Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikatoliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikatoliki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sokomoko, Jun 25, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Si jambo la tetesi tena kwamba sera na mrengo wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) ni ule wa kikristo. Hii ni kutokana na hatua yake ya kuweka wazi urafiki wake wa karibu na chama cha kikristo cha ujerumani, christian democratic union (cdu). Kutokana na urafiki huo, cdu kimesema kuwa kitawapa nafasi za mafunzo nchini ujerumani vijana na viongozi wa chadema, kusomea maadili na uongozi.

  Maadili na uongozi ambao kwa mujibu wa mtizamo na sera za cdu ni yale ya kikristo kama yalivyobuniwa na mwasisi wa chama hicho konrad harman joseph adenauer. Taarifa zilizotolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa chadema mhe freeman mbowe zinasema kuwa fursa hiyo imetolewa kwa chama chake baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na ujumbe wa cdu uliokuwa ukiongozwa na rais wa zamani wa ujerumani profesa dk. Horst kohler. Mazungumzo hayo yalimshirikisha katibu mkuu wa chama hicho dk wilbrod slaa na viongozi wengine wa juu.

  Mbowe meviambia vyombo vya habari kuwa katika mazungumzo yao kohler alisema dhamira ya kuwapa nafasi za masomo vijana viongozi wa chadema inalenga kuwafanya wawe viongozi wenye maadili mazuri kwa taifa lao. "tumekubaliana ambapo tutapata nafasi za masomo kwa vijana ambao ni viongozi wa chadema kwenda kusomea uongozi na maadili chini ujerumani" alisema. Kwa hapa nchini imeelezwa kuwa chadema itafanya kazi kwa karibu na kwa kushirikiana na taasisi ya conrad adenauer foundation ambayo ni ya taasisi ya kikristo iliyo chini ya chama cha cdu.

  Cdu kikiwa kimeanzishwa mwaka 194, ni chama cha kikristo kilichowaunganisha wakatoliki na protestant kikilenga kujenga ujerumani yenye maadili ya kikristo katika siasa, kijamii, maadili na kila kipengele cha maisha.mwanzilishi wake konrad hermann joseph adenauer anatajwa kuwa mfuata ukatoliki aliyekuwa tayari kuufia ukatoliki wake na ambaye amefanya kazi kubwa kutaka kuona maadili ya kikristo yakitawala na kuongoza siasa za ujerumani na kimataifa. Anatajwa kutoa mchango mkubwa katika kujenga ulaya mpya ya kikristo na umoja chini ya nato baada ya vita kuu ya pili ya dunia.

  Kwa upande mwingine rekodi zinaonyesha kuwa konrad alichangia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa taifa la israel, jambo lililoenda na kuporwa ardhi ya wapalestina na kudhalilishwa hadi hii leo.

  Ujerumani ikitajwa kama nchi ya kikristo hii leo, mchango mkubwa unatokana na konrad hermann joseph adenauer na chama chake cha cdu pamoja na ile taasisi yake konrad adenauer foundation ( konrad - adenauer - stiftung ) (kas). Hii ni taasisi iliyo chini ya chama rafiki wa chadema, yaani cdu ambayo iliundwa mwaka 1956 ikiwa taasisi ya kikristo ya kutoa elimu ya siasa na kiraia kwa mtizamo wa kikristo. Awali ilipoanzishwa mwaka 1956 ilijulikana kwa jina la "society for christian democratic education work" ndio mwaka 1964 kikapewa jina la konrad adenauer kwa heshima ya mwanzilishi wake.

  Ni taasisi ambayo ina miradi 200 katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo hii ya kutoa elimu ya siasa, maadili, uongozi na hata uchumi kwa vyama vya siasa ambavyo vinakubaliana na sera zake za kikristo. Kwa upande wa chama cha cdu ambacho ni rafiki wa chadema inaelezwa wazi kuwa "is christian- based applying the principles of christian democracym and emphasizes the christian understanding of humans and their responsibility toward god" kwa japo wale ambao sio wakristo wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho lakini wajue misingi yake ni kinafuata maadili na kanuni za kikristo katika siasa zake na namna ya kumwelewa binadamu na wajibu wake kwa "mungu"

  kutokana na msimamo wake huo wa kikristo chama tawala cha ujerumani cdu kimekuwa mstari wa mbele madhubuti kupinga uturuki isikubaliwe kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya. Uturuki inaonekana kama nchi ya kiislamu kwa vile wananchi wake karibu wote ni waislamu. Wakristo wa ndani ya uturuki ni wale wahamiaji. Hata hivyo, pamoja na jitihada za cdu na konrad yake kufanya juhudi za kujenga jamii ya kikristo ujerumani, ulaya na ulimwenguni dalili zinaonyesha kuwa ujerumani inazidi kusilimu kila uchao. Hali hiyo imepelekea kiongozi wa nchi hiyo chancellor angela merkel kutoa kauli akiwazindua wajerumani wenzake kwamba nchi yao hivi sasa inakimbilia kuwa ya kiislamu. Akinukuliwa na vyombo vya habari mwaka jana kansela angela amesema kuwa wajerumani (wakristo) wameshindwa kugundua jinsi waislam walivyojipenyeza na kupenyeza dini yao ulaya jambo ambalo limebadili hali ya mambo. Akasema kutokana na hali hiyo sasa itabidi wajerumani wajifunze kuona misikiti mingi zaidi ya makanisa waliyo kuwa wamezoea kuyaona huko nyuma. Kwa mujibu wa gazeti la frankfurter allgemeine zeitung, si muda mrefu misikiti ujerumani itakuwa mingi kuliko makanisa.

  My take

  wasio kuwa vijana viongozi wa wakristo jiandaeni kufundishwa maadili ya kikristo nawatakieni kila la heri.

  Ukipata muda pitia hizi links f

  http://www.germanculture.com.ua/library/facts/bl_cdu_csu.htm

  http://www.ena.lu/manifesto_christian_democratic_union_cdu-022500194.htmlhttp://www.cdu.de/en/3440_3457.htm


  Mwisho napenda kuwapa tahadhari kama mtu hana cha kuchangi ni bora aache kuliko kutoka nje ya mada kwani hatavumilika na anaweza kuambulia BAN

  7 - Off-Topic Posts:

  There is no major punishment for off-topic posters. But lets be honest, it drives us all mad!! If you have something to say but it really has nothing to do with the current thread you are in, please open a new thread for it. Otherwise it will just be deleted and won't solve anything at all.

   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mbowe sio Mkatoliki ni M-lutheri, acha sokomoko!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  SOKOMOKO, salamu kwa wafuatao:

  -Rafiki yangu KUPENG'E
  -Best yangu MALARIA SUGU
  -
   
 4. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huna hoja unajaza server ya JF tu,
   
 5. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Chadema kama chama cha Siasa kinaogozwa na Katiba yake. Iwapo katiba hiyo inaelekeza masuala ya kiimani hapo kutakua na tatizo na si vinginevyo. Ushirika katika siasa haumaanishi kufuata katiba ya chama unachoshirikiana nacho. Katika maelezo yako unaelezea CDU itasaidia kujenga uwezo kwa kutoa mafunzo ya uongozi kwa vijana wa chadema na kwako unaona kuwa ni tatizo.

  Kwa mtazamo wa kidunia ya leo masuala ya uongozi yanafundishwa kama sehemu ya sayansi ya jamii na kunamitaala inayotumika na hayana uhusiano wowote na masuala ya theolojia ambayo ni elimu ya dini. Kwa maneno mengine kusomea uongozi hakufanyi kuwa Kasisi au Mchungaji wala Padre au muumini hata kama umepata mafunzo hayo kwenye chuo cha kidini.

  Kwa msingi huo na kwa kufahamu kiwango cha maendeleo kilichopo Ulaya hakuna mtu wa kuchanganya mambo ya imani na Uongozi wa kisiasa. Huu ni mtazamo wangu ambao unapingana na hoja yako.
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mazee,

  Unajua kuna vitu ukisikia na kumeza vizima vizima, unaamini na kudhani ni kweli.

  German nimefika mara kadhaa na nimeongea na Wajeruman wengi sana na jamaa ambao wameishi German miaka mingi.

  Hiyo hali uliyoandika hapo si kweli hata kidogo. German ni moja ya nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na watu wasioamini. Jamaa wakitaka, wanabadilisha mambo hata bila kusema sana. Kama ulifika Berlin miaka ya 90 wakati karibu Berlin yote ikiwa ni BUILDING SITE, kulikuwa na wageni wengi sana. Kulikuwa na mpingo kama vile umefika Africa, Waarabu kama vile umefika Uarabuni, nk nk. Ukifika sasa hivi huwezi amini jinsi walivyosafisha na mipingo wote wamekimbia.

  Pia hata hao Waislaam, wao wakija ni kweli wanakuwa na dini ila watoto wao wanaanza kuchukua tabia na mila za Ki-German. Ulevi, Ufuska, Ustaarbu, Hard work na mengine mengi wanayosifika Wajeruman.

  Vijana wa Kiarabu huwa ndiyo wanaoongoza kwa ULEVI wa kupindukia. Wanabadilisha wanawake kama hawana akili nzuri na kama wanatoka Saudi Arabia na wana hela, wanatumia vibaya sana UHURU wanaoukuta Ulaya.

  Hizo blaa blaa zako, waambie washamba wenzio wasiofahamu kitu gani hasa kinaendelea huko Ulaya. Wazungu kama wakiona wanazidiwa, watabadilisha tu mapigo na kuwafukuza kwa makosa hata madogomadogo Waarabu. Watoto wao wengi watabaki kuwa Wakristo au hata kuwa hawana dini. Hata kama wazazi wanawabana sana watoto, tumesikia mauwaji mengi ya mzazi akibishana na mwanae. Watoto Wamezaliwa Ulaya na kukulia Ulaya, wanakuwa wanataka kuishi kama Wa Ulaya na baba/mama akileta za kuleta, wanatukunana na hapo unazuka ugomvi mkubwa sana kati ya Mzazi na mtoto na hadi mzazi kumuuwa Mwanae.

  Ikalaga baho.
   
 7. S

  Sikubali Member

  #7
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani chadema wote ni wakatoliki? Prof.safari je mkatoliki? Usipende kushabikia udini bwana c vizuri. Thanks.
   
 8. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [​IMG]avatar yako

  mtoa mada anaoneka sio mpenda ukristo , avatar umeweka ya nyerere na papa (mkuu wadini yake alipokuwa hai)
  kwa maana nyingine uwezi kuwa na mawazo ya kujenga hapa una misingi yako ya kutopenda ukristo kwama maana hiyo hata kama hii ya CDM NA CDU iwe safi au mbaya wewe itakuwa MBAYA tu

  MODS hii ifutwa mtoa mada ana vita ya kidini
  hata profile picha yako nayo unaonyesha bado una mambo hayo
  kama hii itaruhusiwa kwa kisingizio chochote sijui inaleta matiki yeyote
   
 9. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sokomoko acha longolongo
  CDU kutoa mafunzo kwa wanachama wa CHADEMA, sio kitu cha ajabu sema wewe mwenyewe umeweka hii thread kwa lengo lako.
  Mbona watoto wa kiislamu hapa TZ wanasoma shule za seminari zenye maadili ya Kikristo kwani kitu gani huwa kinaharibika??
  Tuache mawazo ya kipuuzi kama ya Waarabu na Wapalestina ya kujitoa mhanga.
  KAMA VIPI MODS IFUTENI TU HII THREAD NA SOKOMOKO APIGWE BAN.
   
 10. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn

  hii ni kuipinga kisarafina tu.
  burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn burn
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu sana kutofautisha Ukiristo na Chadema! Ndio maana umeona Chama cha Kikiristo cha Ujerumani (CDU) kinashirikiana na Wakiristo wenzao Chadema, sababu sera zao zinafanana kuendeleza Ukiristo.
  Hamas ni chama cha kiislam unadhani kama utashirikiana nacho kwenye mafunzo yao unadhani watu watasemaje!
  WE DARE TO TALK OPENLY
   
 12. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata chama cha Gaddaf kikiwa tayari tupeleke vjana kwenda kujifunza kwake,TUTAKWENDA,Hata hivyo katiba ya Tz,hairuhusu vyama vya kidini,mwambie boc wako,Jk akivute kama mnaamini ni cha kidini
   
 13. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  post za sokomoko

  Je Kikwete ni mdini? Started by Sokomoko‎, 3rd December 2010 03:29 PM

  Utumwa, Ukristo, Uislam, na Mapinduzi Started by Sokomoko‎, 6th December 2010 11:13 AM
  Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikatolikiStarted by Sokomoko‎, Today 03:19 PM
  Moto wa katiba mpya wazidi kushika kasi, KANISA KATOLIKI WAJITOSA,Started by Sokomoko‎, 17th January 2011 09:04 AM

  [​IMG]

  Join Date : 29th March 2008
  Location : Kijijini

  Posts : 1,584


   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red: Kama ilivyo vigumu kutenganisha UFISADI na CCM.
   
 15. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  wawe wakatoriki ama wasiwe utafanya nini na muhammed alishakufa zamani?
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Zitto ni muislam lakini najuwa alipataya mafunzo fulani ya kuendeleza vijana wa chini ya Jangwa la sahara huko Ujemani labda achangie hii hoja kutusaidia kupambanuwa ukweli wowote.
   
 17. M

  Mponjori JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 2,210
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona kikwete aliwah kusoma seminary za kikristo na hajabadili dini?acha kuchochea udini,wa2 2lishasahau habari za udini uc2rudshe nyuma mkubwa!
   
 18. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Modssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssss
  plz peleka jukwaa la dini hii kitu
   
 19. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwanza tittle na habari yako haviendani, pilli we mswahili wa wapi? ni MLENGO sio MRENGO, bure kabisa. Tatu So what? tangaza basi na wewe huo MRENGO wako, ovyo kabisa!
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Wewe kama upendi kuchangia waachie wenzako wachangie, hii thread ni muhimu sana kwa taifa letu
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...