Speaker Makinda so is this "Wanawake Wakiwezeshwa Wanaweza?"

Speaker Makinda so is this "Wanawake Wakiwezeshwa Wanaweza?"

Wanawake!! Wanawake!! Asha Rose Migiro aliwezeshwa huko UN, akapwaya vibaya!! Gertrude Mongera aliwezeshwa AU, akakwapua hadi furniture za ofisi!! Makinda aliwezeshwa, lakini ni balaa; hadi anatia kinyaa kama sio kichefuchefu!!! Poleni wanawake!
 
Akimaliza muda wake pale aatasema kwa nguvu zake alikuwa spika ambae ameendesha bunge kwa makini na kiwango cha juu!!yaani angeona comments za nchi za magharibi juu ya serikali yetu!basi tu wanakuja sababu ya ku balance gesi iliyopo!wamestuka sana china kupata deal zote!
 
Na Naibu wake ni mwanamke?
Wawaziri kibao wanaovurundwa ni wanawake?
Mkuu wa kaya ni mwanamke?
Yule aliwekwa strategically, kwanza as an excuse ya kumtoa Sitta, so uanamke ulitumika tu ili kelele zipungue; lkn sio kumpa mwanamke nafasi.
Ukishakuwa gamba ni lazima ukinde maslahi ya gamba na sio wananchi na ndio maana wanaojaribu (fikikunjombe mfn) wanapata wakati mgumu sana.

Wanawake tunaweza na tumeweza mengi tu most of them never documented na ndio maana, dunia imefika hapa ilipo. Na haihitajiki kila mwanamke kuwa politician ili apimwe uwezo wa KUWEZA.
 
The strategies used by Speaker Makinda to solve the crisiss at Mtwara are too local, outdated and can not work at all.
 
What she has done needs to go into the books of history!
Posponing the Bunge activities while the MP's doing nothing in rescue of the situation is more or less useless!
Hata watakachofanya baada ya kukutana ni kutafuta mchawi na si kujadili root cause ya shida hii!
 
"Always Do the Right Thing Even if is a Little Dangerous;Thats how a Man Defines Himself!"
hicho kitu ulichokiandika naamini ndio falsafa yako so lazima ukifuate

Hasa maana ya falsafa hiyo ni kuwataka watu wasinyamaze tu hata kama wanaumia bila sababu za kuridhisha. Wakati wa uhujumu uchumi miaka ya 70 Mwalimu aliwaomba waTanzania wafunge mikanda ili kulinusuru Taifa kutokana na kuanguka kwa uchumi. Wananchi walimwelewa kwa sababu walijua kuwa mbele kutakuja kheri. Hivi leo hawa wana excuse gani? Watanzania wavumilie ili kije nini?

Cha kusikitisha is like serikali hii haiskii lugha nyingine zaidi ya vurugu. Mikopo ya wanavyuo mpaka wagome! Wananchi kudai maendeleo mpaka waandamane!

Siwaambii watu wafanye fujo asilani. Ila na serikali iamke. Watu hawa hawatakuwa hivi forever. Leo polisi watasaidia, kesho jeshi. Sawa ila kuna siku itaandamana Nchi nzima. Hapo sijui watapeleka nini?

Narudia kitu nilichowahi kusema kitambo.." Kama nchi hii itaingia kwenye machafuko, siyo kwa sasababu ya wapinzani, ni kwa sababu serikali imeyasababisha!
 
The strategies used by Speaker
Makinda to solve the crisiss at
Mtwara are too local, outdated and
can not work at all.
 
Hasa maana ya falsafa hiyo ni kuwataka watu wasinyamaze tu hata kama wanaumia bila sababu za kuridhisha. Wakati wa uhujumu uchumi miaka ya 70 Mwalimu aliwaomba waTanzania wafunge mikanda ili kulinusuru Taifa kutokana na kuanguka kwa uchumi. Wananchi walimwelewa kwa sababu walijua kuwa mbele kutakuja kheri. Hivi leo hawa wana excuse gani? Watanzania wavumilie ili kije nini?

Cha kusikitisha is like serikali hii haiskii lugha nyingine zaidi ya vurugu. Mikopo ya wanavyuo mpaka wagome! Wananchi kudai maendeleo mpaka waandamane!

Siwaambii watu wafanye fujo asilani. Ila na serikali iamke. Watu hawa hawatakuwa hivi forever. Leo polisi watasaidia, kesho jeshi. Sawa ila kuna siku itaandamana Nchi nzima. Hapo sijui watapeleka nini?

Narudia kitu nilichowahi kusema kitambo.." Kama nchi hii itaingia kwenye machafuko, siyo kwa sasababu ya wapinzani, ni kwa sababu serikali imeyasababisha!
Malcom X alishawahi kusema kitu kama hiki"I am for violence if non-violence means we continue postponing a solution to the American black man's problem just to avoid violence."

Ni wazo zuri ambalo linaweza kutufikisha tunapopataka na hicho ndicho tunachotakiwa kukifanya na sio kuendelea kushikilia wimbo wetu wa Tanzania ni kisiwa cha amani wakati tukijua wazi kwamba wanaoihubiri hiyo amani ndio haohao wanaotuibia mali zetu.
 
Mkuu, qualification ilikuwa ni jinsia ya kike hivyo Mhe.Samwel Sitta hakuwa na hiyo sifa........................
 
Mkuu, Tatizo lilikuwa kwamba CCM waliongeza sifa kwenye chama ya kuwa spika lazima awe mwanamke hivyo Mhe.Samwel Sitta akakosa...............Walimuandaa Chenge ila JK haamini mioyo hata ya wabunge wa CCM hivyo hakutaka kufanya Jaribio
 
Wanawake!! Wanawake!! Asha Rose Migiro aliwezeshwa huko UN, akapwaya vibaya!! Gertrude Mongera aliwezeshwa AU, akakwapua hadi furniture za ofisi!! Makinda aliwezeshwa, lakini ni balaa; hadi anatia kinyaa kama sio kichefuchefu!!! Poleni wanawake!

Please do not put all women in one basket. There are women who are very able. Kama hao walishindwa hawawakilishi wanawake wote. Kila mtu ahukumiwe as an individual. Kwa kweli Mongella alikuwa strong ila sifahamu ni kitu gani kilimfanya afanye yale madudu alipokuwa kwenye Bunge la Afrika. Tatizo la baadhi ya wanawake ni kuwategemea wanaume katika kufanya maamuzi. Wakati mwingine wanawake hao wanakuwa wamewekwa kwenye nafasi hizo kwa makusudi maalum na kwa sababu hiyo haitakuwa rahisi kwao kwenda kinyume na matakwa ya waliowaweka. Kumbukeni kuwa kwenye mcahakto wa kuandaa katiba mpya Makinda amependekeza spika asifungamane na chama cha siasa. Kuna kitu hidden hapa. Pengine anaona yeye anashindwa kuwa yeye kwa kuwa ni lazima atii masharti ya chama chake. So, wanawake wote wasionekane kuwa hawawezi. Wengi wao wanaweza kama wataaminiwa na kuachwa wafanye maamuzi wanayoona ni sahihi. na wale walioko ninawashauri wasiende kulialia kwa wanaume ili wawaonee huruma. Stand up with all confidence. Remember people learn through mistakes. Kama wewe mwanamke kiongozi umewahi kufanya kosa usilirudie. Kumbuka kufanya kosa si kosa, bali kosa ni kurudia kosa.:target:
 
Niliwai kupost uzi kama kuna uwezekano wa wa spika mwanamke kuchaguliwa tena...........bibi huyu anajiabisha pale mbele, anaona sifa kutoa comments za kijinga....TS NOT FUNNY ANYMO....Just one ding MAKINDA...mm pia ni mwanamke, a lady actually, c ambitions za kuongoza....but I would rather be not lead ...kuliko kuishi mtumwa, ua killing our dreams,and someday u'll b answerable to God...
 
Matukio mbali mbali yamekuwa yanajitokeza katika siku za karibuni ikiwa ni pamoja na-;
1. Uchomwaji wa makanisa
2.Kuteshwa/kuuwawa kwa waandishi wa habari
3.Kuteshwa/kuuwawa viongozi wa dini
4. Serikali kuingia mikataba ya hovyo
5.mafisadi kutokuchukuliwa sheria n.k
matukio yote yamekuwa yakitokea kutokana na udhaifu wa bunge kutokutaka kuisimamia serikali na kuona kuwa kuisimamia ni kuidhoofisha mfano yaliyotokea mtwara bunge likiamua ambacho wananchi wanataka na wala si serikali ni kazi ndogo tu ni kutopitisha bajeti mpaka irekebishwe katika suala flani tena kwa kauli moja lakini wanaachia kakundi kadogo kaamue na wao kupitisha wasichokijua mfano mwingine ni kama wizara ya fedha hatupitishi mpaka majina ya epa yaletwe bungeni, wizara ya elimu hatupitishi mpaka kawambwa ajiuzuru n.k
mytake
namuunga mkono mheshimiwa John john mnyika kwa kueleza kuwa bunge ni dhaifu dhidi ya serikali japo lina nguvu zaidi ya serikali kwa kutotumia nguvu na kuishia kujikomba kwa serikali. Ilitakiwa mawaziri wakisikia bunge linaanza vichwa viwaume lakini hali ni tofauti
na hapa nawazungumzia wabunge wa ccm, cuf ambao wanapenda kuishauri badala ya kuisimamia serikali
naomba kutoa hoja
 
Mkuu, Tatizo lilikuwa kwamba CCM waliongeza sifa kwenye chama ya kuwa spika lazima awe mwanamke hivyo Mhe.Samwel Sitta akakosa...............Walimuandaa Chenge ila JK haamini mioyo hata ya wabunge wa CCM hivyo hakutaka kufanya Jaribio

May be true. But why am I smelling this awkward smell as if they did it on purpose so they can hold off upinzani? Is like hawakutaka makosa ya Sitta yajirudie, so wakamweka huyo mtu kwa kuwa historia yake ya nyuma inaonyesha hajui kufikiria. "She wouldn't have had balls". But she doesn't have guts either.
 
Anachoweza ni mziki.
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1369318559822.jpg
    uploadfromtaptalk1369318559822.jpg
    48.7 KB · Views: 65
Ni kweli kabisa mheshimiwa,mimi nashikwa na butwa kwani serikali inataka mitambo ijengwe Mtwara lakini viongozi wa serikali hawataki(wananchi ndiyo serikali na viongozi ni viongozi tu wala wao si serikali km wanavyodhani) tatizo lipo kwenye muhimili wa kibunge umeshindwa kuwa msimamizi wa serikali na hautaweza kuisimamia labda km tutapata katibu yenye mwelekeo wa kupata bunge lenye uwezo wa kuisimamia serikali,wabunge wetu wengi ni ccm na pia ndio mawaziri wa serikali hiyohiyo ,sasa ujiulize nani kumsimia nani?
 
Tanzania tumerithi mengi toka uingereza. Moja ya mambo hayo ni mfumo wa bunge ingawa hatukurithi kila kitu. Bunge la Uingereza lilikuwa na hata sasa bado ni supreme juu ya serikali na mahakama. Nguvu za bunge la uingereza ni kubwa sana kiasi kwamba linaweza kupitisha sheria itakayoondoa uwepo wa dola hiyo, na imesemekana kuwa, linaweza hata kupitishia sheria inayoweza kubadili jinsia ya mtu.

Pamoja na Tanzania kurithi kutoka uingereza mifumo mingi, iliamua kurithi pia mfumo wa supremacy of parliament ingawa iliamua kuwaweka wananchi juu ya yote (Article8(1)(a)). Madaraka haya yaliyowekwa kwa watu yamekasimiwa kwa bunge na hivyo wabunge wanafanya kazi kwa niaba ya watu!Ndio maana Artcle 4(1) imelipa bunge legislative and supervisory powers.Ni bunge hili hili kwa nguvu zake linaweza kumwondolea kinga raisi na kisha kumshtaki(Art46A). Ni bunge hili ambalo kwa mujibu wa ibara ya 63(2) limepewa power to oversee and advise Government and all its organs in discharging thier respective responsibilities. Bunge hili ni sauti ya wananchi.

Hata hivyo yanayotokea sasa ni kinyume na tamaduni na asili ya bunge. Tanzania imeamua kurudi miaka ya sabini ambapo bunge lilikuwa ni sehemu ya chama cha mapinduzi. Kwamba jambo linakubaliwa na ccm kwanza kisha bunge linalipa jambo hilo uhalali wa kisheria(rubber stamping). Bunge haliwasemei wananchi badala yake linaisemea serikali. Yaani bunge limekuwa kama ni baraza la mawaziri. Wabunge wameamua kuisemea serikali kuliko mawaziri wenyewe.

Kitendo cha Makinda kuahirisha bunge kila yatokeapo maswala mazito kitaifa hakikubaliki. Ni sawa na kuwaziba mdono wananchi. Huu ni mpango unaoakisi ndoa ya serikali na bunge wenye lengo la kuhakikisha bunge haliisimamii serikali vyema. Ni dharau kwa wananchi. Kisingizio cha kuwa hatuna information ni uongo. Hivi tukisikia Wamalawi wametwaa ziwa nyasa tutaahirisha bunge ili kusubiri kauli ya serikali? Who is supreme between the people and the poor gvt like this one? Janja hii ya kuzuia mamboya msingi kwa kisingizio cha taarifs ni uhuni kama uhuni mwingine. Bunge lina wabunge ambao ni wananchi na wanapata taarifa kama wananchi wengine. Utaratibu wa kusubiria serikali kutoa taarifa ni uvivu na malezi hovyo ya serikali na chama chake.

Ndio maana nasema hili bunge ni majanga tuu! Na hatutamsahau Makinda kwa uongozi mbovu kabisa wa bunge kupata kutokea Afrika mashariki na kusini mwa sahara. Majanga matupu.
 
Bunge gani hili lisiloweza kujadili crucial issues, wanapoahirisha bunge kwenye suala amabalo waTz wanapoteza maisha kwa suala ambalo kama lingejadiliwa vizuri bungeni bila prejudice lazima utatuzi ungepatikana.
Ni upuuzi kwa kila mbunge wa ccm na spika wake kutekeleza majukumu yake huku mawazo yake yakitarajia uteuzi wa Rais, huo ndiyo ugonjwa mkubwa wa Bunge letu. Nilisikia JK anawaagiza wabunge wa Ccm kwamba WAISHAURI SERIKALI LAKINI WASIIBOMOE SERIKALI, nikajiuliza kwa serikali hii ya leo ni ushauri upi wa mbunge unaweza kutekelezwa. Kuna ushauri mzuri mno tena sana unaotolewa na wabunge wa kambi ya upinzani lakini majibu yanayotolewa na serikali ni UCHOCHEZI wa Chadema tutafika wapi! Ki ukweli Serikali imeshindwa akili zao zimefikia ukomo.
 
Back
Top Bottom