Bernard Kamilius Membe niliyemfahamu, Taifa limepoteza mtu!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Bernard Kamilius Membe Waziri wa zamani wa Mashauri ya Kigeni nchini Tanzania, Mwanachama wa chama cha Mapinduzi, na mhudumu wa hadhi ya juu wa Idara ya Usalama wa taifa na "nusu" padre ambae taifa la Tanzania na ulimwengu wa kijasusi utaendelea kumkumbuka daima.

Historia ya Membe inaanzia mbali kidogo toka kusini mwa Tanzania katika kijiji cha Rondo hadi mikono salama ya useminari, chini ya ukasisi wa Namupa Seminari. Bernard Kamilius Membe kijana wa kati mwenye uso angavu akiketi dawati la Tatu kutoka kulia, alikuwa mtoto mwenye akili isiyo ya kawaida akiwa mbele ya watoto wenye vipaji shuleni hapo, Kasisi Mariano anamueleza Bernard kama kijana wa mfano kwa nyakati hizo ambaei hakuwa wakusimamiwa kila jambo,

Hayo ni ya Namupa Seminari, lakini sifa zake zinazidi hadi alipojiunga na shule ya upadre kule Itaga Seminari katika mapito yake kielimu, Kanisa katoliki Useminari wa Itaga wanajiuliza hadi leo ilikuwaje kijana huyu mtawa akaacha utume wa upadre na akaibukia ofisi ya rais tena kitengo nyeti cha kuchakata marundo ya taarifa za nchi toka kila pande ya nchi.

Bernard Membe kutoka Darasa la awali hadi High School yani upadre, hakuna mahali panapotaja mapungufu yake kiakili darasani wala hakuna tukio lolote la utovu wa nidhamu la kukumbukwa, iwe katika mitiahani, michezo, uongozi shuleni ama sifa yoyote mbaya toka kwa wakufunzi wake. Pengine hii ndio sifa kuu iliyompendeza Mkuu wa majasusi Tanzania kumchukua. Kwaujumla alikuwa ni mwanafunzi wa vipaji maalumu kwa mtazamo wa kikatoliki kabisa ambae kanisa lilimtarajia kumtawaza kama padre wake,

Mwaka 1978 Membe aliingia kwenye ajira rasmi ya serikali akihudumu Ofisi ya Rais Idara ya Usalama wa Taifa kitengo cha uchambuzi wa taarifa za kijasusi, Kazi hiyo amehudumu kwa miaka kumi na mbili tu hadi 1989 na kisha akaenda masomoni katika chuo cha Johns Hopkins Marekani, alikosomea Diplomasia katika Uhusiano wa Kimataifa kutoka 1990 hadi 1992 akarejea nchini na akahamishiwa Wizara ya Mashauri ya Kigeni na kwenda Ottawa Canada kuwa mshauri wa Kibalozi kutoka 1992-2000,

Korido za Ujasusi zinaeleza kuwa, Utumishi wake ndani ya Idara ya Usalama ulikuwa wa kutukuka na ameacha kumbukumbu yake nzuri hasa katika medani ya Ujasusi unaovuka mipaka, mfano akiwa masomoni Johns Hopkins, alikuwa ni mmoja ya maafisa waliofanya vizuri katika masomo ya vitendo yaliyofanyikia London katika idara ya Ujasusi ya Scotland Yard (Polisi ya Uingereza) na kupewa tuzo maalumu ya Banquets ikitolewa na the greater wa Scotland Yard Sir Kenneth Newman. Nje ya Diplomasia, Membe alichukua kozi muhimu ya Forensic Criminology.

Mwaka 2000 aliingia kwenye siasa akawa Mbunge wa Jimbo la Mtama, nakisha tarehe 17/10/2006 hadi 1/11/2007 aliteuliwa kuwa naibu Waziri wa Nishati na Madini, na kisha 1/12/2007 mpaka 2015 akawa Waziri kamili wa Mashauri ya Kigeni. Katika kipiti cha utmishi wa Bernard Membe ndani ya Wizara taifa lilipitia migogoro mikubwa ya Kidiplomasia na mataifa ya kigeni na yeye kwa nafasi yake alitatua, Mathalani Mgogoro na Malawi wa Ziwa Nyasa, Mgogoro na Rwanda, Mgogoro na Kenya, Mgorogoro na Uingeraza, Mgogoro na ummoja wa nchi wa Hisani wa Maendeleo za Ulaya, mgogoro wa Comoro, Afrika Magharibi nk. Haya yote yalitukia katika uongozi wa Bernard Membe katika Wizara namba mbili ya kidiplomasia inayohusika na mashauri ya Kigeni.

Baada ya kustafu utumishi, Membe alifanya kazi binafsi za ushauri wa kiusalama Nchini Uturuki kwa rafiki yake mkubwa Recep Tayyip Erdoğan Rais wa Uturuki, Nchini Zimbabwe kwa rafiki yake mkubwa Jenerali Mnanagwa rais wa Zimbabwe, nchini Malta kwa rafiki yake mkubwa Joseph Muscat Waziri mkuu wa zamani wa Malta nk. Lakini kubwa zaidi, Bernard Membe, ndie mwanaccm pekee ambae hakumuogopa Rais Magufuli pamoja na utawala wake wote wa mkono wa chuma, alimpinga hadharani hadi kufukuzwa ndani ya ccm, kwakusimamia msimamo wa haki ya kisiasa ndani ya ccm. Baada ya Magufuli kufariki na Rais Samia kushika madaraka, Membe alirejea CCM kwa uchangamfu uleule bila kutetereka .

Tumuenzi Membe kwa ujasiri na uthubutu wake, Tumuenzi kwa malezi yake mema kwa vijana, Vijana wengi wamepita katika mikono ya Membe, amelala akijivunia kulea na kukuza vijana ambao sasa wanalitumikia taifa kwa weledi mkubwa.

Nina msiba mzito, Nina historia ndefu na Hayati Membe, tutasimuliana kadiri Mizimu ikinijaalia...! Pumzika kwa amani Bernard Membe

Na Yericko Nyerere.

FB_IMG_1683912065012.jpg
 
Hahahaa leo mtatuzajia uongo wa kutosha ilimradi kumtakasa

Lini aliwahi kuwa karibu na erdogan mshauri binafsi wa mambo ya kiusalama uturuki waijua kweli ndugu mwandishi? Anyway

Wema hawafi

Mungu kaamulia ugomvi na musiba na kwa sasa kwa upande wa sukuma gang naweza sema bahari imeanza kutulia
 
Baada ya kustafu utumishi, Membe alifanya kazi binafsi za ushauri wa kiusalama Nchini Uturuki kwa rafiki yake mkubwa Recep Tayyip Erdoğan Rais wa Uturuki, Nchini Zimbabwe kwa rafiki yake mkubwa Jenerali Mnanagwa rais wa Zimbabwe, nchini Malta kwa rafiki yake mkubwa Joseph Muscat Waziri mkuu wa zamani wa Malta nk

View attachment 2619873
Kumbe unaeongea ni yeriko nyerere....Ningekuuliza maswali ila naona hautokua na majibu sahii mdogo wangu,,,,,,ila kwa kifupi ni kwamba kila mwamba ngoma huvutia kwake
 
Nyie si ndo mmeandika na kitabu cha kumchafua Maghufuli....!! Tunawatamani Sana
 
Hahahaa leo mtatuzajia uongo wa kutosha ilimradi kumtakasa

Lini aliwahi kuwa karibu na erdogan mshauri binafsi wa mambo ya kiusalama uturuki waijua kweli ndugu mwandishi? Anyway

Wema hawafi

Mungu kaamulia ugomvi na musiba na kwa sasa kwa upande wa sukuma gang naweza sema bahari imeanza kutulia
Mambo ya usalama wa nchi yoyote ni mazito ati "rafiki wa karibu kwenye mambo ya usalama wa nchi husika"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bernard Kamilius Membe Waziri wa zamani wa Mashauri ya Kigeni nchini Tanzania, Mwanachama wa chama cha Mapinduzi, na mhudumu wa hadhi ya juu wa Idara ya Usalama wa taifa na "nusu" padre ambae taifa la Tanzania na ulimwengu wa kijasusi utaendelea kumkumbuka daima.

Historia ya Membe inaanzia mbali kidogo toka kusini mwa Tanzania katika kijiji cha Rondo hadi mikono salama ya useminari, chini ya ukasisi wa Namupa Seminari. Bernard Kamilius Membe kijana wa kati mwenye uso angavu akiketi dawati la Tatu kutoka kulia, alikuwa mtoto mwenye akili isiyo ya kawaida akiwa mbele ya watoto wenye vipaji shuleni hapo, Kasisi Mariano anamueleza Bernard kama kijana wa mfano kwa nyakati hizo ambaei hakuwa wakusimamiwa kila jambo,

Hayo ni ya Namupa Seminari, lakini sifa zake zinazidi hadi alipojiunga na shule ya upadre kule Itaga Seminari katika mapito yake kielimu, Kanisa katoliki Useminari wa Itaga wanajiuliza hadi leo ilikuwaje kijana huyu mtawa akaacha utume wa upadre na akaibukia ofisi ya rais tena kitengo nyeti cha kuchakata marundo ya taarifa za nchi toka kila pande ya nchi.

Bernard Membe kutoka Darasa la awali hadi High School yani upadre, hakuna mahali panapotaja mapungufu yake kiakili darasani wala hakuna tukio lolote la utovu wa nidhamu la kukumbukwa, iwe katika mitiahani, michezo, uongozi shuleni ama sifa yoyote mbaya toka kwa wakufunzi wake. Pengine hii ndio sifa kuu iliyompendeza Mkuu wa majasusi Tanzania kumchukua. Kwaujumla alikuwa ni mwanafunzi wa vipaji maalumu kwa mtazamo wa kikatoliki kabisa ambae kanisa lilimtarajia kumtawaza kama padre wake,

Mwaka 1978 Membe aliingia kwenye ajira rasmi ya serikali akihudumu Ofisi ya Rais Idara ya Usalama wa Taifa kitengo cha uchambuzi wa taarifa za kijasusi, Kazi hiyo amehudumu kwa miaka kumi na mbili tu hadi 1989 na kisha akaenda masomoni katika chuo cha Johns Hopkins Marekani, alikosomea Diplomasia katika Uhusiano wa Kimataifa kutoka 1990 hadi 1992 akarejea nchini na akahamishiwa Wizara ya Mashauri ya Kigeni na kwenda Ottawa Canada kuwa mshauri wa Kibalozi kutoka 1992-2000,

Korido za Ujasusi zinaeleza kuwa, Utumishi wake ndani ya Idara ya Usalama ulikuwa wa kutukuka na ameacha kumbukumbu yake nzuri hasa katika medani ya Ujasusi unaovuka mipaka, mfano akiwa masomoni Johns Hopkins, alikuwa ni mmoja ya maafisa waliofanya vizuri katika masomo ya vitendo yaliyofanyikia London katika idara ya Ujasusi ya Scotland Yard (Polisi ya Uingereza) na kupewa tuzo maalumu ya Banquets ikitolewa na the greater wa Scotland Yard Sir Kenneth Newman. Nje ya Diplomasia, Membe alichukua kozi muhimu ya Forensic Criminology.

Mwaka 2000 aliingia kwenye siasa akawa Mbunge wa Jimbo la Mtama, nakisha tarehe 17/10/2006 hadi 1/11/2007 aliteuliwa kuwa naibu Waziri wa Nishati na Madini, na kisha 1/12/2007 mpaka 2015 akawa Waziri kamili wa Mashauri ya Kigeni. Katika kipiti cha utmishi wa Bernard Membe ndani ya Wizara taifa lilipitia migogoro mikubwa ya Kidiplomasia na mataifa ya kigeni na yeye kwa nafasi yake alitatua, Mathalani Mgogoro na Malawi wa Ziwa Nyasa, Mgogoro na Rwanda, Mgogoro na Kenya, Mgorogoro na Uingeraza, Mgogoro na ummoja wa nchi wa Hisani wa Maendeleo za Ulaya, mgogoro wa Comoro, Afrika Magharibi nk. Haya yote yalitukia katika uongozi wa Bernard Membe katika Wizara namba mbili ya kidiplomasia inayohusika na mashauri ya Kigeni.

Baada ya kustafu utumishi, Membe alifanya kazi binafsi za ushauri wa kiusalama Nchini Uturuki kwa rafiki yake mkubwa Recep Tayyip Erdoğan Rais wa Uturuki, Nchini Zimbabwe kwa rafiki yake mkubwa Jenerali Mnanagwa rais wa Zimbabwe, nchini Malta kwa rafiki yake mkubwa Joseph Muscat Waziri mkuu wa zamani wa Malta nk. Lakini kubwa zaidi, Bernard Membe, ndie mwanaccm pekee ambae hakumuogopa Rais Magufuli pamoja na utawala wake wote wa mkono wa chuma, alimpinga hadharani hadi kufukuzwa ndani ya ccm, kwakusimamia msimamo wa haki ya kisiasa ndani ya ccm. Baada ya Magufuli kufariki na Rais Samia kushika madaraka, Membe alirejea CCM kwa uchangamfu uleule bila kutetereka .

Tumuenzi Membe kwa ujasiri na uthubutu wake, Tumuenzi kwa malezi yake mema kwa vijana, Vijana wengi wamepita katika mikono ya Membe, amelala akijivunia kulea na kukuza vijana ambao sasa wanalitumikia taifa kwa weledi mkubwa.

Nina msiba mzito, Nina historia ndefu na Hayati Membe, tutasimuliana kadiri Mizimu ikinijaalia...! Pumzika kwa amani Bernard Membe

Na Yericko Nyerere.

View attachment 2619873
Watoto wa kishua mna tabu sana,,tofauti na sie wa keko magurumbasi wakati ule babu yako kapiga marufuku nguo za mitumba ila yeye anavaa vitu high quality...
 
Ujinga tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom