GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Mwanzoni mwa mwaka 2020, nilifanya mazungumzo na kijana mmoja muuza mahindi ya kuchoma Mjini Kahama. Nilitaka kufahamu, pamoja na mambo mengine, manufaa wanayoyapata kutokana na hiyo biashara.
Aliniambia, ni biashara inayomlipa sana. Alipokosa nafasi ya kuenedelea na masomo baada ya kuhitimu kidato cha Nne, aliondoka kwao Tabora na kwenda kutafuta vibarua Kahama. Alifanya vibarua vya ujenzi kwa muda na kisha baadaye kuingia kwenye biashara ya kuchoma mahindi.
Biashara hiyo ilimpa manufaa yafuatayo:
1. Kuihudumia familia yake kwa mahitaji muhimu
2. Kulipa pango la chumba alichokuwa akiishi huko Kahama
3. "Kumwajiri" mtu aliyekuwa akikisimamia "kijiwe" chake kingine cha kuuzia mahindi. Alikuwa na jumla ya vijiwe viwili.
4. Alifanikiwa kujenga "kanyumba kake" nyumbani kwao Tabora.
5. Alikuwa akikusanya faida isiyopungua shilingi elfu thelathini kila siku. Hiyo inamaanisha endapo atafanya kazi kila siku, kwa mwezi atakuwa na wastani wa sh 900,000/=.
Baada ya miezi kadhaa, nilipata tena safari ya kwenda Kahama. Kabla sijaondoka huko, nilimtafuta mtu mwingine mchoma mahindi kwa lengo la kumfanyia usaili kuhusu biashara anayoifanya.
Alikuwa ni Muha kutoka Kigoma. Japo hakuwa amefanikiwa kumaliza shule ya Msingi (lakini alikuwa anajua kusoma na kuandika), lakini biashara ya kuuza mahindi ilimwezesha kuendelea kuwepo mjini.
1. Alikuwa akiishi kwenye nyumba yake mwenyewe, ingawa haikuwa imefanyiwa "finishing". Ni biashara ya mahindi ndiyo iliyomwezesha kununua kiwanja Kahama na kujenga.
2. Alikuwa anamudu kuihudumia familia yake kwa mahitaji muhimu.
3. Alikuwa na jumla ya "vijiwe" viwili vya kuuzia mahindi, ambapo kimoja alikuwa akisimamia mwenyewe na kingine "alimwajiri" mtu
4. Alikuwa anauza mahindi kwa bei ya jumla na rejareja. Alikuwa akiyafuata mahindi shambani, akiishayatenga atakayoyauza kwenye vijiwe vyake, yanayobaki huyauza kwa bei ya jumla kwa wachomaji wengine.
5. Alikuwa na duka la kuuzia bidhaa za nyumbani
6. Aliweza kununua pikipiki aliyokuwa akiitumia kufuata mzigo shambani na kuusamabaza kwa wateja.
Kama hayo waliyoniambia ni kweli, kuna la kujifunza kutoka kwao. Huenda, kwa yanayofanywa na hao wachuuzi wadogo wadogo, mtu akifanya tafakuri yakinifu, anaweza akaibuka na wazo litakalozaa biashara kubwa itakayozaa mafanikio makubwa.
Naamini, kwa kutumia wachuuzi wadogo, mfano, wauza mchicha kama "case study", kupitia tafakuri tunduizi, kampuni kubwa inaweza kuzaliwa. Ubunifu haujafikia ukomo. Unaendelea kila siku iitwayo leo. Na kitu chochote kile kifanywacho na mtu, kiwe kikubwa au kidogo, huanza kama wazo.
Kama "mwewe" alimtia mwanadamu wivu hadi akaamua kutengeneza chombo kitakachomwezesha kuruka angani kama yeye, biashara ya muuza karanga inaweza kumfikirisha mtu hata akamiliki kampuni kubwa ya kibiashara.
Kuna wanaume na wanawake, japo wana Elimu ndogo sana ya darasani, na wakati mwingine, hawajui hata kusoma na kuandika, lakini kwa mtaji usiozidi shilingi elfu hamsini, wameweza kuzihudumia familia zao, alau, mahitaji muhimu.
Kuna wanawake, ambao kwa biashara ya kukaanga samaki na mihogo, wamewasomesha watoto wao hadi Vyuo Vikuu.
Kuna wanaume, ambao kwa biashara ya kuchemsha kahawa, watoto wameendelea kuwa na imani kuwa mahitaji yao yatatimizwa kwa kuwa baba yao anafanya biashara ya kuuza kahawa.
Kwa biashara ya kuuza mchicha, familia nyingi zimeweza kuishi.
Kwa biashara ya kuuza matunda, watu wengi wameweza kulipa kodi ya vyumba vyao.
Kuna watu waliotumia mtaji wa shilingi elfu ishirini kuanzisha kabishara kadogo, na wakafanikiwa kuepuka aibu ya kuwa omba omba.
Ikiwa kwa mtaji usiozidi shilingi elfu hamsini, mtu mwenye Elimu ndogo ya darasani amemudu kuishi, msomi atashindwa "kutoboa" kimaisha kwa shilingi laki moja endapo atafanya tafakuri yadidi?
Tutafakari!