Money Heist VS Squid Game

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
967
1,693
Nimebahatika kuziangalia hizi zote, kitu cha kwanza kabisa, hazifanani, ni muvi tofauti ila ukija kwenyr uandishi, huyu aliyeandika hii Squid Game, ameiandika kiuandishi kabisa.

Muvi A: Series ya Money Heist inaanza vizuri sana, inakufanya uvutike na kutamani kuiangalia zaidi lakini baadaye, udhaifu unaonekana waziwazi, muvi inaanza kukaa kitoto, kuna matukio ambayo ni very simple kutokea, mwandishi akiyaandika kirahisi sana.

Duniani, pesa hazilindwi sana kama karatasi za kutengenezea pesa. Ni bora uingie benki ya dunia uibe mabilioni ya dola lakini si karatasi za kutengenezea pesa, hizo zina ulinzi mkubwa mno kwani ukifanikiwa kuzipata, wewe ni bilionea. Lakini kwenye hii series, yaani watu wanaingia kirahisi sana, huo ni udhaifu wa kwanza, halafu wa pili, watu wanaanza kuingizia mapenzi humohumo.

Jaribu kufikiri tu, sehemu kama hiyo ambayo inatakiwa milango yako yote ya fahamu iwe wazi, kinatokea kitu kama hicho, kiuhalisia, hamna kitu kama hicho.

Tokyo alibahatika kuondoka, akatoka humo, kilichotokea baadaye, akarudi tenayaani very simple tu, ni kitu abacho hakiwezi kutokea hata kidogo.

Ukifuatilia yule mama aliyekuwa akifuatilia hilo suala, naye alikuwa na udhaifu mkubwa. Hafuatilii kama mfuatiliaji, anafuatilia kama muigizaji na ndiyo maana watu wanasema kama kazi ya kumfuatilia angepewa Mahon wa Prison Break, series ingeishia season ya kwanza tu.

Nimeangalia muvi nyingi za kipelelezi, ila sijamuona mtu anayefuatilia kesi kama yule mama, mwandishi amekuwa dhaifu sana upande huo, hakutaka kumpa nguvu, alimpa nguvu Profesa.

Tazama Prison Break, Scofield alikuwa na akili sana, naye Mahon alikuwa na akili mno, alipewa nguvu sana na mandishi na ndio maana wakisumbuana sana.

Kwa Rate, kule IMBD nimeweka 6/10.

Nakuja kuichambua na Squid Game.

Uandishi wa Squid Game nineupenda sana. Kabla ya kumpa character nguvu kwanza tuambie kwa nini anapewa hizo nguvu.

Hii series imezungumzia zaidi mtu masikini, mwenye madeni ambaye hawezi kuyalipa, ili kuyalipa, anakuwa tayari kufanya lolote lile kwa ajili ya pesa.

Watu wenye madeni wamechukuliwa na kuwekwa sehemu moja. Kila mtu mbali na madeni, ana matatizo binafsi, huyu mama yake mgonjwa, yule hivi na vile.

Hapo mtazamaji unaona kabisa huyu mtu anahitaji pesa. Michezo ambayo wameicheza, ni kweli inasumbua kichwa, mbele ya bastola, huku ukiwa unatetemeka, unaambiwa uufanye mtihani fulani.

Hii muvi imenikumbusha muvi nyingi kama Escape Room na Saw. Games walizocheza ni za utotoni, ila kwa kipindi hiki zimejaa hatari.

Vitu ambavyo vimeifanya series hii kupendwa ni namna michezo ilivyochezwa, ukatili uliofanyika na hata mwisho kugundua babu ndiye mratibu, ni kitu ambacho hakuna mtu yeyote aliyehisi hilo.

Dhima kubwa ya series hii ni kukuonyesha mtu mwenye matatizo ya pesa, yupo tayari kufanya lolote lile ilimradi kupata pesa hata kama litagharimu maisha yake.

Endapo hii series ingetoka mwaka 2008 ilivyoandikwa, isingevutia kama sasa hivi kwa kuwa bado hatukuwa na muvi za namna hii, ila kwa sasa ni lazima tuipende kwa kuwa tumeona vitu ambavyo tumeviona kwenye Escape Room, Saw na nyinginezo.

Kwa kule IMBD nimeipa Rate ya 7/10.
FB_IMG_1633557802833.jpg
 
Kwa kule IMBD nimeipa Rate ya 7/10.View attachment 1966185

Unajua sanaaa
 
Unajua sanaaa
Dah Squid Game nimelianza jana Money Heist ilikuwa bora pale mwanzo Professor alikuwa mchanganuaji kweli wa mambo lkn sasa imekuja kiovyoo sana je QUEEN OF THE SAUTH .Lakini Squid Game inanitia mashaka haya mambo yapo Duniani wale maiti wanakatwa viungo vyote muhimu baadae nafikiri wanawawachoma moto hakuna sijamaliza naendelea na burudani langu nilikua naangalia HOUSE OF CARDS nimeliacha kwanza ni siasa tu lkn kuna mauwaji ni kweli wana siasa kuua ni jambo la kawaida tu.
 
Hii movie ina series ngap mpaka sasa
 
Mkuu Sasa unababaika nini unaelewa maana ya movie!! Mi bora hata niangalie hiyo money heist kuliko baadhi ya bongo movie!.

Usishangae mbona hata ktk maisha halisi majambazi wakivamia wakikuta chakula kwako wanakula..🤣 Kama hujawahi sikia haya matukio jua bado unajifunza kuishi! Watu wanaenda kwa misheni ya kuiba lakini wanakutana na toto nzuri wanabaka!.. unashangaa watu kuanzisha mapenzi wakiwa wapenzi tena ktk kundi moja!.
Hii picha inamambo mengi sana ndani yake mengine ni saikolojia namaanisha Kuna watu mule wamecheza kama wanamatatizo ya kisaikolojia kutokana na kazi wanazozifanya za uhalifu kumbuka wale wote mpk wanakuja kupatikana na professor walikuwa ni wahalifu!.. sikatai Kuna makosa pia haiwezi kuwa perfect well.
Movie ni movie tu ndugu let's say Kama huyo mama kapewa hiyo misheni ya kuwakamata wezi wa fedha lakini mabosi wake pia ni wezi lakini kwa njia za kisiasa,kifisadi n.k we unashikishwa mtutu kulinda wezi wasiibe lakini mabosi zako na viongozi ni wezi pia!.. this shits happen in real life!.

Mkuu usipende kutoa matamko kabla muvi haijafika tamati huwezi jua nini kitakuja mwishoni just ikifika mwisho ndo utoe judge zako sahivi baki nazo akilini tu subiri wamalize movie yao,Kisha tuje hapa tuwachambe sasa!.

But yote kwa yote niwapongeze hata wale wanaofanya kitu heri wamefanya kitu na ndio maana tunapata vya kuwachallenge. Wanasema mkaa bure sio Kama mtembea bure.
 
Mkuu sio lazima kila siku mhalifu ndo hushindwa nenda kacheki miles 22. Have you ever think vipi huyo mama je Kama bado anafanya kazi ya serikali akaja kuwauza wakina professor..?!

Ngoja tuone ujumbe wanaotaka kutupa kuhusu ulimwengu wa kihalifu let's see.
 
Andiko la NYEMO CHILONGANI hili... Mkuu jifunze kutoa credit, inawezekana we hujaangalia hata moja hapo lakin umelibandika hapa km we ndo ulieona na kutoa uchambuzi wako

MY TAKE
Edit post yako umpe credit kijana NYEMO
 
Watu wa Prison Break wanajaribu sana kuipinga Money Heist na series zao za kijinga. Kwanza story ya Squid na Money Heist hazina hata uhusiano hii comparison hata sijui inatoka wapi au kwa kua nao wamevaa masks?

Money Heist >>>>>Prison Break, nipo Tengeru Arusha karibu na shule ya Akheri njooni mniuwe.
 
Kwahiyo Prison break ni ya kijinga?...
 
Keyword "ENTERTAINMENT"

Movie siyo maisha halisi, movie inaonyesha mambo yanayotokea katika maisha: mambo halisi na yasiyo halisi. Kwenye maisha halisi kinachoonekana kigumu kwenye movie kinaweza kuwa rahisi sana. Moja ya kitu watu wengi hawajui ni maana ya neno "MOVIE"

Unavyoiona Money Heist ina vitu vingi ambavyo haviwezekani katika maisha ya kawaida, hivyo vitu ndiyo vinaleta burudani kwa watu mbalimbali. Kila mtu ana aina yake ya movie aipendayo, ukiona hupendi uongo wa kwenye movies angalia movie based on real events au documentary.

Professor kwenye Money Heist amecheza character ambayo katika maisha ya kawaida ni ngumu mtu kuwa na success rate katika mambo namna ile ila jinsi alivyokuwa anafaulu katika mipango yake ndiyo ilimfanya kuwa popular na kuifanya series kupendwa.

One of the childish comparison on the internet after "Ronaldo & Messi" inafuata hii ya "Money Heist & Prison Break"
20211007_195431.jpg
 
Nimebahatika kuziangalia hizi zote, kitu cha kwanza kabisa, hazifanani, ni muvi tofauti ila ukija kwenyr uandishi, huyu aliyeandika hii Squid Game, ameiandika kiuandishi kabisa.

Muvi A: Series ya Money Heist inaanza vizuri sana, inakufanya uvutike na kutamani kuiangalia zaidi lakini baadaye, udhaifu unaonekana waziwazi, muvi inaanza kukaa kitoto, kuna matukio ambayo ni very simple kutokea, mwandishi akiyaandika kirahisi sana.

Duniani, pesa hazilindwi sana kama karatasi za kutengenezea pesa. Ni bora uingie benki ya dunia uibe mabilioni ya dola lakini si karatasi za kutengenezea pesa, hizo zina ulinzi mkubwa mno kwani ukifanikiwa kuzipata, wewe ni bilionea. Lakini kwenye hii series, yaani watu wanaingia kirahisi sana, huo ni udhaifu wa kwanza, halafu wa pili, watu wanaanza kuingizia mapenzi humohumo.

Jaribu kufikiri tu, sehemu kama hiyo ambayo inatakiwa milango yako yote ya fahamu iwe wazi, kinatokea kitu kama hicho, kiuhalisia, hamna kitu kama hicho.

Tokyo alibahatika kuondoka, akatoka humo, kilichotokea baadaye, akarudi tenayaani very simple tu, ni kitu abacho hakiwezi kutokea hata kidogo.

Ukifuatilia yule mama aliyekuwa akifuatilia hilo suala, naye alikuwa na udhaifu mkubwa. Hafuatilii kama mfuatiliaji, anafuatilia kama muigizaji na ndiyo maana watu wanasema kama kazi ya kumfuatilia angepewa Mahon wa Prison Break, series ingeishia season ya kwanza tu.

Nimeangalia muvi nyingi za kipelelezi, ila sijamuona mtu anayefuatilia kesi kama yule mama, mwandishi amekuwa dhaifu sana upande huo, hakutaka kumpa nguvu, alimpa nguvu Profesa.

Tazama Prison Break, Scofield alikuwa na akili sana, naye Mahon alikuwa na akili mno, alipewa nguvu sana na mandishi na ndio maana wakisumbuana sana.

Kwa Rate, kule IMBD nimeweka 6/10.

Nakuja kuichambua na Squid Game.

Uandishi wa Squid Game nineupenda sana. Kabla ya kumpa character nguvu kwanza tuambie kwa nini anapewa hizo nguvu.

Hii series imezungumzia zaidi mtu masikini, mwenye madeni ambaye hawezi kuyalipa, ili kuyalipa, anakuwa tayari kufanya lolote lile kwa ajili ya pesa.

Watu wenye madeni wamechukuliwa na kuwekwa sehemu moja. Kila mtu mbali na madeni, ana matatizo binafsi, huyu mama yake mgonjwa, yule hivi na vile.

Hapo mtazamaji unaona kabisa huyu mtu anahitaji pesa. Michezo ambayo wameicheza, ni kweli inasumbua kichwa, mbele ya bastola, huku ukiwa unatetemeka, unaambiwa uufanye mtihani fulani.

Hii muvi imenikumbusha muvi nyingi kama Escape Room na Saw. Games walizocheza ni za utotoni, ila kwa kipindi hiki zimejaa hatari.

Vitu ambavyo vimeifanya series hii kupendwa ni namna michezo ilivyochezwa, ukatili uliofanyika na hata mwisho kugundua babu ndiye mratibu, ni kitu ambacho hakuna mtu yeyote aliyehisi hilo.

Dhima kubwa ya series hii ni kukuonyesha mtu mwenye matatizo ya pesa, yupo tayari kufanya lolote lile ilimradi kupata pesa hata kama litagharimu maisha yake.

Endapo hii series ingetoka mwaka 2008 ilivyoandikwa, isingevutia kama sasa hivi kwa kuwa bado hatukuwa na muvi za namna hii, ila kwa sasa ni lazima tuipende kwa kuwa tumeona vitu ambavyo tumeviona kwenye Escape Room, Saw na nyinginezo.

Kwa kule IMBD nimeipa Rate ya 7/10.View attachment 1966185
Sio kwamba Kwenye Money heist Pesa zilikuwa zinalindwa sana bali walikuwa wameshikilia watu wa muhimu sana Kama Gavana Na wale wengine ambao walikuwa watoto wa Matajiri na Mabalozi,Money Heist Hukuielewa Mimi nimeangalia zote Hila Money heist Ni Top Sababu Yenyewe ina Account zake Mfano ya insta ina zaid ya 12M followers hapo Ujaweka za sehem nyingne ,Halafu Squid Game ni Mini series kama Wandavision hila Money Heist Ni moto wakuotea mbali zile theory za Profesor ni Noma ,kitu Kilichobeba Squid Game ni kwamba wamekuja na Idea Mpya Ya games
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom