Sms iliyoniumiza kupita zote

Sms iliyoniumiza kupita zote

Shukuru mungu kakwambia so tafuta sehemu nzuri na kumweleza yote hayo na kumweleza umuhimu wa uwazi na faida zake katika mahusiano
 
Kupigwa kibuti nilisha wahi pigwa na ninayempenda zaidi kwa kunitumia sms fanya mambo yako, mimi na wewe basi! sikupata kuumia kama hii sms ya mpenzi wangu wa sasa ambayo si ya kunipiga kibuti!
sms yenyewe ni hii:
Sema July! pole kwa uchovu wa jana! mwaka unaisha sasa tunaanza mwaka mpya muda si mrefu kama tukibahatika, ila kuna mambo manne ulinifanyia mwaka huu yalinikera sana japo sikusema ningependa kuona hayajirudii mwakani kama tutabahatika kuuona!
1. kumbuka mwezi wa tatu kunasiku ulitokea Riverside kwenye kikao ukanipitia Mwenge tukaenda Don bosco baadae posta na kurudi tena Don bosco, nilikulipia nauli muda wote huo nikabakiwa na mia tano tu, nikakuomba tutembee kwa muguu mpaka magomeni ili nipande gari za Mabibo nikidhani utauliza kwa nini tutembee kwa muguu ni kujibu sina nauli badala yake ukakubali tukatembea hadi magomeni sema kweli niliumia sana na niliumwa miguu wiki nzima bila nafuu! naomba isijirudie jaribu kunijali kama nami nifanyavyo kwako!
2. Kuna siku nilipata taarifa za kweli ulitaka kupeleka barua ya uchumba kwa mtu tofauti na mimi huku uko kwenye mahusiano ya kimapenzi nami niliumia sana japo sikusema.
3.Nilipo ugua mwezi wa tisa nikakutumia sms kuwa naumwa sikua na senti hata kidogo, ukaishia kusema pole bila kujua naponaje ilinilazimu kukopa kinyume na jadi yangu napo niliumia sana!
4.Nilipo kuwa na birthday pamoja na wewe kunipatia fedha ila hukufika niliumia sana japo nilikubaliana na taarifa yako kuwa hutofika uliyoitoa dakika za mwisho naomba lisijirudie mwakani!
Ndugu zangu wana jamvi sikupata kujua alikuwa anakereka moyoni hata kidogo kwa lolote maana alionekana mwenye furaha muda wote, na siku tunatembea kwa muguu nilijua namsaidia kufanya zoezi maana fedha sio siri ilikuwepo si tu kupanda dala dala bali hata kukodi tax! lakini hakupata kusema mpaka jana alipo nitumia hiyo sms niliumia sana kila muda nawaza juu ya sms hii na hakuna aliloongopa yote ni kweli! hata jibu hapa sina najibuje sasa?
Naye ni mwanaJF tukusaodie sound ili uendelee kupiga mambo yetu yale????
 
Nadhani umri wangu hauniruhusu kuchangia hii thread.

Ngoja niwahi jukwaa la wakubwa.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Changia babu..ili nasi wajukuu tupate shule si unajua elimu haina mwisho..

Afu uko jukwaa la wakubwa ni kuanzia miaka mingapi?

afu mimi sijakusikiliza bali nimekusoma..
 
Kama akili yako ndo inavowaza basi nenda jandoni, hujui maana ya kuwa mwanaume na utakuwa unagongewa na kwasababu hujali hutakuja kugundua mpk azaliwe mtoto wa kiarabu kwa mpenzio/mkeo.
Achana naye huyo sio wife material atakusumbua hadi ujisahau mwenyewe. Angalia kuhusu passive aggressive behaviour. Ana personality disorder - ni almost monster. Mtu mwenye mahusiano ya kweli huwa muwazi na kujadili mambo yamuhusuyo wazi kwani pamoja na mahusiano kuna mambo ni yake mwenyewe na ni responsibility yake. Huwezi mwanadamu kumtupia mwenzio responsibilities zako kisha ikawa ni mapenzi hayo. Utakuwa na mzigo maisha yako yote. Wewe ni sms gani umemwandikia. See you are very perfect man with sound personality. Kimeo hicho. Siku hizi rahisi kubaini mwenza kuliko zamani. Life is very fast so in a minute you can learn million times the speed of our parents. watch out! Utaniambia.
 
Hiyo sio 'sms'. sms ni ujumbe mfupi, huo ni mrefu sana!! Usiwaze cha kumjibu, kasema 'yasijirudie mwakani', mwambie tu 'nakuahidi hayatajirudia'.
 
Hapo huna demu/ kuna siku atapata taarifa za njama za kukung'oa kucha/kuuwawa na asikwambie anasubiri madhara yanakupata/unakufa ndipo anamwomba Mungu amsahehe kwa nini hakukwambia. Mahusiano mazuri ni pamoja na kuwa muwazi kwa mwenzio.
 
!
!
pole.....tatizo ni kwamba huwa tunajisahau sana tunapokuwa katika mahusiano na huwa tunabadilika mno. Unavyoanza mahusiano unakuwa tofauti na tunabadilika kutokana na muda. Unaweza kukuta mlipoanza ulikuwa unamjali mno ila kujali huko kukapungua kadri muda unavyokwenda na kibaya huwa hatugundui kuwa tumebadilika mpaka its too late.
Kizuri ni kwamba umekubali hayo aliyosema,badilika mkuu na pia tumia fursa hii kumwambia na yeye ni yapi alikukwaza na usingependa kuyaona tena.
Nakutakia mafanikio mema.
 
atleast amekuwa wazi, unabahati huyu naye angekuacha solemba, acha ubahili kijana!we unapenda kuchomeka tu , kuhudumia hutaki, alaa.
 
hahhhaa ooonh kitu ambacho nichakweli afu sio lahisi kukizania
 
ili pia ulilifanya? ina maana ulikuwa na wapenzi zaidi ya mmoja. bidada naye alijua na alikaa kimya hata asikuulize, kweli huyo ana kifua

yeah nilifanya! hakuwa mpenzi wangu ni mtu nilimufahamu vizuri hasa kwa kuwa alikuwa na hofu ya Mungu na vitu vingi anavyotakiwa mke kuwa navyo kajaliwa!
 
we jamaa kiboko.....yaani una hela ya tax afu ukajikausha....sometimes inabidi kujiongeza
 
Back
Top Bottom