Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikatoliki

Status
Not open for further replies.
2nasumbuliwa na mzmu wa wa2 waliojtokeza hadharan na kudai kuna u-dini hvyo kila knachofanyka 2nakiangalia kwa mrengo wa kidini jaman 2mechoka kuckia malalamiko khs udin kwa kuwa 2na serikali 'halali' km vithbtsho vipo ichukue hatua siasa mufilis zmesha2boa.
 
Mkuu, karibu sana JF, jifunze kutoka members utapata faida humu huwa tunapambana kwa hoja wala sio porojo! Hoja ya ikiwa nzuri members wenyewe wataifata na kuichangia na Thanks utagongewa na Like pia, wewe unaweza kujifungia chumbani kwako ukaandika post yako ukadhani Nondo ukiileta jamvini inaonekana upupu tu, mpaka unalalamika mbona watu awajibu post yangu! Kumbe hamna cha kujibu ni pumba tupu, unaposema mjadala ufungwe unatoa amri huwo ni udhaifu mkubwa sio lazima kila thread uchangie majukwaa yapo mengi nenda jukwaa la Mahusiano na Mapenzi nadhani huko ndio panakufaa mkuu

leta hoja basi...wajibu hata hao wengine wenye hoja zinazokupinga zenye mashiko..! kwani wote wana hoja dhaifu kama zangu? hauna akili ndiyo maana hauwezi kujibu! mnaweza mkawa kwenye madrassa mkaandika post zenu mkifikiri ni nondo kumbe upupu tu humu jamvini!
toa hoja kwa watu wachache waliokupinga humu kama unaweza.....haiwezekani wote wakawa wanaandika upupu tuu!
nadhani umshafikia level ya kuitwa Gaidi!
 
Nimefuatilia kwa muda mrefu hii mada nikaona kinyaa cha kuichangia ila naona sijitendei haki kukaa kimya wakati naweza kuandika japo mistari kadhaa.

Bila chembe ya shaka huyu aliyeweka hii mada ni muislamu mwenzangu. Mimi ni muislamu kama yeye japo sijajua kiwango chake cha elimu na uwezo wa kuchakata mambo. Lakini pia sijajua uwezo wake wa kuhimili joto lake kiitikadi. Leo ana ona Cdm ni wadini, juzi aliambiwa Cuf ni wadini na vyama vyote hivi vina wanachama wa dini zote, inawezekana hajui lakini imetamkwa wazi kwenye katiba juu ya uanzishwaji wa vyama vya siasa. Kama Cdm au Cuf kingekuwa cha waislamu au wakristo pekee visingekuwepo. Atambue ccm inatumia ujinga wa wananchi ili kuwagawa na kuleta fikra za udini, na imefanikiwa mara kadhaa kama ilivyofanikiwa kwake. Lakini pia asidhanie wasabato, wakatoliki, walutheri, walokole nk wana kauli ya pamoja kushawishi waumini wao wafuate chama flani, hivyo hivyo shia, sunn, ahmadiyyah nk ndio maana haijawahi na haitatokea viongozi makini wabobezi wa elimu zote wasimame na kuwaambia waumini wao kuwa msifuate chama hiki kwa kuwa ni cha dini hii.

Kulalamika huku wenzetu wakichanja mbuga si dawa. Ulevi wa kiitikadi kuona chama flani nicha udini wakati si kweli ni ukame wa fikra. Tukazanie elimu zote kwa watoto wetu, bakwata ifumuliwe wakae viongozi wenye vision na elimu ya juu ili wasimamie shule zetu vizuri ziwe mfano wa kuigwa kwa kutoa elimu bora ili kuondokana na kizazi cha huyu sokomoko kinacho angalia sarafu upande mmoja.

kwa kiasi nataka kukubaliana na wewe,
ila
- elimu imeshuka kwa watanzania kwa ujumla, sio waislamu peke yao, upeo wa vijana wa sasa, ni tofauti na upeo wa vijana wa miaka kumi iliopita, bila kujali dini. Vijana wa kikristu, wanajidanganya na elimu ya waliowatangulia na kutembea kichwa juu wakati wao ni wajinga, wasioelimika, japo inawezekana wameenda shule na maksi zao ziko juu, lakini maisha yao hayako deep. Ni viumbe shallow (pls mnisamehe) lakini tunaona arguments, tunaona priorities, tunaona choices na tunafanya judgements. Vijana wa sasa ni shallow, hawana upeo (ukitoa wachache waislamu na wakrstu)
- Je inawezekana title ya hii post ikabadilika? iwe mrengo/mlengo wa kikristo sio kikatoliki, manake nadhani hapo kidogo mada imeposhwa?
- Maamuzi haya ya chama ni ya watu hawa wawili? je misimamo yao binafsi au ni misimamo ya chama chao, meaning structure ya chama chao?
- JE kupoke misaada kutoka kwenye chama chenye mirengo ya kidini, kuna effect kwenye katiba ya chama, ambayo imtengenezwa kufuata katiba na miongozo y a katiba ya nchi yetu?
- Mie ni mkristu, ila nisingependa tujenge ushirika wa kutubana kufuata maadili mengine yoyote iwe ya kidini au kiimaadili, ambayo hatuyajui vizuri, lazima waheshimu siasa zetu hapa Tanzania.
- Ningependa kupata contents za maelezo ya hao viongozi, manake naona hii habari kama imechakachuliwa sana kusuit agenda fulani, na watu wamehamaki sana,
kwani hapa hatuna waandishi makini waliosikia hii habari?
 
leta hoja basi...wajibu hata hao wengine wenye hoja zinazokupinga zenye mashiko..! kwani wote wana hoja dhaifu kama zangu? hauna akili ndiyo maana hauwezi kujibu! mnaweza mkawa kwenye madrassa mkaandika post zenu mkifikiri ni nondo kumbe upupu tu humu jamvini!toa hoja kwa watu wachache waliokupinga humu kama unaweza.....haiwezekani wote wakawa wanaandika upupu tuu!nadhani umshafikia level ya kuitwa Gaidi!
Chadema-kata-JF, naona kakasirika! Ahahaha! Mambo ya ugaidi yametoka wapi tena.Ingorance is Bliss
 
wewe pia ni magamba, huna lolote, SOKOMOKO WA SIASA UNAEBURUZWA NA CHAMA CHA BABU! UDINI WAKO HAUTAKUPELEKA POPOTE!
 
Kwa jinsi nilivyokuelewa mimi, huna mantiki kwa kile unachojaribu kuwaaminisha watu wenye akili na upeo wa kuchanganua mambo, sioni nini kibaya CHADEMA wamefanya kama chama kuwa na urafiki na chama kingine kinachafanya shughuli za siasa kama CDU, halafu hivi vyama vinaendeshwa kwa katiba ya chama, katiba ya CHADEMA haina sehemu yoyote inayojipambanua inakumbatia ukristo na hapo ndipo inapoonekana hoja zako zinaongozwa na chuki, uzandiki na ghilba, Isitoshe hata hayo maadili ya kikristo uanayotaka kuwaaminisha watu hakuna hata siku mmoja kanisani kunafundishwa kuwabagua au kuwachukia waislam siku zote tunafundishwa UPENDO na tunaishi kwa kushirikiana sana waislam na wakristu, ni nyie tu kwa sababu zenu mnazozijua wenyewe ndo mmeanza kuleta choko choko za udini na ukabila. Umekwenda mbali mpaka unajadili masuala ya Angela Merkel kuwazindua wajerumani, sisi kama watanzania inatuhusu nini? Ujue mi nilidhani hoja yako ingekuwa na mashiko kama ungesema katiba ya CHADEMA imebadilishwa inafuata misingi ya ukristo kwa Influence ya CDU hapo kungekuwa na kitu cha kujadili otherwise yote unayotaka watu wayaamini ni upuuzi na unaishi kwa hisia wala hakuna uhalisia wa kisayansi wa kile unachokieleza.Tanzania tumekuwa na utamaduni adimu sana kuuona sehemu nyingine, hujawahi kuona siku za sikukuu iwe pasaka, christmas,mwaka mpya waislam wanashirikiana na wakristo? wanachinja wanyama wanavaa nguo mpya? hujawahi kuona wakristo katika sherehe za Idd wanasherekea na kunywa na kuchinja wanyama? unaweza ukaona ni vitu vidogo kwa ufinyi wako wa mawazo lakini tambua ni kitu adimu sehemu nyingine.SHIME! TUUNGANE PAMOJA KUTOKOMEZA HIZI HISIA ZA KIDINI ZINAZOZIDI KUOTA MIZIZI, TUTAHUKUMIWA NA HISTORIA SIKU MOJA.
Mkuu umemaliza kila kitu nilichotaka kukisema kwa huyu mleta mada.Pamoja sana nnadhani kwa haya machache uliyoyaandika yatakuwa yamempa somo na Kama alikuwa anetumwa humu kuichafua Chadema atajifunza.
 
urafiki wa CDM na CDU hauna maana CDM inabadilika kuwa CDU kwani hata CCM ina mahusiano Na COmmunist Party ya Uchina ambayo haiamini katika dini hizi za kwetu. Hii haina maana kuwa CCM pia imezifuta dini hapa Tanzania. Halafu umezungumzia Uprotestant na Ukatoliki huko Ujerumani kweye maelezo yako, likini kwa CDM unazungumzia Ukatoliki sijui lengo ni kupotosha au kuhabarisha
 
Kama Katiba ya CDU inatamka wazi kuwa ni Marufuku kwa Mtu yeyote asiye Mkristo kuwa kiongozi basi ni dhahiri Values zake ni tofauti na za CDM, lakini sasa inakuwaje CDM ifanye urafiki na chama chenye "Udini" kama hiki cha CDU?. Hapo kuna mawili either (1) CDM iko sympathetic na ajenda ya "Ukiristo" lakini haitaki kukiri wazi (2) Chadema haijali kwamba kinafanya urafiki na Chama gani kiwe cha kidini au si cha kidini. Lakini hatari ya namba (2) ni hii, ni kwa namna gani CDM itajipambanua kuwa huru dhidi ya kamba za influence kutokana na vyama hivyo vya kidini?.

Kwa hiyo Tanzania kupokea misaada na kuwa na uhusiano na Islamic Republic of Iran inayoongozwa kwa Kuran, nchi yetu imesilimishwa? Na Watanzania wenzetu wote wanaosoma kwenye islamic republics wanajifunza uislam? Kama nimeenda kusomea Saudi Arabia masomo ya udaktari, masomo yangu yote yatageuka kuwa ni masomo ya dini ya kiislam kwa vile nchi niliyosomea inaongozwa na serikali ya kiislam? Kwanza Ujerumani siyo nchi inayoongozwa kwa misingi ya kidini hata kama kuna vyama vyenye mwelekeo wa kidini. Chama chochote kinachoshinda ni lazima kifuate katiba ya nchi, siyo katiba ya chama.
 
Haya Mnataka kujadili Udini au Ukabila? Mbowe ni Mmachame na Wamachame Wengi ni Walutheran na Sio Wakatoliki
 
Bila ya mafundisho na ustaarabu wa kikristo, basi dunia ingekuwa giza kama akili ya alitoa mada hii
Mkuu ustaarabu upi? Wa kuzini na kuzaa mpaka watoto wanakuwa wakubwa kisha mnabariki ndoa? Au ule wa kutumia karatasi maliwatoni? Hujaweka wazi ustaarabu unaouzungumzia. Tena kuhusu hilo naweza kusema kwa kinywa kipana kwani ushahidi upo kuwa kuna kiongozi padre ndani ya chama amezaa na mwanamke bila kumwoa akamtema na sasa yule aliekuwa nae ameshamtundika mimba bila kumwoa huu ndio ustaarabu unaouzungumzia? Ni vema uwe wazi ili tuujue huo ustaarabu. Au unataka kusema ustaarabu wa kuanzisha mashirika kama save the children huku wazazi wao wakifa kwa majanga ya ukimwi na uasherati kwa kuwa tunabariki ndoa baadae kwanza inakuwa ni uzinifu? Kwa ustaarabu huo mie bora nisistaarabike.
 
Mkuu umesoma mpaka la ngapi? Anyway very simple Irani ni nchi ya kiislam kadhalika na Saudia ikiisaidia Tanzania itakuwa nchi moja imeisaidia nchi nyingine hapo ni misaada ya nchi kwa nchi mada inazungumzia vyama ungetolea mfano Tanu na Frelimo au na ANC na sio Tanzania na Uingerza, Ujerumani na Irani ni matumaini yangu umeelewa tofauti ya nchi na chama.
Kwa hiyo Tanzania kupokea misaada na kuwa na uhusiano na Islamic Republic of Iran inayoongozwa kwa Kuran, nchi yetu imesilimishwa? Na Watanzania wenzetu wote wanaosoma kwenye islamic republics wanajifunza uislam? Kama nimeenda kusomea Saudi Arabia masomo ya udaktari, masomo yangu yote yatageuka kuwa ni masomo ya dini ya kiislam kwa vile nchi niliyosomea inaongozwa na serikali ya kiislam? Kwanza Ujerumani siyo nchi inayoongozwa kwa misingi ya kidini hata kama kuna vyama vyenye mwelekeo wa kidini. Chama chochote kinachoshinda ni lazima kifuate katiba ya nchi, siyo katiba ya chama.
 
Haya Mnataka kujadili Udini au Ukabila? Mbowe ni Mmachame na Wamachame Wengi ni Walutheran na Sio Wakatoliki
Well umejibu kwa juu juu kutokana na kichwa cha thread ila cdu one of the mission ni kukuza ukristu haijalishi ulutheran wala usabato masalia.
 
Mnavyojua Nyerere hakumwalika Pope yoyote Tanzania

Pope alialikwa Tanzania Mwaka 1990 na Rais Ali Hassan Mwinyi; Miaka yote Nyerere angefanya hivyo lakini hakuwaalika Mapope wowote
 

Attachments

  • Mwinyi na Pope John Paul II.docx
    28.6 KB · Views: 33
Well umejibu kwa juu juu kutokana na kichwa cha thread ila cdu one of the mission ni kukuza ukristu haijalishi ulutheran wala usabato masalia.

Unauhakika? Eleza sababu za Chadema kukuza Ukristo kwani kuna Dini nyingi za kikristo; halafu utuambia kujenga Misikiti sio kukuza dini ya kiislamu ndani ya CCM?
 
The Rise of Muslim Militancy in Tanzania1970 - 2000
Mohamed Said
Contents
Prologue
Introduction
  1. The Beginning of Islamic Movement: The Legacy of Prof. Muhammad Hussein Malik
  2. Muslim Writers Workshop (Warsha)
  3. The Buzuruga Muslim - Sungusungu Conflict of 1983
  4. The Second Muslim Crisis and the Formation of the Supreme Council of Islamic Organisations and Institutions of Tanzania (Baraza Kuu) 1991
  5. Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis and the Reign of President Ali Hassan Mwinyi 1985-1995
  6. The Pork Riots of 1993
  7. Zanzibar Membership to the Organisation of Islamic Conference (OIC) and Islam in Africa Organisation
  8. Muslim Bible Scholars
  9. Prof. Kighoma Ali Malima (1938-1995)
Epilogue
Index
  1. Mwembechai Upheavals (Abu Aziz)
  2. Waraka wa Kamati ya Kupigania Haki za Waislam
  3. Warsha Documment 28 Ramadhan, 1408/ 15 May, 1988 Open Letter to Sophia Kawawa and Jaji Msumi
 
Wadau ebu piteni hapa mjionee Ukiristo wa rafiki wa CDM.
CDU Wikipedia
 
Unauhakika? Eleza sababu za Chadema kukuza Ukristo kwani kuna Dini nyingi za kikristo; halafu utuambia kujenga Misikiti sio kukuza dini ya kiislamu ndani ya CCM?
Unapopekea pesa za misaada lazima utekeleze sera za anaekupa misaada huwezi kupokea pesa za rapid fund envelope kwa ajili ya kuhudumia maswala ya ushauri nasaha na kupima bila kuwaambia watu watumie kondomu! Ikiwa sera ya CDU ni ""is Christian- based applying the principles of Christian democracym and emphasizes the Christian understanding of humans and their responsibility toward God" Kwa japo wale ambao sio wakristo wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho lakini wajue misingi yake ni kinafuata maadili na kanuni za Kikristo katika siasa zake na namna ya kumwelewa binadamu na wajibu wake kwa "Mungu" katika MoU ya CDU na chama chochote lazima itimize malengwa yake. Mbona hivi vitu vipo wazi mkuu? Wewe unadhani cdm watapewa mafunzo bure? Hakuta kuwa na give and take? Kama unafikiria hivyo basi una walakini.
 
urafiki wa CDM na CDU hauna maana CDM inabadilika kuwa CDU kwani hata CCM ina mahusiano Na COmmunist Party ya Uchina ambayo haiamini katika dini hizi za kwetu. Hii haina maana kuwa CCM pia imezifuta dini hapa Tanzania. Halafu umezungumzia Uprotestant na Ukatoliki huko Ujerumani kweye maelezo yako, likini kwa CDM unazungumzia Ukatoliki sijui lengo ni kupotosha au kuhabarisha
Mkuu awali ya yote ufahamu Ukristo na Ukatoliki hauna tofauti yoyote na ukatoliki ni moja ya madhehebu meeeengi ya kikristo. Kuhusu la CCM na Chama cha uchina jibu ni jepesi sana ndio maana jamaa wa ccm wanasema kwenye manifest yao chama chao ni cha ujamaa.
 
Sasa ina Maana Shiite na Sunni miongozo yao ni pamoja? or nimesahau Dini ya watu wa House of SAUD nadhani Bakwata wanawakimbia sababu siasa zao ni kali haswa hawapendelei wanawake kuwa huru ukienda sokoni lazima Mwanamme akuongoze, hawaruhusu wanawake kuendesha Magari; Bakwata ilifanya vizuri kuwakimbia
 
Mkuu awali ya yote ufahamu Ukristo na Ukatoliki hauna tofauti yoyote na ukatoliki ni moja ya madhehebu meeeengi ya kikristo. Kuhusu la CCM na Chama cha uchina jibu ni jepesi sana ndio maana jamaa wa ccm wanasema kwenye manifest yao chama chao ni cha ujamaa.

Sasa ina Maana Shiite na Sunni miongozo yao ni pamoja? or nimesahau Dini ya watu wa House of SAUD nadhani Bakwata wanawakimbia sababu siasa zao ni kali haswa hawapendelei wanawake kuwa huru ukienda sokoni lazima Mwanamme akuongoze, hawaruhusu wanawake kuendesha Magari; Bakwata ilifanya vizuri kuwakimbia

Unaona walivyokuwa wanatwangwana Bahrain?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom