Speaker Makinda so is this "Wanawake Wakiwezeshwa Wanaweza?"

need i say more?

Unaweza kuwa na jambo la kujenga ukalisema. Kwa haraka ningeshauri bunge lifutwe tuu mana sioni mchango wake. Ila nachelea kusema hivyo kwa sababu mbili.Moja, wapo wabunge wachache ambao michango yao ni muhimu kwa ujenzi wa taifa na mbili mwenendo huu hovyo wa bunge pengine ukachangia katika wanachi kufanya maamuzi sahihi 2015 maana kama ndugai apendavyo kusema, ni kweli, wananchi wananona!
 
Nakubaliana na wewe moja kwa moja. Hivi kuna aliyewahi kufikiria ule mzuka wa viti maalum umetokea wapi? wanamwakilisha nani kama hautukuwachagua sisi? Hawaoni hata aibu kupewa pewa tu wakati wengine wanasota na kampeni?
mkuu vipi wale wa kuteuliwa na rais kama mbatia? Wanamuwakilisha nani?
 
Ndugu yangu,

Akili wanazo, wengine shule ipo.... shangaa matendo!. Sasa naanza kufikiria wana pepo special ambapo kina Lwakatare au Mch. Msigwa wanapaswa kuwaombea rasmi!
Huwa akili zao wanaziweka pembeni wanapojadili suala lenye maslahi kitaifa, ndiyo maana huoni wakilitetea taifa ila vyama vyao. Kutana nao baadA ya kikao wanayo yaongea watakushangaza mpaka utajiuliza kwanini hawakuongea wakiwa bungeni, jibu ni alipokuwa bungeni aliweka akili yake kubwa pembeni kutetea chama.

hamjamsikia NKAMIA akisema MCT haifanyi lolte, wakati ni hao hao MCT walimpeleka mpaka kwa WAHINDI KULE BARA ASIA kwenye mafunzo, leo anasema hawafanyi lolote ni NGO ya mtu, tatizo ni kuweka pembeni akili zao wawapo bungeni
 
kama kwa kigezo cha mwanamke spika wangu ni J.Mhagama na ndo hata akamatapo bunge huwa linaonyesha kuwa linaongozwa na kiongozi, na liongozwapo na Idd Zungu huwa ndo nafurahi na kupendezezwa na jinsi anavyoipotezea miongozo kwa pande zote pale ndani kwa kigezo cha kuichukua mwisho wa mjadala na kupelekea hoja kuchangiwa na wabunge wengi.

lakini kwa upande wa huyo mama na Job Ndugai ndo hovyo kabisa, wanajifanya wakali kwa kuficha udhaifu wao wa kutokujua kuongoza bunge. na laiti kama wangekuwa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2012 wangekuwemo miungoni mwa wale laki mbili na arubaini (240,000).
 
Swala hapa si wanawake kuwezeshwa,ni kweli hakuna mwanamke atakaye wezeshwa akashindwa.

Kinacho watatiza viongozi wa kike wengi tulionao,wako katika nafasi kwa mambo Mawili.

1. wamewekwa kwa makusudi maalum,hivyo wanaoongoza wako nyuma ya pazia.
2.wamepata nafasi,kama kulipwa fadhira.

kwa sababu hizo mbili,hatuna kiongozi bali ni watu walioshika nafasi.
 
Shame on them all.
 
True that! But hii inakatisha tamaa na inakera. Ifikie wakati waone aibu kwa kuweka agenda binafsi mbele na kusahau kutumikia wananchi.
 
Natoka nje kidogo ya mada ...mimi kuna jambo moja huwa linanisikitisha na kunishangaza sana kwa mama zetu na hawa dada zetu wa kitanzania....huu umaskini wetu ulioletwa na CCM unawaathiri sana wanawake kuliko wanaume lakini ukiangaliakwa asilimia kubwa sana wanajaza mikutano ya CCM na washabiki wakubwa sana wa CCM(hasa zikipita khanga)...hawa wakina dada zetu na mama zetu wa kitanzania kuna shida gani...?
 
Unaweza kuwa na jambo la kujenga ukalisema. Kwa haraka ningeshauri bunge lifutwe tuu mana sioni mchango wake. Ila nachelea kusema hivyo kwa sababu mbili.Moja, wapo wabunge wachache ambao michango yao ni muhimu kwa ujenzi wa taifa na mbili mwenendo huu hovyo wa bunge pengine ukachangia katika wanachi kufanya maamuzi sahihi 2015 maana kama ndugai apendavyo kusema, ni kweli, wananchi wananona!

Wabunge tunaoweza kuwategemea zaidi ni hawa wa upinzani, ambao nao kwa ajili ya uchache wao na migawanyiko wanakosa nguvu. Wapuuzi wengingine walobaki kama kina Lusinde na wenzake bado hawana maana kwani there is no point at all mtu mzima asimame kuchangia hotuba, atoe kasoro kibao then mwisho aunge mkono hoja 100%( Kama siyo ujinga alikuwa anakosoa nini?). Huu ni upuuzi wa kulindana na kutojali maslahi ya Taifa, tatizo zililopelekea kuwa na wezi wa maliza umma ambao wako huru na uchumi wa kusikitisha, huku tukibaki kuwa katika historia ya nchi zenye rasilimali lukuki.

Kwa maoni yangu, wanakoelekea hata vipofu wanaanza kuona upuuzi wao. Kote yalianza hivihivi.
 
kama kwa kigezo cha mwanamke spika wangu ni J.Mhagama na ndo hata akamatapo bunge huwa linaonyesha kuwa linaongozwa na kiongozi, na liongozwapo na Idd Zungu huwa ndo nafurahi na kupendezezwa na jinsi anavyoipotezea miongozo kwa pande zote pale ndani kwa kigezo cha kuichukua mwisho wa mjadala na kupelekea hoja kuchangiwa na wabunge wengi.

lakini kwa upande wa huyo mama na Job Ndugai ndo hovyo kabisa, wanajifanya wakali kwa kuficha udhaifu wao wa kutokujua kuongoza bunge. na laiti kama wangekuwa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2012 wangekuwemo miungoni mwa wale laki mbili na arubaini (240,000).

Mhagama naye ni tatizo. Bado ameonyesha kuwa na jazba na wakati mwingine ameshindwa kuwa fair kwenye maamuzi,hasa inapokuja kwenye ku-weigh hoja za upinzani na CCM. Zungu anatosha kuwa Spika kabisa. Nakubaliana na wewe na naamini waTanzania wengi wataunga mkono hoja.
 
Natoka nje kidogo ya mada ...mimi kuna jambo moja huwa linanisikitisha na kunishangaza sana kwa mama zetu na hawa dada zetu wa kitanzania....huu umaskini wetu ulioletwa na CCM unawaathiri sana wanawake kuliko wanaume lakini ukiangaliakwa asilimia kubwa sana wanajaza mikutano ya CCM na washabiki wakubwa sana wa CCM(hasa zikipita khanga)...hawa wakina dada zetu na mama zetu wa kitanzania kuna shida gani...?

Kwa maoni yangu,

Kwenye familia nyingi za kiTanzania mzigo wa kutunza familia huwa anao baba. Hata kwa wale ambao hawajaolewa bado mahawara zao ndiyo wanabeba mzigo. Na hata kwa madada poa bado wanategemea wanaume flani wawachukue ili wakatatue "matatizo yao"! Ukitaka kujiridhisha fuatilia hata wale wenye uwezo unaowajua, utagundua kuwa huenda hata mali wanazomiliki wengi wa wanawake unaowafahamu hawajachuma wenyewe. Mtu atakuwa na gari si kwa sababu anaweza kununua gari, ila kwa sababu alihongwa na mwanaume flani.( siyo wote ila wengi) Na kama hakuhongwa basi alipata nafasi ya kununua gari kwa kuwa baba alibeba majukumu yote ya maisha, hela yake ikaonekana haina kazi , akanunua gari. Au alitumia influence ya kuwa mwanamke tu kupata mkopo ambao hakuupotezea mda kufuata masharti. All in all, ni mwanaume ndiyo anabeba dhamana na uzito wa Uchumi mbovu! wanawake wapo ila wachache.

Kwa hiyo kama utasimama hadharani ukauliza kwa nini wana hali ngumu hawatakwambia serikali ni ya ovyo, watakwambia
baba ni mpuuzi, au mbahili au ana nyumba ndogo inamzuzua na mengine kama hayo. Kwa wengi wao baba ndiyo tataizo!

Kwa hiyo kwao kushabikia khanga na Tshirts za chama ni staili ya maisha. Kuwa kwenye CCM au CUF haina tofauti sasa na kuwa TOT au Zanzibar modern taarab. Kwao siasa haimaanishi mustakabali wa maisha. Ni ajabu kidogo
 
Akimaliza muda wake pale aatasema kwa nguvu zake alikuwa spika ambae ameendesha bunge kwa makini na kiwango cha juu!!yaani angeona comments za nchi za magharibi juu ya serikali yetu!basi tu wanakuja sababu ya ku balance gesi iliyopo!wamestuka sana china kupata deal zote!

Ndugu yangu Lambardi,
Kama unategemea hajui watu wanasemaje au kama unadhani yeye mwenyewe hajui anafanya madudu gani utakuwa uko mbali kidogo. Ukweli ni kwamba hata yeye anajua kuwa katika maspika wote tangu kina Sapi, Msekwa na Sitta ni yeye anayeongoza kwa kuboronga. Nna uhakika akimaliza haendi hata kwao kwani wote wanamwona kituko. Pia ataingia kwenye lile kundi linalokufa kifo cha kienyeji kisisasa kwani hataweza hata kuwa katika jamii ya viongozi wastaafu kwani ataondoka akiwa hana hata chembe ya heshima katika jamii ya kiTanzania. Kama unafikiri mimi natania angalia akimaliza muda wake atakavyojifukia.

Na usidhani anapenda la hasha! Ni kuwa tu amejua wakati ameshachelewa. Alishakubali kiti hana namna ya kukitelekeza. Kwa hiyo anajitahidi kubaki tu basi afanyeje huku waliomweka pale wakitegemea kulipwa fadhila kwa kukingiwa kifua kwenye hoja zinazowahusu. Na kwa kuwa alikubali tangu mwanzo hana la kufanya ila kuendelea kutumiwa tu.

Mh. Spika,
Najua hili siyo zuri kuliongea, lakini napenda ujue kuwa watu wanaona na wanafikiria, hata kama kuna wakati mnafanya mambo kama hii nchi mliinunua na ni mali binafsi.
 
This lady is a puppet. Inasikitisha kumsema hivi kwani alikuwa ni mama mmoja ninayemheshimu sana kabla ya kuwa spika. Mama Makinda anafanya maamuzi ya msingi au ya nchi kwa kuegemea upande mmoja ambao ni wa chama chake tawala (CCM). CCM pamoja na viongozi wake wote wamepitwa na wakati na hawana jipya katika kuendeleza nchi yetu, hivyo Mama Makinda kama kweli anataka kuleta hoja za maana bungeni inambidi awe neutral ila si kutumia ubabe wa kijinga wa wana CCM. CCM haipendi maendeleo na haitaki Tanzania iendelee kwani wakileta maendeleo hapa nchini wataibaje hela na kutajirisha familia zao?
 
Uko barabarani sana ndugu yangu. Maendeleo wanayataka. Ila tatizo ni kuwa kila mtu ni mwizi ndani ya serikali. Pale inapotokea Kiongozi mkuu wa nchi ana tuhuma za ufisadi unafikiri nani tena atakemea uhujumu?

Umaskini unakuja tu kwa kuwa tabia ya mafisadi hawa ni kufilisi mali na rasilimali za taifa na kuzihamishia mifukoni mwao. Siyo kweli kwamba serikali haioni viwanda vilivyobinafsishwa vinakufa. Kwa nini wawekezaji hawabanwi ili hali kuna mikataba ya kuwabana kama hawazalishi? Ila kwa kuwa lengo ni kuua viwanda ili bidhaa hizo hizo ziiingizwe na wafanyabiashara kutoka nje, wafanyabiashara ambao ni wao wenyewe, sidhani kama watauliza kwa nini viwanda haviendelei! Na ni kwa sababu hiyo hiyo tmefikia kuagiza mpaka pamba za masikio na tooth pick ili hali pamba tunalima wenyewe na miti tunayo. Shangaa viwanda vya tooth pick na pamba za masikio vingegharimu shilingi ngapi! Inatia aibu kuwa magari kutengeneza tumeshindwa, hata kuviringa pamba kwenye vijiti tu napo tumeshindwa! Nchi ya ajabu kwelikweli!

Kwamba hushangai ni kwa nini shirika la ndege lina filisika wakati ambapo kuna ndege za mtu binafsi ndiyi zinashamiri? Au hushangai ni kwa nini bandari haina matairi haitumii mafuta eti nayo inashindwa kujiendesha? Kwani huoni maajabu kuwa kuna watu wenye dhamana ya kuendesha makampuni na mashrika hayo na bado wapo huru mitaani? hushangai wakaguzi (Auditors) huwa wanafanaya nini? wanakagua wapi kama wameshindwa kugundua upotevu wa fedha? Na wao bado wanadunda mtaani huru kabisa?

Ndiyo maana mie nahitimisha kwa kusema hii serikali ya CCM haitufai kabisa kwa sasa. Haina uchungu na nchi yetu kama ambavyo haina uwezo wa kutatua matatizo ambayo yenyewe ndiyo chanzo. Kwa mtizamo wangu hawa upeo wao ndiyo umeishia hapo, hawana jipya. Waache akili tofauti ije kutatua matatizo ya upuuzi wao. Na sitashangaa kwa kwa jinsi walivyo binadamu wa ajabu wasio na haya, watakavyong'ang'ania madaraka mpaka damu imwagike, wakati wanaona hali ya nch ni mbaya!
Laiti wangekuwa wazalendo! wangeshakiri kushindwa! Laiti wangekuwa na uchungu japo kidogo kwa nchi hii! Wangejua ni wao ndiyo wataabishaji wa Nchi hii. Wangekuwa wa kwanza kuweka tofauti za ajabu pembeni na kuitisha kila nguvu inayoweza kupatikana ili kuinusuru nchi. Mkionacho sasa ni ishara ya ubinafsi uliokithiri na kukosa uchungu na Nchi yetu
 
Na Naibu wake ni mwanamke?
Wawaziri kibao wanaovurundwa ni wanawake?
Mkuu wa kaya ni mwanamke?
Yule aliwekwa strategically, kwanza as an excuse ya kumtoa Sitta, so uanamke ulitumika tu ili kelele zipungue; lkn sio kumpa mwanamke nafasi.
Ukishakuwa gamba ni lazima ukinde maslahi ya gamba na sio wananchi na ndio maana wanaojaribu (fikikunjombe mfn) wanapata wakati mgumu sana.

Wanawake tunaweza na tumeweza mengi tu most of them never documented na ndio maana, dunia imefika hapa ilipo. Na haihitajiki kila mwanamke kuwa politician ili apimwe uwezo wa KUWEZA.

Sure! ni kweli wote hao siyo wanawake kama ulivyosema. Nilichokuwa nasema hasa ni kuwa Spika huyu kama political figure amekuwa mfano mbovu kabisa wa jinsi wanawake wanavyowakilishwa. Siyo tu kuwa anakatisha tamaa, anatia aibu pia hasa kwa kuwa nilitegemea yeye awe mfano kwenye harakati za kumkomboa mwanamke! Kwa haraka ni kuwa ametumia nafasi yake VIBAYA hasa kwa vile tulidhani "Wakiwezeshwa Wanaweza!"

Na kama nilivyosema tatizo siyo kuwa mwanamke. Tatizo ni kuacha kufanya wajibu wake kama spika wa bunge, kubwaga majukumu ya kuwakomboa kinamama wenzie kama vila hayamhusu na kujitwika bila haya kazi ya kutetea CCM, jambo ambalo kwa nafasi yake hakupaswa kabisa kulifanya. And that my dear.., is a shame!
 
Niliwai kupost uzi kama kuna uwezekano wa wa spika mwanamke kuchaguliwa tena...........bibi huyu anajiabisha pale mbele, anaona sifa kutoa comments za kijinga....TS NOT FUNNY ANYMO....Just one ding MAKINDA...mm pia ni mwanamke, a lady actually, c ambitions za kuongoza....but I would rather be not lead ...kuliko kuishi mtumwa, ua killing our dreams,and someday u'll b answerable to God...

I wish wanaompelekea habari wamwonyeshe na posti ya huyu dada !
 
What she has done needs to go into the books of history!
Posponing the Bunge activities while the MP's doing nothing in rescue of the situation is more or less useless!
Hata watakachofanya baada ya kukutana ni kutafuta mchawi na si kujadili root cause ya shida hii!

Most likely iko hivyo. nilitegemea itakuwa like " nasitisha shughuli za kawaida za bunge ili tujadili kwa kina utata wa Swala la gesi Mtwara"... It was like hawajui kama wana dhamana ya kuamua kwa niaba ya wananchi!
 
Uko barabarani sana ndugu yangu. Maendeleo wanayataka. Ila tatizo ni kuwa kila mtu ni mwizi ndani ya serikali. Pale inapotokea Kiongozi mkuu wa nchi ana tuhuma za ufisadi unafikiri nani tena atakemea uhujumu?

Umaskini unakuja tu kwa kuwa tabia ya mafisadi hawa ni kufilisi mali na rasilimali za taifa na kuzihamishia mifukoni mwao. Siyo kweli kwamba serikali haioni viwanda vilivyobinafsishwa vinakufa. Kwa nini wawekezaji hawabanwi ili hali kuna mikataba ya kuwabana kama hawazalishi? Ila kwa kuwa lengo ni kuua viwanda ili bidhaa hizo hizo ziiingizwe na wafanyabiashara kutoka nje, wafanyabiashara ambao ni wao wenyewe, sidhani kama watauliza kwa nini viwanda haviendelei! Na ni kwa sababu hiyo hiyo tmefikia kuagiza mpaka pamba za masikio na tooth pick ili hali pamba tunalima wenyewe na miti tunayo. Shangaa viwanda vya tooth pick na pamba za masikio vingegharimu shilingi ngapi! Inatia aibu kuwa magari kutengeneza tumeshindwa, hata kuviringa pamba kwenye vijiti tu napo tumeshindwa! Nchi ya ajabu kwelikweli!

Kwamba hushangai ni kwa nini shirika la ndege lina filisika wakati ambapo kuna ndege za mtu binafsi ndiyi zinashamiri? Au hushangai ni kwa nini bandari haina matairi haitumii mafuta eti nayo inashindwa kujiendesha? Kwani huoni maajabu kuwa kuna watu wenye dhamana ya kuendesha makampuni na mashrika hayo na bado wapo huru mitaani? hushangai wakaguzi (Auditors) huwa wanafanaya nini? wanakagua wapi kama wameshindwa kugundua upotevu wa fedha? Na wao bado wanadunda mtaani huru kabisa?

Ndiyo maana mie nahitimisha kwa kusema hii serikali ya CCM haitufai kabisa kwa sasa. Haina uchungu na nchi yetu kama ambavyo haina uwezo wa kutatua matatizo ambayo yenyewe ndiyo chanzo. Kwa mtizamo wangu hawa upeo wao ndiyo umeishia hapo, hawana jipya. Waache akili tofauti ije kutatua matatizo ya upuuzi wao. Na sitashangaa kwa kwa jinsi walivyo binadamu wa ajabu wasio na haya, watakavyong'ang'ania madaraka mpaka damu imwagike, wakati wanaona hali ya nch ni mbaya!
Laiti wangekuwa wazalendo! wangeshakiri kushindwa! Laiti wangekuwa na uchungu japo kidogo kwa nchi hii! Wangejua ni wao ndiyo wataabishaji wa Nchi hii. Wangekuwa wa kwanza kuweka tofauti za ajabu pembeni na kuitisha kila nguvu inayoweza kupatikana ili kuinusuru nchi. Mkionacho sasa ni ishara ya ubinafsi uliokithiri na kukosa uchungu na Nchi yetu

Elly B shikamoo na pia naomba ninywe chai kwa niaba yako this morning. Siyo kama sitaki kukualika ila niko mbali na nyumbani kwa sasa. Yote uliyo ongea ni ya kweli na inasikitisha sana kutawaliwa na watu wasio na upeo wa maendeleo. Yaani watu wanaiba Tanzania kama hawana akili kushindana na rais wao. Kikwete as a president hawezi kusema kitu kwani anajuwa akiwachukulia hatua hawa watu (mawaziri wezi) huenda watamgeuka na kumshtaki yeye ndiyo maana amekuwa mtu wa kucheka kwa kutopenda. Najiuliza siku zote hivi ni kwa nini jeshi letu lisichukue nchi mpaka hapo 2015? Waafrika wenzetu wameweza kujikomboa toka kwa utawala wa kipuuzi kwa nini sisi tusindwe? Jeshi la TZ liko wapi jamani? Kikwete hatufai anaangusha nchi huyu mtu jamani, enough is enough.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu Lambardi,
Kama unategemea hajui watu wanasemaje au kama unadhani yeye mwenyewe hajui anafanya madudu gani utakuwa uko mbali kidogo. Ukweli ni kwamba hata yeye anajua kuwa katika maspika wote tangu kina Sapi, Msekwa na Sitta ni yeye anayeongoza kwa kuboronga. Nna uhakika akimaliza haendi hata kwao kwani wote wanamwona kituko. Pia ataingia kwenye lile kundi linalokufa kifo cha kienyeji kisisasa kwani hataweza hata kuwa katika jamii ya viongozi wastaafu kwani ataondoka akiwa hana hata chembe ya heshima katika jamii ya kiTanzania. Kama unafikiri mimi natania angalia akimaliza muda wake atakavyojifukia.

Na usidhani anapenda la hasha! Ni kuwa tu amejua wakati ameshachelewa. Alishakubali kiti hana namna ya kukitelekeza. Kwa hiyo anajitahidi kubaki tu basi afanyeje huku waliomweka pale waktegemea kulipwa fadhila kwa kukingiwa kifua kwenye hoja zinazowahusu. Na kwa kuwa alikubali tangu mwanzo hana la kufanya ila kuendelea kutumiwa tu.

Mh. Spika,
Najua hili siyo zuri kuliongea, lakini napenda ujue kuwa watu wanaona na wanafikiria, hata kama kuna wakati mnafanya mambo kama hii nchi mliinunua na ni mali binafsi.

Dada yangu Elly B wacha dhambi. Yaani unataka kuniambia kuwa Makinda anajuwa kuwa anaboronga? Kama ni kweli basi hata yeye mwenyewe hajitendei haki kwani anafanya madudu anayotumwa na viongozi wa CCM haswa Bw. Vituko (JK). Kwa kweli huyu mama anajidhalilisha sana, hivi kuna mwenye namba zake za simu huyu mama nimpigie?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom