Nilisikitika kale kadada kufa vile alikuwa amemuahidi maisha mazuri mdogo wake,
Lakini nimeipenda character ya yule Mama mkorofi anayekataa kuitwa Mama anataka aitwe mtoto kwa kweli anastahili tuzo ameitendea haki sana ile character na alinifurahisha alivyodondoka na yule jamaa katili wakafa wote,
Main character historia yake ilikua inasisimua lakini nimesikitika Mama yake hakuweza kuona matunda ya mwanae na vile alivyoona pesa si kitu kama hana furaha akagoma kuchukua pesa alizoshinda,
Wakorea hua wana story nzuri sana nawapenda kwa hilo, natumaini Season 2 itakua bora zaidi.
PS: Mtu kuifananisha Squid Game na Money Heist ni uzuzu wa hali ya juu sababu ni story mbili tofautiii,
SG ifananishwe na SAW na kweli story zimefanana lakini SG naipa kongole zaidi sababu watu walienda kwenye Game wenyewe hawakulazimishwa.