Siungi mkono Rais kutukanwa!

Siungi mkono Rais kutukanwa!

Lema umechemka tena mbona ulikaa kimya mkapa alipowaita sumaye na Lowasa wapumbavu. Kwangu mimi upumbavu ni tusi kubwa kuliko bwege. Sheria lazima zifuatwe na watanzania wote akiwemo rais na mawaziri

Kwahiyo kama alifanya kosa kwa kutokemea wakati huo aendelee kufanya kosa?
 
Walipokuwa wanawasilisha michango walikuwa wanakabidhi na kadi zao za chama mpaka useme ni amechangiwa na wanachama?
Katafute uzi ule utaona na mpaka viongozi wa chadema walitajwa kumchangia na kumkabidhi! Kamuangalie aliye mkabidhi
 
Unawezaje kujilinganisha na rais wakati hata ujumbe wa mtaa huna,lazima utambue heshima anayopewa rais ni taasisi si kama mtu binafsi

Kwani rais yeye ni breed tofauti na sisi watu wengine?

Hanyi huyo rais wenu? Hapumui? Hali chakula? Hanuki mdomo asubuhi akiamka? Haogi?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kwa ujumla si haki hata kidogo kumwita mtu yoyoyte - awe kiongozi au si kiongozi - jina baya linalomtweza utu wake. Ni muhimu tukajenga utamaduni wa kuheshimiana miongoni mwetu hata kama tunapingana kimtazamo katika mambo mbali mbali yanayohusu maisha yetu sisi watu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Ni vizuri pia watanzania wakajifunza.
Kama uko na mkata mkaa mwenzio au muuza genge mwenzako huko kumuita bwege ni kawaida tu,ila kumuita bwenge mtu anaeamua hatma ya taifa lako,anaeheshimiwa na kila idara ni utovu wa nidhamu usiovumilika!
Watu wajadili hoja,kutukana ni kukosa maadili!
 
Matusi sio jambo zuri kwa yeyote yule sio Rais tuu.
Lakini neno bwege nadhani sio tusi ndio maana hata wewe Lema pale naibu spika alipomwambia mbunge 'wewe bwege acha Ubwege" hukuomba afute kauli.
Watu hawakuchanga kuunga mkono kosa bali kuipinga adhabu ile na sheria yake.
Ni sawa kuwe na sheria itakayo muhukumu Sugu kwa kuonyesha kidole cha kati kuwa akatwe kidole au alipe faini milioni 20, watanzania tutamchangia sio kwa kuunga mkono kidole kati bali adhabu hiyo sio sahihi na sheria yake.
 
Kama hii ni hoja yako vasi kulikuwa hakuna umuhimu wa Rais kuwa na ulinzi kama anaopata kwa gharama ya walipa kodi.

Ulinzi wa rais na hoja yangu vina uhusiano gani?

Tatizo unaongelea nadharia. Mimi ninaongelea uhalisia.

Nope. Ni kinyume chake. Mi naongelea uhalisia wewe unaongelea ya kufikirika kama ilivyo kawaida yako.

Rais wa nchi ni tofauti na mwananchi mwingine nchini.

Hapana. Rais wa nchi anatokana miongoni mwa hao hao wananchi. Hatokei sayari nyingine kama Mushtara huko hadi awe tofauti na siye binadamu wengine.

Heshima kwa Rais lazima ilindwe lakini vilevile ni lazima na Rais ajiheshimu.

Heshima ya rais lazima ilindwe....na heshima ya wengine haina ulazima wa kulindwa eh?
 
Ni Kweli, Lakini Busara Ya Kumkanya Na Kumsaidia Ni Bora Zaidi Kuliko Kumwacha Akaozee Jela Wakati Inawezekana Kumrekebisha Mtaani.
Je, Huyo Hakuwa Mmoja Kati Ya Vijana Walioitwa Wapumbavu Kisa Wanataka Mabadiliko?
" Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko , Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu .

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono , lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara " Godbless Lema (Mp)
Ulichosema ni kweli kabisa lakini usipofunzwa adabu na wazazi wako hakuna atakayekufunza hapa duniani. Huyo Rais aliyesemwa ni Bwege ni sawa sawa na baba yake kiumri. Hivyo huyo kijana hana adabu huo ndio ukweli na utabaki kuwa ukweli
 
Kwani rais yeye ni breed tofauti na sisi watu wengine?

Hanyi huyo rais wenu? Hapumui? Hali chakula? Hanuki mdomo asubuhi akiamka? Haogi?
Tumuite msaliti Lema na ikiwezekana tuandamane basi kama unaona kakosea,mambo mengine hayahitaji akili nyingi kuona hili sawa au la
 
Siyo rais wa Marekani tu.

Hata wa Kenya tu hapo.

Achilia mbali akina David Cameron, Jacob Zuma, Francois Hollande na wengineo huko kwenye demokrasia kutushinda sisi.
University student jailed for insulting President Uhuru Kenyatta
Alan Wadi Okengo alias Lieutenant Wadi was jailed for two years after pleading guilty on two counts of hate speech and abusing the Head of State.

Friday January 2 2015

















DNCOURTHATESPEECH0201B.jpg




Moi University student Alan Wadi Okengo alias Lieutenant Wadi in a Nairobi court January 2, 2015, where he was charged with hate speech and insulting President Uhuru Kenyatta. He pleaded guilty and was jailed for two years. PHOTO | PAUL WAWERU | NATION MEDIA GROUP

In Summary
  • Milimani Law Courts resident magistrate Ann Kaguru said the harsh penalty would serve as a deterrent measure to others with a similar motive.
  • Mr Wadi was arrested while trying to flee the country at the Busia border on December 31, 2014. He was repatriated to Nairobi by the police.
Advertisement
 
" Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko , Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu .

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono , lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara " Godbless Lema (Mp)
Kama tunaamnini binadamu wote ni sawa, basi wote tuna haki ya kuheshimiwa na Hakuna binadamu anayepaswa kutukanwa.

Kumtukana yeyote yule ni utovu wa nidhamu, sio Rais tu. Tunachopinga sisi ni double standard.
Lowassa, Mbowe na viongozi wengine wametukanwa matusi yote huku duniani, lakini hakuna yeyote aliyewahi kuchukuliwa hatua.

Tulijitolea kumchangia Isack Habakuk sio kwa sababu alichokifanya ni kizuri ila tulitaka kutuma ujumbe kwa watawala.
 
Siyo rais wa Marekani tu.

Hata wa Kenya tu hapo.

Achilia mbali akina David Cameron, Jacob Zuma, Francois Hollande na wengineo huko kwenye demokrasia kutushinda sisi.

Nakumbuka mwaka juzi kuna cartoonist alimchora Zuma with his genitalia hanging. Hakuna walichomfanya huyu cartoonist zaidi ya baadhi ya watu kulalamika tu. Walichobahatika kufaulu watu wa serikali ni kuiomba mahakama iamrishe ile katuni isiwekwe tena public. Lakini cartoonist hakufanywa chochote kwa sababu ya umuhimu mkubwa wa fredom of speech kwa SA. Ingekuwa kwetu sijui ingekuwaje!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mmmmmmm. Kuna harufu nimenusa hapa. Waliochangisha fedha ni Ephatha Nanyaro na Malisa Godlisten. Kuna jambo nyuma ya pazia
Hao wote wanampango wa kumnyang'anya Lema jimbo! Halafu huyo Malisa ana kiherere sana
 
Back
Top Bottom