St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Elimu ya siku hizi imekuwa mdebwedo sana! Ukitaka kujua hili waulize walimu wa vyuo na waajiri. Binafsi sio Mara moja nimewafanyia interview vijana kwenye mambo ya kazi na naishia kusikitika jinsi uelewa wao ulivyo wa mashaka.
Watoto wa sasa hivi wanaakili kuliko watoto wa zamani huo ndo ukweli
 
Hio shule inanunua mitihani na kufanya mwezi mmoja kabla ya mitihani ya taifa na huwa maswali yanarudiwa kwa msisitizo mkubwa Sana ......

Hao watoto wanaomaliza huko hawana uwezo kabisa wa kufaulu hivyo, never ever....

Hapa bongo ukishakuwa na pesa hakuna kinachoshindikana, paper za NECTA zinanunuliwa na watoto Wana solve mapema kabisa ...

Hio shule ada yake tu unaweza kula mwaka mzima ,kununua pepar wizaran kupitia kwa mamuruki ni kitu rahisi Sana .....mbaya zaidi wafanyakazi wengi wa serikali dawa yao ni pesa ,kwa million 20 anakuletea pepar la necta lotee mwezi mmoja kabla .....


Niamaini Mimi haya nayoyasema
Hivi ukiwa mwongo unapata faida gani?
 
Watanzania bhana, watoto wakifeli mnawaita vilaza, wakifaulu wamepewa mitihani. Sijui hata mnataka nini
 
Record yao haikuwa nzuri miaka ya tisini tu.
Ni mwaka mmoja tu 1997 ambao St. Francis walikuwa nje ya kumi bora tangu shule ianzishwe. Na mwaka huo ndiyo ilikuwa form four ya kwanza na hapo walikuwa wa 17 kitaifa.
IMG-20220113-WA0019.jpg
 
Millardayo alifunga safari mpaka shulen. Kajifunza mengi sana. Wametoa sababu zaidi ya kumi zinazowafanya wafanye vizuri
 
Maswali mepesi lakini mbona wanafunzi wengine kule Kazulamimba wanafeli? Hawa watoe strategies tujue wengine waige vipi. Inaniuma kuona karne hii wanafunzi wanashindwa kufaulu hata kidato cha nne. Kuna jamaa yangu alifeli form 2 nilisoma name shule moja ya ajabu ajabu uko. Juzi akanambia eti daktari alivyompima akamwambia anaumwa ugonjwa unaitwa "INFECTIONS", nikamuuliza mara mbili na akasisitiza sana.

Sasa taifa linakuwa na watu wa hivi hata kutumia mbolea shambani hawataweza, lishe kwa watoto hawawezi, uzalishaji wao kitaifa ni duni. Shule walienda kuishi, kuvaa sweta na kunywa uji. Elimu ya bongo hasa uswahilini uko ni ile wazazi wanawaambia watoto wao wakiwa wamefunga eti "mmetuchosha hebu shule zifunguliwe wazazi tupumzike". Hapo usitegemee maajabu ya kufaulu. Sasa hawa waliofaulu wangetoa strategies imekuwaje ingesaidia wengine
Nimekumbuka nilipatwa na maradhi ya ajabu mwaka jana,, nilikua nawashwa mwili mzima yaan nilikua najikuna balaa kahosptal fulan akanipima damu akasema eti una infections !!! Nikamuuuliza tatizo ni nn hasa maana nateseka? akasema takuandikia tu dawa uchukue hapo nje pharmacy utumie utapona.. nilivoskia sikia hivo nikamwambia haya alivonipa karatas hata pharmacy sikukwenda ..

Nikaenda hosptal ya kueleweka ya binafs nikaelezea wakanipeleka kwa daktar special wa magonjwa ya ngoz nikapimwa nikaelezewa kila kitu wakaniandikia sindano 5 nikachoma nilivomaliza sindano baada ya sku 2 nilipona kabisa..

Yule daktar wa mchongo wa mara ya kwanza alikua muhun tu.

Miaka ya nyuma niliumwa usiku nikazdiwa palivo kucha saa 11 tukaenda pale magomen hosptal kwanza hatukukuta daktar hiyo saa 11 nikalala kwenye mabench et tunasubir daktar!! Nikalala pale kweny bench mpk saa 1 asubui nesi mmoja akanichukua mpka chumba fulan akaniwekea drip nikalala pale akaja na sindano akanichoma ya tako ile sindano nilikaa zaid ya miez 6 naiskia tu maumivu yake na uvimbe hauishi,, mpaka leo najiuliza yule alikua muuguzi kweli au alikua mfanya usafi akajiongeza
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom