Speaker Makinda so is this "Wanawake Wakiwezeshwa Wanaweza?"

Speaker Makinda so is this "Wanawake Wakiwezeshwa Wanaweza?"

Elly B

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2011
Posts
1,194
Reaction score
906
​Watanzania wenzangu,
Kuna wakati huwa nafikiria sana kuhusu hatima ya Bunge kama litaendelea kuwa na viongozi wa ovyo, wasiojali kanuni na taratibu walizopitisha wao wenyewe. Lakini pia huwa nikiona madudu ya Spika Anna Makinda, nashangaa zile concept za CCM za " huu ni msimu wa Wanawake". What was that for? Kuna haja gani ya kuwaachia nafasi watu wasio na uwezo wa kuongoza Bunge eti kwa sababu tu ni wanawake? This is why kuna wakati niliwahi kusema kwenye posti za awali kuwa hakuna maana ya Kuwawezesha wanawake ili waweze kwa sababu wanaonyesha wataendelea kuwa tools za watu wengine kwa muda mrefu ujao, mpaka watakapoamka from huo usingizi waliolala!( mniwie radhi dada na mama zangu,sikusudii kuwadhalilisha wanawake)

Mfano wa wazi wa uwajibikaji wa Makinda (kwa uchache wake) unaweza kuusoma hapo chini. Ni kutoka kwenye gazeti la Tanzania Daima. Naamini huu ni ukweli mtupu......

KUNA wakati wakubwa wanaweza kukuona wewe mbaya kwa kumuona mwizi na wakahangaika na tukio la aliyeona mwizi kwa nguvu na fujo nyingi kuliko wanavyohangaika na mwizi na pengine wakamwacha mwizi kabisa akatokomea. Hii si afya njema kwa taifa letu ambalo sasa inaelekea Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameamua kutumia ubabe badala ya hoja katika kukabiliana na ukweli kwamba watu wa leo si wa jana.

Nalazimika kusema kwamba kuna nyakati msemo maarufu unaofaa ni ule wa mkuki kwa nguruwe. Yapo matukio mengi lakini hapa nitadurusu machache sana nikianzia na kilichotokea bungeni wakati Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr. Sugu akisoma hotuba yake.

Nimeiona hotuba yake kwenye mitandao ya kijamii. Ni hotuba ambayo inatia simanzi kubwa. Amefanya marejeo ya matukio makubwa yaliyowakuta wanahabari.

Ametukumbusha matukio ya Ndimara Tegambwage na Said Kubenea. Ametutekenya akili zetu tufikirie tena yaliyomkuta Frederick Katulanda wa Mwanza na kifo chenye utata cha mwandishi, Richard Massatu wa huko huko Mwanza.
Sugu akaendelea kutufahamisha namna maiti ya mwandishi Issa Ngumba ilivyookotwa porini na jinsi wazazi wa Erick Kabendera walivyojikuta katika misukosuko.

Mauaji ya mwandishi John Lubungo nayo yalitajwa kwenye hotuba hiyo na akaelezea mauaji ambayo hata shetani asingeweza kuyafanya ya Daudi Mwangosi.

Katika hali ya kustaajabisha amri ya spika ikawa hotuba hiyo isitishwe kwa maoni kwamba ni ya uchochezi.
Katika mazingira haya unashangaa, mchochoezi ni nani? Ni yule aliyeyaona matukio yaliyomaliza uhai wa watu au waliofanya matukio hayo?

Kwa maana ya Makinda ni kwamba ukiona ubaya kaa kimya, maana ukiuzungumza unachochea?
Mama Makinda waliokufa au kujeruhiwa au kutishiwa wangekuwa watoto wako wa kuzaa ungemzuia yule anayejaribu kukitaka chombo kikuu cha kuidhibiti serikali kujadili matukio hayo? Wabunge wa CCM mko tayari kukitetea chama chenu kwa gharama ya kutokujadili damu ya waandishi inayomwagika bila kujua nani anaimwaga na kwa dhamiri ipi?
Hamkushtuka kusikia kwamba mbunge alisema Tanzania inashikilia nafasi ya saba kati ya nchi ishirini duniani ambapo ni hatarishi kwa waandishi wa habari?

Kama majina yanamaanisha dini, basi wengi wa wabunge ni watu wenye dini zao na wanakwenda kumwabudu Mungu.
Nawaomba au waende kuabudu na kutubu au waache kabisa kukanyaga katika nyumba za ibada maana huwezi kujidai unampenda Mungu lakini huwapendi wanadamu.

Nani mwenye mapendo kwa mtu angethubutu kutafuta mbinu za kuzuia mjadala wa hali mbaya inayowakumbwa watu?
Kwani ni uongo kwamba kuna mwandishi alitekwa na kuteswa vibaya? Kwani ni uongo kwamba kuna waandishi walivamiwa ofisini kwao na kujeruhiwa vibaya?

Kwani ni uongo kwamba kuna mwandishi alipigwa na kuuawa akiwa amezingirwa na polisi? Katika hili mbunge anatoa kauli gani ya uchochezi kutaka kuyajadili haya?

Na uchochezi ni pale tu anapokuwa mbunge wa upinzani? Nilimsikia Katibu Mwenezi wa CCM akizungumza kwenye mkutano wa hadhara huko Igunga na akawa anazungumzia siasa za kigaidi.

Mwenye macho haambiwi tazama. Wote tunajua alilenga nini na nini madhara ya uvumi wake huo wa kipumbavu kutaka kuwasadikisha Watanzania kuna vyama vya siasa vya kigaidi. Lakini kwa CCM huo si uchochezi.
Anne Makinda atakapokaa na wenzake ndani ya chama ninamtuma na kumwagiza au kumwelekeza aongee nao na kuwakemea kuhusu uchochezi. Awaulize ni kina nani walianza kuita vyama vya wenzao ni vya kikabila, kidini na sasa wanajaribu kupanda mbegu mpya ya ugaidi katika fikra za Watanzania?

Makinda aone uchochezi upi ni mkubwa lakini asali sana amuombe Mungu ampe busara na hekima ya kujua nini tofauti ya kuchochea na kujadili matukio ya kichochezi.

Pili, spika huyu arejee tena hadithi ya mbuni aliyeficha kichwa chake kwenye mchanga na kudhani yuko salama wakati mwili wote ulikuwa juu ya ardhi.
Tanzania haiwi salama kwa kunyamazia matukio machafu yanayoikumba bali kuyajadili, kujua chanzo chake na kutafuta suluhu ya matatizo hayo.
Bunge letu sasa limekuwa Bunge la kisiasa. Na upendeleo uliokuwa ukisemwa sasa unaonekana waziwazi.
Sikiliza majibu ya baadhi ya mawaziri wa serikali hii kwenye hoja nzito. Yanatolewa kwa kebehi na bahati mbaya unapozungumzia lugha ya kuudhi inakuwa kama vile mama yangu Makinda anaelewa au kuisoma kanuni hiyo kwa maana ya lugha ya kuwaudhi mashabiki wa CCM.
Vinginevyo tungekuwa tumemuona amekasirika kusikia wabunge wakiropoka ujinga kama ‘mimba zisizotarajiwa', ‘Siongei na mbwa, naongea na mwenye mbwa', ‘Fuc* you' na mengine mengi yaliyosemwa na watu wa chama chake lakini hawakuguswa wala kuonywa.

Ikifika hapo ndipo tunaposema ama kweli mkuki kwa nguruwe!
Na jambo jingine ambalo Mama Makinda na wenzake wanapaswa kulitazama upya ni kwamba hizi si zile zama za redio moja na magazeti mawili, hivyo wana uwezo wa kuzuia mbubujiko wa fikra. Hizi ni zama ambazo taarifa zinasafiri kwa kasi inayokaribia ile ya mwanga. Kumzuia Mbilinyi kusoma hotuba yake kumepunguza tu wigo wa wale ambao wangetoa ujumbe.

Lakini katika zama hizi za teknolojia ya habari, hotuba hiyo ipo katika mitandao ya kijamii na imewafikia wengi wanaoisaka. Wakajifunze Ethiopia ambako ujumbe wa simu za mkononi ulitosha kufanya mabadiliko kwenye kupiga kura.

Jambo la kumkatisha Joseph Mbilinyi kumalizia hotuba yake linanikumbusha matukio mengine mawili na namna ambavyo watu wanaweza kuacha kabisa jambo la msingi na kuhangaika na makando kando yake. Wakati Willibrod Slaa alipokuwa akishusha makombora mazito kwa serikali kufichua uozo na ubadhirifu serikalini huku akitumia vielelezo kutoka ndani ya serikali, Hawa Ghasia, aliibuka na kusema watamkamata yeyote anayetembea au kumiliki nyaraka za siri za serikali.

Akili ya ajabu kabisa. Kwamba badala ya kuwakamata wanaofanya wizi na hujuma dhidi ya serikali, wao watapambana kwa nguvu na yule aliyefanikiwa kuona ushahidi wa wizi huo! Majuma machache yaliyopita tulishuhudia huko Arusha namna ambavyo nguvu kubwa ilitumika kumkamata Godbless Lema badala ya nguvu hiyo hiyo kutumika kumkamata muuaji wa mwanafunzi! Na bahati mbaya Watanzania ni wepesi wa kupelekwa wanakotaka wanasiasa.

Wote wanaacha kujadili matukio ya msingi wanakubali kuanza mjadala wa porojo za woga zinazoficha ukweli.
Sasa wakubwa wa Bunge letu wamepata kisingizio kipya cha lugha za uchochezi. Tumeshabaini sasa kila atakayejadili jambo zito wasilothubutu kulitolea maelezo au litakaloiacha serikali utupu wataambiwa wanachochea.
Katika hili la uchochezi sasa tunahitaji kuwepo na maelezo zaidi vinginevyo tutaambiwa ni lugha ya uchochezi na sisi tutakenua meno kumbe nyuma yake tumefichwa mengi.

Kama ni uchochezi waanze kuonyana wao kwa wao ndani ya chama chao na waanze kujiuliza nini kimeleta udini katika nyakati hizi za serikali inayoongozwa na chama chao?

(the bellow is from me personaly)

Mama Makinda,
Napenda ujue waTanzania wengi wanakuheshimu kama mama.( Namaanisha siyo vizuri kumsema vibaya mama yeyote kwa sababu ni viumbe wenye heshima kubwa hata mbele za Mungu) Ni vema nikiri kuwa najisikia vibaya ninapolazimika kusema kama hivi. Lakini pia ni vizuri ufahamu kuwa nafasi uliyopewa inabeba hatima ya taifa hili kwa muda mrefu na huenda ukasaidia kuandika historia ya ajabu kwa miaka yote iliyobaki. Its a shame kuwa unatuweka kwenye position ya kuchagua kuendelea kukuheshimu kama mama au tutetee the little that is left of our Country. Tunajua huwezi kufikiria kuupendelea upinzani ever na hatutaki ufanye hivyo asilani. But at least acha kunyanyasa Wawakilishi wetu hata pale wanaposema ukweli. Wakikosea waonye, ikishindikana wachukulie hatua. Lakini wanapofanya kazi tulizowaagiza waache wafanye wajibu wao for the sake of Tanzania please.

Naamini Watanzania wenzangu wataendelea kukwambia maoni yao hapo chini!
 
Makinda amewaangusha kina mama wengi waliokuwa wakijiandaa kugombea nafasi mbalimbali mwaka 2015! Hatutachagua mwanamke kwa nafasi ya rais, makamu wa rais na hata spika! Uchochezi kwa mujibu wa makinda ni kuisema vibaya ccm!
 
Huyu Mama amepwaya vibaya sana pale bungeni. Aliwezeshwa, hakuweza na wala hataweza!!!!
 
Huyu Mama amepwaya vibaya sana pale bungeni. Aliwezeshwa, hakuweza na wala hataweza!!!!

Makinda hajapwaya... ila ni uwezo wake umeishia hapo,unaposema amepwaya ni kama unampandisha chati!!! ni sawa na kumuona mtu mwembamba ambaye hajawahi kunenepa halafu unasema amekonda NO, HAJAKONDA KWASABABU HAJAWAHI KUWA MNENE..sijui kama nimejieleza lol watu wengi hawafahamu kuwa makinda alikuwa ni mpika chai ofisi za CCM lumumba... sasa mnataka nini kutoka kwake tatizo ni hao waliompa hiyo nafasi ili waweze kumtumia kama kikaragosi... of course anatumika kama kikaragosi!!!
 
Tatizo siyo kupwaya wala uwezo. tatizo la huyu mheshimiwa ni kujawa na roho ya UCCM bila kujali maslahi ya Taifa hili. Ugonjwa huu wanaCCM wote wanao. Ila kitu alichoshindwa kutofautisha yeye kama Spika ni kuwa nafasi yake ikitumika vibaya inaleta picha ya ovyo kabisa kwa jamii na nchi kwa ujumla na inalipeleka Taifa mashimoni.
 
Makinda amewaangusha kina mama wengi waliokuwa wakijiandaa kugombea nafasi mbalimbali mwaka 2015! Hatutachagua mwanamke kwa nafasi ya rais, makamu wa rais na hata spika! Uchochezi kwa mujibu wa makinda ni kuisema vibaya ccm!

Naona wewe sasa unamwelewa vizuri
 
Hivi kuna mtu kweli na alikuwa ana expect Makinda afanye vema?
 
saivi wataanza kujiwezesha wenyewe coz wakibebwa wanakuwa watumwa

Ikifikia hapo mie ntakuwa wa kwanza kuwapongeza walau kwa kuamka! Tatizo ni kuwa wanaweza kupona ugonjwa wa Uchama na udini walioupalilia kwa muda mrefu? Wataweza kutofautisha maslahi binafsi( Kama ya Kinana), maslahi ya chama (kama pale wanapolazimisha matangazo yaende gazeti la UHURU wakati Tanzania Daima na Ijumaa yana wasomaji wengi kuzidi UHURU?) , na maslahi ya Taifa( Kama pale Serikali ya CCM inapoingia madeni yasiyo ya msingi kwa niaba ya watoto wetu? huku wakoloni wanachukua madini yetu kienyeji bila kulipa hata kodi?) Wataweza kweli kusimamia haki na usawa ndani ya hii nchi? Niambie wataweza kweli?

Hapo bado nitakuwa na wasiwasi mpaka waje wanihakikishie wenyewe!
 
Kwa nchi yetu ilipofikia hatuitaji kuweka mwanamke katika nafasi zinazohitaji maamuzi magumu coz wengi wao hawana misimamo.Tunaweza kuchukulia mfano wa wanawake wachache waliopewa fursa ya kuwakilisha wananchi bungeni lakini wamegeuka kuwa viongozi wa serikali wa kujitolea,tukiangalia mtu kama Anna Kilango Malechela ambaye ana sifa kubwa ya kufoka pindi anapoongea bungeni lakini mwisho huishia kuunga mkono hoja licha ya bundle la matatizo aliyoyatoa.

Tukimuangalia spika wetu ndio hopeless ni bora tukaweka gogo pale mbele maana yeye ana kazi ya kutoa albamu za taarabu tu pale bungeni badala ya kutimiza wajibu wake wa kuliongoza bunge katika kuisimamia serikali,Infact ameshakua makamu wa waziri mkuu.Ila tatizo lingine linalofanya wao kudharaulika ni wingi wa viti maalum ambao kazi yao kuu ni kusema ndio.
 
Nakubaliana na wewe moja kwa moja. Hivi kuna aliyewahi kufikiria ule mzuka wa viti maalum umetokea wapi? wanamwakilisha nani kama hautukuwachagua sisi? Hawaoni hata aibu kupewa pewa tu wakati wengine wanasota na kampeni?
 
na wenyewe wana msoto wao usidhan vyeo vinatolewa bure......!wanakaa bungeni kusema ndio but ukifungua vichwa vyao stress kibao. Arafu zamani nilikuwa nadhani viti maalumu huwa ni mamiss tz wa zamani sijui huwa wanatumia vigezo gani kuwapata hao watu
 
Nadhani kuna haja ya kureview hii michakato isiyo rasmi. Pamoja na kupunguza madaraka ya rais ya kuteuateua kila kitu mpaka nchi inajaa viongozi wa ovyo wasiowajibika, wauaji, wezi na mafisadi.
 
Nadhani kuna haja ya kureview hii michakato isiyo rasmi. Pamoja na kupunguza madaraka ya rais ya kuteuateua kila kitu mpaka nchi inajaa viongozi wa ovyo wasiowajibika, wauaji, wezi na mafisadi.
hayo ndiyo yanatakiwa kujadiriwa katika mchakato wa katiba mpya but kwa hali ilivyo saivi inawezekana yakaachwa jinsi yalivyo kwa maana mabaraza ya katiba yanamilikiwa na wenye serikal
 
hayo ndiyo yanatakiwa kujadiriwa katika mchakato wa katiba mpya but kwa hali ilivyo saivi inawezekana yakaachwa jinsi yalivyo kwa maana mabaraza ya katiba yanamilikiwa na wenye serikal

Ni kweli. ila hapo kwenye kuachiwa katiba mbovu na kulazimisha waTanzania waikubali katiba ya CCM kuna vita nyingine inakuja
 
Ni kweli. ila hapo kwenye kuachiwa katiba mbovu na kulazimisha waTanzania waikubali katiba ya CCM kuna vita nyingine inakuja
sasa hapo si watu watalipua magari yao kabisa!
 
Ikifikia hapo mie ntakuwa wa kwanza kuwapongeza walau kwa kuamka! Tatizo ni kuwa wanaweza kupona ugonjwa wa Uchama na udini walioupalilia kwa muda mrefu? Wataweza kutofautisha maslahi binafsi( Kama ya Kinana), maslahi ya chama (kama pale wanapolazimisha matangazo yaende gazeti la UHURU wakati Tanzania Daima na Ijumaa yana wasomaji wengi kuzidi UHURU?) , na maslahi ya Taifa( Kama pale Serikali ya CCM inapoingia madeni yasiyo ya msingi kwa niaba ya watoto wetu? huku wakoloni wanachukua madini yetu kienyeji bila kulipa hata kodi?) Wataweza kweli kusimamia haki na usawa ndani ya hii nchi? Niambie wataweza kweli?

Hapo bado nitakuwa na wasiwasi mpaka waje wanihakikishie wenyewe!
Mkuu mimi huwa sielewi kama huwa wanauwezo wa kufikiri sijui ule msemo wa kunywa maji ya bendela una ukweli. Kila ukijiuliza hivi watu hawa hawana uwezo kabisa wa kutambua baya na zuri hupati jibu. Mama ametuangusha.
 
sasa hapo si watu watalipua magari yao kabisa!

Nachukia vurugu sana. But if it is a price Tanzanians have to pay to gain their freedom so be it!
 
Nachukia vurugu sana. But if it is a price Tanzanians have to pay to gain their freedom so be it!
"Always Do the Right Thing Even if is a Little Dangerous;Thats how a Man Defines Himself!"
hicho kitu ulichokiandika naamini ndio falsafa yako so lazima ukifuate
 
Mkuu mimi huwa sielewi kama huwa wanauwezo wa kufikiri sijui ule msemo wa kunywa maji ya bendela una ukweli. Kila ukijiuliza hivi watu hawa hawana uwezo kabisa wa kutambua baya na zuri hupati jibu. Mama ametuangusha.

Ndugu yangu,

Akili wanazo, wengine shule ipo.... shangaa matendo!. Sasa naanza kufikiria wana pepo special ambapo kina Lwakatare au Mch. Msigwa wanapaswa kuwaombea rasmi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom