Spika Makinda achezea Kibano - Bungeni Live!

Yameibuka malumbano mengine, wahojiwe kwa lugha gani, Kiswahili au Kiingereza.
Kiingereza kimepita, hebu tuwasikie wabunge wetu wakimwanga ung'eng'e, sijua kama Prof. Maji Marefu (Stand 7).
 
Spika Makinda ameshindwa kabisa kazi...Masikini Anna!
Anambembeleza Wenje,
Wenje anawithdraw neno Dark Market na kusema White Market.
Mbunge kaomba kutoa hoja, Spika kagoma kasema kutoa hoja
Uchaguzi uendelee.
wasioitakia nchi hii mema watasema unatania lakini ameshindwa, tunamkumbuka mzee 6 angalau. Nimeona kipindi kabla ya huo uchaguzi akitoa tangazo ...juu ya mbunge aliyesahau miwani yake ofisini kwa katibu wa bunge aende mezani kwake akaichukue!
 
Nikimuona Makinda kwenye kiti hamu ya kufuatilia yanayojiri mjengoni huyeyuka. Afadhali ya Ndugai mara mia.
Kama anavinjari kwenye hili jamvi basi namuomba Ana Makinda kwa heshima na taadhima aombe kujiuzulu nafasi hiyo. Hilo litakuwa jambo jema sana amewafanyia watz na historia haitamsahau.

Kwa kutumia msamiati wao: Wabunge wa CCM wajivue gamba kwa kupiga kura ya no confidence kwa Spika Annayo Makinda
 
Mgombea Mary Mwanjelwa ajitambulisha kama Dr. Mhe. Tundu Lissu amtaka kuuthibitisha udakitari wake, akiri kumbe ni wa heshima tuu!-aibu!
 
Sasa walimu wa UDOM watapata dili kufundisha English course hao wabunge kwani wngi lugha hiyo ni mama mkwe.
 
hahahahahaha ndio watambue ubunge si wa kukimbilia bila kuweka resume vema. Poor National Assembly
 
Mgombea Mary Mwanjelwa ajitambulisha kama Dr. Mhe. Tundu Lissu amtaka kuuthibitisha udakitari wake, akiri kumbe ni wa heshima tuu!-aibu!

Hapo kwenye red - 'Like father like children'. Baba yao JK anapenda sana kuitwa Dr? Hivi amefikisha doctorate pipi ngapi?
 
Yameibuka malumbano mengine, wahojiwe kwa lugha gani, Kiswahili au Kiingereza.
Kiingereza kimepita, hebu tuwasikie wabunge wetu wakimwanga ung'eng'e, sijua kama Prof. Maji Marefu (Stand 7).
Kama Mtanzania naona aibu wabunge kukubaliana kutumia Kiingereza bugeni badala ya Kiswahili. Uamuzi huu ni hatua 10 nyuma kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya Taifa kweli.
 
Back
Top Bottom