Speaker Makinda so is this "Wanawake Wakiwezeshwa Wanaweza?"

Speaker Makinda so is this "Wanawake Wakiwezeshwa Wanaweza?"

Hivi zile nafasi za upendeleo wanazopewaga wanawake zina tija kwa maendeleo ya taifa letu? Nadhani wakati umefika sasa hizo nafasi za upendeleo kwa wanawazi zitupiliwe mbali na kwa 'mwanamke' anayeweza uongozi na kujali maslahi ya Watanzania akagombee na wanaume huko majimboni na kama anafaa basi atatoka kidedea kama hafai tupa kule!!

Haya ndiyo mawazo mbadala yenye tija kwa taifa! Naunga mkono hoja 100%
 
Wana JF

Nafikiri sote tunajua jinsi ambavyo spika wa bunge letu kiti chake kinavyopwaya, baada ya watu wengi kuongea juu ya kupwaya kwa kiti chake, Spika alichokifanya ni yeye kupunguza tu ile jazba aliyokuwa nayo lakini ninachoweza kusema ni kwamba amekuwa mbaya kuliko hata alivyokuwa hapo mwanzo

Muogope sana mtu anayeweza kukuua huku anaendelea kukuchekea, Spika wetu amekuwa ni spika wa kuilinda CCM na serikali yake badala ya kuisimamia serikali, ameshindwa kabisa kujua kwa nini mihimili mitatu ya serikali ipo na kazi zake pia, yanayoendelea bungeni ya kuziba vinywa vya wabunge ili wasiikosoe na kuisimamia serikali ni matumizi mabaya ya fedha za watanzania ,

Kuna haja gani ya kuendelea kukaa vikao vya bunge ambavyo havina masilahi kwa taifa ? Ili suala linawaumiza Watanzania walio wengi

Kuna siku ntakuja kusema maneno ya ajabu hapa. Hawa wahuni hii nchi siyo yao. Ni ya waTanzania wote. Ila wamepata haki ya kufanya hayo wanayofanya kwa sababu tuliwaamini na tukawapa nafasi hiyo. Ila sasa wajue tumesha wachoka na hatutaendelea kuwaangalia tu.

Yana Mwisho haya. Na siku yakifika mwisho!
 
Ukiangali bunge na hasa namna Spika wa bunge,mama Makinda,namna anavyoendesha bunge bila shaka utagundua kuwa spika Makinda amejipanga kwa hali na mali kuhakikisha serikali haikwami bungeni!Mifano ya namna gani anatumia kiti cha spika kuzima hoja za wabunge wanaoibana serikali na kuitaka iwajibike ni mingi na bila shaka hali hii itaendelea kwani licha ya spika kusemwa mara kwa mara katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii haonyeshi kubadilika waka kujisahihisha.

Ni wazi spika anafahamu wajibu wa bunge ni kuisimamia na kuishauri serikali.Sasa spika anapofanya kinyume na wajibu wake tumueleweje?

Hii juhudi ya huyu mama si ya bure bila shaka ina mkono kutoka kwa waliomuweka hapo.Sasa Kikwete tueleze huyu mama mlimuahidi nini?

'
Kama ana akili timamu, hata yeye Makinda anatakiwa ajue ametolewa kafara kumalizia muda wa "Mabwana" zake. Otherwise hata chizi anatakiwa ajue kuwa chochote walichomwahidi is not gonna happen kwa sababu muda hautoshi tena! hii nchi inabadilika tu hata kama kuna mataahira hawataki.

Narudia kusema cha mno watakachopata yeye Makinda, Kikwete na wanafiki wengine ni aibu ya kudumu katika historia ya nchi hii itakayosomwa na watoto wa watoto wetu na wengine baada yao. Kuwa Yeye Makinda pamoja na chama chake walikuwa binadamu wenye roho za nguruwe na ambao hawakujali maisha ya Watanzania wenzao ili mradi tu wao wanaishi! Aibu hii hawawezi kuikimbia, Itawafuata milele!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom