Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

Hii alichora baada ya yule kamanda ya mwanza kule butiama kutoa salamu ya kidumu chama,ila inalandana na hili la leo la aijipii na sisitivii
 
Hahahahahahajhahahahahahahaah nimecheki hadi nimepaliwa

Kipanya made my day hahahahah
 
Akikosea timing ya kuachia anaweza jikuta katupwa kusikojulikana upande wa pilim
 
Wakuu huyu jamaa ana akili nyingi mno
received_957439304453177.jpeg
 
Hahahah, ila kweli watunzi wa muvi za kibongo hawajishughulishi sana kutaka kuendana na mazingira!

Kama hii muvi tuliyotoka kuicheki, eti watu wamemteka mtu karibu na ulinzi mkuu halafu wanamrudisha na kumtupa karibu na ulinzi huo huo mkuu nchini.

Halafu mtekwaji anapiga simu home wamfuate,anakaa anasubiri ndugu zake wamfuate,ndugu wanafika,wanamchukua wanaenda naye haooooo...nyumbani.....muda wooooote huo hakuna hata mlinzi wa kibanda aliyeshituka achilia mbali walinzi wa eneo kuu!!!!.....

Wanafamilia nao,badala ya kwenda polisi wanaenda nyumbani halafu wanawaita polisi.....polisi nao kweli wanaenda nyumbani....tehe tehe tehe.....

Ila naamini wangeandika wale wa hollowod,angalau angetupwa mpakani (labda mbeya)huko kwa sababu tulishasikia aliyemteka ni mgeni na dsm yote tuliambiwa askari hawalali usiku na mchana wanamsaka mtekaji!
 
Back
Top Bottom