Sms iliyoniumiza kupita zote

Sms iliyoniumiza kupita zote

hapo kwenye bold! hata kama alitaka kupeleka barua ya posa kwa mtu mwingine huku ana mpenzi mwingine?

uliyoyasema ni kweli, na imekuwa kawaida kwa wadada kuhamishia responsibilities zao kwa wanaume

ila mi naona kuna tatizo la communication kati ya hao wapenzi wawili. kwanini asiwe huru kusema sina nauli. inaonekana mrembo hayupo huru kwa Jul.

pia Jul, hana mapenzi ya dhati kwa huyo bidada. nahisi ni spare tyre yake tu (labda julius mahinya aliweke hilo wazi.
mpz katuma msg anaumwa, mwanaume anayejali atapiga simu kuulizia mwenzake anaendelaje, katumia dawa gani etc, kuonyesha anajali. sasa huyu jamaa yeye katuma sms akisema pole tu, kashindwa hata kuuliza mwenzie anaendeleaje?

kapeleka posa kwa mwanamke mwingine?? wkt ana mpz mwingine. hapo lazima mmoja anadanganywa, na ni huyu aliyetuma sms

Nampenda sana kwa namna alivyo tena sana, anaonekana mwenye aibu kwangu sana ila kifupi anapenda kuniona nafurahi muda wote! skupeleka posa ila nilitaka na hii ni kwa historia yetu ya kukutana na kufikia tulipo sikua namfahamu kivile maana tulikutana kimjini mjini sikufikiria mwanzoni ni mtu sahihi kuwa mke bt kimapenzi niliona yuko sahihi! ila sasa nasema nampenda mno na ndio maana nimeumia kuliko hata nilipopigwa kibuti!
 
Achana naye huyo sio wife material atakusumbua hadi ujisahau mwenyewe. Angalia kuhusu passive aggressive behaviour. Ana personality disorder - ni almost monster. Mtu mwenye mahusiano ya kweli huwa muwazi na kujadili mambo yamuhusuyo wazi kwani pamoja na mahusiano kuna mambo ni yake mwenyewe na ni responsibility yake. Huwezi mwanadamu kumtupia mwenzio responsibilities zako kisha ikawa ni mapenzi hayo. Utakuwa na mzigo maisha yako yote. Wewe ni sms gani umemwandikia. See you are very perfect man with sound personality. Kimeo hicho. Siku hizi rahisi kubaini mwenza kuliko zamani. Life is very fast so in a minute you can learn million times the speed of our parents. watch out! Utaniambia.

You are joking, right?
 
Mpe pole,dinner date ya ukwee,na zawadi juu,say sorry,af mwambie na ye ajirekebishe ur not an angel to read her mind

I seriously want to like this, sema hata sehemu yenyewe ya kulike imepotea, dang! Naona tu sehemu ya send PM. hata sijui why
 
Ni hatari sana kwa kijana kutokujijua na kujua majukumu yake kiasi hiki

No wonder ni kwanini mabinti wanatusema sana siku hizi
Unashindwa kujua kuwa unatakiwa mrembo wako afike nyumbani bila karaha???
AAAARRRRRRRRRRGGGGGGGGHHHHHHH!!!!!!!!!!!!!!

Ni bora ungekuwa huna hela na yeye anajua hilo

Jirekebishe kijana
Kama hawakuchapii basi shukuru Mungu!!!
bawelage
 
Nampenda sana kwa namna alivyo tena sana, anaonekana mwenye aibu kwangu sana ila kifupi anapenda kuniona nafurahi muda wote! skupeleka posa ila nilitaka na hii ni kwa historia yetu ya kukutana na kufikia tulipo sikua namfahamu kivile maana tulikutana kimjini mjini sikufikiria mwanzoni ni mtu sahihi kuwa mke bt kimapenzi niliona yuko sahihi! ila sasa nasema nampenda mno na ndio maana nimeumia kuliko hata nilipopigwa kibuti!
kwani ulisha shake well before use
 
asa kwanini ulitaka kwenda kupeleka barua kisirisiri?we nae!omba radhi km unampenda km unamzuga mwambie ukweli muache usimpotezee muda....kama ulivyokiri hapa, na ukikutana naye kiri hivyohivyo ili msala uishe muendelee na maisha.
 
