Spidi ya wakinga kwenye biashara inatisha, tuna lipi la kujifunza?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Kuna jambo la kustukiza sana katika miaka ya hivi karibuni kuanzia 2010, kuna hawa jamaa wanaitwa wakinga wamejipatia umaarufu ndani ya miaka hii michache kwa spidi ya 4g.

Ni kabila dogo sana ambalo haliingii hata kwenye orodha ya makabila 20 yenye watu wengi hapa nchini, Ni kabila ambalo lipo chini mno kwenye elimu lakini wana kipaji cha kufanya biashara, kama samaki alipewa kipaji cha kuogelea, farasi alipewa mbio, basi wakinga walipewa akili ya biashara, siongei maneno matupu maana nayashuhudia kwa macho yangu.

leo hii ukienda pale kariakoo ni ya wakinga, kiukweli inastua.


Kwa mimi binafsi nikiwa chuoni, kuna mkinga flani alimaliza form 4 akaja kuanza certificate, nilipata kumjua, yule dogo hata hakumaliza certificate alianza kuuza mitumba ya nguo ila leo hii ana duka lake la simu za iphone hajafika hata miaka 25 na maisha yake yamebadilika.

Kuna mwengine alipomaliza chuo alipata ajira, analipwa vizuri tu kama 1.3 M take home na allowances kibao, ila alikaa kazini mwaka moja tu, aliacha hio kazi watu walimshangaa sana, alifungua biashara yake, hatua aliyofikia kwa sasa inavutia kwa kweli,

Mwengine namjua alimaliza chuo, hata hakuhangaika kitafuta kazi, alichangiwa mtaji wa biashara, nilitegemea atafungua duka mkoa anaoishi ila alivuka mategemeo yangu, huyu kaenda huko Zambia kwenye mikoa ya kawaida kabisa tena ndani ndani huko hata hana ndugu, bwana! bwana! bwana! duka ni la vitu general kama kina mangi ila anauza si mchezo! ndani ya miezi 8 tu aliweza kupanua duka lake, na saizi kaongeza duka la ziada basi ni mwendo wa bampa to bampa,

Nafkiri kuna namna tunaweza jifunza kupitia hili kundi,

Kumekua na fununu za ndumba na uchawi ila kwa bidii nayoona waliyo nayo unaona kabisa the juice is worth the squeeze, kama unahisi ni ndumba basi na wewe karoge,!!
 
Uchawi pekee wa wakinga ni wanapeana michongo yaani ni kabila wanalobebana lakini pia, Uaminifu huwezi kukuta mkinga mdhulumati kwenye biashara, matumizi bora ya pesa yao, wanawekeza zaidi kwa mfano unakutana nae chuoni nyumbani toka akiwa form one anashamba la miti ekari 20 la kwake hivo hata mkimaliza mkaajiriwa pamoja anakua anasubiri kuuza miti akajiajiri mwenyewe na kumbuka ataenda kujiajiri sehemu sahihi maana atakua na taarifa toka kwa wenzake
 
Hamna kitu sipendi kama watu kama nyie. Nafurahi kusikia unaonekana ni kijana wa makamo.. early 20’s.

Endelea kuwaza hivyo ila kkoo ya sisi tuliopo. Wapi wakinga, wabena, wachaga, wahindi na wote tunafanya kazi.

Cha msingi ni determination mbona kkoo unatakeover.

kkoo ina hadi wachina , waturukinna ndio wenye biashara huwezi waona.

Sasa naomba mods either mfute au muonganishe hii thread.
 
Hamna kitu sipendi kama watu kama nyie. Nafurahi kusikia unaonekana ni kijana wa makamo.. early 20’s.
Endelea kuwaza hivyo ila kkoo ya sisi tuliopo. Wapi wakinga, wabena, wachaga, wahindi na wote tunafanya kazi...
Gussie Mkinga Nipo hapa,

Kama una swali karibu sana sana, Wale wazee wa kununua Fuzo karibuni sana

Wale wote wanaoona biashara rahisi nawapongeza sana

Kwa sisi wakinga tatizo sio mtaji ni kiasi gani? Tatizo ni matumizi na mipango

Mipango.

Kuwa mwana ccm kama mimi ni maamuzi magumu sana kuliko kuuza Pipi
 
Kuna jambo la kustukiza sana katika miaka ya hivi karibuni kuanzia 2010, kuna hawa jamaa wanaitwa wakinga wamejipatia umaarufu ndani ya miaka hii michache kwa spidi ya 4g....
Ni kweli unachosema ila tatizo wanakumbwa mno na vifo vya utatanishi wakiwa wadogo na miaka michache tu baada ya kupata utajiri. Ukienda Njombe na Makambako kuna wajane hadi utasikitika
 
Mleta mada unaweza kuwa sahihi kwa swala la uchawi maana kwenye biasha hizi mambo zipo Sana Sana .
 
Sasa wewe umeona wapi mtu una miela kitimtim afu unashindia viazi vya kuchemsha kama sio mashart ya mganga ni nini! Wanga tu wale,,,,,
Mkuu hili ni jukwaa la great thinkers, bora ukae kimya kuliko kujiweka wazi ujinga wako kwa kutoa maoni kwa kitu ambacho unakisikia tu kijiweni.

Mtu ambae anakula viazi vya kuchemsha ni mwanga?? wachungaji au mashehe hawali viazi??

kwenye hili swala la viazi Ishu ni kubana matumizi.

Kiufupi hata wachaga walikuwa wanabana matumizi ila hawajafikia kwa wakinga aisee, hawa jamaa kwenye kubana matumizi inabidi walegeze kamba kidogo
 
Mkuu hili ni jukwaa la great thinkers, bora ukae kimya kuliko kujiweka wazi ujinga wako kwa kutoa maoni kwa kitu ambacho unakisikia tu kijiweni.

Mtu ambae anakula viazi vya kichemsha ni mwanga?? wachumgaji au mashehe hawali viazi??

kwenye hili swala la viazi Ishu ni kubana matumizi.

Kiufupi hata wachaga walikuwa wanabana matumizi ila hawajafikia kwa wakinga aisee, hawa jamaa kwenye kubana matumizi inabidi walegeze kamba kidogo
Unatetea usichokijua
 
Back
Top Bottom