Speaker Makinda so is this "Wanawake Wakiwezeshwa Wanaweza?"

Speaker Makinda so is this "Wanawake Wakiwezeshwa Wanaweza?"

Dada yangu Elly B wacha dhambi. Yaani unataka kuniambia kuwa Makinda anajuwa kuwa anaboronga? Kama ni kweli basi hata yeye mwenyewe hajitendei haki kwani anafanya madudu anayotumwa na viongozi wa CCM haswa Bw. Vituko (JK). Kwa kweli huyu mama anajidhalilisha sana, hivi kuna mwenye namba zake za simu huyu mama nimpigie?

Aaaaaaaah!... "we Lambardi wewe, Mheshimiwa Lambardi tusianze kutafutana" ( in Makinda's voice)......just kidding though. Napenda kutoa taarifa tu kuwa mimi ni Likaka li kubwa na siyo Mdada jamani...........tehe ..tehe teh

Tukirudi kwenye mada:

Trust me anajua kabisa kuwa anaboronga, ila kwa kukosa aibu tu kama ilivyo kwa WanaCCM wote, ameamua kutekeleza maagizo ya waliomtuma. Wanaokufa, potelea mbali! Kwa hiyo hayo yote uliyoandika yamhusu kwa kina!
 
Elly B shikamoo na pia naomba ninywe chai kwa niaba yako this morning. Siyo kama sitaki kukualika ila niko mbali na nyumbani kwa sasa. Yote uliyo ongea ni ya kweli na inasikitisha sana kutawaliwa na watu wasio na upeo wa maendeleo. Yaani watu wanaiba Tanzania kama hawana akili kushindana na rais wao. Kikwete as a president hawezi kusema kitu kwani anajuwa akiwachukulia hatua hawa watu (mawaziri wezi) huenda watamgeuka na kumshtaki yeye ndiyo maana amekuwa mtu wa kucheka kwa kutopenda. Najiuliza siku zote hivi ni kwa nini jeshi letu lisichukue nchi mpaka hapo 2015? Waafrika wenzetu wameweza kujikomboa toka kwa utawala wa kipuuzi kwa nini sisi tusindwe? Jeshi la TZ liko wapi jamani? Kikwete hatufai anaangusha nchi huyu mtu jamani, enough is enough.

Nafikiri hili wazo la kuwaachia wanajeshi wetu linaweza kuwa jibu kwa sasa. Tatizo ni kuwa hawa ndugu zetu wana viapo vigumu! Mpaka kufikia wao kujiingiza kwenye kuchukua dola kuna mambo mengi ya kuzingatia. Kwa haraka ni ngumu sana.
Ila bado nina maswali machache na hawa waheshimiwa. Kuna wakati kuna vi operation vya CCM huwa wanavifanya. Sijajua tu kama hawajui kama wanafanya kazi haramu.
Ila kwa haraka nina imani nao sana kama wanaweza kushiha hatamu kwa muda mpaka nchi iwe ya kizalendo.
 
Makinda amewaangusha kina mama wengi waliokuwa wakijiandaa kugombea nafasi mbalimbali mwaka 2015! Hatutachagua mwanamke kwa nafasi ya rais, makamu wa rais na hata spika! Uchochezi kwa mujibu wa makinda ni kuisema vibaya ccm!
Mimi sioni tofauti yoyote kati ya Makinda na Ndugai. Wote wanaipendelea CCM. Na siku ambayo Serurope ametukana aliyekuwa akiongoza bunge alikuwa ni Naibu Spika Job Ndugai na hakumchukulia hatua yoyote na badala yake aliwatoa na kuwasimamisha wabunge watano wa Chadema. Kama ni kupendelea CCM Spika na Naibu Spika ambaye ni mwanaume wote wanafanya hivyo. Msihukumu wananwake wote kwa uzembe au makosa ya mwanamke mmoja
 
Aaaaaaaah!... "we Lambardi wewe, Mheshimiwa Lambardi tusianze kutafutana" ( in Makinda's voice)......just kidding though. Napenda kutoa taarifa tu kuwa mimi ni Likaka li kubwa na siyo Mdada jamani...........tehe ..tehe teh

Tukirudi kwenye mada:

Trust me anajua kabisa kuwa anaboronga, ila kwa kukosa aibu tu kama ilivyo kwa WanaCCM wote, ameamua kutekeleza maagizo ya waliomtuma. Wanaokufa, potelea mbali! Kwa hiyo hayo yote uliyoandika yamhusu kwa kina!

Kwa kweli kama ni hivyo basi anasikitisha na inabidi tumuuombee tu kwani anajidharaulisha mno. Angekuwa nchi za wenzetu wangeshamtengenezea film ya kumkashifu tayari.
 
Nafikiri hili wazo la kuwaachia wanajeshi wetu linaweza kuwa jibu kwa sasa. Tatizo ni kuwa hawa ndugu zetu wana viapo vigumu! Mpaka kufikia wao kujiingiza kwenye kuchukua dola kuna mambo mengi ya kuzingatia. Kwa haraka ni ngumu sana.
Ila bado nina maswali machache na hawa waheshimiwa. Kuna wakati kuna vi operation vya CCM huwa wanavifanya. Sijajua tu kama hawajui kama wanafanya kazi haramu.
Ila kwa haraka nina imani nao sana kama wanaweza kushiha hatamu kwa muda mpaka nchi iwe ya kizalendo.

Mkuu Elly B, naomba unirudishie shikamoo yangu, tena haraa sana. Eti unasema una imani na hawa viongozi wa CCM, kwa lipi jema walilo litendea taifa letu? Hapa umeniudhi sana, yaani unaridhika na ujinga uliopo?
 
Last edited by a moderator:
Nimekupata mkuu Elly B...lakini akina dada zetu na mama zetu wamezidi ndo tuseme hawawezi chochote....mana ukiangalia nchi za wenzetu wanawake wanainfluence uchaguzi....na wanajua kuchagua kilicho bora na siushabiki...lakini huku kwetu wengi wanashabikia kitu cha muda mfupi...wanateseka miaka mitano...
 
Kwa kweli kama ni hivyo basi anasikitisha na inabidi tumuuombee tu kwani anajidharaulisha mno. Angekuwa nchi za wenzetu wangeshamtengenezea film ya kumkashifu tayari.

Unamjua ?hakujui na humfikii hata ufanye nini ?Next president Anne na atapita kilaini mtajibebaje .
 
Wewe una matatizo na Mbaguzi, hayo yote uliyoyaandika yanaonyesha jinsi unavyodharau na kubagua Jinsia nyingine, usichokielewa ni kwamba hata wewe pia kama Mwafrika na Mtanzania watu wengine wanakuona kama Sokwe na wakikuona watakutupia Ndizi ule, hii Dunia tumeshatoka huko, kuna wakati sisi Waafrika tulikuwa tunawekwa kwenye human zoo huko Marekani na Ulaya ili Watalii waje watuangalie, lkn sasa hivi tumetoka huko, na nimeweka hizo Picha hapo chini ili ujue kwamba kama wewe unaona ni Haki kubagua Wanawake basi pia hao waliowaweka mababu zetu kwenye human Zoo pia walikuwa na Haki!

Kama unasema hakuna haja ya kuwawezesha Wanawake usichokijua pia kuna Watu wengi wanauliza kama kuna haja ya kumuwezesha Muafrika kama wewe (Sokwe) kwa maana hauna Akili na hauna juwezo wa kujifunza!

Nimeandika haya yote ili kukumbusha tu kwamba Ubaguzi Mbaya, kama una matatizo na Mama Makinda umuongelee yeye kama yeye na sio kuanza kukebehi Jinsia nzima!

tumblr_mcu446jE9C1qek8f0o1_1280.jpg human_zoos_or_640_03.jpg images.jpeg
 
Unamjua ?hakujui na humfikii hata ufanye nini ?Next president Anne na atapita kilaini mtajibebaje .

Ah box I missed your lame comments, where were you? Suala hapa si mimi kumjua, you are missing the point as usual. Huyu Mama ni dhaifu tena wa kutupwa na kwa vyovyote vile huyu hawezi kupewa tena uspika, she's just not fit enough, just like you. Imagine wewe unapewa uspika na hivyo ulivyo, we unafikiri bunge litakuwaje. Si wabunge watapena malavi davi hadharani huku ukishabikia?
 
Ndugu zanguni nazungumza hili kwa uchungu sana. Mh spika amejikita kwenye kupindisha haki bungeni na kuitetea serikali huku jimbo lake likiwa hoi bin taabani.Nianze na hospitali ya kibena ambayo ni tegemeo kwa wanyonge wengi haina majokofu ya kuhifadhia maiti ktk chumba cha kuhifadhia maiti, hivyo ndugu zetu wakifa unalazimika kuzika faster otherwise majanga. Pia huduma ya maji ktk mji wa njombe ni tatizo kubwa sana nduguzanguni, maji sehemu nyingi hazina na wanaopata walio wengi ni kwa wiki mara moja au nil kabisa.Hivyo naomba uje utatue hizi kero mapema,sio unakuwa mbabe bungeni,ubabe huo ulete maendeleo huku.Angalizo ulichaguliwa na wananchi.
 
Mama Makinda,
Napenda ujue waTanzania wengi wanakuheshimu kama mama.( Namaanisha siyo vizuri kumsema vibaya mama yeyote kwa sababu ni viumbe wenye heshima kubwa hata mbele za Mungu) Ni vema nikiri kuwa najisikia vibaya ninapolazimika kusema kama hivi. Lakini pia ni vizuri ufahamu kuwa nafasi uliyopewa inabeba hatima ya taifa hili kwa muda mrefu na huenda ukasaidia kuandika historia ya ajabu kwa miaka yote iliyobaki. Its a shame kuwa unatuweka kwenye position ya kuchagua kuendelea kukuheshimu kama mama au tutetee the little that is left of our Country. Tunajua huwezi kufikiria kuupendelea upinzani ever na hatutaki ufanye hivyo asilani. But at least acha kunyanyasa Wawakilishi wetu hata pale wanaposema ukweli. Wakikosea waonye, ikishindikana wachukulie hatua. Lakini wanapofanya kazi tulizowaagiza waache wafanye wajibu wao for the sake of Tanzania please.

Naamini Watanzania wenzangu wataendelea kukwambia maoni yao hapo chini!
Last edited by Elly B; 23rd May 2013 at 00:46.
​

Makinda ni tunda la mfumo wa chama kimoja na hata uspika aliwezeshwa kwa kumzuia chaguo la wengi Sitaa asigombee kwahiyo tusitegemee lolote hapo.
 
Makinda uwezo wake ni mdogo hivyo ni makosa kuamini kuwa kushindwa kwake ni mfano mzuri wa uwezo wa wanawake katika kuongoza.
 
haya ni mfano wa aina ya kazi inayofanywa na serikali yote ya ccm kushughulika na nani kaleta hoja badala ya aina ya hoja na nia ya mleta hoja ni nini LAKINI MIMI SISHANGAI MAANA SERIKALI YEYOTE YA WATAWALA INAYOANGUKA HUPOTEZA HEKIMA
 
Kwa kweli kama ni hivyo basi anasikitisha na inabidi tumuuombee tu kwani anajidharaulisha mno. Angekuwa nchi za wenzetu wangeshamtengenezea film ya kumkashifu tayari.

I hope ujumbe sent
 
Mkuu Elly B, naomba unirudishie shikamoo yangu, tena haraa sana. Eti unasema una imani na hawa viongozi wa CCM, kwa lipi jema walilo litendea taifa letu? Hapa umeniudhi sana, yaani unaridhika na ujinga uliopo?

Aaaa Mkereketwa Huyu bana!
Shikamoo Naweza kukurudishia kama utaidai kwa nguvu..... Kuhusu Imani yangu nilimaanisha kidogo nina imani na Wanajeshi wetu kama watachukua dola. Sikumaanisha CCM. Sidhani kama CCM ninaweza kuwaelewa hata wakiongea lugha ipi!
 
Mimi sioni tofauti yoyote kati ya Makinda na Ndugai. Wote wanaipendelea CCM. Na siku ambayo Serurope ametukana aliyekuwa akiongoza bunge alikuwa ni Naibu Spika Job Ndugai na hakumchukulia hatua yoyote na badala yake aliwatoa na kuwasimamisha wabunge watano wa Chadema. Kama ni kupendelea CCM Spika na Naibu Spika ambaye ni mwanaume wote wanafanya hivyo. Msihukumu wananwake wote kwa uzembe au makosa ya mwanamke mmoja

Ndugu Mtengule,

Kama ningeambiwa, hata saa nane ya usiku niizungumzie CCM, ningekurupuka na kuropoka "CCM ni mbovu yote!" Usishangae! Hivyo ndivyo ninavojua, ndivyo ninavyoamini. Hakuna atakayenishawishi kuwa kuna wasafi mule wakati wako mule, wako kimya tuuu...hata hao kina Bulaya, Serukamba na wenzao mimi nawaweka kwenye kundi la wanafiki. SABABU:

1.There is no point tunaishia kutoa sera mpya kila mwaka, ambazo tunajua hatutazitekeleza, kama ambavyo hatujazitekeleza za nyuma tangu UHURU. Halafu na hao kina Serukamaba hawahoji kwa dhati kuhusu mapungufu ya Seriakli ya CCM. Kwa nini nasema si kwa dhati?

2. Hakuna maana kwa mbunge yeyote anayejitambua, asiye mnafiki, mzalendo kweli toka ndani, na mwenye uchungu na hii nchi na wananchi wake, hasa tabaka la chini la maskini na wasio na sauti....halafu asimame huyu Mbunge kuchangia hotuba...akosoe saaaana..kasoro kibao. Halafu mwisho anaunga mkono hoja! Huu ni umbumbumbu wa kutojua wewe ni nani na uko hapo kufanya nini! Otherwise kama unajitambua ni sawa na kusema unajua fika kuwa Bajeti hiyo ni mbovu, haitekelezeki, haina tija kwa nchi (ndiyo maana ukakosoa!) halafu kwa unafiki wa kuogopa wakuu wako, kwa kujipendekeza kwao ukaunga mkono hoja! Na kwa kuwa aslilimia 70 ya bunge ni hao wanafiki,Wasaliti na wasiojali hatima ya wananchi wao, bajeti mbovu kabisa inapitishwa kwa kuitikia kama watoto wa darasa la pili" ndiyoooooo!" Huu ni UNAFIKI na USALITI.

Nikirudi kwenye hoja,
Sijawasema wanawake wote.Nimemsena Makinda. Sijasema Job Ndugai ana unafuu wowote.Job Ndugai, kama alivyo Makinda ni mbovu, wa ovyo na asiyejitambua! naamini hana haya hata kidogo kwa anayoyafanya, wala sidhani kama hata ana fununu na ni nini alitakiwa afanye kwa nafasi yake. Najua utapenda kujua ni kwa nini nimemsema Makinda zaidi..Nitakwambia:

1.Nimemsema Makinda kwa sababu kama mama amekosa uchungu na kinamama wenzake na watoto wanaopata shida kila siku na huduma mbovu za maji na matibabu ndani ya hii nchi, kutokana na sera mbovu na bajeti zisizokidhi haja zinazopitishwa na bunge lenye uongozi mbovu (wa Makinda na wenzake), ambapo kwa makusudi kabisa, huku akijua, anafanya bidii kunyamazisha wapinzani wanapokosoa kasoro hizo ambazo kama zingerekebishwa tusingekuwa kwenye mashimo haya!,

2. Nimeamua kumsema Makinda kwa sababu amekuwa mfano mbaya kwa wanawake wenzake, pale alipokubali kuingizwa kwenye mchakato wa hila wa kupewa uSpika, wakati akijua hana uwezo na nafasi hiyo, na akijua fika wanampa nafasi hiyo kwa sababu hawataki Sitta arudi kwenye nafasi ya Uspika, ili hali akielewa fika sababu za kumtoa Sitta ni kwa kuwa hakuudhibiti upinzani na kupelekea hoja nzito za ufisadi kufanya CCM ikose umaarufu ghafla! Hivyo kwa kukubali nafasi hiyo aliamua kuwa msaliti wa harakati za kutetea hali mabaya za maisha ya waTanzania, na hata yeye anajua anachofanya siyo sawa na wala siyo haki,

3. Nimemsema Makinda kwa sababu Spika wa bunge la vyama vingi anatakiwa kuwa ni kiongozi asiyeongozwa na itikadi yoyote ya kisisasa wala mashinikizo toka upande wowote kati ya makundi yanayounda Bunge, ambapo hata wewe unajua kuwa Makinda na wasaidizi wake ameamua kwa makusudi kutoheshimu hoja za upinzani hata kama ni za kweli( amekosa uzalendo), ameamua kuvunja kanuni za bunge kwa makusudi, kutoheshimu sheria ndogo ndogo za Bunge walizopitisha wenyewe. Mfano mzuri (kati ya mingi) ni siku alipoamua yeyote atakayetoa lugha za kuudhi au matusi atolewe nje ya ukumbi wa bunge, halafu kesho yake Mbunge wa CCM anatukana matusi ya nguoni anaachwa tu kisha anaposimama mbunge wa upinzani kuomba mwongozo wa Spika anatolewa nje. Najua Spika Mwenyewe hakuwepo lakini anawajibika kumsimamia msaidizi wake, ila yeye aliamua kukaa kimya, ishara ya kukubaliana na yaliyotokea! HUU SIYO UADILIFU NA NI KUPUNGUKIWA BUSARA na ni dalili za kushindwa kuimudu nafasi yake,

4. Na nimechagua kumsema Makinda kwa sababu yeye ndiye Spika wa bunge. Na kwa kuwa naibu wake pamoja na wasaidizi wake wengine, anawajibika kwake, ameonyesha udhaifu na kushindwa kumsimamia, na hivyo namlaumu spika kwa kuwa ameshindwa kumsimamia Ndugai na wasaidizi wake wengine ipasavyo, na ameshindwa kujiuzulu nafasi yake kama Spika ili kupisha mtu mwenye uwezo wa kutosha kuongoza, hivyo kuonyesha kiwango cha juu cha kukosa UZALENDO, na kukosa mfano kwa viongozi wengine wabovu, wakiwemo wasaidizi wake.

Sidhani kama una swali na hilo tena. kama lipo I will be more than willing to make myself clear on the matter. So this is all about Makinda seriously, kama mama na amechagua kuitelekeza jamii inayomtegemea, kama Spika na ameamua kuacha majukumu yake ya kulisimamia bunge, instead amebeba kazi ya kufumbia macho uvunjwaji wa kanuni za bunge na kuunyanyasa upinzani Bungeni ikiwemo kuutetea uongo kama wa Waziri Mkuu na wengine Bungeni na kwingineko na kama political figure na amepwaya vibaya.

Kama kuna wasiwasi na hilo tafadhali kuwa huru kuuliza.
 
Nimekupata mkuu Elly B...lakini akina dada zetu na mama zetu wamezidi ndo tuseme hawawezi chochote....mana ukiangalia nchi za wenzetu wanawake wanainfluence uchaguzi....na wanajua kuchagua kilicho bora na siushabiki...lakini huku kwetu wengi wanashabikia kitu cha muda mfupi...wanateseka miaka mitano...

Mheshimiwa Dr.Mo,

Hapa kwetu hali imegubikwa na utata mwingi. Tatizo siyo kuweza chochote, tatizo ni wao kutojitambua kuwa wanaweza. Utakuta mtu anapiga kelele kuwa apewe nafasi, anaweza.Mpeni nafasi sasa, atakaa anashangaa shangaa tu, mpaka ajitolee mtu flani wa kujipendekeza. This sounds awkward I know. Najua kinadada wengine pia watjisikia vibaya. But plese endure me nitoe mifano kabla hamjanihukumu!

1. Waliopitia vyuo hasa vya elimu ya juu watakubali kama siyo kukumbuka jinsi mlivyokuwa na kinadada flani kwenye vikundi vyenu vya kujisomea. hivi hamshangai ni kwa nini wale kinadada wengi mlikuwa mnawasaidia? hamkumbuki jinsi wengine walivyokuwa hata kuchangia point kwenye discussion hawawezi? Mbona hamjashtuka pale matokeo yalipokuwa yanatoka halafu ni kinadada haohao ndiyo wanoongoza? mbona hamjashangaa jinsi wao mwishoni walivyoibuka na maGPA mazuri kuliko ninyi? Jibu liko wazi sana. ni kwa kuwa wale pamoja na kujibanabana kwenu lakini hawakujikubali kuwa wnaweza wakasoma na kuelewa. Hivyo wakjirahisi kwa walimu wenu flani ili wafanyiwe urahisi wa matokeao ikiwemo kupewa mitihani.( Nina mifano hapa siyo mijungu) Laiti wangejitambua tu leo nisingeandika hivi! ( Sijasema ni kinadada wote)

2. Kwa wale mlioajiriwa nadhani mnaona scenario zifuatazo:
Mnaona jinsi wanavyotangaza nafasi za kazi, halafu wanakuja kufanya interview, halafu wewe unamjua mtu flani yuko tight sana tu kwenye fani (taaluma) halafu anachemka interview, halafu kazi anapewa dada mmoja ambaye baada ya yeye kuanza kazi unagundua ni horrible kabisa, hajui lolote, halafu mnamfundisha kazi wenyewe, halafu anaonekana haeleweki eleweki pale inapokuja ishu ya yeye kuboronga kazini na bosi yuko kimya tofauti na mkiboronga nyie. Halafu anapanda cheo wakati nyie mnatoatoa mimacho tu hapo, pamoja nakuja hapo "long time ago". Mara huyooooo kwenye semina na kozi..... hivi huwa hamsahangai ni nini kinawatokea? Majibu ni yaleyale...kwa kufikiria hataweza kupata kazi, akaamua kujifanya "available" ili kupata kazi. Na kwa kuwa yule jamaa yenu( ni mfano tu) hakuwa " available" kwa vile haingewezekana, alikosa. Na kwa kuwa bado "mkuu mbalimbali ana hisa kwa huyo mwenzenu ndiyo maana hatafoka akiboronga, atakwenda semina hata kama hamtaki na atapandacheo tu hata kama kampuni mliianzisha nyie. (Pia siyo wanawake wote wako hivyo. Wengi huwa hivyo, either anajirahisi au anaahidi ama anajulikana na mtu!)

Kwa hiyo Dr.Mo hapa kwetu tatizo ni kutojitambua tu. Kuhusu kuweza...wote wanaweza. Kama Fatuma hawezi kuendesha gari akidhamiria ataendesha tu! ila kwa kuwa kuna mentality ya kuwa inferior, watabaki wanajipendekeza kwa wanaume washenzi na tutabaki na stori hizi hizi every now and then. Wakati mwingine unaweza kumfunga punda wenye kijiti cha diameter ya mm 4 na akabaki hapo siku nzima kwa kujua kamba iko kwenye lijamu....nimefungwa kamba! Kume tatizo siyo kamba, ni akili yake tu!

Mnisamehe sana. Sijaandika hivi kuwadhalilisha dada zetu,la hasha. Naongea hali halisi ilivyo, ili muanze kuangalia upya jinsi ambavyo hamjitendei haki wenyewe huku mkitegemea kina kaka wawatendee haki!!!

Sijui kama nimejibu hoja sawia.
 
Wewe una matatizo na Mbaguzi, hayo yote uliyoyaandika yanaonyesha jinsi unavyodharau na kubagua Jinsia nyingine, usichokielewa ni kwamba hata wewe pia kama Mwafrika na Mtanzania watu wengine wanakuona kama Sokwe na wakikuona watakutupia Ndizi ule, hii Dunia tumeshatoka huko, kuna wakati sisi Waafrika tulikuwa tunawekwa kwenye human zoo huko Marekani na Ulaya ili Watalii waje watuangalie, lkn sasa hivi tumetoka huko, na nimeweka hizo Picha hapo chini ili ujue kwamba kama wewe unaona ni Haki kubagua Wanawake basi pia hao waliowaweka mababu zetu kwenye human Zoo pia walikuwa na Haki!

Kama unasema hakuna haja ya kuwawezesha Wanawake usichokijua pia kuna Watu wengi wanauliza kama kuna haja ya kumuwezesha Muafrika kama wewe (Sokwe) kwa maana hauna Akili na hauna juwezo wa kujifunza!

Nimeandika haya yote ili kukumbusha tu kwamba Ubaguzi Mbaya, kama una matatizo na Mama Makinda umuongelee yeye kama yeye na sio kuanza kukebehi Jinsia nzima!

View attachment 95106 View attachment 95107 View attachment 95109

Ndugu Kijakazi,
Point taken! Lakini rudia kusoma na utaona yafuatayo:

1. Sijasema Wanawake wasiwezeshwe! La hasha. Wawezeshwe kwa nguvu zote. Ila wanapowezeshwa wafanye yale yanayoendana na kuwezeshwa kwao. Kuwezeshwa na kuendelea kujipendekeza ni KUJIDHALILISHA. Pia inapowezekana ( kwa kuwa naamini inawezekana), ifikie mahali pale unapopewa nafasi( kama ilivyokuwa kwa Makinda) ili hali unajua kuna hila iliyojificha nyuma( kama ilivyokuwa lengo ni kumtoa tu Sitta na kudhibiti upinzani), tufikie mahali tukatae ili kupisha haki, tuwe wazalendo na tutangulize maslahi ya taifa mbele.

2. This was all about Makinda. Siyo wanawake wote. Wala sijasema wanawake wote wana matatizo. Nimejitahidi kusema kwa sauti kubwa tu kuwa Makinda ana Matatizo, ameshindwa kusimamia nafasi yake na ameonyesha mfano mbaya.

Nasikitika tu kuwa wewe umeona hivyo na umeelewa vinginevyo.
 
Umkome Anne Makinda unasikia,humjui
hakujui .Kapike maharage na utauza mkaa sana mwaka Huu na giza.Achana na Makinda wewe humuwezi

Dear Natalia,
This was never personal. As I am sure, we would have appreciated very very much if you had challenged the motion by displaying facts than kuwapa wenzio lugha za kuudhi. Siyo vizuri na siyo lengo la hii forum.

I do finally hope tuko pamoja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom