Spika apata wageni toka Malawi!

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,829
8,619
Wadau punde spika Anna Makinda ametambulisha wageni toka Malawi akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Malawi.

Je inawezekana ni mwanzo mzuri wa mazungumzo baada ya vile vitisho vya ziwa Nyasa au ndo kuzidi kwa mkorogano wa viongozi wetu katika kuiuza nchi yetu?

Membe anapiga marufuku kuanzia leo shughuli zote za utafiti katika maeneo yalio ndani ya mipaka ya Tanzania.

huenda kama serikali ni ishara hawakufurahishwa na kauli ya mmoja wa mawaziri wake wakati "mazungumzo" yakiendelea. tumsikie Membe anasemaje
 
Tanzania tukiingia vitani Malawi itakuwa koloni letu. Malawi nikuichapa kwa siku saba tu.Halafu hata walie hatuwapi uhuru si wameyataka wenyewe. Kiherehere chao cha kujitanua kitawaponza. Hebu nawazidishe chokochoko tuifute nchi inayoitwa Malawi au Nyasa na iwe mkoa wa Tanzania.
 
Wimbo wa miss tanzania wa solo thang ni jibu tosha ya haya yanayoendelea.
 
walete zao waone kichapo chake na hivi tumegundua gesi marekani watajipendekeza kutupa ile mioto isiyokuwa na rubani.
 
Sijasikia kauli ya Membe wala braza wake J.k,Inawezekana wameuza ziwa hawa mana wanapenda pesa
 
Wadau punde spika anna makinda ametambulisha wageni toka malawi akiwemo naibu spika wa bunge la malawi.
je inawezekana ni mwanzo mzuri wa mazungumzo baada ya vile vitisho vya ziwa Nyasa au ndo kuzidi kwa mkorogano wa viongozi wetu katika kuiuza nchi yetu?
Si wamalawi wote wenye msimamo mkali juu ya umiliki wa ziwa hilo, ukisoma magazeti yao na maoni ya wananchi utagundua wapo wanaopendekeza mazungumzo na wapo pia wanaotambua mtafaruku uliopo baina ya mipaka tuliyorithishwa na wakoloni na uamuzi wa Baraza la usalama la UN linalosema wazi wazi kwamba mipaka baina ya nchi inapokutana kwenye ziwa, kila nchi itakuwa na haki ya kumiliki nusu ya eneo husika. Wapo wamalawi werevu na wapo pia wajinga kama ilivyo huku kwetu. Sote tu ndugu, hakuna haja ya kugombana maana wabaya wetu ni umasikini, ujinga na maradhi.
 
Leo ndiyo WIZARA YA MAMBO YA NCHI ZA NJE inasoma budget yake.

Hii ni nafasi adhimu kwa WABUNGE wetu leo, kutoa UJUMBE kwa SERIKALI YA MALAWI kuwa mpaka ni katika ya Ziwa Nyasa and is NOT NEGOTIABLE. Tuko tayari kuingia VITANI na Malawi. Hata DHAIFU Spika akiwaomba wabunge waondoe hizo kauli lakini message itakuwa tayari delivered kwa Joyce Banda.

Huyo Naibu Spika wa Malawi amekuja kupima UPEPO apewe vidonge vyake LAIVU.
 
Huo ni ujumbe wa serikali ya Malawi kujakujua je Serikali itasema..nini na sasa membe anasema kuhusu malawi!
 
Si wamalawi wote wenye msimamo mkali juu ya umiliki wa ziwa hilo, ukisoma magazeti yao na maoni ya wananchi utagundua wapo wanaopendekeza mazungumzo na wapo pia wanaotambua mtafaruku uliopo baina ya mipaka tuliyorithishwa na wakoloni na uamuzi wa Baraza la usalama la UN linalosema wazi wazi kwamba mipaka baina ya nchi inapokutana kwenye ziwa, kila nchi itakuwa na haki ya kumiliki nusu ya eneo husika. Wapo wamalawi werevu na wapo pia wajinga kama ilivyo huku kwetu. Sote tu ndugu, hakuna haja ya kugombana maana wabaya wetu ni umasikini, ujinga na maradhi.

Samahani pamoja na mahaba yangu na TANGANYIKA lakini sio kweli kwamba UN inasema mipaka ya nchi inapokutana na ziwa basi kila nchi imiliki nusu ya eneo husika.

Kama ingekwa hivyo, mbona Tangayika tunamiliki > 60% ya LAKE VICTORIA na < 40% inayobaki ndiyo inamilikiwa kwa pamoja na Kenya na Uganda?!
 
Bunge sio kamati teule katika mazungumzo ya mpaka lakini itakuwa busara kama Mama Anne na Naibu spika huyo watagusia hali tete ya mpaka kama wadau wa nchi hizi mbili. Mvutano wa mpaka kwa sasa ni jambo lililo wazi.
 
Membe anapiga marufuku kuanzia leo shughuli zote za utafiti katika maeneo yalio ndani ya mipaka ya Tanzania.
 
Wadau punde spika Anna Makinda ametambulisha wageni toka Malawi akiwemo Naibu Spika wa Bunge la Malawi.

Je inawezekana ni mwanzo mzuri wa mazungumzo baada ya vile vitisho vya ziwa Nyasa au ndo kuzidi kwa mkorogano wa viongozi wetu katika kuiuza nchi yetu?

Kwa serikali hii dhaifu majibu yote mawili yanaweza kuwa sahihi.
kama ni a) yaani mwanzo mzuri basi Mugu amekaa upande wetu
kama ni b) yaani viongozi kuuza nchi- usishangae maana hawa wanaweza kuuza mama na watoto zao ili wapewe kitu kidogo. Hebu fikiria mukuu wa kaya anavyo fisadi njia kuu zote za uchumi wa nchi hii na kuwatetea mafisadi atashindwa nini kutuchuuza?
 
tukizipiga sijui nitakuwa upande gani?babu zangu na ndugu kibao ni wamalawi.............ee mungu tuepushe na hii kadhia............
 
Mwanzo mzuri ingekuwa ni kufanya mazoezi ya kijeshi ya kufa mtu mkoa wa Ruvuma kwenye maeneo ya Mbamba Bay na amiri jeshi mkuu aseme wazi, kabla ya mazungumzo, kuwa "options" zote zinafanyiwa kazi. Wakati mwingine ili mazungumzo yafanikiwe yanahitaji motisha kidogo.
 
Kwa jinsi wanauza kila kitu huku ndani ya nchi hata visivyohamishika wanauza na vinahamishwa, wamalawi watakuwa wako sahihi. Walishauziwa sasa wanataka eneo lao walilokwisha uziwa.

Sidhani kama malawi hawaelewi, wanaelewa mipaka kila kitu suala ni kwamba walishauziwa na hawa kina Mkapa, J. K na team zao.
 
Back
Top Bottom