Spika Sitta Kung'olewa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Sitta Kung'olewa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Indume Yene, Jun 8, 2008.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ama kweli yetu macho. Habari hizi toka katika gazeti la MWANANCHI zinadai MAFISADI wamemwaga hela kwa baadhi ya wabunge wa CCM ili waweze kumuondoa SPIKA SITTA. Naamini kama atasimama imara huku akiondolewa basi hapo ndipo kutakuwa na UTAMU, maana wananchi watapata nafasi ya kujua mengi ambayo wameyaficha. Na mtoa habari hizo atakuwa Sitta mwenyewe UNLESS WAM-BALALIZE. Kwa maelezo zaidi soma hapo chini:

  Richmond: Kundi la wabunge lajipanga kutetea bungeni

  *Nia ni kuonyesha waliotuhumiwa wameonewa
  *Laweka mkakati kutaka kumng'oa Spika


  MZIMU wa Kampuni iliyopewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond Development, unatarajia kuibuka kwa kasi mpya kwenye Kikao cha Bunge cha Bajeti kinachotarajia kuanza Keshokutwa.

  Kuibuka upya kwa suala hilo, inaelezwa ni kutokana na kuibuka kwa baadhi ya wabunge waliobadilika ghafla na kuanza kutetea kampuni hiyo inayolipwa, huku wengine wakisubiri utekelezaji wa maazimio ya Kamati ya Bunge iliyochunguza mchakato wa ushindi wa zabuni hiyo.

  Pia, suala la Spika Samuel Sitta linatarajiwa kutawala mjadala, huku kukiwa na kundi linalotaka kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka kumng'oa madarakani kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

  Imeelezwa kundi hilo la wabunge lililoibuka kutetea Kampuni ya Richmond, linadaiwa kutumia mamilioni ya shilingi kuwashawishi wabunge kubadilisha msimamo wao, ili wasimame kutetea watuhumiwa wa Richmond kuwa wanaonewa.

  Kundi hili ambalo linaundwa na baadhi ya wabunge wakongwe na wenye ushawishi mkubwa, lilikuwa limejiandaa kuwasilisha ajenda kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wabunge wa chama hicho, kilichokuwa kifanyike Alhamisi katika Hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam.

  Richmond iliuzwa kwa Kampuni ya Dowans ambayo inalipwa Sh152 milioni kila siku, licha ya uzalishaji wa umeme hivi sasa kurejea katika hali ya kawaida. Dowans ndiyo inayolipwa fedha za mitambo hiyo.

  Taarifa kutoka Wizara ya Fedha, zinabainisha kuwa mmoja wa wafanyabiashara amekuwa akifuata hundi za malipo hayo kila mwezi, huku akidiriki kuwa mkali pindi malipo yanapocheleweshwa.

  Katika hoja ya kundi hilo, linadai Richmond licha ya kutajwa kwenye Kamati ya Mwakyembe iliyochunguza kashfa hiyo haijawahi kulipwa hata senti moja, lakini imekuwa ikisakamwa bure.

  ''Nakwambia kwenye Bunge la Bajeti mtashangaa, kuna watu wamebadilika. Kuna kundi la wabunge ambalo limeandaliwa na lilikuwa liwasilishe hoja ya Richmond kwenye kikao chetu cha CC (kamati kuu) na wabunge kule White Sand, baada ya kuahirishwa tangu juzi (Jumanne) wanatapa tapa," kilisema chanzo chetu.

  Inadaiwa kundi hilo pia limeanzisha kampeni ya kujijenga kisiasa na limeapa kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2015 baada ya kumaliza ngwe yake.

  Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa kundi hili la wabunge limekuwa likifanya mambo mbalimbali likijipanga na sasa limefanikiwa kumega wabunge katika suala la Richmond.

  ''Wamefanya vikao vingi na vyote serikali inavifahamu, baada ya kuona wameanza kujulikana, walivipeleka kwa mbunge mmoja (jina tunalo) kule Mikocheni na wanamwaga fedha kweli kweli,'' kilisema chanzo kingine.

  Kundi hilo linadaiwa kufanikiwa kushawishi baadhi ya viongozi wa juu wa CCM na wabunge ambao walikuwa na mtazamo tofauti awali, lakini hivi sasa wanaliunga mkono.

  Chanzo chetu cha habari kilisema, wiki hii kuwa kundi la wabunge ambalo 'limenunuliwa' lilikuwa limejiandaa kupeleka ajenda mbili kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM na wabunge.

  ''Moja ilikuwa hiyo ya kutetea Richmond na nyingine ya kutokuwa na imani na Spika. Kwa sababu gani? Spika ndiye ameruhusu hoja mbalimbali ambazo zimewasilishwa bungeni, mojawapo ni hiyo ya Richmond,'' kilisema chanzo hicho na kuongeza:

  ''Pia, kundi hilo lilikuwa limeandaliwa ukikumbuka wakati wa kesi ya Adam Malima na Reginald Mengi, lakini busara ya Spika ikaliacha linahangaika. Aliyeandaliwa kutoa hoja ya kutokuwa na imani na spika alikasirika akatoka nje.''

  Inadaiwa kundi hilo hivi sasa linajenga hoja kuwa, katika mazungumzo yake na wahariri wa habari, Sitta alitamka kanuni za bunge zimempa madaraka makubwa yeye na naibu spika, ndio maana anapitisha hoja za kukandamiza CCM
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Haya ndio aliyokuwa akiyahitaji Muungwana, kwa vipi akiyahitaji?

  Siku zote ukishakuwa na watuhumiwa hutakiwi kuwaweka nje hata kwa dhamana serikali ilikwishashituliwa kuwa hawa watu wana fedha ,aambayo wanaweza kuwalipa wabunge kiasi ambacho hawajawahi kukiona maisha yao , na ndio hivyo ilivyo au inavyofanywa.

  Sasa wakimaliza hapa wanampigia kura ya kutokuwa na imani na raisi mtindo inaonyesha utakuwa ule ule wa kutembeza donge na wakiongeza itakuwa aliekuwa hajapata nae atalipwa kwa mkupuo huku akiulizwa ulikuwepo wapi wewe , inaonyesha sasa mambo ni magumu kwa Muungwana labda ikiwa na yeye yumo katika mpango wa kutaka kumuenzi swaiba wake.

  Haya tuone hao takukururu wawaumbue wabunge waliokatiwa donge katika vijisenti .
   
 3. M

  Msesewe Senior Member

  #3
  Jun 8, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh Mwaka huu... Kweli Mungu amesikiliza sala zetu. Muungwana asipoamka usingizini amekwisha
   
 4. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wananchi watasimama imara pale panapohitaji HAKI, yeye naye ana uozo wake maana ni walewale CCM lakini wote mtakwenda tu. Mtampigia KURA ya "NO CONFIDENCE" kwa mapenzi yenu lakini kumbuka kuwa kuna kura zingine za No Confidence zitakuwa zinawasubiri na nyie vilevile kwenye ballots kwa mapenzi ya wananchi. Mtaumana sana maana CCM sasa hivi ni kama MANYANG'AU. Hata mkimnyamazisha huko Bungeni hatakubali kuondoka peke yake, dawa ni BALALIZATION mapema mapema. Kisha muanze kurushiana mpira oh sijui yuko India, Bangladesh, China, US or Mirambo. Mwenzio akinyolewa wee tia maji. Keshajifunza kutoka kwa MDHANIWA MAREHEMU(Balali), yeye ataweka upupu wote ambao mmekuwa mkiendesha kwenye vikao vyenu vya siri kabla hajachomoka.
   
 5. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hapa mafisadi wanapambana wenyewe kwa wenyewe.Pengine yanayosemwa ni kweli, lakini ukisoma utaona article ni one sided na si ajabu muandishi analipwa na Sitta.
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ina maana Sitta anajihami? na kama anajihami atakuwa anajihami na kitu gani hasa?
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kuonya hapa .Kwamba Media na hata rupia itapenyezwa kujenga majihna na kwa baraka za CCM.Media wale wajanja wamekataa kutumiwa na ndiyo maana wanafichua nategemea kabisa kwamba sasa hakuna siri na move hii itakufa .Ni kweli Sitta ni Fisadi lakini kampeni chafu sasa zinamwandama .Yetu macho
   
 8. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kama ni kweli hiyo ni kazi ya lowasa na rostam. kwa jinsi lowasa navyopenda kusikika na kwa jinsi hata alivyihudhuria zile sherehe za kijeshi pale monduli academy na kuwa mkimya kuna kitu wanafikiri huenda watamwondoa sita na ukashangaa lowasa akawa spika.

  pesa hasa za wizi huwapa mafisadi kiburi cha ajabu
   
 9. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2008
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kibaraka hawezi kubadilika hata siku moja, pesa ya peremende ndio inafanya kazi.
   
 10. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..mwaka wa maasi huu!

  ..ndugu kuchinja ndugu!
   
 11. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..hii mpya ya siku!
   
 12. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Spika haendi kokote hao wabunge ambao wanafahamika sana na ambao walitumika sana kwenye kugawa hela ili Lowassa asiondolewe, lakini walishindwa,

  Tunajua nani yuko behind this, lakini angejua tu maana hizi ni hasira zaidi za Roostam kukataliwa kutoa ile ripoti yake, ni vyema hawa wabunge wapewe nafasi ya kujaribu ili waone kali ya Spika, maana wanajua kuwa bila ya yeye Lowassa asingeondoka, sasa subiri uone the backlash, na this nonesense ikitokea the beneficiary tutakuwa ni sisi wananchi!
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wacha ccm wamalizane tu maana hakuna Sita wala Rostam au Lowasa wote ni chukua chako mapema tu. Sasa wagombea mgao. Wacha wamalizane tu.
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Indume Yene ninakuaminia sana najua hizi ni za jikoni kabisaa, lete vitu mwanangu!
   
 15. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nitazidi kufuatilia nyeti kisha kuzimwaga. Masikio yatakuwa mjini Dodoma.
   
 16. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2008
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Sitta ni Fisadi lakini kampeni chafu sasa zinamwandama .Yetu macho[/QUOTE]

  Sasa kaka Lunyungu kama na yeye ni fisadi hilo suala la kampeni chafu linatoka wapi?. Hata Lowassa alisema anachafuliwa. Kila mtu atasema anachafuliwa. Ukweli ni kwamba watanzania sio mahasidi wanaowafanyia ufisadi viongozi. Viongozi wamefanya ufisadi wenyewe na kila mtu ataumbuliwa kwa wakati wake. Wengine tunaendelea kukodolea kama kawa
   
 17. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Yetu masikio wataumbuana mpaka makarani wao. Hapo ndipo kuna utamu. Hakuna atakayesalimika maana hakuna anayependa kudondoka peke yake kama anajua kuna wengine wa kudondoka. UFISADI wao wote utaweka nje nje tena hapa hapa JF. Subirini utamu bado waja.
   
 18. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nafikiri mwaka huu tunaweza kufanya sherehe ya kuanguka kwa dola linalowatafuna wanyonge Tanzania.

  Napenda wamalizane wao wenyewe kwa rahana za kula bila kunawa na kuwafanya watanzania waendelee kuishi kama yatima.

  Naomba Mzee Sitta akomae tu mpaka waondoke wote(wakose wote). Hakuna kuondoka peke yake tunahitaji akishikwa tu kabla ya kudondoka kabisa arushe makablasha yote mbele ya kandamnasi.

  Asisubiri akawa kama Balali aliyeamua kwenda na documents halafu akazirudisha serikali kabla hajapotea.
   
 19. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Shy hivi unakumbuka maneno yako haya?
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hizi habari zisizokuwa na jina la chanzo chake inakuwa tabu kuzitathmini kwa undani.
  yaweza kuwa sita anajihami kama baadhi ya watu walivyochukulia.
  au inaweza kuwa wenye nazo wanamtisha sita ili baadae maamuzi yake yawe yana base zaidi kwa mafisadi.
  au ni habari tu za tetesi ambazo zipo unfounded
   
Loading...