Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikatoliki

Status
Not open for further replies.
Haya ni matokeo ya binary philosophy: either you are a muslim or you are against islam.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Nimeipitia katiba ya chama cha Kikiristo cha Ujerumani (CDU) ni marufuku mtu yoyote asie kuwa Mkiristo kugombea nafasi yoyote kwenye chama, sasa chama kama hiki unategemea ukiwa na urafiki nacho na wanakupa misaada bila kuwa mwenzao kwenye Ukiristo?

Mbona mnatuaibisha waislamu kwa hoja zenu zisizokuwa na miguu wala vichwa.Tatizo hawa ijana ambao waliishia madrasa uelewa wao ni mdogo.
Mimi sijaona mwislamu mwenye upeo na ilimu yakutosha anaye endekeza upuuzi huu.Ushauri wangu, endapo tutapuuza topic kama hizi zitakufa natural death.
 
Mbona mnatuaibisha waislamu kwa hoja zenu zisizokuwa na miguu wala vichwa.Tatizo hawa ijana ambao waliishia madrasa uelewa wao ni mdogo.Mimi sijaona mwislamu mwenye upeo na ilimu yakutosha anaye endekeza upuuzi huu.Ushauri wangu, endapo tutapuuza topic kama hizi zitakufa natural death.
Hivi wewe mbona unakuwa Scatty! Kila siku mnajidanganya eti mmesoma, ebu niambie hizo Elimu zenu unazojitapa nazo zimeishaidia nini taifa letu kutoka kwenye umasikini wa kutupwa dunia, au zimewasaidia kufanya ufisadi mkubwa kwenye nchi yetu, halafu nipe kiwango cha Elimu cha YESU, tujadili vizuri
 
Acheni jazba ni vema mkaichambua hii hoja kwa hoja wengi mnatoka nje ya mada sijui ni makusudi ili kupoteza mwelekeo wa mada au na nyie hamna elimu kama mleta mada? Naona ndugu zanguni mnakimbilia hoja nyepesi nyepesi hii mada imekuwa mwiba kwenu. Hii hoja ukijumlisha na symbion unaweza ukapa kitu ila watu mmekuwa vipofu basi hata kusikia hamsikii?
 
Hivi wewe mbona unakuwa Scatty! Kila siku mnajidanganya eti mmesoma, ebu niambie hizo Elimu zenu unazijitapa nazo zimeishaidia nini taifa letu kutoka kwenye umasikini wa kutupwa dunia, hawo zimewasaidia kufanya ufisadi mkubwa kwenye nchi yetu, halafu nipe kiwango cha Elima cha YESU, tujadili vizuri
Mimi ya Yesu cjui ila najua ya mtume asiyejua kusoma wala kuandika. Mtume wa kwanza kutokanyaga hata ngumbaru. Ala alikuwa na elimu ya juu sana pamoja na kutojua kusoma na kuandika. Alikuwa na elimu ahera. Balaa nakuambia yuko juu mtume wa jangwani.
 
Yusuph Makamba alisoma seminary lakini hakubadili dini na wala hakubadilishwa dini. Ni wazi Sokomoko ni mtu anayependa kuja kuona nchi inaingia kwenye machafuko ya kidini siku moja ndiyo maana hana Post nyingine zaidi ya kuchochea udini. Niweke wazi kuwa Taaluma huongozwa na mitaala na si hisia kwa hisia mbovu kama za sokomoko. Pia ni wazi utambue Dira au Injini,malengo na makubaliano ya Pamoja ya CDM ni katiba yao na si blaa blaa au kuangalia nani anashirikiana na yupi. Katiba ya CDM KATIKA IBARA 3.1.9 inasema' CDM inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya Dola'. Ubinafsi,uvivu wa kufikiri,uchochezi na ufedhuli ndiyo vinavyomuongoza SOKOMOKO. Hii dhambi itakuja kumgharimu. Aachane nayo brazaz.
 
Nimefuatilia kwa muda mrefu hii mada nikaona kinyaa cha kuichangia ila naona sijitendei haki kukaa kimya wakati naweza kuandika japo mistari kadhaa.

Bila chembe ya shaka huyu aliyeweka hii mada ni muislamu mwenzangu. Mimi ni muislamu kama yeye japo sijajua kiwango chake cha elimu na uwezo wa kuchakata mambo. Lakini pia sijajua uwezo wake wa kuhimili joto lake kiitikadi. Leo ana ona Cdm ni wadini, juzi aliambiwa Cuf ni wadini na vyama vyote hivi vina wanachama wa dini zote, inawezekana hajui lakini imetamkwa wazi kwenye katiba juu ya uanzishwaji wa vyama vya siasa. Kama Cdm au Cuf kingekuwa cha waislamu au wakristo pekee visingekuwepo. Atambue ccm inatumia ujinga wa wananchi ili kuwagawa na kuleta fikra za udini, na imefanikiwa mara kadhaa kama ilivyofanikiwa kwake. Lakini pia asidhanie wasabato, wakatoliki, walutheri, walokole nk wana kauli ya pamoja kushawishi waumini wao wafuate chama flani, hivyo hivyo shia, sunn, ahmadiyyah nk ndio maana haijawahi na haitatokea viongozi makini wabobezi wa elimu zote wasimame na kuwaambia waumini wao kuwa msifuate chama hiki kwa kuwa ni cha dini hii.

Kulalamika huku wenzetu wakichanja mbuga si dawa. Ulevi wa kiitikadi kuona chama flani nicha udini wakati si kweli ni ukame wa fikra. Tukazanie elimu zote kwa watoto wetu, bakwata ifumuliwe wakae viongozi wenye vision na elimu ya juu ili wasimamie shule zetu vizuri ziwe mfano wa kuigwa kwa kutoa elimu bora ili kuondokana na kizazi cha huyu sokomoko kinacho angalia sarafu upande mmoja.
 
Hivi wewe mbona unakuwa Scatty! Kila siku mnajidanganya eti mmesoma, ebu niambie hizo Elimu zenu unazijitapa nazo zimeishaidia nini taifa letu kutoka kwenye umasikini wa kutupwa dunia, hawo zimewasaidia kufanya ufisadi mkubwa kwenye nchi yetu, halafu nipe kiwango cha Elima cha YESU, tujadili vizuri

vilaza bana ..... teh tehh tehhh
 
CDU=CHRISTIAN DEMOCRATIC UNION
CDM=CHRISTIAN DEMOCRATIC MOVEMENT-Padree Slaa

we are watching your movement.
 
Chadema kama chama cha Siasa kinaogozwa na Katiba yake. Iwapo katiba hiyo inaelekeza masuala ya kiimani hapo kutakua na tatizo na si vinginevyo. Ushirika katika siasa haumaanishi kufuata katiba ya chama unachoshirikiana nacho. Katika maelezo yako unaelezea CDU itasaidia kujenga uwezo kwa kutoa mafunzo ya uongozi kwa vijana wa chadema na kwako unaona kuwa ni tatizo.

Kwa mtazamo wa kidunia ya leo masuala ya uongozi yanafundishwa kama sehemu ya sayansi ya jamii na kunamitaala inayotumika na hayana uhusiano wowote na masuala ya theolojia ambayo ni elimu ya dini. Kwa maneno mengine kusomea uongozi hakufanyi kuwa Kasisi au Mchungaji wala Padre au muumini hata kama umepata mafunzo hayo kwenye chuo cha kidini.

Kwa msingi huo na kwa kufahamu kiwango cha maendeleo kilichopo Ulaya hakuna mtu wa kuchanganya mambo ya imani na Uongozi wa kisiasa. Huu ni mtazamo wangu ambao unapingana na hoja yako.

Nimekuwa nikiwaasa wanajamiiforums hasa vijana wa CHADEMA kuacha kushabikia mambo kibubusa pasi na kutafakari.Evi katika hali tu ya kawaida inawazekanaje taasisiau chama fulani kuunda ushirikiano fulani masherti? Au hujui kuwa Nchi mbalimbali zinapoenda kuomba misaada katika WB na IMF hupewa misaada hiyo kwa masherti?
Sasa 'if that the case' iwaje CDM washirikiane na CDU pasi na masherti? wakati huo ikifahamika kuwa lengo kuu la CDU ni kusambaza
ukristu kama ilivyolengwa na mwaasisi wake? acha ububusa kaka,ukweli ni kwamba,kama CDM wameunda ushirikiano na ,CDU fahamu kabisa chadema kitaendeshwa kwa itikadi ya CDU kwani chama kinapata misaada mingi kutoka CDU
 
Kwa ruhusa ya one of the mods ameniruhusu kuibandika tena hii tread baada ya kuchakachuliwa hapo awali. Ni matumaini yangu hapa JF ni "we dare to talk openly" nategemea watakaoijibu hii hoja watajibu kwa kutumia busara na hoja zilizofanyiwa uchambuzi wa hali ya juu. Najua hoja hii ni chungu na ndio maana awali mod aliei "move" ikawa haiwezi kusomeka alishindwa kuimeza kwa uchungu wake. Tuvumiliane tujadiliane kwa ajili ya ustawi wa taifa letu. Tukumbuke Uislam na Ukristo upo nchini na sisi ndio wenye hizo dini na ni "Watanzania" basi tuwe kitu kimoja mpaka mwisho wa Tanzania. Kila la kheri na anza kusoma...............Si jambo la tetesi tena kwamba sera na mrengo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni ule wa Kikristo. Hii ni kutokana na hatua yake ya kuweka wazi urafiki wake wa karibu na Chama cha Kikristo cha Ujerumani, Christian Democratic Union (CDU). Kutokana na urafiki huo, CDU kimesema kuwa kitawapa nafasi za mafunzo nchini Ujerumani vijana na viongozi wa Chadema, kusomea maadili na uongozi.Maadili na uongozi ambao kwa mujibu wa mtizamo na sera za CDU ni yale ya Kikristo kama yalivyobuniwa na mwasisi wa chama hicho Konrad Harman Joseph Adenauer. Taarifa zilizotolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa Chadema Mhe Freeman Mbowe zinasema kuwa fursa hiyo imetolewa kwa chama chake baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na ujumbe wa CDU uliokuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa Ujerumani Profesa Dk. Horst Kohler. Mazungumzo hayo yalimshirikisha katibu mkuu wa chama hicho Dk Wilbrod Slaa na viongozi wengine wa juu.Mbowe meviambia vyombo vya habari kuwa katika mazungumzo yao Kohler alisema dhamira ya kuwapa nafasi za masomo vijana viongozi wa Chadema inalenga kuwafanya wawe viongozi wenye maadili mazuri kwa taifa lao. "Tumekubaliana ambapo tutapata nafasi za masomo kwa vijana ambao ni viongozi wa Chadema kwenda kusomea uongozi na maadili chini Ujerumani" alisema. Kwa hapa nchini imeelezwa kuwa Chadema itafanya kazi kwa karibu na kwa kushirikiana na taasisi ya Conrad Adenauer Foundation ambayo ni ya taasisi ya Kikristo iliyo chini ya Chama cha CDU.CDU kikiwa kimeanzishwa mwaka 194, ni chama cha Kikristo kilichowaunganisha Wakatoliki na Protestant kikilenga kujenga Ujerumani yenye maadili ya Kikristo katika siasa, kijamii, maadili na kila kipengele cha maisha.Mwanzilishi wake Konrad Hermann Joseph Adenauer anatajwa kuwa mfuata Ukatoliki aliyekuwa tayari kuufia Ukatoliki wake na ambaye amefanya kazi kubwa kutaka kuona maadili ya Kikristo yakitawala na kuongoza siasa za Ujerumani na Kimataifa. Anatajwa kutoa mchango mkubwa katika kujenga Ulaya mpya ya Kikristo na umoja chini ya NATO baada ya vita Kuu ya pili ya dunia.Kwa upande mwingine rekodi zinaonyesha kuwa Konrad alichangia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa taifa la Israel, jambo lililoenda na kuporwa ardhi ya wapalestina na kudhalilishwa hadi hii leo.Ujerumani ikitajwa kama nchi ya Kikristo hii leo, mchango mkubwa unatokana na Konrad Hermann Joseph Adenauer na chama chake cha CDU pamoja na ile taasisi yake Konrad Adenauer Foundation ( Konrad - Adenauer - Stiftung ) (KAS). Hii ni taasisi iliyo chini ya chama rafiki wa Chadema, yaani CDU ambayo iliundwa mwaka 1956 ikiwa taasisi ya Kikristo ya kutoa elimu ya siasa na kiraia kwa mtizamo wa Kikristo. Awali ilipoanzishwa mwaka 1956 ilijulikana kwa jina la "Society for Christian Democratic Education Work" ndio mwaka 1964 kikapewa jina la Konrad Adenauer kwa heshima ya mwanzilishi wake.Ni taasisi ambayo ina miradi 200 katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo hii ya kutoa elimu ya siasa, maadili, uongozi na hata uchumi kwa vyama vya siasa ambavyo vinakubaliana na sera zake za Kikristo. Kwa upande wa chama cha CDU ambacho ni rafiki wa Chadema inaelezwa wazi kuwa "is Christian- based applying the principles of Christian democracym and emphasizes the Christian understanding of humans and their responsibility toward God" Kwa japo wale ambao sio wakristo wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho lakini wajue misingi yake ni kinafuata maadili na kanuni za Kikristo katika siasa zake na namna ya kumwelewa binadamu na wajibu wake kwa "Mungu" Kutokana na msimamo wake huo wa kikristo chama tawala cha Ujerumani CDU kimekuwa mstari wa mbele madhubuti kupinga Uturuki isikubaliwe kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Uturuki inaonekana kama nchi ya Kiislamu kwa vile wananchi wake karibu wote ni Waislamu. Wakristo wa ndani ya Uturuki ni wale wahamiaji. Hata hivyo, pamoja na jitihada za CDU na Konrad yake kufanya juhudi za kujenga jamii ya Kikristo Ujerumani, Ulaya na Ulimwenguni dalili zinaonyesha kuwa Ujerumani inazidi kusilimu kila uchao. Hali hiyo imepelekea kiongozi wa nchi hiyo Chancellor Angela Merkel kutoa kauli akiwazindua Wajerumani wenzake kwamba nchi yao hivi sasa inakimbilia kuwa ya Kiislamu. Akinukuliwa na vyombo vya habari mwaka jana Kansela Angela amesema kuwa Wajerumani (Wakristo) wameshindwa kugundua jinsi Waislam walivyojipenyeza na kupenyeza dini yao Ulaya jambo ambalo limebadili hali ya mambo. Akasema kutokana na hali hiyo sasa itabidi Wajerumani wajifunze kuona Misikiti mingi zaidi ya Makanisa waliyo kuwa wamezoea kuyaona huko nyuma. Kwa mujibu wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung, si muda mrefu misikiti Ujerumani itakuwa mingi kuliko makanisa. My takeWasio kuwa vijana viongozi wa wakristo jiandaeni kufundishwa maadili ya kikristo nawatakieni kila la heri.Ukipata muda pitia hii link The manifesto of the Christian Democratic Union (CDU)
Bila ya mafundisho na ustaarabu wa kikristo, basi dunia ingekuwa giza kama akili ya alitoa mada hii
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Acheni jazba ni vema mkaichambua hii hoja kwa hoja wengi mnatoka nje ya mada sijui ni makusudi ili kupoteza mwelekeo wa mada au na nyie hamna elimu kama mleta mada? Naona ndugu zanguni mnakimbilia hoja nyepesi nyepesi hii mada imekuwa mwiba kwenu. Hii hoja ukijumlisha na symbion unaweza ukapa kitu ila watu mmekuwa vipofu basi hata kusikia hamsikii?

mwehu hana alama
 
Nimekuwa nikiwaasa wanajamiiforums hasa vijana wa CHADEMA kuacha kushabikia mambo kibubusa pasi na kutafakari.Evi katika hali tu ya kawaida inawazekanaje taasisiau chama fulani kuunda ushirikiano fulani masherti? Au hujui kuwa Nchi mbalimbali zinapoenda kuomba misaada katika WB na IMF hupewa misaada hiyo kwa masherti? Sasa 'if that the case' iwaje CDM washirikiane na CDU pasi na masherti? wakati huo ikifahamika kuwa lengo kuu la CDU ni kusambaza ukristu kama ilivyolengwa na mwaasisi wake? acha ububusa kaka,ukweli ni kwamba,kama CDM wameunda ushirikiano na ,CDU fahamu kabisa chadema kitaendeshwa kwa itikadi ya CDU kwani chama kinapata misaada mingi kutoka CDU
Kama Katiba ya CDU inatamka wazi kuwa ni Marufuku kwa Mtu yeyote asiye Mkristo kuwa kiongozi basi ni dhahiri Values zake ni tofauti na za CDM, lakini sasa inakuwaje CDM ifanye urafiki na chama chenye "Udini" kama hiki cha CDU?. Hapo kuna mawili either (1) CDM iko sympathetic na ajenda ya "Ukiristo" lakini haitaki kukiri wazi (2) Chadema haijali kwamba kinafanya urafiki na Chama gani kiwe cha kidini au si cha kidini. Lakini hatari ya namba (2) ni hii, ni kwa namna gani CDM itajipambanua kuwa huru dhidi ya kamba za influence kutokana na vyama hivyo vya kidini?.
 
Nimekuwa nikiwaasa wanajamiiforums hasa vijana wa CHADEMA kuacha kushabikia mambo kibubusa pasi na kutafakari.Evi katika hali tu ya kawaida inawazekanaje taasisiau chama fulani kuunda ushirikiano fulani masherti? Au hujui kuwa Nchi mbalimbali zinapoenda kuomba misaada katika WB na IMF hupewa misaada hiyo kwa masherti?
Sasa 'if that the case' iwaje CDM washirikiane na CDU pasi na masherti? wakati huo ikifahamika kuwa lengo kuu la CDU ni kusambaza
ukristu kama ilivyolengwa na mwaasisi wake? acha ububusa kaka,ukweli ni kwamba,kama CDM wameunda ushirikiano na ,CDU fahamu kabisa chadema kitaendeshwa kwa itikadi ya CDU kwani chama kinapata misaada mingi kutoka CDU

kama mtu hujaenda shule halafu ukajazwa na udini basi unakuwa kipofu kabisa..! hoja yako hapo juu imeshajibiwa mara nyingi kwenye thread hii !
nakuuliza na ujibu kwa hoja! hivi serikali ya CCM inashirikiana na nchi ngapi hapa duniani? CCM yenyewe inashirikiana na vyama vingapi hapa duniani?
Ina maana gani kwa Tanzania kupokea misaada na kushirikiana na nchi ya Kiislamu ya Iran ? Je serikali ya ccm inataka na sisi wote tuwe waislam?
Nyinyi mnaondekeza udini ni watu msio na mbele wa nyuma...nadhani ahueni yenu mtaipata endapo tu machafuko yatatokea!
 
Status
Not open for further replies.
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom