Spika Sitta Kung'olewa?

Huyu ni mchapakazi mzuri, tatizo lake ni lile la kuukumbatia waraka wa katoliki.

Kama kiongozi wa Bunge anaweza kuutekeleza waraka huo ndani ya Bunge na sio kuwapa jumuiya na taasisi za dini kazi ya serikali. Kwa hilo atakaa na ajute maisha yake yote.

Kwa sasa hivi hawezi kuungwa mkono na wananchi wote isipokuwa wale watu wa makanisa... Doa!!!!!!

Labda kama ataomba msamaha na kurudi katika mstali.
 
Ama kweli yetu macho. Habari hizi toka katika gazeti la MWANANCHI zinadai MAFISADI wamemwaga hela kwa baadhi ya wabunge wa CCM ili waweze kumuondoa SPIKA SITTA. Naamini kama atasimama imara huku akiondolewa basi hapo ndipo kutakuwa na UTAMU, maana wananchi watapata nafasi ya kujua mengi ambayo wameyaficha. Na mtoa habari hizo atakuwa Sitta mwenyewe UNLESS WAM-BALALIZE. Kwa maelezo zaidi soma hapo chini:

Richmond: Kundi la wabunge lajipanga kutetea bungeni

*Nia ni kuonyesha waliotuhumiwa wameonewa
*Laweka mkakati kutaka kumng'oa Spika


............

Japo hii habari imerusha vijimawe kwa Richmond angali jinsi habari yenyewe ilivyoandaliwa, mwandishi amehakikisha anahighlight kile anataka uondoke nacho kwa kukiweka mwanzoni mwa habari na in caps or bold letters.

Style ya uandishi wa aina hii inatumika sana na sehemu wasiyotaka usome wanaandika kwa font ndogo zaidi ya ile walitaka usome. Mara nyingi hii style inafanikiwa kwa vile wasomaji wengi hawapendi kusoma habari ndefu wakishasoma para ya mwanzo wanaishia.

Kibaya zaidi Rostam Azizi ni shareholder mkubwa wa gazeti la Mwananchi, vibosile Kenya wanapokea amri toka kwake za kuwalinda mafisadi wenzake, hivyo tuwe makini na nini tunaambiwa.
 
Last edited:
Japo hii habari imerusha vijimawe kwa Richmond angali jinsi habari yenyewe ilivyoandaliwa, mwandishi amehakikisha anahighlight kile anataka uondoke nacho kwa kukiweka mwanzoni mwa habari na in caps or bold letters.

Style ya uandishi wa aina hii inatumika sana na sehemu wasiyotaka usome wanaandika kwa font ndogo zaidi ya ile walitaka usome. Mara nyingi hii style inafanikiwa kwa vile wasomaji wengi hawapendi kusoma habari ndefu wakishasoma para ya mwanzo wanaishia.

Kibaya zaidi Rostam Azizi ni shareholder mkubwa wa gazeti la Mwananchi, vibosile Kenya wanapokea amri toka kwake za kuwalinda mafisadi wenzake, hivyo tuwe makini na nini tunaambiwa.

Mimi nilifikirishwa na kuaminishwa kuwa jamaa alishauza hisa zake. Mwenye ukweli atudondoshee hapa kama jamaa bado anamiliki gazeti la Mwananchi.
 
i ve never trusted Mr President. in wateve the move Tanzania is passing through, be it Richmond, EPA or this one of Sitta, I strongly believe though in absence of admissible authorities that he is one of them or at least knows wat z goin on and of course bless it
 
Unavyoongelea Nguvu Ya Ummma Una Maanisha Nini ? Ule Umma Ambao Uko Pale Unachekelea Anavyolipwa Mil 2 Kila Mwezi Kwa Ajili Ya Matababu ? Ule Umma Ambao Unashangilia Spika Anavyofoji Risiti Za Malipo Na Kulidanganya Bunge Kila Siku ? Ule Ummah Ambao Hauambiwi Ukweli Kuhusu Spika Siku Zote Au Ummah Upi Huo ?

Kama Ndio Ummah Huo Basi , Muda Umefika Ummah Umeshasema Hatumtaki Na Aondoke Aende Zake Kama Hasikii Badi Ataondolewa Kwa Njia Zingine Ambazo Yeye Mwenyewe Na Jamaa Zake Wanaokula Nae Fedha Za Walipokodi Watashangaa Na Itakuwa Ndio Ya Moja Kwa Moja Tutamsahau


:mad:Unajua ndugu yangu, kuna watu haasa hawa wakubwa who do not like to be consoled neither advised in their wrong doings. Take an example of UDOM kuna jamaa huko ambae amewekwa na KIKwETE who is called MLACHA KIKULA. Aisee ule jamaa ni mshenji akuna mfano. U cannot imagine kwa ameweza kutumia campuni kufanya fumigation worth 100,000,000. One hundred Million ? Now my question is what type of fumigation which will cost such big amount of money ? Alafu kuna jamaa wengine kwa jina Ally Mchenje ambae pia ni jamaa wa JK amefungua shule kubwa tuu huko SAME. We want to know where they get all these money from. If it is a BANK loan let it be clarified.

Huyo KIKULA haasaaaa anakiburi na kufanya UDOM kama yake. Ana nyanyasa hata wakubwa zake eti : I AM APPOINTED BY THE PRESIDENT ETI WEWE NI NANI: That's what he tells his superiors>>> Very checky and rude. Sisi tumechoka sana na JK na hawa watu wake amewekwa kwenye eneo nyeti. Huyo KIKULA we want him out of UDOM because he is actually not fit for that University kabisa. Anakula wazi wazi, walimu na academicians wanaondoka kwa sababu ya shida ya huyo Idiot. Tuna taka Kikula ajieleze hizo fumigation ya million mia kwa one house ya walimu emelipwaje na pesa imetoka wapi ???

Thks - Blessings, NL, The Hughe.
 
:mad:Unajua ndugu yangu, kuna watu haasa hawa wakubwa who do not like to be consoled neither advised in their wrong doings. Take an example of UDOM kuna jamaa huko ambae amewekwa na KIKwETE who is called MLACHA KIKULA. Aisee ule jamaa ni mshenji akuna mfano. U cannot imagine kwa ameweza kutumia campuni kufanya fumigation worth 100,000,000. One hundred Million ? Now my question is what type of fumigation which will cost such big amount of money ? Alafu kuna jamaa wengine kwa jina Ally Mchenje ambae pia ni jamaa wa JK amefungua shule kubwa tuu huko SAME. We want to know where they get all these money from. If it is a BANK loan let it be clarified.

Huyo KIKULA haasaaaa anakiburi na kufanya UDOM kama yake. Ana nyanyasa hata wakubwa zake eti : I AM APPOINTED BY THE PRESIDENT ETI WEWE NI NANI: That's what he tells his superiors>>> Very checky and rude. Sisi tumechoka sana na JK na hawa watu wake amewekwa kwenye eneo nyeti. Huyo KIKULA we want him out of UDOM because he is actually not fit for that University kabisa. Anakula wazi wazi, walimu na academicians wanaondoka kwa sababu ya shida ya huyo Idiot. Tuna taka Kikula ajieleze hizo fumigation ya million mia kwa one house ya walimu emelipwaje na pesa imetoka wapi ???

Thks - Blessings, NL, The Hughe.

Mkuu nafikiri ingekuwa vyema kama ungedondosha data ukiwa na BACK UP EVIDENCE. Lakini kama ni mwendo wa kuongea tu kwa kuweka tarakimu sidhani kama kutasaidia kitu. matokeo yake JF tutaonekana kama tunapiga majungu. Dondosha data hapa watu wachambue pumba na mchele.
 
siita.jpg


(Picha) Spika wa Bunge la Tanzania Bw. Samuel Sitta

*Shilingi milioni 50 zilimwagwa kummaliza
*Mrithi wake aliandaliwa kabla ya kikao
*Kikwete adaiwa kuweka mtego kubaini ukweli


SIKU mbili baada ya mkakati wa kumng'oa Spika wa Bunge la Tanzania Bw. Samuel Sitta, kukwama ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), siri nzito zimeendelea kubainika.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Kikao NEC kilichomalizika Jumatatu iliyopita zilidai kwamba zaidi ya sh. milioni 50 zilitumika kugawa kwa baadhi ya wajumbe kuhakisha kwamba wanasimama kidete kuhakikisha wanamng'oa Bw. Sitta na kwamba Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete aliwatega ili ajiridhishe na tuhuma hizo.

“Unajua ni wazi kwamba hawa jamaa walitumia zaidi ya sh. milioni 50 kuwagawia baadhi ya wajumbe waliowaandaa ili wahakikishe wanaibua hoja dhidi ya Sitta kwenye kiti chake, lakini bahati nzuri Mwenyekiti alidokezwa na huenda hata vielelezo kadhaa alipewa,”kilidai chanzo chetu ndani ya NEC

Ilielezwa kwamba kama mpango wa kumng'oa Bw. Sitta ungefanikiwa zingefanyika kampeni za papo kwa papo kumpata mtu wa kumrithi ambapo mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini alikwishaandaliwa kugombea na kuchukua nafasi hiyo kwa gharama yoyote ile.

“Tayari timu ya kampeni ilikwishaandaliwa kutembea nchi nzima kwa wabunge ili aliyeandaliwa apate Uspika na kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kutangaza kwamba tuhuma zote zinazotikisa Serikali ndani ya Bunge zitajadiliwa upya au kufungwa kwa kuwa zimeleta mgawanyiko, huo ndio ungekuwa mwisho wa CCM kuongoza nchi,”kilisema chanzo chetu bila kutoa ufafanuzi wa kina wa kauli hiyo.

Habari zaidi kutoka kwa watu walio karibu na Rais Kikwete zilidai kwamba Kiongozi huyo wa CCM alipata taarifa zote za maandalizi ya genge hilo la kifisaidi na kwamba katika kikao chao kilichofanyika mjini hapa ndicho kilichoandaa hoja ya kumng'oa Bw. Sitta na kwamba baada ya kupata taarifa hizo, aliwatega kwa kuwaacha wafanye kila wanachotaka kwanza ili awabaini na kujiridhisha na ushahidi aliopewa.

Ilielezwa kwamba katika siku ya kwanza ambapo baadhi ya Wajumbe walifika mbali kwa kutoa lugha zinazoweza kutafsiriwa kuwa ni matusi kwa Bw. Sitta ndani ya NEC, siku ya pili Rais Kikwete aliwaacha wajumbe hao kujieleza kwa kina wakidhani wanatumia uhuru wao kama wajumbe kumbe alikuwa amewatega ajiridhishe na yale aliyopewa na vyombo husika vinavyofuatilia nyendo za mafisadi.

“Unajua hata hawa jamaa hawamtambui vizuri Kikwete (Rais), wanadhani ukimya wake hawaujui, jamaa anawatega tena safari hii amewapatia kweli kweli, anajua fika mipango yao yote lakini kama tunavyomjua ni mtu asiyekurupuka katika maamuzi na anafanya kwa upole, alipojiridhisha dakika za mwisho alimaliza mzizi wa fitna kwa kuunda Kamati ya kurejesha umoja na kumaliza mgongano ndani ya chama,”kilisema chanzo chetu na kuongeza;

“Ni wazi kwamba CCM sasa inataka kwenda kinyume na matakwa ya Watanzania, lakini bahati nzuri Mwenyekiti ni mwerevu sana, amekiokoa chama kufuata mkumbo wa KANU, lakini kama asipokuwa makini zaidi wanaweza kumweka pabaya mwakani, hawa wana mbinu nyingi na kila siku wanakuja na jipya.”

Habari zaidi zilieleza kwamba Kamati hiyo inayojumuisha Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Bw. Pius Msekwa na Spika mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki Bw. Abdulrahman Kinana imepewa jukumu la kukutana na wabunge wote wa CCM na kuzungumza nao kwa undani na kuhakikisha vikao vya wabunge wa chama hicho vinafanyika vizuri na kuweka msimamo mpya wa jinsi ya kumaliza mambo mzito yenye maslahi kwa chama kupitia vikao hivyo kabla ya Bunge.

Kwa kumjibu wa taratibu za Bunge ni wazi kwamba Kamati hiyo ambayo ina watu wenye sifa za ushawishi itakutana na wabunge katika Kikao cha 17 cha Bunge Oktoba mwaka huu mjini hapa.

Majira lilipomtafuta Bw. Sitta ili kujua msimamo wake kuhusu uendeshaji Bunge kwa kasi na viwango kutokana na mashambuzi yaliyoelekezwa kwake kwenye NEC hakupatikana mara moja.

Hata hivyo habari za uhakika kutoka kwa watu waliokaribu na kundi linalopinga ufisadi zilisema hivi sasa wabunge hao wanaendelea na mikakati mizito ya kuendeleza vita hivyo kwa mbinu za kisasa.

