SMZ: Baadhi ya misikiti yafungwa kabisa Zanzibar kuepuka maambukizi zaidi ya Corona

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,741
2,000
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia kwa waziri wake, Mheshimiwa Hamad Rashid imesema misikiti kadhaa ndani ya nchi ya Zanzibar imefungwa kabisa kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan ili kuepuka kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Hata hivyo ameshindwa kufafanua kama hatua hiyo imetokana na amri ya serikali, hiyari ya waumini au ushauri kutoka kwa wataalamu wa Afya.

Pia SMZ imeamua kununua mashine maalum ya maabara ya kupima virusi vya Corona na wakati wowote itawasili Zanzibar na kuanza kufanya kazi. Siku zote Zanzibar imekuwa ikitumia maabara kuu ya Tanzania iliyopo Dar kupima sampuli za wagonjwa wa Corona.

Hatua hii inatazamiwa kuirahisishia Zanzibar kupima na kupata majibu kwa haraka na uhakika kwa watu waliopo Zanzibar huku ikiondoa urasimu wa upimaji uliopo katika maabara ya Dar ambayo inasemekana kwa sasa kusitisha kwa muda usiofahamika upimaji Corona/utoaji wa majibu ili kupisha uchunguzi wa shutuma za kudaiwa kuchakachua majibu ya vipimo vya Corona, madai ambayo yalitolewa na Mheshimiwa Rais wa Tanzania.

Chanzo: BBC-swahili
 

Daemusin

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
14,180
2,000
msikiti wa nyumbani tunasali umbali wa takribani meter 1 haijalishi iwe ni sala ya jam'aa.

baadhi ya wanazuoni wanapingana sheria hiyo hivyo basi huamua kuifunga misikiti...
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,589
2,000
Huku bara walijaribu hilo wakaambiwa na mkulu 'nyumba zenyewe hizo za ibada mnazifunga utafikiri mlizijenga wenyewe',keshokutwa yake pale kwa mtoro pakafunguliwa chap.
 

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,902
2,000
kama umeona lockdown inanukia mikono juu,tutasalimu tu.
Pilipili ikiwasha sana lazima unywe maji.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
81,833
2,000
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia kwa waziri wake, Mheshimiwa Hamad Rashid imesema misikiti kadhaa ndani ya nchi ya Zanzibar imefungwa kabisa kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan ili kuepuka kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Hata hivyo ameshindwa kufafanua kama hatua hiyo imetokana na amri ya serikali, hiyari ya waumini au ushauri kutoka kwa wataalamu wa Afya.

Pia SMZ imeamua kununua mashine maalum ya maabara ya kupima virusi vya Corona na wakati wowote itawasili Zanzibar na kuanza kufanya kazi. Siku zote Zanzibar imekuwa ikitumia maabara kuu ya Tanzania iliyopo Dar kupima sampuli za wagonjwa wa Corona. Hatua hii inatazamiwa kuirahisishia Zanzibar kupima na kupata majibu kwa haraka na uhakika kwa watu waliopo Zanzibar huku ikiondoa urasimu wa upimaji uliopo katika maabara ya Dar ambayo inasemekana kwa sasa kusitisha kwa muda usiofahamika upimaji Corona/utoaji wa majibu ili kupisha uchunguzi wa shutuma za kudaiwa kuchakachua majibu ya vipimo vya Corona, madai ambayo yalitolewa na Mheshimiwa Rais wa Tanzania.

SOURCE: BBC-swahili
Mungu ibariki Jamhuri ya watu wa Zanzibar
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,710
2,000
Hivi ukisali nyumbani kwako Mungu hakusikii?

Wafuasi wa Kibwetere bado wanaishi!

Inakubali sana tu kama kuna hali ya hatari au maambukizo kama haya kujitenga ni amri sio ombi Mkuu ila watu ni wabishi na hawasomi historia


Sent from my iPhone using Tapatalk
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom