Chama cha CDU cha nchini Ujerumani kinataka wahamiaji wanaoishi nchini humo kuheshimu utamaduni wa Ujerumani na kuitambua taifa la Israel

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
12,903
15,335
Chama cha CDU cha nchini Ujerumani kinataka hatua za haraka zichukuliwe ili kudhibiti wahamiaji wanaoishi nchini humo wanaotaka utamaduni wao na imani zao za kidini ndizo ziwe juu ya zile za mwenyeji wao yaani Ujerumani.

Pia wanataka wahamiaji hao watambue haki ya kuwepo kwa taifa la Israel.

---

Chama kikuu cha upinzani nchini Ujerumani, CDU kimezindua mpango wake wa kisera Jumatatu, kwa wito wa kufanya mabadiliko makubwa katika sera ya uombaji hifadhi ya Umoja wa Ulaya.

Rasimu ya programu kutokaCDU inataka Waislamu nchini Ujerumani kukumbatia maadili ya Ujerumani ambayo kwa kiasi kikubwa yanafuata misngi ya Kikristo, na kwamba wahamiaji lazima watambue haki ya kuwepo kwa taifa la Israel kama sehemu ya "utamaduni elekezi" wa Ujerumani (Leitkultur).

Rasimu hiyo ya programu ya CDU pia inataka Ujerumani irejee kutumia tena nishati ya nyuklia pamoja na kufanya mageuzi ya pensheni na soko la ajira.

"Wale wote wanaotaka kuishi hapa lazima watambue utamaduni wetu elekezi bila masharti," inasema rasimu hiyo. "Ni wale tu ambao wamejifunga kuheshimu utamaduni wetu elekezi ndiyo wanaweza kujumuika na kuwa raia wa Ujerumani."

Katibu Mkuu wa CDU Carsten Linnemann aliielezea rasimu ya mpango-msingi huo kama hati elekezi ya kutayarisha chama kwa ajili ya uchaguzi ujao wa nchi nzima, unaotazamiwa kufanyika 2025.

"Kama kutaitishwa uchaguzi mkuu wa mapema, tutakuwa tayari," alisema Linnemann, wakati akiwasilisha rasimu ya kwanza mjini Berlin. Watu nchini Ujerumani wanahisi kutokuwa salama na wanahitaji mwelekeo na msaada, alisema Linnemann. ""Na tutatoa mwelekeo huu kupitia mpango huu wa kisera.

Uislamu hautakuwa tena 'sehemu ya Ujerumani'

Rasimu ya mpango huo inakitenganisha chama na matamshi ya rais wa zamani wa Ujerumani Christian Wulff, mwanachama wa CDU ambaye alitangaza mwaka wa 2010 kwamba "Uislamu sasa pia ni sehemu ya Ujerumani."

Badala yake, rasimu ya programu inasema kwamba "Waislamu ambao wanashiriki maadili yetu ni sehemu ya Ujerumani."

Kuhusu uhamiaji, rasimu ya mpango wa CDU inataka kila mhamiaji anayeomba hifadhi katika Umoja wa Ulaya apelekwe "nchi ya tatu salama" ambapo maombi yatazingatiwa, na kuweka viwango vya hiari vya idadi ya wakimbizi ambao kila nchi ya Umoja wa Ulaya itakubali.

"Muungano wa hiari" kutoka miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya unaweza kujitolea kupokea baadhi ya wakimbizi kila mwaka - lakini hadi kiasi fulani tu, kulingana na rasimu hiyo. Chama hicho hakikubainisha ni watu wangapi ambao CDU itakuwa tayari kupokea kwa ajili ya hifadhi nchini Ujerumani kila mwaka.

Waraka huo wenye kurasa 70 umepewa kichwa cha habari "Kuishi katika Uhuru: Kuiongoza Ujerumani kwa Usalama katika Wakati Ujao." Rasimu hiyo imewasilishwa kwa kamati za ngazi za juu za chama cha CDU na inatazamiwa kupitishwa rasmi na bodi kuu ya chama katika mkutano wa faragha katikati ya mwezi wa Januari.

Soma pia: Merkel awaomba wanasiasa kuweka pembeni tofauti zao

Kisha itajadiliwa na wanachama na kupitishwa na wajumbe 1,001 wa CDU katika mkutano wa chama mwezi Mei.

Chama cha CDU, cha kansela wa zamani Angela Merkel, kilizindua mchakato wa kuandaa mpango mpya wa sera ya msingi baada ya kupoteza madaraka katika uchaguzi wa bunge wa 2021 uliomweka madarakani Kansela Olaf Scholz.

Mpango wa msingi wa sasa wa chama hicho uliandaliwa mwaka 2007.

Chanzo: Chama cha CDU chataka hatua kali dhidi ya uhamiaji Ujerumani – DW – 11.12.2023
 
Wasitupangie
Wakitaka watufukuze mpaka mnalazimisha watu kuitambua israhell kweli mna hali mbaya
Hamas kamatieni hapo hapo vilio vishaanza kusikika sehem nyingi
 
When you're in a host country you're entitled to observe the laws of the land however unfriendly they're to you.

Failure to abide by that may automatically lead to your indictment for the breach of the law and without recourse for argument, the best thing you can do to avoid a collision with the authorities is to vacate such country and settle in a country whose laws you can find easy to comply with.
 
Back
Top Bottom