kumpata mkaka huyo. najieleza tena huku nasikitika.

Naye ana ahidi kurudi kwangu kweli baada ya muda mfupi anarudi kwangu .

Dada wa Dstv. “ Kaka samahani kwa kuchelewa kurudi kwako, naomba kujua kuwa je una Dstv zaidi ya moja ? “

Namjibu ” Yes lakini kwa sasa natumia moja ile nyingine sijaotumia muda mrefu”

Dada wa DSTV.” Pole sana kaka , Ofa uliotangaziwa ni ya hiyo Decoder nyingine inayoishia na namba 9 na sio hii inayoishia na namba 5”
Namjibu” Mbona sasa mtoa huduma wenu aliyetutangazia ofa hakusema hivyo, hakusema ni decoder ipi inatumika kwenye ofa? “

Dada wa DStv “ Pole kaka sijui kwa nini hakukufahamisha hivyo labda hakujua kuwa una Decoder mbili”

Namjibu” Wewe umejiaje?”

Dada wa Dstv” Nikufungua kwenye account yako naziona decoder zote tatu”

Namuuliza” Sasa yeye alishindwa kuziona?”

Kimya …

Nauliza Tena “ Dada imekuaje yeye hakuziona “

Dada wa Dsv” Ahsante kwa kuwa mteja wetu na nkuomba umalizie kulipia kifurushi ili kuendelea kupata huduma zetu “ akakata simu .

Nikabaki nimeduwaaaaa….

Nikawa najiuliza maswali bila kupata majibu

1. Je ni kweli kuwa yule dada wa kwanza wa ofa alikosea ? na kama alikosea watoa huduma kwa wateja walikuwa na kigugumizi cha nini kunieleza haya tangi siku ya kwanza nilopopiga huduma kwa wateja?
2. Je ni mtindo wanaotumia DSTV kulaghai wateja ili walipie vifurishi vyao?

Sina kitu kingine cha kuiita hii zaidi ya kusema ni utapeli .. Naomba DStv muache Tabia hii….
 
Back
Top Bottom