FT: Tanzania 1-1 Zambia | AFCON 2024| Laurent Pokou Stadium | 21.01.2024

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
7,579
10,811
Match Day
20240121_000237.jpg


Leo Jumapili 21.01.2024.
Tanzania (Taifa Stars) Tunatupa karata yetu ya pili katika Mashindano haya ya AFCON 2024 kumenyana na Timu ya Taifa ya Zambia a.k.a Chipolopolo.

Zambia hawakupata mwanzo mzuri katika Mashindano haya walipokubaliana na Congo DR kwa sare ya 1-1 Jumatano.
King Kangwa alianzishia Chipolopolo kwa bao katika dakika ya 23, lakini mshambuliaji wa Brentford, Yoane Wissa, alirudisha bao hilo ndani ya ya dakika nne tu. Nakufanya mchezo huo kuisha kwa Sare.

Tanzania, kwa upande mwingine, tulichapwa vibaya na Morocco katika mchezo wetu wa kundi F, tukipoteza 3-0 mbele ya Morocco (Simba wa Atlas.)

Roman Saiss alifunga bao katika dakika ya 30 kuwapa Morocco mwanzo mzuri wa mashindano kabla ya Azzedine Ounahi na Youssef En-Nesyri kufunga mabao katika kipindi cha pili.

Tanzania sasa tumepoteza mechi tatu mfululizo Katika wigo wa Kimataifa, tukifungwa magoli saba na kushindwa kufunga tangu ushindi wa 1-0 dhidi ya Niger Mwezi June 18, 2023.

Kazi kubwa tunayo lakini hatuna haja yakukata tamaa.

HISTORIA YA TANZANIA VS ZAMBIA.
IDADI YA MICHEZO NI 32.
ZAMBIA WAMESHINDA MICHEZO 18
SARE NI Tisa(9).
TANZANIA IMESHINDA MICHEZO MITANO(5) tu.


Mara ya Mwisho Tanzania Kuishinda Zambia ilikuwa 21 Nov 2007 katika Mchezo wa Kirafiki. (Matokeo yalikuwa 1-0)

Mungu Ibariki TANZANIA.
Mungu Ibariki Taifa Stars.

KIKOSI CHA TANZANIA KINACHOANZA.
20240121_192322.jpg


KIKOSI CHA ZAMBIA KINACHOANZA
20240121_193610.jpg


Mpira Umeanza...
Tanzania ndio tumeanza ball hapa.

Dk 2'
Zambia wanapata free kick nje kidogo ya 18.
inapigwa inakataliwa hapa.

Dakika 5'
Taifa Stars wanapata kona yao ya kwanza.
Inapigwa haileti madhara.

Zambia wanaotea.

Dakika 8'
Taifa Stars wanapata free kick inapigwa inapotea.

Dakika 11'
Mpira unaendelea
Goooooooooooal.
Msuvaaaaaa anavunga goli zuri sana akipokea Assist mujarabu kabisa kutoka kwa Samatta.

DK 18'
Samatta anajaribu hapa inakuwa off target.
Game On..
Tanzania 1-0 Zambia.

DK 22'
Zambia wanapiga kona
inakataliwa na Samatta.

DK 23'
Msuva anachezewa rafu mbaya hapa..
mpira unaendelea.
Taifa stars wametulia sasa.
Tunafanya shambulizi linaokolewa na Zambia

DK 29'
Mpira unaendelea hapa.
Kwa kifupi mpira unachezwa kwataadhari sana.

DK 30'
Samatta alikuwa anaigarimu timu ya Taifa.
Zambia wanakosa goli la wazi kabisa. Hapa.

DK 33'
Taifa stars wanapata free kick nje kidogo ya 18.
Anapiga Shabalala.
Inakuwa goli kick.
Zambia (Musonda) amapata yellow kadi.

DK 38'
Game on...

DK 40'
Zambia wanapata Free kick
inaokolewa na Mwamyeto.

Wakati huo huo, Manula anafanyiwa Faulu hapa

DK 43'
Kabwe Jr wa Zambia anapata Yellow kadi ya Pili.
Analambwa Red Card
Anatoka.
Ni Dakika ya 44 sasa kipindi cha kwanza.

Lameck Banda anapigwa Yellow kadi hapa baada ya kumzonga zonga refa.

Dk 45'+2'
Kibu Denis anafanyiwa mazambi nje kidogo ya 18.
VAR check, Possibility ya Penalt.
No penalty, No Faulo.

HT.
Zambia 0-1 Tanzania.
20240121_205525.jpg

Tukutane kipindi cha pili.

Kipindi cha Pili Kimeanza.
Taifa Stars Substitute
Haji Mnoga Out.
Lusajo Mwaikenda Inn

Zambia pia wanafanya mabadiliko pia hapa.

DK 46'
Kibu D anapaisha mpira, alikuwa yeye na nyavu tu

DK 48'
Zambia wanapata Kona
Inaokolewa.

DK 50'
Feisal anachezewa Faulo na yukochini anaugulia maumivu.

DK 54'
Tanzania wanafanya shambulizi la kushtukiza kupitia kwa Shabalala

Mwaikenda anafanyiwa faulo mbaya.
Anaendelea na mpira.

DK 57'
Zambia wameanza kuingia mara kadhaa kwenye ulinzi wa Taifa stars.

DK 58'
Sub kwa Taifa Stars
Feisal Out
Moris Inn.
Mpira unaendelea.

DK 63'
Bakari Nondo amefanya mistake ambayo Manula anasaidia kuokoa mpira mkali, iliokuwa na madhara.
Anatolewa nje kwa ajili ya usaidizi zaidi.
Inaonekana kama alifanyiwa faulo.

DK 66'
Game On..
Kibu anafanyiwa faulo hapa.
Inapigwa free kick, yakizembe kidogo hapa. Taifa Stars wanapoteza mpira.

DK 69'
Taifa stars wanafanya Sub mbili.
Mudathir Inn
Charles Mm'ombwa Inn
Kibu D Out
Himid Mau Out...
Mpira unaendelea!!

DK 70'
Taifa Stars wanapata kona inapigwa haraka haraka haileti impact.
Taifa Stars inapoteza nafasi za wazi hapa...

DK 75'
Kennedy Musonda Inn
Chama C. Inn.
Sakala Out.
Kangwa Out...

DK 87'
Zambia wanapata kona hapa.
inapigwa Bakari anatoa inakuwa kona nyingine.
Inapigwa, inakuwa goli.

DK 88'
Zambia wanasawazisha.
Daka anawapa Zambia goli la kichwa akiunganisha mpira wa kona.

DK 90'
Additional time ni DK 7.
Game On...

DK 90+ 6'
Zambia wanapata Kona.
Inakataliwa hapa.

Full Time.

Zambia 1-1 Tanzania.
20240121_220711.jpg
 
Hivi hizi threads za michezo kuanzisha usiku wa manane ndio nini?

Nimemiss kipindi threads zinaanzishwa karibia na muda wa mechi, homa iko juu tunachangia kwa mihemuko & mchecheto.

Hizi za mapema hadi kufika muda wa mechi tumeshachoka!
 
Back
Top Bottom