Spika Sitta Kung'olewa?

Hii kitu bwana ni kampeni za Kikwete kwa namna moja au nyingine...!

Kajifanya kuwaumbua mafisadi wakati nayeye ni mmoja wao!

Of course utendaji wa Sitta ni mzuri,sasa kwa nini aliiomba CCM radhi huku akijua fika kuna mafisadi?! Angeonyesha msimamo wake uko wapi.

Lengo la Kikwete ni kulimaliza nguvu hilo kundi la MAFISADI ambalo lipo against yeye kwa kumtumia Sitta!!!

Check vizuri hii kitu, but simlazimishi mtu akubali/aamini ni mawazo yangu tu!
 
Ndiyo yaliyotokea kwenye NEC juzi, 6 alisema hatatetereka. wacha tuone
 
Ni kawaida ya CCM kucheza michezo ya namna fulani ili kupumbaza watu au kujenga picha fulani kwenye akili za watanzania ilihali si kweli bali tu ni mchezo wa kuigiza. Me huwa nayaita maigizo nyuma ya pazia ambayo hayana maana unapozungumzia demokrasia na utawala bora.

Wanachotaka hapa ni kutuonyesha kuwa mwenyekiti wa NEC yupo kinyume na mafisadi na ana dhamira ya kutokomeza hilo kundi.. sidhani kama kuna ukweli hapa. Hii ni namna fulani ya kumweka JK kwenye nafasi nzuri ya kupata uongozi 2010, kuonyesha kuwa ana pambana na ufisadi. Tanzania bila ufisadi inawezekana, na tanzania bila CCM inawezekana pia!

Mimi nasema sidanganyiki!
 
Hii inaonyesha ni Janja ya CCM kutaka kupooza wananchi ambao wanawasiwasi na jinsi wanavyooendesha mabo yao
 
NEC ya CCM haina mamlaka ya kumwondoa spika madarakani. Spika siyo lazima awe mwanachama wa chama chochote kama ilivyo kwa wabunge, na wala halazimiki kuwa mbunge.
 
Hii kitu bwana ni kampeni za Kikwete kwa namna moja au nyingine...!

Kajifanya kuwaumbua mafisadi wakati nayeye ni mmoja wao!
Of course utendaji wa Sitta ni mzuri,sasa kwa nini aliiomba CCM radhi huku akijua fika kuna mafisadi?!Angeonyesha msimamo wake uko wapi.
Lengo la Kikwete ni kulimaliza nguvu hilo kundi la MAFISADI ambalo lipo against yeye kwa kumtumia Sitta!!!

Check vizuri hii kitu,but simlazimishi mtu akubali/aamini,ni mawazo yangu tu!

Jamani siyo kweli kuwa Sitta aliomba radhi katika kikao kile. Unless mimi ni mbumbu wa lugha. Aliwashukuru wajumbe kwa kutumia uhuru wao wa maoni na kuiomba meza kuu iyafanyie kazi yaliyosemwa.

Kinachonitesa mimi ni role ya mwenyekiti wetu katika sakata lile. Mwaka jana alikataa kuingilia bunge ili kumwokoa rafiki yake EL. Safari hii anakubali mambo ya bunge yaongolewe kiasi hiki!
 
Ingekuwa busara kwamba sita aachane nao hao wazushi yeye atizame haki za wananch na yupo kwenye kile kiti kutetea maslahi ya nchi hivyo yeye asipoteze yunit zake kupigishana makele na mifisadi yeye akazane hivyo hivyo kuwakomali mpaka waone aibu.
 
Kama kweli walipenyeza 50m na hawakufanikiwa basi. Ni funzo. ila pengine basi ni Mwenyekiti wao alikuwa na msimamamo vinginevyo angekubaliwana nao lengo lingetimia "Kumng'oa Sitta". Kazi kweli kweli.
 
Pamoja na yote wanashindwa kuelewa kwamba wananchi wote sasa hivi wanaakili walizani wangemg'oa sita ndio wangewin na ufisadi wao tungeandamana si tunaangalia wanaotetea haki zetu sasa kawa wanaotupigania ccm hawawataki sisi tutawataka wao mi sasa hivi nachukua mazoezi mwakani au 2010 vita ni vita mura tutakuwa kama tarime we waache tu
 
Karata waliyonayo fisadiz ambayo wanaweza kuitumia kumuondoa Sitta ni ya kumnyang'anya kadi ya uanachama lakini tofauti na hapo hakuna jinsi nyingine.
This time imeshindikana, sasa tusubiri bunge lijalo tuone Sitta kasi yake itakuwa vipi. Maana yeye atakuwa kwenye himaya yake. Anachotakiwa ni kusimama kidete bila kuyumbishwa na hao wahuni wa NEC. Halafu sasa hapo ndipo tuone kama kitaitishwa kikao kingine cha dharura cha NEC kumnyang'anya kadi.
 
Nimepata kahabari kutoka watu waliokua huko wanasema jamaa s.s anasema subiri muone bunge lijalo kuna watu watakimbia nchi

moto gwansanzu lol ukiuchokonoa moto lazima ujue jinsi ya kuuzima

mafisadi alikua anawaedea na speeed ndogo inasemekana tusubiri mwezi wa kumi mhhh ngoja nikae mkao wa kula , hivi kuna njia ya ku forward mwezi wa tisa he he he eh
 
Urambo Tabora,

Wewe mnyanyembe hebu acha maneno yako hapa, moto ngwa nsanzu? haya tunausubiri tuuone
 
Urambo Tabora,

Wewe mnyanyembe hebu acha maneno yako hapa, moto ngwa nsanzu? haya tunausubiri tuuone
yomba yomba ha ha ha ha ,kaka kiluga kimenikaa kushoto ila nahamu nijue saana , haya mambo ya kuishi mijini mhh mpaka lugha tunaharibu lakinni moto gwa nsanzu ni moto wa kuachia mbali unaonukia, si unajua ukimjerui simba inakuaje mmmh macho yetu
 
Pamoja na yote wanashindwa kuelewa kwamba wananchi wote sasa hivi wanaakili walizani wangemg'oa sita ndio wangewin na ufisadi wao tungeandamana si tunaangalia wanaotetea haki zetu sasa kawa wanaotupigania ccm hawawataki sisi tutawataka wao mi sasa hivi nachukua mazoezi mwakani au 2010 vita ni vita mura tutakuwa kama tarime we waache tu

Mmmh mkuu hata gari ikikimbia gia huwa inabadilishwa au kujibadilisha yenyewe. Sentensi hii ukiisoma ukiwa unaongea utakuwa umemaliza majagi 6 ya maji wakati unafika kwenye kituo cha sentensi. Hata mie naona unachukuwa mazoezi.......aaahha teh teh..... No fight, tunaelimishana tu.
 
he he nhe he nhe he

yani humu ndani unaweza cheka mpaka kufa lol
 
Duh Mwaka huu... Kweli Mungu amesikiliza sala zetu. Muungwana asipoamka usingizini amekwisha

Huu ni usingizi PONO mkuu, anatamani kuamka lakini ndoto bado tamu.....na ndoto ikishanoga kuamka mpaka uote unachapwa bakora.
 
Back
Top Bottom