Pepombili,
Jamvi hili si maahali pa kutoa ushahidi. Kuna mahali pa kutolea ushahidi. Kauli zangu zimetolewa kwenye hotuba ya kuwaelimsha Watanzania, tena in this case wa Jimbo la Igunga Jimbo la Rostam Aziz. Kazi yangu kama Katibu Mkuu katika mikutano ya hasdhara si kutoa ushahidi bali kueleza na kuonyesha uozo ndani ya CCM na Serikali yake ili Watanzania waweze kufunguka macho. Mwenye kuona kaonewa ana mahali pa kutaka "redress" kama anafikiri nilichosema siyo kweli.
Nilikwisha kueleza kuwa "mahakamakubwa kuliko zote kwa mwanasiasa ni 'wananchi' (Ibara ya 8 ya Katiba). Tuliowataja leo wako mahakamani, Fedha za EPA mlizobishia angalau JK aliutangaza Bungeni kuwa zimerudishwa sehemu (Japo CAG katika Taarifa yake ya Hesabu za Serikali Kuu anasema fedha hizo hadi Machi 2011 hajaona zimeingizwa akaunti gani japo zilihamishiwa TIB June, 20, 2010 (Jambo linalozua utata mpya kabisa katika historia ya ufisadi ikizangatiwa kuwa 2010 ilikuwa mwaka wa Uchaguzi-au zilirudishwa zikaenda tena kwenye uchaguzi kuisaidia CCM au hazikurudishwa kabisa na inakuwa usanii tu).
Kama Rizwani anaona ameonewa aende yeye mahakamani mimi nimemaliza kesi kwenye mahakama ya wananchi, lakini nadhani ni vema ungelinukuu vizuri "conclusion yangu badala ya kuchakachua statement yangu".