Spika apata wageni toka Malawi!

Suluisho ni kuwa na serikali nne. Ya zanzibar, tanganyika, malawi, na ya muungano - TAZAMA
 
Tanzania tukiingia vitani Malawi itakuwa koloni letu. Malawi nikuichapa kwa siku saba tu.Halafu hata walie hatuwapi uhuru si wameyataka wenyewe. Kiherehere chao cha kujitanua kitawaponza. Hebu nawazidishe chokochoko tuifute nchi inayoitwa Malawi au Nyasa na iwe mkoa wa Tanzania.
Vita inaambatana na uchumi wa nchi kwanza tuangalie uchumi wetu unaruhusu kuingia vitani?Tusiseme kama tuandakika mistari ya bongofleva.athari ya vita ya Uganda ki-uchmi tunaiona hadi leo.
 
Tanzania tukiingia vitani Malawi itakuwa koloni letu. Malawi nikuichapa kwa siku saba tu.Halafu hata walie hatuwapi uhuru si wameyataka wenyewe. Kiherehere chao cha kujitanua kitawaponza. Hebu nawazidishe chokochoko tuifute nchi inayoitwa Malawi au Nyasa na iwe mkoa wa Tanzania.

Kwa uchumi upi tulionao??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Tanzania tukiingia vitani Malawi itakuwa koloni letu. Malawi nikuichapa kwa siku saba tu.Halafu hata walie hatuwapi uhuru si wameyataka wenyewe. Kiherehere chao cha kujitanua kitawaponza. Hebu nawazidishe chokochoko tuifute nchi inayoitwa Malawi au Nyasa na iwe mkoa wa Tanzania.
Yes, kama tulivyochukua unguja na pemba.
 
Wadau punde spika Anna Makinda ametambulisha wageni toka Malawi akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Malawi.

Je inawezekana ni mwanzo mzuri wa mazungumzo baada ya vile vitisho vya ziwa Nyasa au ndo kuzidi kwa mkorogano wa viongozi wetu katika kuiuza nchi yetu?

Wasiwasi wangu ni kwamba huyo naibu spika wa bunge la malawi atakuwa amekuja kushuhudia reaction ya watanzania baada ya wao kutamka bayana kwamba ziwa nyasa ni lao lote.
Kwa kutambua kwamba leo ministry of Foreign affairs wanafanya presentation ya budget yao basi wakaona waje kushuhudia kwa macho yao msimamo wa nchi ya Tanzania na wananchi wake kupitia chombo chetu cha bunge.

Sasa kama wabunge wetu wasipoonyesha kwa dhati kwamba hawawezi kuruhusu kamwe uchokozi wa aina yoyote kutoka kwa malawi, na wakaendelea kutema mipasho bungeni, basi atarudi kwao na kuwaambia waendelee na uytafiti wao kama kawaida.
 
Sisi hatuna na hatujawahi kuwa na urafiki na malawi huyu mama wa malawi antaka kujaribu kila kitu hata sumu anataka kuionja! Yeye kama hajui umuhimu wa ardhi ya Tanzania ni lazima sasa tumuoneshe kuwa yeye ni kilaza wa siasa za kimataifa
 
Wadau punde spika Anna Makinda ametambulisha wageni toka Malawi akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Malawi.

Je inawezekana ni mwanzo mzuri wa mazungumzo baada ya vile vitisho vya ziwa Nyasa au ndo kuzidi kwa mkorogano wa viongozi wetu katika kuiuza nchi yetu?

Ni mwanzo mzuri! mambo mazuri hayati haraka watanzania

Wasiwasi wangu ni kwamba huyo naibu spika wa bunge la malawi atakuwa amekuja kushuhudia reaction ya watanzania baada ya wao kutamka bayana kwamba ziwa nyasa ni lao lote.
Kwa kutambua kwamba leo ministry of Foreign affairs wanafanya presentation ya budget yao basi wakaona waje kushuhudia kwa macho yao msimamo wa nchi ya Tanzania na wananchi wake kupitia chombo chetu cha bunge.

Sasa kama wabunge wetu wasipoonyesha kwa dhati kwamba hawawezi kuruhusu kamwe uchokozi wa aina yoyote kutoka kwa malawi, na wakaendelea kutema mipasho bungeni, basi atarudi kwao na kuwaambia waendelee na uytafiti wao kama kawaida.
mkuu heshima yako.
tahadhari mkuu, vita ya kuusaka urais ndani ya CCM ni mbaya sana, hata huyu mheshimiwa sana Membe huenda analake jambo. bwanawe, nimejikuta nahusisha tukio la hawa wageni toka malawi na hotuba ya Membe na urais 2015. usiniulize kivip, teh teh!
 
Tanzania tukiingia vitani Malawi itakuwa koloni letu. Malawi nikuichapa kwa siku saba tu.Halafu hata walie hatuwapi uhuru si wameyataka wenyewe. Kiherehere chao cha kujitanua kitawaponza. Hebu nawazidishe chokochoko tuifute nchi inayoitwa Malawi au Nyasa na iwe mkoa wa Tanzania.

Kama tutakavyowafanya waZenji wakileta za kuleta, tena Zenji tutaigawa vipande vipande, vingine vitakuwa wilaya za mikoa wa Mafia, Kinondoni, Bagamoyo, Tanga na Kilimanjaro
 
Soon ntakuwa wa Malawi mie.....

Labda Mwanangu pia atakuwa adopted na Mwimbaji Madonna....

Malawi njooni haraka basi.......................

madonna-malawi-school.jpg
 
Wimbo wa miss tanzania wa solo thang ni jibu tosha ya haya yanayoendelea.

Nimeupenda sana huo wimbo..ngoja niweke mashairi yake hapa wadau msome:
MISS TANZANIA-SOLO THANG
"[Ubeti wa Kwanza]
Baba yake alikuwa mkoloni kipindi huyu Miss mwali
Mchonga alikata utepe lakini hakuvinjari
Sababu alikua busy kumlinda na geti kali
Kumbe wenzake wanabinjuka, kushtuka akakaa mbali
Demu alikua na heshima kabla haijatangazwa Rukhsa
Chukua Chako Mapema ukimkonyeza tu umegusa
Ana kifua kimebetuka sio maziwa ni madini
Kayaacha wazi, watu wanashika hapo ndio anaponiudhi mimi
Watu wanagonga tu Ikulu tena kwa mitindo huru
Kavu kavu bila kinga hajali vinavyodhuru
Kawa shangingi na amedata hana uwoga wa kunguru
Anapenda sana chapaa haimtoshi kodi na ushuru
Ana kijungu matata laini kama nyanya masalo
Anatingisha Afrika nzima na mzigo Kilimanjaro
Usimchezee kwa vidani sio pete sio hereni
Anamiliki tanzanite kama ardhi ya Mererani
Sura dhahabu inaita kama amezaliwa Geita
Tatizo ndio kicheche kila mwanaume ndio amepita
Hata Benja hakutoka Kapa huyu demu hajatulia
Kama rushwa ndio kikwapa ananuka na kunukia
[Kiitikio]
Miss Tanzania
Nakupenda ila hujatuliaa
Vitendo vyako sitojivunia
Sifa yako kubwa umefulia
Miss Tanzania
[Ubeti wa Pili]
Bora angebaki kuwa modo kama Flavian Matata
Ila demu amejiachia kisa anaendekeza bata
Sitachoka kuwakilisha jinsi anavyoniacha hoi
Juzi juzi kaopolewa na Handsome Boy
Kabla hapo shoga zake wote kashawaona mabwege
Sababu hawana dira na yeye ameshahongwa ndege
Anafaa kuwa Miss Dunia maandalizi longolongo
Tatizo anakula sana akijamba ni Songosongo
Mara ghafla kanenepa kumbe mimba B.O.T.
Kumbe demu aligawa EPA watu wamepiga hafu jii
Alizugwa na akaunti hewa kuwadi Bwana Bilal
Mara mdomo naye kazimwa bila hata picha ya kaburi
Kinachomponza huyu shawty utulivu sifuri
Ila hakuna anayepinga kwamba huyu demu ni mzuri
Mixer siasa na biashara demu ameshakuwa chotara
Mishe za Dar akimaliza Mjengoni anakwenda lala
Kadri miaka inavyokwenda demu anazidi fulia
Kumbe weupe ni mkorogo ona mwili sasa umefifia
Demu kazidi umalaya wacha mabwana wamteme
Haogopi kuliwa mtungo kisa anagawa umeme
[Kiitikio]
[Ubeti wa Tatu]
Wadaku walishamfuma anakula denda na Richmond
Dowans akazidi kete akamvisha pete ya diamond
Binti masikini akanasa bwana mshenga ndio Lowasa
Shemeji hataki hata picha ndio tabia gani sasa
Ndoa ilifungwa kwa vifijo vigogo wakala pizza
Keki nzima wale wao share yetu si ni giza
Sio hayo demu ana mengi ya kuchukiza
Malighafi ashazinadi for sale anajiuza
Mtaani ilivuma rumor demu kawa mama huruma
Uchumi umefungwa drip maendeleo ndio kali homa
Mali asili ndio kitasa kila ufunguo ndio unapita
Toka alipovunja ungo nusu karne imeshapita
Mapenzi kafanya mradi anamegwa na mafisadi
Amani kwa time bomb binti amekumbatia radi
Vitendo vyake vibaya vinafanya adharaulike
Tabia Katiba sio Msahafu ndio useme isibadilike
Mikosi inayomkuta ndio kwanza anatabasamu
Hajali waliomzunguka kama nao binaadamu
Mbagala walimbaka mpaka akamwaga damu
Na juzi Gongo la Mboto kaanza kujamba mabomu
[Kiitikio]"
 
Hv, wewe umemaliza hata la saba, mbona uko nje ya mada kabisa. JF ni mtandao wa wajinga wengi wanazungumza bila mpangilio.
Kwa jinsi wanauza kila kitu huku ndani ya nchi hata visivyohamishika wanauza na vinahamishwa, wamalawi watakuwa wako sahihi. Walishauziwa sasa wanataka eneo lao walilokwisha uziwa.

Sidhani kama malawi hawaelewi, wanaelewa mipaka kila kitu suala ni kwamba walishauziwa na hawa kina Mkapa, J. K na team zao.
 
Samahani pamoja na mahaba yangu na TANGANYIKA lakini sio kweli kwamba UN inasema mipaka ya nchi inapokutana na ziwa basi kila nchi imiliki nusu ya eneo husika.

Kama ingekwa hivyo, mbona Tangayika tunamiliki > 60% ya LAKE VICTORIA na < 40% inayobaki ndiyo inamilikiwa kwa pamoja na Kenya na Uganda?!
Ni kwa sababu tuna mpaka mpana zaidi na ziwa hilo kuliko nchi yoyote miongoni mwetu. Kwa hiyo hata umiliki wetu utakuwa mkubwa. Umeelewa?
 
Mi naona ingefaa kama wangeuza ikulu yaani pango la wala rushwa. Maana maamuzi yote ya kipuuzi yanatoka mle. Wameshindwa kukanusha kuwa hata watekaji wa Ulimboka walitoka mle. Badala yake wanafungia magazeti. Kama wana ubavu waje waifunge JF waone walichoona akina Gaddafi.
 
Kama tutakavyowafanya waZenji wakileta za kuleta, tena Zenji tutaigawa vipande vipande, vingine vitakuwa wilaya za mikoa wa Mafia, Kinondoni, Bagamoyo, Tanga na Kilimanjaro

Tanzania tukiingia vitani Malawi itakuwa koloni letu. Malawi nikuichapa kwa siku saba tu.Halafu hata walie hatuwapi uhuru si wameyataka wenyewe. Kiherehere chao cha kujitanua kitawaponza. Hebu nawazidishe chokochoko tuifute nchi inayoitwa Malawi au Nyasa na iwe mkoa wa Tanzania.

Acheni unazi wa kijinga usio na tija nyinyi! mnavijua vita au mnavisikia? Hivi hizo bangi huwa mnachanganya na gongo la...au.....? Muwapige wamalawi kwa sababu zipi? kuhoji mipaka waliyoachiwa kisheria na wakoloni sawa na sisi tulivyoachiwa? Ukweli ni kwamba katika mzozo wa Malawi nchi zote ziko sahihi na kinachotakiwa ni busara hata kidogo tu, yaani kuvuta viti, kukaa pamoja na kuelewana mbele ya mashuhuda (AU/UN); na hili la Zanzibar limetokea wapi? wamefanya nini hadi muwagawe vipande vipande? Kwani ni koloni la Tanganyika lile? Zanzibar ni taifa huru lililoridhia kwa hiyari yake kuungana na taifa jingine kwa maslahi ya nchi mbili. Wana uwezo wa kuamua kujitoa kama walivyoamua kujiunga na sisi. Licha ya kuwa na eneo dogo na watu wachache; wanasimama kama taifa lenye hadhi sawa na Tanganyika, Kenya, Marekani au nchi yoyote unayoifahamu na kwa taarifa zenu walevi wa namna hiyo Zanzibar si taifa dogo sana kiasi hicho kwani kuna nchi zina watu elfu kumi na zina hadhi sawasawa na Marekani na Uingereza! Sasa sina shaka kwamba chokochoko baina ya pande hizi mbili mara nyingi huchochewa na walevi msiojua kabisa athari za vita. Kelele za namna hii zikikutana na watu wa aina yenu kule ndiyo yanatokea yanayotokea! Mungu ibariki Tanzania, dumisha amani na umoja!
 
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika, Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, nisaidie kwa jambo hili kwanza, hivi Uamsho ni nani nchi hii, je nao pia wanaimba Mungu Ibariki Tanzania, Dumisha Uhuru na Umoja.....Tanzania na watu wake, je uamsho nao huwa wanaimba wimbo huu kwa kusisimka? Makanisa yaliyounguzwa huko zenj ni kwa ajili ya nini, Pili umoja ni nguvu na utengano ni uzaifu kwa kuna ubaya gani, kuwa na taifa moja - mbona wilaya za Iringa zimepelekwa Njombe, vijiji na wilaya za mwanza na kagera vimekuwa Geita, kwa nini Zenji isiwezekane, maana ni umoja huo huo?

Back
Top Bottom