#COVID19 Wachina washikamana kukabiliana na virusi vya Corona

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111413547676.jpg
Wiki mbili zilizopita, ghafla nilipata homa kali na maumivu makali mwili mzima. Mke wangu alikwenda katika maduka mbalimbali ya dawa karibu na nyumbani kwetu ili kutafuta dawa, lakini alirudi mikono mitupu. Siku mbili baadaye, mimi, mke wangu pamoja na mtoto wetu sote tulipatwa na virusi vya Corona. Niliomba msaada kupitia mtandao wa kijamii, na siku hiyohiyo, zaidi ya watu 30 wakiwemo majirani, marafiki na wafanyakazi wenzangu walinijulia hali na kutaka kunipa dawa. Mwishowe, jirani yangu mmoja alituletea dawa za kupunguza homa, na wiki moja baadaye tulipata nafuu.

Kutokana na kupungua kwa sumu ya virusi vya Corona aina ya Omicron na kuongezeka kwa maambukizi yake, mwanzoni mwa mwezi Desemba, China ilianza kulegeza hatua kali za awali za kudhibiti virusi. Chini ya hali mpya ya kuenea kwa kasi kwa virusi vya Corona, kila mtu amekabiliwa na hatari ya kuambukizwa virusi hivyo moja kwa moja. Serikali imechukua hatua za kuimarisha mwongozo na kuratibu rasilimali, na watu binafsi wameshikamana ili kushinda virusi.

Kama nchi kubwa yenye idadi ya watu bilioni 1.4, chini ya maambukizi ya haraka ya virusi, ni wazi kwamba China imekabiliwa na uhaba wa rasilimali za kukabiliana na virusi, haswa dawa na vifaa ya kupima virusi ndani ya muda mfupi. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Baraza la Serikali ya China limeagiza kuongeza kasi ya utengenezaji na upangaji wa vifaa muhimu kama vile dawa na chanjo. Hospitali nyingi nchini China zimeongeza nguvu katika kuhudumia watu wenye homa, hata katika baadhi ya miji, serikali imebadilisha vibanda vya kupima virusi vilivyoko kila mahali kuwa vituo vya muda vya matibabu ya homa, ambapo madaktari wanatibu wagonjwa na kuwapatia dawa zinazohitajika. Licha ya hayo, China pia inahimiza chanjo kwa nguvu zaidi, na hivi karibuni kiwango cha utoaji wa chanjo kwa kila siku kimeongezeka zaidi ya mara mbili kuliko hapo awali.

Mbali na hatua zilizochukuliwa na serikali, watu wa jamii mbalimbali nchini China wameshikamana na kusaidiana katika vita hiyo dhidi ya virusi. Katika makazi ya mijini, watu wanasaidiana dawa na vifaa vya kupima virusi kupitia mitandao ya kijamii, na pia wameanzisha “masanduku ya dawa za upenzi” kwenye makazi ili kuwasaidia wale watu wasio na dawa. Kwa wazee wanaoishi peke yao na wasio na uwezo wa kutembea, watu wa kujitolea wamewasaidia mambo yote yakiwemo kuwaletea dawa, na kuwanunuliwa chakula. Wiki iliyopita, wakati Beijing ilipokabiliwa na uhaba wa wasambazaji wa vifurushi kutokana na maambukizi ya virusi, baadhi ya makampuni ya kusafirisha vifurushi yalituma zaidi ya wafanyakazi 2,300 kutoka sehemu nyingine hadi Beijing ili kutoa msaada.

Kupitia juhudi za pamoja, China hatimaye itashinda vita hiyo dhidi ya virusi vya Corona.
 
waliniuzi kipindi kile madaktari wamejua ugonjwa wao wakawa wanaficha mpaka ukasambaa dunia nzima.
itakuwa walifanya makusudi
 
Back
Top Bottom