Kwa maono yangu, yaani hao kuku wote walikuwa ndani, wakiwa ndani wakanyolewa tens wakiwa hai. Baadaye mlango ukafunguliwa ili yule kuku aliyeko ndani tayari kashonyolewa akiona huko ndani matezo yamemzidi basi atoke nje aungane na maisha ya mnyoaji. Huyo aliyeko nje yeye kashatoka na anamgeukia yule aliyebaki ndani na kumtazama kwa majonzi huku akimshangaa kwanini aendelee kuteseka huko ndani wakati anaweza kutoka. Cha ajabu ni kwamba kuku aliyeko ndani haoni kisu kilichoko hapo juu iliyoandaliwa tayari kumchinja endapo ataendelea kukaigi kutoka nje lakini kuku wa nje yeye hicho kisu anakiona na hiki ndicho kinamfanya azidi kumuonea huruma huku mwenzake aliyebaki ndani kimoyo moyo. Huu mchoro kama hujaishi maeneo ya NORTH KIVU, SOMALIA, DARFUR, huwezi kulielewa vzr. Hii kawachorea wanaishi kwenye maeneo hayo ambayo nadhani ndiyo mambo ya kutesa watu wenye mawazo tofauti na wenye nguvu, kuwaiba hao wenye mawazo tofuti kwa njia mbali mbali kama vitisho, pesa au vyeo na baadaye kuwachinja wale wanaokaidi yanafanyika. Huu mchoro kwa hapa kwetu ni uchochezi na ni kama uhaini, sasa kwavile analeta chokochoko na anawashwawashwa asije akatulilia tena hahahahahaa