Spika amtwisha Zitto Kabwe zigo la UDA

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
SAKATA la kuuzwa kwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) limezidi kugonganisha vichwa vya mamlaka mbalimbali, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhamisha mchakato wa uchunguzi huo kutoka Kamati ya aweli na kumtwisha jukumu hilo Zito Kabwe.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

9/08/2011

BUNGE KUCHUNGUZA UFISADI UDA

Ndugu Wanahabari, Suala la Ubinafsishaji wa Shirika la UDA limeibua hisia kali miongoni mwa Wabunge, vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla. Suala hili limekuwa tata na kuzusha kila aina ya maneno. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma imeona ipo haja ya msingi ya suala hili kuchunguzwa kwa kina na mhimili wa Bunge.

Kwa hiyo, imemuandikia barua Spika wa Bunge, ikimuomba aridhie mapendekezo ya wabunge watakaoundakamati ndogo ya Bunge chini ya Kamati hii ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, ili ichunguze sakata zima la uuzwaji wa Shirika la UDA.
Uchunguzi huu umependekezwa kufuatia hisia kwamba taratibu za kuuza Shirika hili pamoja na mali zake hazikuzingatia Sheria za nchi na hivyo kupelekea Taifa kuwa katika hatari ya kupoteza mali.

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Toleo la mwaka 2007, nyongeza ya sita kifungu cha 13(e), Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ina jukumu la kufuatilia ‘Utekelezaji wa Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma' na kanuni ya 13(d) ‘kufanya tathmini ya ufanisi wa Mashirika ya Umma'. Ili kutekeleza majukumu haya, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma imemuomba Mhe. Spika aridhie kuundwa kwa kamati ndogo ili kufanya uchunguzi wa suala la Shirika la UDA.

Hadidu Rejea
Hadidu rejea za Kamati ndogo ya uchunguzi inayopendekezwa ni kama ifuatavyo:
1. Kuchunguza kama katika zoezi la kubinafsisha Shirika la UDA taratibu zote za Sheria zilifuatwa.
2. Kuchunguza kama Ofisi ya Msajili wa Hazina na Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) walitimiza wajibu wao ipasavyo katika zoezi zima la ubinafsishaji wa Shirika la UDA.
3. Kuchunguza kama Bodi ya Shirika la UDA ilifuata sheria na kanuni katika kuuza hisa zilizouzwa za Shirika la UDA na kama walikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo bila kuhusisha wana hisa. Pia kuchunguza nafasi ya Bodi kwa umoja wake na mjumbe mmoja mmoja wa Bodi katika zoezi zima husika.
4. Kuchunguza nafasi (role) ya wana hisa (Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali) katika zoezi zima la kuuzwa kwa hisa (unalloted shares) za UDA kwa Kampuni ya Simon Group.
5. Kuwaita mbele ya Kamati wadau wote wa suala la UDA hususani Bodi ya UDA iliyokuwepo, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UDA, Mmiliki wa Kampuni ya Simon Group ltd, Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mkuu wa CHC, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na mtu mwingine yeyote yule itakavyoonekana inafaa.
6. Kufanya tathmini ya Shirika la UDA katika mazingira ya sasa ya biashara ya usafirishaji Jijini Dar es Salaam.
7. Kutoa Mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya watakaobainika kuwa na makosa katika zoezi zima la Ubinafsishaji wa Shirika la UDA.
8. Kupendekeza namna bora ya kuendesha Shirika la UDA.
Ukomo
Kwa kuwa mamlaka nyingine za Uchunguzi zinaendelea na uchunguzi wake, Kamati hiyo ya Bunge itajikita katika maeneo yaliyoainishwa hapo juu tu na haitahusika na suala kama la rushwa au Mahesabu ambayo yanashughulikiwa na TAKUKURU na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Isipokuwa Kamati inaweza kuhitaji msaada wa Taasisi hizi katika kutimiza wajibu wake wa uchunguzi wa kibunge. Bunge, kwa namna yoyote ile, halitazuiwa kuendelea na uchunguzi wake wakati Serikali (Executive) ikitimiza wajibu wake. Izingatiwe kuwa uchunguzi huu pia unahusisha Taasisi za Serikali zenye mamlaka ya masuala ya Ubinafsishaji na utunzaji wa Mali ya Umma (hivyo Serikali pia inachunguzwa).

Muda wa Uchunguzi

Nimependekeza kuwa uchunguzi huu uchukue jumla ya Siku 14 (kumi na nne tu) na kuwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na kisha kwa Spika ambaye ataelekeza hatua zitakazofuatia.

Wajumbe wa Kamati Ndogo ya Uchunguzi.

Kwa kuwa Uchunguzi huu unahusisha mambo mengi, nimependekeza kamati hiyo ndogo ihusishe Wabunge wengine katika uchunguzi huu badala ya wajumbe wa Kamati ya Mashirika ya Umma peke yake.

Wajumbe wafuatao wanapendekezwa kuunda Kamati ndogo.
1. Mhe. Murtaza Mangungu, Kilwa Kaskazini (Kamati ya POAC) – Mwenyekiti
2. Mhe. Esther Bulaya, Viti Maalum (Kamati ya POAC)
3. Mhe. Amina Mwidau, Viti Maalumu (Kamati ya POAC)
4. Mhe. David Kafulila, Kigoma Kusini (Kamati ya LAAC)
5. Mhe. Angellah Kairuki, Viti Maalumu (Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala)
6. Mhe. Herbert Mtangi, Muheza (Kamati ya Miundombinu)
7. Mhe. John Mnyika, Ubungo (Mwakilishi Wabunge wa Dar es Salaam)
Katibu wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma na Katibu wa Kamati ya Sheria ndogo wanapendekezwa kuwa Makatibu wa Kamati ndogo ya Uchunguzi wa Ubinafsishaji wa Shirika la UDA.

Ni matarajio yangu na ya wenzangu kuwa Spika wa Bunge, Mhe.Anne Makinda ataridhia kuundwa kwa Kamati hiyo, ili Bunge liweze kuchukua wajibu wake wa kiuchunguzi na wa kuisimamia Serikali. Ninaamini, uchunguzi huo ndio utakaokata mzizi wa fitina kuhusu nani amehusika na achukuliwe hatua gani zichukuliwe kwa maslahi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Taifa zima kwa ujumla.

Nashukuru kwa kunisikiliza.

Kabwe Zuberi Zitto (Mbunge)
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma

Zitto ndo alie ibua mjadala/tuhuma juu ya UDA ndo maana amepewa zigo hilo. Mi-CCM inaogopa lawama coz ni hiyohiyo miongoni mwao ndo ilio lifisidi shirika, kwa hiyo haiwezi kuadhibiana ipaswavyo!

Hata Zitto naye tunaweza tusipate kile tunachokitegemea!! Tanzania ni nchi ya ajabu, viongozi wake bado wajabu ajabu, wananchi ndo usiseme. Tusubirini!

Ccm huwataki....chadema huwataki....na ndiko viongozi waliko, sasa wewe ungetaka vipi..mi mwenyewe ulishanchanganya sasa..au sio mtanzania? Naona sasa hizo ni chuki za nchi....

SAKATA la kuuzwa kwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) limezidi kugonganisha vichwa vya mamlaka mbalimbali, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhamisha mchakato wa uchunguzi huo kutoka Kamati ya aweli na kumtwisha jukumu hilo Zito Kabwe.

Tunaandaa maandamano ya amani jijini Washington DC Rais Kikwete atakapowasili kwenye kikao cha DICOTA 2011. Tayari watu 150 wamekubali kushiriki kwenye maandamano hayo. Tunataka watu wengi zaidi kujitokeza. Hii ni kumshinikiza huyu fisadi papa na mzururaji kushugulikia matatizo yanayowakabili wananchi wa kawaida. Maandamano yetu yatahitimishwa na kupokelewa na viongozikutoka United States Department. Tayari tumetuma maombi kupinga misaada marekani inayopa Tanzania, kwani hayasaidii Jamii bali Kikwete na genge lake la majambazi

Wote mnakaribishwa karibishwa. Maandamano ya Amani yanaruhusiwa marekani ilimradi mtu hajavunja sheria nchini. Ukiwa na makaratasi yako, njoo tulikomboe taifa letu. Ukombozi wa TANZANIA upo mikononi mwetu. Mabango yanachapishwa tarehe 24, Tunaomba mawazo tofauti kuhusu ujumbe tutakaobeba kwenye mabango yetu. Tumechoka na Kikwete, dawa nikuanza maandamano.Tupo tayari kufa sasa. Tunisia iliokolewa na watu tu kama sisi, tukifa bahati mbaya vizazi vijavyo vitafaidi. Tafadhali sambaza ujumbe. Tutatoa tamko rasmi ya maandalizi tarehe 20 mwenzi huu Ukitaka kushiriki tuma barua pepe EliakimMallya@yahoo.com

Raia wa kawaida anayo haki ya kumfanya Kikwete Anyimwe VISA. Kwa Kupinga Ujio wa Kikwete, au yeye kunyimwa VISA tumeni emails nyingi iwezekanavyo kwenda East African Affairs Bureau. Email Adress
wiegertjr@state.gov

SAKATA la kuuzwa kwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) limezidi kugonganisha vichwa vya mamlaka mbalimbali, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhamisha mchakato wa uchunguzi huo kutoka Kamati ya aweli na kumtwisha jukumu hilo Zito Kabwe.

kweli Zitto anapendwa sana na Spika

kweli Zitto anapendwa sana na Spika

Nikizingatia ni jinsia mbili tofauti, sasa anapendwaje? Je, na Zitto anajibu positively kwenye mapendo hayo yanayooneshwa na Spika makini, Anne Makinda!!!?

hii ni namna ya kumtoa zitto kwenye MEREMETA na kupoteza ushaidi wa uozo katika kashfa za wakuu wa jeshi

Tunaandaa maandamano ya amani jijini Washington DC Rais Kikwete atakapowasili kwenye kikao cha DICOTA 2011. Tayari watu 150 wamekubali kushiriki kwenye maandamano hayo. Tunataka watu wengi zaidi kujitokeza. Hii ni kumshinikiza huyu fisadi papa na mzururaji kushugulikia matatizo yanayowakabili wananchi wa kawaida. Maandamano yetu yatahitimishwa na kupokelewa na viongozikutoka United States Department. Tayari tumetuma maombi kupinga misaada marekani inayopa Tanzania, kwani hayasaidii Jamii bali Kikwete na genge lake la majambazi

Wote mnakaribishwa karibishwa. Maandamano ya Amani yanaruhusiwa marekani ilimradi mtu hajavunja sheria nchini. Ukiwa na makaratasi yako, njoo tulikomboe taifa letu. Ukombozi wa TANZANIA upo mikononi mwetu. Mabango yanachapishwa tarehe 24, Tunaomba mawazo tofauti kuhusu ujumbe tutakaobeba kwenye mabango yetu. Tumechoka na Kikwete, dawa nikuanza maandamano.Tupo tayari kufa sasa. Tunisia iliokolewa na watu tu kama sisi, tukifa bahati mbaya vizazi vijavyo vitafaidi. Tafadhali sambaza ujumbe. Tutatoa tamko rasmi ya maandalizi tarehe 20 mwenzi huu Ukitaka kushiriki tuma barua pepe EliakimMallya@yahoo.com

Raia wa kawaida anayo haki ya kumfanya Kikwete Anyimwe VISA. Kwa Kupinga Ujio wa Kikwete, au yeye kunyimwa VISA tumeni emails nyingi iwezekanavyo kwenda East African Affairs Bureau. Email Adress wiegertjr@state.gov

Hayo ni mawazo chanya, endeleeni na maandalizi ya maandamano ya amani, tumechoka na huyo VASCO DAGAMA wetu kuzurula kila wakati.

Hapo sasa mwenye kipele kapewa kucha! Kamati ya Zito ni ya mashirika ya umma likiwemo shirika la UDA. Kwahiyo kamati yake ndio ilistahili hasa kufanya huo uchunguzi na sio vinginevyo! Haya maoni kwamba wanadivert hoja yake ya meremete, Zito ndiye aliyeibua au Zito anapendwa na spika sio sahihi sana. Kamati ya Zito ndio inayokagua hesabu za mashirika ya umma na ndio maana amepewa hiyo kazi yeye kama M/kiti.
Tusubiri matokeo sasa maana kipele kimeshapata mkunaji!

kuna kitu lazima ukitambue , hatusemi ya kuwa kamati hii isifanye kazi za kuchunguza UDA lakini si wakati huu kwani kutakuwa na mwingiliano wa kazi wa tume na kamati,

kamati ilistahili kufanya kazi baada ya kufahamu serikali kupitia kwa CAG wamefanya nini katika uchunguzi na nini maamuzi ya serikali , kwani ili lipo wazi kabisa kwa CAG anafahamika kwa utendaji wake na pindi tunapoingiza mikono mingine ni marudio ya kazi zile zile

kwa sasa taasisi zilizotumwa kuchunguza UDA ni kama zifuatazo

1.CAG

2.TAKUKURU

3.KAMATI YA ZITTO

4. Halmashauri ya jiji

5.Usalama wa taifa

je kwa mwenye kutazama kwa nini ifike wakati tukatumia mabilioni ya shillingi kufanya kitu kimoja wakati taifa linaupungufu mkubwa wa fedha na nchi inaelekea kwenye janga la ukosefu wa mafuta , kwanini tume zingine sisiende kwenye majanga mengine kama ukosefu wa mafuta

Tunaandaa maandamano ya amani jijini Washington DC Rais Kikwete atakapowasili kwenye kikao cha DICOTA 2011. Tayari watu 150 wamekubali kushiriki kwenye maandamano hayo. Tunataka watu wengi zaidi kujitokeza. Hii ni kumshinikiza huyu fisadi papa na mzururaji kushugulikia matatizo yanayowakabili wananchi wa kawaida. Maandamano yetu yatahitimishwa na kupokelewa na viongozikutoka United States Department. Tayari tumetuma maombi kupinga misaada marekani inayopa Tanzania, kwani hayasaidii Jamii bali Kikwete na genge lake la majambazi

Wote mnakaribishwa karibishwa. Maandamano ya Amani yanaruhusiwa marekani ilimradi mtu hajavunja sheria nchini. Ukiwa na makaratasi yako, njoo tulikomboe taifa letu. Ukombozi wa TANZANIA upo mikononi mwetu. Mabango yanachapishwa tarehe 24, Tunaomba mawazo tofauti kuhusu ujumbe tutakaobeba kwenye mabango yetu. Tumechoka na Kikwete, dawa nikuanza maandamano.Tupo tayari kufa sasa. Tunisia iliokolewa na watu tu kama sisi, tukifa bahati mbaya vizazi vijavyo vitafaidi. Tafadhali sambaza ujumbe. Tutatoa tamko rasmi ya maandalizi tarehe 20 mwenzi huu Ukitaka kushiriki tuma barua pepe EliakimMallya@yahoo.com

Raia wa kawaida anayo haki ya kumfanya Kikwete Anyimwe VISA. Kwa Kupinga Ujio wa Kikwete, au yeye kunyimwa VISA tumeni emails nyingi iwezekanavyo kwenda East African Affairs Bureau. Email Adress wiegertjr@state.gov

Pamoja sana mkuu! Sisi tulio mbali tunawatakia maandalizi mema.

Back
Top Bottom