Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Nimestushwa sana na kauli ya Spika wa Bunge la Tanzania, aliyoitoa jana kuhusiana na wabunge wa Chadema, waliofukuzwa uanachama katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema.
Spika Ndugai amenukuliwa akiwaambia wabunge hao kuwa hatambui kufukuzwa kwao uanachama na chama chao cha Chadema na hivyo waendelee na vikao hivyo vya Bunge, kwa kuwa yeye ndiye aliyewaapisha kuingia Bungeni humo na hivyo hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kuwavua ubunge wao!
Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 71(1)(e) inatamka hivi "Mbunge atakoma kuwa mbunge ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge" mwisho wa kunukuu
Huyu Spika Ndugai anasahau kuwa hata yeye kabla hajakabidhiwa mamlaka aliyo nayo aliapa kuitii na kuiheshimu Katiba hiyo ya nchi
Sasa nimuulize Spika Ndugai, hicho kiburi cha kuwaambia wabunge hao waliovuliwa uanachama wa chama chao, waendelee na ubunge wao anakipata wapi?
Katiba ya nchi ipo wazi kabisa kuwa mtu anaendelea kuwa Mbunge pale tu anapoendelea kuwa mwanachama wa chama cha siasa.
Hivi hawa akina Silinde, hivi sasa wameshafukuzwa uanachama wa chama cha Chadema, kilichowapa ubunge huo, sasa yeye Spika Ndugai anapowaambia waendelee na ubunge wao, wanakuwa wabunge wa chama kipi cha siasa?
Kwa kuwa kwa kufukuzwa uanachama wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba ya nchi "automatically" wamepoteza pia ubunge wao.
Kama Spika Ndugai anawaambia hao wabunge waendelee na ubunge wao, wanakuwa ni wabunge wa Spika Ndugai na wala siyo wabunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo yeye Spika Ndugai aliapa kuitii na kuiheshimu kabla hajakabidhiwa madaraka hayo aliyo nayo hivi sasa.