Soma vizuri ushauri wangu na utilie maanani. Mapenzi sio utumwa kwamba ukose uhuru wa kufanya mambo yako. Yeye atakuwepo na anatakiwa kujua kuwa una uhuru wa kufanya chochote - free will -- na hata yeye ana free will yake. Hiyo hakuna binadamu anatakiwa kuingilia - si mama wala baba wala mke na hata Mungu anaiheshimu hiyo. Ukipoteza hii mara moja unakuwa katika hali uliyonayo sasa - tayari umeshajisahau na hujifahamu tena kwani unatumia muda wako wa kufanya free will kufikiria mambo yake na yeye ama kwa hakika hafikirii chochote kukuhusu wewe ndio maana hakukuambia wakati mambo yanatokea kwa kuwa alikuwa anatumia muda wake kufanya mambo yake. Sasa kwa dakika kama 10 tu ametumia kukufikiria na kukuharibia mwaka. Ona free will inavyofanya kazi. Wa kupoteza ni wewe na yeye hana cha kupoteza, muda wake kautumia vizuri kwa mambo yake na sasa dakika chache tu kakumaliza -- FUNGUKA acha uzembe. Vijana wa karne hii hawawazi tena hivyo kama wewe kuwa HURU! Tafuta marafiki kadri free will yako inakutuma na atakayekufanya na furaha muda wote - huyo ndio bana naye.

Nitakupa mfano: sms hizo kama angekuwa hana passive aggressive disorder angeandika hivi:
1. kumbuka mwezi wa tatu kunasiku ulitokea Riverside kwenye kikao ukanipitia Mwenge tukaenda Don bosco baadae posta na kurudi tena Don bosco, nilikulipia nauli muda wote huo nikabakiwa na mia tano tu, nikakuomba tutembee kwa muguu mpaka magomeni ili nipande gari za Mabibo nikidhani utauliza kwa nini tutembee kwa muguu ni kujibu sina nauli badala yake ukakubali tukatembea hadi magomeni sema kweli niliumia sana na niliumwa miguu wiki nzima bila nafuu! naomba isijirudie jaribu kunijali kama nami nifanyavyo kwako!
SAHIHI: Nakupenda sana, na nakumbuka siku ile tulivyotembea kwa miguu ilikuwa zoezi zuri natamani siku nyingine tufanye tena mwakani.

2. Kuna siku nilipata taarifa za kweli ulitaka kupeleka barua ya uchumba kwa mtu tofauti na mimi huku uko kwenye mahusiano ya kimapenzi nami niliumia sana japo sikusema.
SAHIHI: Ingawa wewe ni mtu huru kifikra nakupenda sana na natamani siku moja tutakuwa pamoja. Nijibu kama wanipenda zaidi yangu.

3.Nilipo ugua mwezi wa tisa nikakutumia sms kuwa naumwa sikua na senti hata kidogo, ukaishia kusema pole bila kujua naponaje ilinilazimu kukopa kinyume na jadi yangu napo niliumia sana!
SAHIHI: Nakutakia mwaka huu ujao mpenzi tupate fedha za kutosha - sitaki kukumbuka kipindi kile nilipoumwa na wote hatuna fedha. Mwaka huu ujao uwe na mafanikio.

4.Nilipo kuwa na birthday pamoja na wewe kunipatia fedha ila hukufika niliumia sana japo nilikubaliana na taarifa yako kuwa hutofika uliyoitoa dakika za mwisho naomba lisijirudie mwakani!
SAHIHI: Mwaka ujao tuwe na muda pamoja zaidi na tupange mipango na kufurahia pamoja


Sasa ukiangalia mifano niliyoweka utaweza kuona jinsi alivyo na personality disorder. Nimekusaidia tu bure bila faranga.

Mapenzi si malalamiko. Usikubali. MAapenzi ni kila mtu kufanya responsibilities zake na kisha mnakutana kwa maongezi na kubadilisha mawazo na of course the thing. Hii ndio love. Kama love ni kuchukua mizigo basi ni aheri wanaume wote wangekuwa na orphanage centres kwani hawa wanahitaji msaada wa fedha zaidi.

Asante

Serioulsy!!! Just stop!!! All the free will stuff, unataka waishi maisha ya kuigiza, eti mtu kataka kutuma barua ya posa kwa mtu mwingine wewe unaanza kuleta issue za nakupenda sana nataman siku moja tutakua pamoja nijibu kama unanipenda zaidi..wewe ndo upo passive aggresive sasa..just be real..kama unampenda mtu utamwambia ukweli ili apone..yeye sio Mungu, ni mwanadam kama wengine..soma vizuri, tatizo hapa ni moja, huyu kaka hajamjua mpenzi wake, ndio, huyo dada nae anaweka vitu moyoni for a long time but at the same time haimaanishi kua hampendi huyo kaka..its vivid kua anampenda sana tu..so usijaribu kuwavunjia wenzio furaha yao, wape good advice!
 
asa kwanini ulitaka kwenda kupeleka barua kisirisiri?we nae!omba radhi km unampenda km unamzuga mwambie ukweli muache usimpotezee muda....kama ulivyokiri hapa, na ukikutana naye kiri hivyohivyo ili msala uishe muendelee na maisha.
mimi huwa namsikiliza sana basi tu yeye! nashangaa hata tabasamu na furaha yake kwangu mara zote maana sikuwahi hata kulifikiria swala la kumkwaza! barua niltaka kupeleka kwa kuwa yeye sikuwa na full information kuhusu yeye kutoka kwenye different source tofauti na yeye mwenyewe kunieleza nikitaka kujua chochote! je ww unaeza kumueleza mpenzi wako mabaya yako bila kuficha?
 
Ni hatari sana kwa kijana kutokujijua na kujua majukumu yake kiasi hiki

No wonder ni kwanini mabinti wanatusema sana siku hizi
Unashindwa kujua kuwa unatakiwa mrembo wako afike nyumbani bila karaha???
AAAARRRRRRRRRRGGGGGGGGHHHHHHH!!!!!!!!!!!!!!

Ni bora ungekuwa huna hela na yeye anajua hilo

Jirekebishe kijana
Kama hawakuchapii basi shukuru Mungu!!!

Na no wonder mabinti wanatung'ang'ania waume za watu...
 
You well said kaka. That is it. Keep it up! Ulimbukeni wa mapenzi. Kwa kifupi ni infatuation ambayo ni kupenda kwa kutokujitambua zamani wanasema limbwata. Unakuwa jinga na kila saa na dakika unamuwaza mtu mwingine na hata unajisahau mwenyewe. Mbaya sana. Huu ni utumwa katika mapenzi.

Hahahaha..Okay..am done..I give up!!!
 
Huu ni uozo wa kifikra kwa sisi wanawake. Tuelimike! Tunda tuwape sisi na tulete taabu duniani kisha fedha watupe sisi kutatua laana tulizozileta kuleee Eden? How come. Kila mtu afe lake na responsibilities zake. Criteria ya wanawake kudai fedha ni nini ikiwa wote wanakaa darasani na kupata kazi na mishahara sawa. Kama mtu akaa kigoigoi hajishughulishi aende magoti huko kuna fedha kibwena. Tusiwasumbue wanaume kila mara na kufanya hii dunia chungu kwao, hata life expectancy ya wanaume duniani ni chini kwa sababu ya wanawake - too stressful to be loved!

.........................................
 
Nawashukuru watu wote mlochangia katika uzi huu kifupi hakuna mchango hata mmoja ambao hauna cha kujifunza! nimejifunza mengi na nadhani naenda kutekeleza kile mlicho nishauri nikiamini kubadilika kama mdada alivyo dai na msamaha ntaomba pia ntaomba awe na uhuru kwangu kusema chochote na mahali popote! japo nilichogundua pia ana tatizo la kukaa na jambo moyoni kwa muda mrefu ntamuomba nami akisamehe awe mwepesi pia kusahau!
 
miss chagga comments ni passive aggressive behaviour. It is the same personality disorder have been narrating!

So Miss Chagga is sick..and so are 80% of all women in the world! Thank you Doctor for the diagnosis.
 
may be lakini napaswa kujua mpenzi wangu anahitaji nini! hajawahi chukia mbele yangu muda wote anaonyesha tabasamu na furaha sikupata jua anaumia ndio maana naumia juu ya sms!
yawezekana ni wajibu wa mwanaume kutoa fedha bila kuombwa ntajitahidi si kutoa fedha bila utaratibu ila kuzungumza naye awe huru kuomba chochote muda mwafaka si kulalamika japo ntatafuta lugha nzuri ya kuongea naye!
You are a good man! No one got no mistakes, but you are a good man!
 
Hebu acha uongo wako: wapi ameandika the girl begged for money. You know what the beauty of Love is--- sharing, sharing and sharing . Ndio maana mdada alilipa nauli expecting the guy would do the same . She did her part and she expresses in the sms she would like the man to treat her better.

Usimpotoshe mwenzio mwenye nia ya kujenga mahusiano yake akaenda zua mengineeee mapyaaa.

Cha msingi amjengee mazingira ya kuwa more open , we dont know mazingira yanayomfanya huyu dada kutokuwa open there and then, maybe fear, maybe ujinga. Ila the bottom line is "Men need to be men ( to care, to protect, to caress), and women need to be women (reciprocating the love they receive, multiply and give back)

I do not see the damn like button!!! This is so true, there is still hope in humanity, : )
 
may be lakini napaswa kujua mpenzi wangu anahitaji nini! hajawahi chukia mbele yangu muda wote anaonyesha tabasamu na furaha sikupata jua anaumia ndio maana naumia juu ya sms!
yawezekana ni wajibu wa mwanaume kutoa fedha bila kuombwa ntajitahidi si kutoa fedha bila utaratibu ila kuzungumza naye awe huru kuomba chochote muda mwafaka si kulalamika japo ntatafuta lugha nzuri ya kuongea naye!
You are a good man! No one got no mistakes, but you are a good man!
 
Back
Top Bottom