utafiti
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 12,783
- 7,671
Ama kweli UALIMU kazi ya wito
MWANAFUNZI mmoja hajui kujumlisha wala kutoa. Mwalimu katumia njia zote kumuelimisha lakini wapi ikabidi ajaribu njia hii.
Mwalimu: Kwenu mnafuga nini?
Mwanafunzi: Kuku na mbuzi
Mwalimu: Mbuzi mnao wangapi?
Mwanafunzi: 25
Mwalimu: Mbuzi 25 toa mbuzi 5 watabaki wangapi?
Mwanafunzi: Unawajua mbuzi wetu au unawasikia? Ukimtoa mmoja tu nje wote wanatoka!
Mwalimu: Mmh! Naacha kazi mimi kama mambo yenyewe ni hivi, basi tena.
teh teh teh