Taarifa hizo zilidai kwamba huenda Bw. Sitta akaongeza kasi na viwango zaidi vya kusimamia Bunge na kuwabana zaidi mafisadi pamoja na mawaziri wazembe jambo ambalo litaibua hasira za kundi hilo kwa kiongozi huyo wa Bunge.

Source: Gazeti la majira.

Hii kitu sio kampeni jamani,embu fikirieni vizuri...!

Hakuna cha werevu wala wala ushuzi dot com, ni upumbavu mtupu viongozi wa serikali na chama chao kuangalia huu utumbo uliofanywa juu ya Sitta.
Huwezi kuniambia JK alikuwa anajua kinachoendelea, watu wanamwaga upupu halafu yeye anakenua meno........anachekelea tu, eti anakusanya data, anajiridhisha na evidence...BS

Haya mambo SISIEMU wasipoyakabili kweli yataendelea kuwagawa zaidi wananchi, na sisi hatuhitaji utumbo kama huo. Kama watu wamemwaga milioni 50 basi vyombo ya sheria/ usalama viingie hapa kuona undani wake zaidi na si kamati ya chama ya kurejesha uelewano ndio ichunguze. Does this make sense???

Eti kukata mzizi wa Fitina JK akaunda tume sijui Kamati ya kuchunguza sijui ya kurejesha uelewano. Sasa wewe umeshapewa taarifa na vyombo husika, na vyombo husika mojawapo naweza kusema Usalama wa Taifa au TAKUKURU. Sasa kwa nini uunde kamati ndani ya chama kuchunguza huo ushuzi badala ya kuachia vyombo ya USALAMA vifanye kazi yao??? Hivi kweli hapo kuna kukata fitina kweli au ndio sindimba yenyewe inachezwa.
JK sometimes anatakiwe awe serious, this is not MDAKO GAME......this is a serious business.
 
Mimi nilifikirishwa na kuaminishwa kuwa jamaa alishauza hisa zake. Mwenye ukweli atudondoshee hapa kama jamaa bado anamiliki gazeti la Mwananchi.


Itakuwa vizuri kama kuna mtu anauhakika huyu fisadi kauza share atujuze, hadi 2007 share alikuwa nazo kama kauza basi ni kati ya mwaka jana na mwaka huu.
 
Nasema kila mara kuwa Sitta sio mtu wa masihara kwa sababu ulinzi wake umo ndani ya himaya ya Mungu. Kum-Kolimba au Kum-Balalize inawezekana lakini ukumbuke tofauti yake ni kuwa wananchi wengi wako nyuma yake. Mzee Sitta kamwe Husirudi nyuma endelea kumweka Mungu kwenye kazi zako zenye maslahi kwa nchi yetu nawe utashinda. Tupo pamoja nawe kwenye vita hii ya mafisadi
 
Kwanza asante sana kwa hoja hii kutuletea. Lakini wafanye wafanyacho, mafisadi kiama chao ndio kimefika. Sitta atabaki 6 na tena safari hii boaded one and increased font. Hiyo hela wanayoisambaza haiwaumi maana ni ya kifisadi. Hata wakinipa nami nitakula.

Leka.
 
Sitta kung'olewa uspika

Na Saed Kubenea, Mwanahalisi

KUNA njama za kuwatoa "kafara" wabunge 15 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili kusafisha njia ya urais wa Edward Lowassa, MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa zinasema iwapo wabunge hao watasalimika kwenye kura za maoni, jambo ambalo halitarajiwi; basi watatoswa kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho.

Wabunge wanaokamiwa ni wale waliojitambulisha kupambana na ufisadi nchini na ambao wamekuwa mwiba kwa kambi inayomuunga mkono Lowassa na swahiba wake Rostam Aziz.

Wengine ni pamoja na wanamtandao ambao wamekuwa wakilalamika kwamba Rais Jakaya Kikwete amemtosa Lowassa na wale wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi.

Hata hivyo, uwezekano wa Lowassa kugombea mwaka huu ni mdogo kufuatia uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumwandaa tayari Rais Kikwete kugombea kwa ngwe ya pili.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, kuangamizwa kisiasa kwa wabunge hao mwaka huu, kutatoa fursa kwa wanaotaka kushika utawala mwaka 2015 kujipanga kwa njia ya kuchukua nafasi muhimu katika bunge lijalo.
Uchaguzi mkuu mwaka huu umepangwa kufanyika 31 Okoba.

Chanzo cha habari kinasema maandalizi yamefanywa katika majimbo ya wabunge walengwa, ili wakipona kwenye kura za maoni wakumbane na uamuzi wa NEC.

Zengwe linalosukwa ni tuhuma za kuhujumu chama chao bungeni na kujivisha "ukamanda dhidi ya ufisadi."

Tayari ushawishi mkubwa umepenyezwa kwenye vikao vya juu vya chama na una baraka za baadhi ya viongozi, taarifa zimeeleza.

Baadhi ya wabunge ambao wanatajwa kusukiwa mkakati wa kuangamizwa ni pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta, mbunge wa Njombe Kusini na Naibu Spika, Anne Makinda, mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe na mbunge wa Nzega, Lucas Selelii.

Wengine ni mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo, mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka; mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, Victor Mwambalasa, mbunge wa Lupa na mbunge wa Viti Maalum, Injinia Stella Manyanya.

Kwenye orodha ya wabunge wa kuangamizwa kisiasa, wapo pia mbunge wa Sikonge, Saidi Nkumba; mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro; mbunge wa Maswa, John Shibuda; mbunge wa Mbozi Mashariki Godfrey Zambi na mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo.

Habari zinasema mpango wa kuwang'oa wabunge hao umetengewa mamilioni ya shilingi na kwamba lengo ni kutaka kampeni dhidi ya ufisadi zisiendelee bungeni katika kipindi cha mwisho cha Rais Kikwete.

Aidha, taarifa zinasema wanaojipanga kwa utawala 2015 wanataka kuchukua nyadhifa za spika, wizara ya mambo ya nje na wizara ya fedha.

Makusudi makuu ya kutaka nafasi ya spika, taarifa zimesema, ni kuunda tume ya kurejea kashfa ya Richmond ambayo itapewa jukumu la kusafisha wote waliohusika.

Mlengwa mkuu katika mradi huu ni Lowassa ambaye alipoteza nafasi ya waziri mkuu kutokana na kushinikiza watendaji serikalini kuipa kazi ya kufua umeme, kampuni ya Richmond ambayo haikuwa na hadhi, uwezo kifedha wala utaalam katika nyanja hiyo. Mbali na wabunge hao, mawaziri wawili, Profesa Mark Mwandosya na John Magufuri, nao wametajwa kuwa wanasukiwa zengwe la kuangamizwa kisiasa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Wanasiasa hao wawili, hawamo katika kundi la wabunge wanaofahamika kama makamanda wa ufisadi. Hata hivyo, kuingizwa kwao kunatokana na kuonekana kuwa wanaweza kujitosa katika kinyang'anyiro cha kutaka kumrithi Kikwete mwaka 2015.

Mwingine ambaye amelengwa na njama hizo ambazo inadaiwa zimetengewa mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kile kinachoitwa "kulainisha wajumbe wa NEC," ni Nape Nnauye aliyetangaza kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo.

MwanaHALISI limeelezwa na baadhi ya wasaidizi wa viongozi waandamizi wa mpango huu kuwa tuhuma za wabunge na makada hao tayari zimeshaandaliwa.

"Lengo ni kuwafukuza kipindi cha lala salama na kuwaacha bila mahala pa kwenda kutokana na muda wa kuwasilisha majina Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumalizika," ameeleza mtoa taarifa.

Kwa mujibu wa ratiba za vikao vya uteuzi vya CCM, mkutano wa Kamati Kuu (CC) unatarajiwa kufanyika Agosti 15, huku NEC ikipangwa kufanyika 16 na 17. Siku ya mwisho ya kupeleka majina Tume ya Uchaguzi ni tarehe 19 Agosti mwaka huu.

Kutokana na mahakama ya rufaa kutotoa uamuzi katika shauri linalotafuta mgombea binafsi, na kucheleweshwa kusajiliwa kwa Chama Cha Jamii (CCJ), wabunge hao watakuwa wameachwa njiapanda.

Gazeti hili lilishindwa kumpata Spika Sitta kueleza iwapo anafahamu njama hizo. Hata hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita, Sitta alinukuliwa na gazeti la kila siku la Mwananchi akikiri kuwapo kwa mwanachama mmoja wa CCM anayewania jimbo lake.

Sitta alisema anaamini kuwa mwanachama huyo ametumwa na watuhumiwa wa ufisadi walioathirika kutokana na msimamo wake wa kupinga ufisadi ndani na nje ya Bunge.

Naye Anne Kilango amesema amewahi kusikia "mpango wa kutushughulikia. Kwa upande wa jimbo langu la Same Mashariki, upo ushahidi wa kutosha kwamba inawekwa mikakati ili mimi nisipate nafasi ya kugombea ubunge mwaka huu."

Akiongea kwa sauti ya uchungu Kilango alisema, "Mtu ambaye anatajwa kutaka kuwania ubunge katika jimbo langu anafanya vitu ambavyo havilingani na uwezo wake.

Anagawa fedha. Mimi na wananchi wengine tumelilalamikia."
Kilango amesema amerekodi kwenye CD ushahidi unaoonyesha namna mpinzani wake mtarajiwa na wenzake walivyokuwa "wakipanga jinsi ya kunishughulikia."

Amesema amepeleka CD hiyo kwa Katibu Mkuu wa CCM kama ushahidi wa dhamira mbaya waliyonayo wapinzani wake. Aliyejitambulisha kuwa anataka ubunge Same ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Michael Kadege.

Dk. Kadege alipoulizwa iwapo anahusika na madai hayo alisema, "Hizo tuhuma za kuhonga anazozitoa Mama Kilango, ni za kupika. Yeye ndiye anayewapa hela watu na kuwaambia waseme mimi ndiye niliyewapa."

Mwalimu huyo wa chuo kikuu amesema CD inayodaiwa kurekodi mikakati ya kumshughulikia Kilango, "ni uongo mtupu. Anatembea nayo kila mahali lakini haina chochote. Ni feki."

Dk. Kadege amesema tayari amewasilisha malalamiko yake kuhusu Kilango "kwa chama chetu kama taratibu zinavyotaka. Mama Kilango ni mvurugaji tu na tuhuma zake ni za kutunga."

Kwa upande wake, mbunge wa Kahama, James Lembeli amesema ana taarifa juu ya kuwapo kwa mpango wa kuwashughulikia.

"Jimboni kwangu tayari nimeanza kuwaona wale waliotumwa kutekeleza mpango huo. Utakuta mtu hana shughuli yoyote pale Kahama mjini na anavaa viatu bila hata ya soksi, lakini ameanza kubadilika ghafla katika siku za karibuni," amesema Lembeli.
Amesema mwanachama huyo amekuwa akichukua teksi kutoka Kahama mjini hadi ndani ya jimbo, umbali wa kilometa 100 hadi 120 kuwaambia wananchi kwamba Lembeli hajafanya kitu jimboni.

"Mimi nawaambia watu hawa kwamba kwanza wanunue soksi za kuvalia viatu, kabla ya kuja kwangu kufanya fitina," amesema Lembeli kwa kicheko na kuongeza, "Nitapambana nao."

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, amegoma kuzungumzia njama za kuangamiza baadhi ya wabunge kisiasa. Amesema, "Sina cha kuwaambia."

Taarifa zinasema jambo linalohitajika kufanywa haraka, hata kama walengwa wa njama wataingia bungeni, ni kuhakikisha kuwa Sitta hachaguliwi kuwa Spika wa bunge lijalo.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, Spika wa bunge amepangwa kuwa ama Edward Lowassa au mfuasi wake ambaye atakuwa na kazi moja tu ya kumsafisha Lowassa kutoka tuhuma za mkataba wa Richmond.

"Tukimaliza uchaguzi, Spika wa Bunge la Jamhuri, atakuwa ama Lowassa au yeyote ambaye atalinda maslahi yetu. Yule bwana aliyejiita speed and standard, uspika atausikia redioni," amesema mtoa taarifa kwa sauti ya kujiamini.
 
kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu, yani wanaofanya maovu ndio wanatakiwa kuzawadiwa nafasi za uongozi wale wanaotetea maslahi ya nchi wanataka kuadhibiwa.
 
These are propaganda of CCM MPs who see danger within their party. No Lowasa Presidency in Tanzania. We must prepare for a new generation of leadership.

Mwanahalisi's assumption is, CCM will continue to be powerful after 2010 and then win 2015, that is miracle. There will be a complete different political landscape in Tanzania after November. Think of new names and Lowasa, Sitta etc.
 
Back
Top Bottom