Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,147
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia kwa waziri wake, Mheshimiwa Hamad Rashid imesema misikiti kadhaa ndani ya nchi ya Zanzibar imefungwa kabisa kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan ili kuepuka kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
Hata hivyo ameshindwa kufafanua kama hatua hiyo imetokana na amri ya serikali, hiyari ya waumini au ushauri kutoka kwa wataalamu wa Afya.
Pia SMZ imeamua kununua mashine maalum ya maabara ya kupima virusi vya Corona na wakati wowote itawasili Zanzibar na kuanza kufanya kazi. Siku zote Zanzibar imekuwa ikitumia maabara kuu ya Tanzania iliyopo Dar kupima sampuli za wagonjwa wa Corona.
Hatua hii inatazamiwa kuirahisishia Zanzibar kupima na kupata majibu kwa haraka na uhakika kwa watu waliopo Zanzibar huku ikiondoa urasimu wa upimaji uliopo katika maabara ya Dar ambayo inasemekana kwa sasa kusitisha kwa muda usiofahamika upimaji Corona/utoaji wa majibu ili kupisha uchunguzi wa shutuma za kudaiwa kuchakachua majibu ya vipimo vya Corona, madai ambayo yalitolewa na Mheshimiwa Rais wa Tanzania.
Chanzo: BBC-swahili