TANZIA Sophia Nyerere, Mjukuu wa Baba wa Taifa afariki Dunia

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,110
2,000
Sophia Nyerere, ambaye ni Mjukuu wa Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere, amefariki dunia leo Jumanne katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu. Marehemu Sophia ni Mtoto wa John Nyerere.

====

SOPHIA Nyerere, ambaye ni mjukuu wa Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Julius Nyerere, amefariki dunia leo Jumanne, tarehe 27 Julai 2021, mkoani Dar es Salaam.

Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo na familia ya Nyerere, ambayo imesema Sophia amefariki dunia kwenye Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu.

Marehemu Sophia alikuwa Mtoto wa Hayati John Nyerere, aliyefariki dunia Mei 2015. John alikuwa mtoto wa nne wa Mwalimu Nyerere.

Taarifa ya familia hiyo imesema, kwa sasa msiba uko nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, maeneo ya Mikocheni mkoani Dar es Salaam.

E7TOV7vXIAAHmxt.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom