Sms iliyoniumiza kupita zote

julius mahinya

JF-Expert Member
May 11, 2013
1,152
1,500
Kupigwa kibuti nilisha wahi pigwa na ninayempenda zaidi kwa kunitumia sms fanya mambo yako, mimi na wewe basi! sikupata kuumia kama hii sms ya mpenzi wangu wa sasa ambayo si ya kunipiga kibuti!
sms yenyewe ni hii:
Sema July! pole kwa uchovu wa jana! mwaka unaisha sasa tunaanza mwaka mpya muda si mrefu kama tukibahatika, ila kuna mambo manne ulinifanyia mwaka huu yalinikera sana japo sikusema ningependa kuona hayajirudii mwakani kama tutabahatika kuuona!
1. kumbuka mwezi wa tatu kunasiku ulitokea Riverside kwenye kikao ukanipitia Mwenge tukaenda Don bosco baadae posta na kurudi tena Don bosco, nilikulipia nauli muda wote huo nikabakiwa na mia tano tu, nikakuomba tutembee kwa muguu mpaka magomeni ili nipande gari za Mabibo nikidhani utauliza kwa nini tutembee kwa muguu ni kujibu sina nauli badala yake ukakubali tukatembea hadi magomeni sema kweli niliumia sana na niliumwa miguu wiki nzima bila nafuu! naomba isijirudie jaribu kunijali kama nami nifanyavyo kwako!
2. Kuna siku nilipata taarifa za kweli ulitaka kupeleka barua ya uchumba kwa mtu tofauti na mimi huku uko kwenye mahusiano ya kimapenzi nami niliumia sana japo sikusema.
3.Nilipo ugua mwezi wa tisa nikakutumia sms kuwa naumwa sikua na senti hata kidogo, ukaishia kusema pole bila kujua naponaje ilinilazimu kukopa kinyume na jadi yangu napo niliumia sana!
4.Nilipo kuwa na birthday pamoja na wewe kunipatia fedha ila hukufika niliumia sana japo nilikubaliana na taarifa yako kuwa hutofika uliyoitoa dakika za mwisho naomba lisijirudie mwakani!
Ndugu zangu wana jamvi sikupata kujua alikuwa anakereka moyoni hata kidogo kwa lolote maana alionekana mwenye furaha muda wote, na siku tunatembea kwa muguu nilijua namsaidia kufanya zoezi maana fedha sio siri ilikuwepo si tu kupanda dala dala bali hata kukodi tax! lakini hakupata kusema mpaka jana alipo nitumia hiyo sms niliumia sana kila muda nawaza juu ya sms hii na hakuna aliloongopa yote ni kweli! hata jibu hapa sina najibuje sasa?
 
Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,842
2,000
Kama na ww unakili yote ni ya kweli napata shida kama kweli huyo mpenzi wako unampenda hata yeye ana wasiwasi kitendo cha kupeleka barua sehemu nyingine ya uchumba wakati uko naye ni wazi kuwa huna malengo naye kabisa tena amefanya uvumilivu tu yawezekana ameshatafuta pa kujihifadhi ikitokea tena,angekuwa mwingine saizi ungekuwa unatumia neno "ex",inaonyesha hayuko huru kwako anafanya mambo huku anakinyongo moyoni na yawezekana hayo yote umesababisha ww kwa kutomuweka karibu na kumjali kama alivyosema mwenyewe,ushauri wangu jirekebishe huyo mwanamke anakupenda sana angekuwa mwingine hata asingekuambia angetafuta kijana anayejitambua fasta.
 
bby C

Member
Jun 12, 2013
68
0
Wanawake tunaumia sana moyon, muonyeshe kumjal tafuta muda mzuri wa kukaa nae kabla mwaka haujaisha na umuambie sms yake imeiona na uonyeshe ni kiasi gani unajali machungu yake na muahidi kitu.
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,267
2,000
Sema July! pole kwa uchovu wa jana! mwaka unaisha sasa tunaanza mwaka mpya muda si mrefu kama tukibahatika, ila kuna mambo manne ulinifanyia mwaka huu yalinikera sana japo sikusema ningependa kuona hayajirudii mwakani kama tutabahatika kuuona!
1. kumbuka mwezi wa tatu kunasiku ulitokea Riverside kwenye kikao ukanipitia Mwenge tukaenda Don bosco baadae posta na kurudi tena Don bosco, nilikulipia nauli muda wote huo nikabakiwa na mia tano tu, nikakuomba tutembee kwa muguu mpaka magomeni ili nipande gari za Mabibo nikidhani utauliza kwa nini tutembee kwa muguu ni kujibu sina nauli badala yake ukakubali tukatembea hadi magomeni sema kweli niliumia sana na niliumwa miguu wiki nzima bila nafuu! naomba isijirudie jaribu kunijali kama nami nifanyavyo kwako!
2. Kuna siku nilipata taarifa za kweli ulitaka kupeleka barua ya uchumba kwa mtu tofauti na mimi huku uko kwenye mahusiano ya kimapenzi nami niliumia sana japo sikusema.
3.Nilipo ugua mwezi wa tisa nikakutumia sms kuwa naumwa sikua na senti hata kidogo, ukaishia kusema pole bila kujua naponaje ilinilazimu kukopa kinyume na jadi yangu napo niliumia sana!
4.Nilipo kuwa na birthday pamoja na wewe kunipatia fedha ila hukufika niliumia sana japo nilikubaliana na taarifa yako kuwa hutofika uliyoitoa dakika za mwisho naomba lisijirudie mwakani!
Ni hatari sana kwa kijana kutokujijua na kujua majukumu yake kiasi hiki

No wonder ni kwanini mabinti wanatusema sana siku hizi
Unashindwa kujua kuwa unatakiwa mrembo wako afike nyumbani bila karaha???
AAAARRRRRRRRRRGGGGGGGGHHHHHHH!!!!!!!!!!!!!!

Ni bora ungekuwa huna hela na yeye anajua hilo

Jirekebishe kijana
Kama hawakuchapii basi shukuru Mungu!!!
 
Mshiiri

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
2,014
1,500
Achana naye huyo sio wife material atakusumbua hadi ujisahau mwenyewe. Angalia kuhusu passive aggressive behaviour. Ana personality disorder - ni almost monster. Mtu mwenye mahusiano ya kweli huwa muwazi na kujadili mambo yamuhusuyo wazi kwani pamoja na mahusiano kuna mambo ni yake mwenyewe na ni responsibility yake. Huwezi mwanadamu kumtupia mwenzio responsibilities zako kisha ikawa ni mapenzi hayo. Utakuwa na mzigo maisha yako yote. Wewe ni sms gani umemwandikia. See you are very perfect man with sound personality. Kimeo hicho. Siku hizi rahisi kubaini mwenza kuliko zamani. Life is very fast so in a minute you can learn million times the speed of our parents. watch out! Utaniambia.
 
julius mahinya

JF-Expert Member
May 11, 2013
1,152
1,500
Kama na ww unakili yote ni ya kweli napata shida kama kweli huyo mpenzi wako unampenda hata yeye ana wasiwasi kitendo cha kupeleka barua sehemu nyingine ya uchumba wakati uko naye ni wazi kuwa huna malengo naye kabisa tena amefanya uvumilivu tu yawezekana ameshatafuta pa kujihifadhi ikitokea tena,angekuwa mwingine saizi ungekuwa unatumia neno "ex",inaonyesha hayuko huru kwako anafanya mambo huku anakinyongo moyoni na yawezekana hayo yote umesababisha ww kwa kutomuweka karibu na kumjali kama alivyosema mwenyewe,ushauri wangu jirekebishe huyo mwanamke anakupenda sana angekuwa mwingine hata asingekuambia angetafuta kijana anayejitambua fasta.

Barua sikupeleka nilitaka kupeleka, nampenda ila wakati ule nilikuwa na hofu juu yake maana sikuwa namfahamu kivile!
 
julius mahinya

JF-Expert Member
May 11, 2013
1,152
1,500
Achana naye huyo sio wife material atakusumbua hadi ujisahau mwenyewe. Angalia kuhusu passive aggressive behaviour. Ana personality disorder - ni almost monster. Mtu mwenye mahusiano ya kweli huwa muwazi na kujadili mambo yamuhusuyo wazi kwani pamoja na mahusiano kuna mambo ni yake mwenyewe na ni responsibility yake. Huwezi mwanadamu kumtupia mwenzio responsibilities zako kisha ikawa ni mapenzi hayo. Utakuwa na mzigo maisha yako yote. Wewe ni sms gani umemwandikia. See you are very perfect man with sound personality. Kimeo hicho. Siku hizi rahisi kubaini mwenza kuliko zamani. Life is very fast so in a minute you can learn million times the speed of our parents. watch out! Utaniambia.

sijamjibu, japo alinipigia kujua kama nimepata sms yake nikamjibu ndio na nikaahidi kujibu! ila nasubiri kasafiri leo akirudi tu next week ntaomba maongezi naye na si sms! ntamtoa out tuongee!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom