Spika Ndugai anaendesha Bunge kwa matakwa yake binafsi na si kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
23,301
2,000
Kuandika katiba mpya hakuna maana kama hii iliyopo haifuatwi, siku Chama cha Mapinduzi kikiondoka madarakani mheshimiwa Ndugai anastahili sio tu kushtakiwa, bali kunyang'anywa stahili za uspika anazofaidi kwa kutumia kodi za wananchi, pamoja na yeye wafuatao nao watakuwa pamoja nae mahakamani kwa kushindwa kusimamia kiapo Chao :
1. Waziri wa katiba na Sheria
2. Mwanasheria mkuu wa Serikali

Mheshimiwa Speaker hastahili kuendelea kuhudumiwa na walipa kodi masikini wa Tanzania View attachment 1447567

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa unachanganya mambo Nyalandu kosa alilofukuzwa na chama sio kuhudhuria vikao vya bunge Uanachama wake ulikoma kwa sababu zingine sio za ubunge wake au kuhudhuria bungeni.Vyama ruksa kuadhibu uanachama wao lakini sio kuadhibu MTU kwa kuhudhuria vikao vya bunge wakati unajua ni wajibu wake hilo hakuna

Usilinganishe ya Nyalandu na hilo wakilofanya chadema

Chadema wanaadhibu mbunge kwa kuhudhuria vikao vya bunge hiyo no haikubaliki popote
 

Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,073
2,000
chadema wanahubiri demokrasia ambayo HAWAIFUATI..
Ndugai ana matatizo na viongozi wa chadema nao wana matatizo.
TUSIANGALIE UPANDE MMOJA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kumbukumbu zipo za wanachama wa vyama tofauti ambo walikuwa wabunge na wakafukuzwa.
Walipofukuzwa walienda mahakamani kupinga kufukuzwa kwao. Siyo spika aliyepinga kufukuzwa kwao kama anavyofanya Job.
Na kama unakumbuka vizuri waliendelea na ubunge wao na vyama vyao vilisema hao ni wabunge wa mahakama.
Hiki anachofanya Job ni kuingilia maamuzi ya chama ambayo kwa kweli hayamhusu kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Salange

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
683
1,000
Mgonjwa ghali zaidi duniani anayepaswa kuingia kwenye Guinness Book of Records anaonesha umahiri wake katika taratibu la kuendesha bunge la vyama vingi.

Jr
Inasikitisha sana nchi maskini kabisa duniani kuingiza mgonjwa aliyetibiwa kwa gharama kubwa kuliko wote duniani kwenye Guinness Book of Records. Walipongia madarakani walisema nchi ilikuwa inapigwa sana hii, lakini kumbe wao katika kipindi kifupi tu nchi inapigwa hadi kuvunja rekodi na bado itaendelea kuchakachuliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Samawia

JF-Expert Member
Dec 6, 2017
487
500
Ndugai ni spika wa ajabu haijawahi kutokea. Utawala wa Jiwe hauachi kuwavua nguo watetezi wake kila siku uchwao. Wacha kina mzee mwanakijiji wakae kimya jukwaani
Naye anapambana arejeshwe kwenye uspika awamu ya pili,lazima awafurahishe watakaomuweka pale,anajua anaikanyaga katika Ila uspika Ni zaidi ya katiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 

ludist

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
373
500
Kwa maelezo ya spika, hayo yalikuwa ni makubaliaono ya wabunge wengi ku karantin, si maamuzi ya mbowe, tatizo mmekariri tu kuwa kila kinachotoka chadema ni mbowe mana yy ndiye aliyesaini hyo taarifa, hata angesain mnyika bado mngesema mbowe
Kosa alianza kulifanya mbowe
Chama cha siasa kinaendeshwa na katiba na kanuni
Haujakaa kikao na mtu yeyote yule unakuja na maazimio makubwa hakuna kuingia bungeni twendeni tukajikarantini
Ni kama vile mwalimu mkuu anawapa amri wanafunzi wake,
Wabunge ni watu wazima wanaamini vikao vya chama, kamati kuu nk
Sio amri ya mtu mmoja kana kwamba chama ni chake,

Ukimlaumu ndugai anaendesha bunge bila kufuata katiba

Vile vile rudi na kwa mbowe anaendesha chama cha siasa kama kampuni yake binafsi
Ili tupate kujenga nchi tuache double Standard kama ni kusema tuwaseme wote..

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,491
2,000
Ndugai haitambui Katiba ya JMT kabisa, bora hata wangetumia mbinu za Mahakama ila hii ni dharau kubwa sana kwa Watanzani.

Tanzania imekabidhiwa kwa washamba.

So sad
Ni jambo la hatari sana kwa Spika wa Bunge Ndugai kuisigina Katiba ya nchi kadri apendavyo
 

Blackjew

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
393
1,000
Huwezi mvua uanachama mbunge kwa kutekeleza majukumu yake ya kibunge bungeni

Kazi ya mbunge ni.kuhudhuria vikao vya bunge sasa Wewe ujlkisema unamfukuza kakosea kuhudhuria vikao vya bunge akili unakuwa huna .Nasimama na spika yuko sahihi mbunge kuhudhuria vikao vya bunge sio kosa .Hakuna awezaye mwadhibu kuwa eti kakosea kuhudhuria vikao vya bunge !!!
Kwa katiba yako wewe na Ndugai sawa kwa hiyo kule wanamwakilisha Ndugai?Mnaakili Kama mmetoa mimba
 

fokonola bokoyoka

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
891
1,000
Hapa unachanganya mambo Nyalandu kosa alilofukuzwa na chama sio kuhudhuria vikao vya bunge Uanachama wake ulikoma kwa sababu zingine sio za ubunge wake au kuhudhuria bungeni.Vyama ruksa kuadhibu uanachama wao lakini sio kuadhibu MTU kwa kuhudhuria vikao vya bunge wakati unajua ni wajibu wake hilo hakuna

Usilinganishe ya Nyalandu na hilo wakilofanya chadema

Chadema wanaadhibu mbunge kwa kuhudhuria vikao vya bunge hiyo no haikubaliki popote
Ni sharti waende Mahakamani ili sheria za Nchi na za Chama chao zitafsiriwe pale.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,491
2,000
Kama vipo unamlaumu job yule mgogo wa watu kwa ajili gani?lile bunge ni jukwaa la siasa hata job anafanya siasa mule
.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo Bunge lazima liwe makini na huyo Ndugai, ili asije rudia yale aliyoyafanya kwenye uchaguzi wa 2015, alipomchapa fimbo mgombea mwenzake wa CCM hadi akazirai na kukimbizwa hospitalini
 

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,236
2,000
Spika ndugai amekuwa alifanya haraka sana kuchukua maamuzi ya kumpoka Lissu ubunge,pia alifanyia kazi haraka sana barua Prf.Lipunga kuhusu wabunge wa CUF,pia alifanyia kazi haraka sana barua ya CCM juu ya Nyalandu.Mbona katika hili la wabunge wa Chadema amekuwa mzito sana? Kuna nini nyuma ya pazia? Au anataka kuthibitisha kauli ya CAG mstaafu?
IMG-20200512-WA0014.jpeg
IMG-20200512-WA0015.jpeg
IMG-20200512-WA0016.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Pelle mza

JF-Expert Member
May 15, 2008
2,881
2,000
KATIBA YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA

5.2 Haki za Mwanachama
5.2.4 Kujitetea, kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa ama kuchukuliwa hatua za kinidhamu kichama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom