Smart TV yenye DVB T2/S2 Ina Faida gani Kwa Soko la Tanzania ikiwa Channels zimezuiliwa kuonekana kwa kutumia builtin Decorder? Wizara Husika?

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,370
7,612
Kuna wakati Mwaka 2019 nilitumia TCL TV ikiwa na builtin Decorder DVB T/T2 na ilikuwa nikiunga antenna napata channel mbalimbali Bure. Ni muda Sasa TV hiyo Toka iharibike. Sasa katika uchunguzi naambiwa hizo channel Sasa hazipatikani zimezuiliwa na Serikali.

Hivi Sasa Kuna TV nyingi sana zimeingia sokoni zikiwa na features nyingi Zaidi ikiwemo Smart TV zenye DVB T2/S2 ambazo ukiwa na antenna au Dish ungeweza kupata channel nyingi Bure.

Hali si hivyo kwa Soko la Tanzania ambapo unagharamika kununua Smart TV yenye DVB T2/ S2 lakini hufaidi hiyo feature.

Je serikali imeshindwa Kuwa Bunifu na kuwawezesha watanzania kutumia feature hizi bila kulazimika kununua Decorder nyingine?

Soko La Tanzania ni Huria hivyo mtu angeweza Kuwa na machaguzi mawili
1. Kununua TV ya Kawaida Kisha aongeze kingamuzi na alipie channels au
2. Anunue Smart TV DVB T2/S2 kwa gharama Zaidi na afaidi Channels zitakazopatikana.

Tunaomba Serikali Mliangalie na hilo Kukusaidia Sisi Wapend technology kwani si vizuri kwa na TV yenye Features ambazo hutumii.
 
Chanel za bure mbona zinapatikana hata ukitumia madish makubwa unapata free to air nyingi tu?
 
Hivi vitu viko integrated kiasi kwamba kiwanda kinafyatua komponent ambazo zina kila kitu built in kutengeneza TV ambazo haina hiyo input inaweza kuwa gharama zaidi kwao kwa upande wa manufacturing/distribution/marketing.

Probably serikali inapata chochote kutokana na hizi dekoda so inaweza kula kwao wakiruhusu free to air TV.
 
Chanel za bure mbona zinapatikana hata ukitumia madish makubwa unapata free to air nyingi tu?
Haongelei satelite anaongelea TV digital ambazo haihitaji dekoda unachomeka hata zile antena za ndani unakamata digital channel yani kama ilivyokuwa zamani kabla ya ujio wa digital bongo.

Sijui kwa bongo tatizo ni sheria au wenye TV station wanaona dekoda zinalipa zaidi.
 
Kuna wakati Mwaka 2019 nilitumia TCL TV ikiwa na builtin Decorder DVB T/T2 na ilikuwa nikiunga antenna napata channel mbalimbali Bure. Ni muda Sasa TV hiyo Toka iharibike. Sasa katika uchunguzi naambiwa hizo channel Sasa hazipatikani zimezuiliwa na Serikali.

Hivi Sasa Kuna TV nyingi sana zimeingia sokoni zikiwa na features nyingi Zaidi ikiwemo Smart TV zenye DVB T2/S2 ambazo ukiwa na antenna au Dish ungeweza kupata channel nyingi Bure.

Hali si hivyo kwa Soko la Tanzania ambapo unagharamika kununua Smart TV yenye DVB T2/ S2 lakini hufaidi hiyo feature.

Je serikali imeshindwa Kuwa Bunifu na kuwawezesha watanzania kutumia feature hizi bila kulazimika kununua Decorder nyingine?

Soko La Tanzania ni Huria hivyo mtu angeweza Kuwa na machaguzi mawili
1. Kununua TV ya Kawaida Kisha aongeze kingamuzi na alipie channels au
2. Anunue Smart TV DVB T2/S2 kwa gharama Zaidi na afaidi Channels zitakazopatikana.

Tunaomba Serikali Mliangalie na hilo Kukusaidia Sisi Wapend technology kwani si vizuri kwa na TV yenye Features ambazo hutumii.
Hazijazuiliwa bali kingamuzi cha continental kimekufa, akitokea mwengine anaeachia tv zitapatikana. Azam, Startimes na wengineo wanaotumia terrestrial tv zao hawajaziachia
 
Serikali ya Tanzania ni adui no 1 wa Mtanzania. Haiwezi kukubali mpate channel za bure bila kulipia iliipate kodi
 
Si Kweli, Chanell za Bure zipo, it's just hazipo kwenye DVB T/T2 ila zipo kwenye satelite, kuna watu wengi wanatumia FTA.

Dvb T2 Inatumia minara kama ya simu, sio profitable kwa kampuni ikuwekee chanell bure, unless kuwe na minara ya Serikali labda.
 
Haongelei satelite anaongelea TV digital ambazo haihitaji dekoda unachomeka hata zile antena za ndani unakamata digital channel yani kama ilivyokuwa zamani kabla ya ujio wa digital bongo.

Sijui kwa bongo tatizo ni sheria au wenye TV station wanaona dekoda zinalipa zaidi.
Haya ndo mambo nayaongelea. Kabla ya Ujio wa "Ulimwengu wa Digitali" Tanzania, Ilikuwa unanunua TV Tuu unapata analog channels Zote Bure Kabisa.

Ujio wa digital ukahitaji tuwe na vingamuzi kwa zile tv zetu za zamani zisizo na vingamuzi.

Sasa Teknolojia imeleta Smart TV zenye king'amuzi, Ilipaswa Tupate Channels Bure.
 
Si Kweli, Chanell za Bure zipo, it's just hazipo kwenye DVB T/T2 ila zipo kwenye satelite, kuna watu wengi wanatumia FTA.

Dvb T2 Inatumia minara kama ya simu, sio profitable kwa kampuni ikuwekee chanell bure, unless kuwe na minara ya Serikali labda.
Hatuongelei Satalite! Tunataka TV ya kawaida ambayo signal yake haiko encrypted, satelite ina gharama za dish/decoda/receiver.
 
Si Kweli, Chanell za Bure zipo, it's just hazipo kwenye DVB T/T2 ila zipo kwenye satelite, kuna watu wengi wanatumia FTA.

Dvb T2 Inatumia minara kama ya simu, sio profitable kwa kampuni ikuwekee chanell bure, unless kuwe na minara ya Serikali labda.
Lakini kabla ya digital kuja kila TV ilikuwa bure na wote walikuwa na transmitter zao, hakuna tofauti kwenye hilo. Nadhani kutakuwa na sheria maana wangepata hela ya matangazo bado kuna biashara hapo.
 
Analog ni rahisi lakini kutransmit, Azam imemcost zaidi ya 50B hizi terrestrial zake na sio nchi nzima, just imagine individual kama ITV ama Chanell 10 atoe kiasi chote hicho kutengeneza minara. Bado gharama nyengine za serikali na nyinginezo.

Satelite yenyewe Sina uhakika ila nasikia ni around 20-30K per month kukodi kurusha tv.
 
Huko majuu na wao wanapimiana vifurushi kama huku kwetu kinamapula?
 
Subscription, unaingia mkataba wanapiga panga kila mwezi moja kwa moja kwenye account au credit card $45 - $150 kwa mwezi kutegemea na bundle unayochagua na umepata discount gani mara nyingi hii ni TV + internet ya nyumbani + landlines.

Ila zipo pia TV za bure maeneo mengi unahitaji antena ndogo ya ndani tu hakuna dekoda wala kulipia of coz haupati vitu vingi hasa michezo na hizi za bure, then kuna hizi service za Netflix/Disney etc ambazo ni za mtandao.
 
Hili lilikua dili la serikali kupata pesa huko japan hata ukiwa unaendesha gar unaweza ukaswitch tv ukaangalia taarifa ya habari sasa huku hadi mabasi yanafungwa madishi ya azam sasa huu si zama za mawe
 
Chanel za bure mbona zinapatikana hata ukitumia madish makubwa unapata free to air nyingi tu?

Huyu anachotaka zisimikwe ardhini (Digital terrestrial) bila dish ziwe free to air kwa antenna. Maana yake ni either wamiliki wa hizo channel wazibroadcast pia kwa mfumo huo wa minara ya kawaida kama walivokua wanafanya kwenye analog au makampuni ya ving'amuzi kama star times na azam tv wazibroadcast hizo local channels bure kwa upande wa antenna ili kila mwenye smart tv azione bila kutumia king'amuzi chao ili alipie.
 
Mzee baba serikali yetu kuna vitu bado sana kuvisimamia, huwa wanaongea ongea tu...

Free to Air ilipaswa iwepo hata kwa DVB-T kwa baadhi ya channels tu especially za serikali (TBC)...
 
Back
Top Bottom